OKTOBA,
mwaka 2006,gazeti la New African, linalochapishwa 7COLDBATH Square, Jijini
London,liliandika katika Toleo lake Nambari 455 kwamba, “ HOW THE ANGLICAN CHURCH TREATED ITS SLAVES”!!
Kwamba kanisa
la Uingereza,Anglican, liliwahi kuwa na watumwa! Tena, watumwa wenyewe WAAFRIKA
ama watu Weusi wa Asili ya Afrika, ‘negros’ wakatumikishwa na kanisa,wakateswa
na kulimishwa katika mashamba ya miwa,kisha wakauliwa!
Kanisa hili,
ambalo siku hizi huunga mkono ndoa za jinsi moja;ushoga,usagaji na kubadili
jinsi(Kanisa la Afrika linajidai kuwa kichwa maji),Mkuu wake ni Malkia.Ndiye
anayeteua maaskofu wakuu,makasisi na maofisa wengine.
Kanisa
maarufu Uingereza,Westminster Abbey,(1050-1760) ndiko wazikwako watu wakubwa
sana wenye kuheshimiwa.
Turejee
katika ajenda ya leo,kwamba Feburuali 8 mwaka 2006,Askofu Mkuu wa
Cantebury,Rowan Williams(mkuu wa Kanisa wakati huo) aliomba msamaha kwa DHAMBI
hiyo ya kanisa kuwatumikisha watumwa,hasa watu WEUSI katika mashamba yaliyokuwa
katika makoloni ya Uingereza huko Barbados,katika Visiwa vya Caribbean.
Nataka
nikwambie msomaji,uwe makini na kila unachoambiwa na
maaskofu,makasisi,wachungaji,manabii wa siku hizi,mitume uchwara na masheikh.Pima
matendo yao na kauli zao kwanza.
Mwandishi, Adam
Hochschild, aliandika makala ndefu
kwamba visiwa vya
Caribbean(walikopelekwa watumwa ndugu zetu wapendwa) viligeuka nyumba za
kunyongea watumwa,kupigwa na kuteswa mithili ya magereza ya Abu Ghraib,Guantanamo
na magereza mengine ya siri Ulaya.
Leo,Uingereza
huongoza mataifa 54 ya Commonwealth,yaliyokuwa makoloni yake ili kuendeleza
ukoloni mamboleo hapa Afrika.
Yangalipo
makanisa na misikiti,masinagogi na nyumba za ibada,yanayopokea shuruti toka
nje,ili yumkini kuzivuruga nchi zetu kwa ghasia na mauaji. Hivi,makanisa na
misikiti,utumwa,mauaji,kunyonga watu na fujo vina uhusiano gani?
Waafrika
wengi,hasa vijana wa siku hizi hawajiulizi ‘repercussions’ za kulipwa posho na
vi NGO vya Ulaya ili kufanya vurugu hapa,na fujo za kijinga,kwa malipo ya
chakula na ahadi.
Tazama Irak
na Libya, siku hizi hamkani si shwari na Syria wameitumbukiza nchi katika miali
mikali ya moto wa mabomu kwa kisingizio cha kutafuta demokrasia, nadhani
tumeona hata Misri na kwingineko. Je, tumeshindwa kudai haki zetu kwa amani?
Wengine,hutumia
dini kama zana za kueneza ‘Imperealism’-utawala wan chi moja dhidi ya mataifa
mengine duniani.Dini zinapogeuka mlango wa kushawishi mataifa ya Afrika kuwa
chini ya akina Malkia ama matajiri wafuasi wa Freemasons Ulaya ama Marekani!
Nakiri,dini
halisi haifanyi unyama ninaosema hapa,mbali na kuwafundisha watu amani na
upendo na heshima kwa viongozi wa serikali. Kuna serikali katiti na fisadi
kuzidi Dola ya Rumi? Mbona Paulo katika Warumi sura 13 anawataka wafuasi wa
Ukristo kuheshimu serikali?
Demokrasia
na Haki za Binadamu hutumiwa siku hizi na hawa wauaji kama njia ya watu
kutafuta haki zaidi,kumbe vijana wanaingia mkenge! Hawa ni wauaji wale wale
ambao baba yao ana jicho moja na mkuki mkononi mwake.
Kuna
kiitwacho, European Hegemony au tuseme ni ‘Political Domination’ ndicho
huwasukuma hawa Wazungu kuvuruga mataifa
ya Afrika kwa vita,fujo,maandamano ya kipuuzi
kwamba ndiyo demokrasia na haki za binadamu!
Wee unachoma
moto nyumba na magari ya wenzako kwamba ndiyo haki gani? Unaua wenzako na
kuwanyima makazi halafu unasema ni kutafuta haki gani?
Bahati mbaya
sana,viongozi wengi wa dini hupokea posho na maagizo kutoka Ulaya na mahali
pengine zinakotoka dini zao,mwisho wa siku Afrika inawaka moto kwa machafuko.Huu
ni ugaidi unaochochewa na dini hizi.
Mtu mmoja
kaandika kwamba, “we need mental decolonization”
kwamba tunahitaji kuondokana na utumwa wa fikra-utumwa wa mawazo.
Vyombo vya
habari vya Afrika vingali utumwani,Marekani,Uingereza,
Ufaransa,Ujerumani,Italia n.k
Kila
kinachosemwa na vyombo hivi hushikiliwa na kushabikiwa pasipo kufikiri. Kila
upuuzi na ujinga hushangiliwa sana. Mke wa Prince William akiingia
hedhi,itatangazwa sana, akipata mtoto ndiyo
‘Burning Issue’ siku hiyo watu wanapiga simu na kutuma SMS siku nzima! Hamnazo?!!
Kuku wa
Mzungu akitaga mayai,watapiga kelele, timu ya Mzungu ikiishinda ya Afrika,watashangilia
usiku mzima! Punguani??!!
Naam, huu
ndiyo UTUMWA WA AKILI. Ili mradi, televisheni na magazeti ya Afrika na
vijiredio vya siku hizi, vimepoteza akili na kutumbukia katika mijadala kuhusu
wavuta bangi na wakola wa Ulaya na Marekani(nakisi ya ubongo) hushabikia ‘biased
stories’ za Mzungu dhidi ya Afrika.
Kila mawazo
ya upumbavu wa Mzungu kwamba Afrika ni nchi iliyopata uhuru mwaka 1994,rais
wake ni Mandela na mji mkuu ni Nigeria,hushabikiwa hapa,SMS zitatumwa kila
mjinga apate cha kujadili siku hiyo!
Nyimbo
zinazopigwa katika vijistesheni vya redio ni upuuzi mtupu,mradi kapiga jambazi
mmoja mbwia unga wa Marekani ama Ulaya.Nyimbo za Msondo Ngoma siku hizi
huonekana za kishamba sana!
Rais wa
zamani wa Marekani,Thomas Jefferson, aliwahi kusema kwamba,
“All men are created equal..But it would be
impossible for black people to understand…”
Kwamba,watu
wote wameumbwa wakiwa sawa,lakini ni muhali Mtu Mweusi kuwa na maarifa. Labda
niseme utabiri wa Jeffersonb ulishatimia,ndiyo maana tumekosa ufahamu?
Sisi
hatujitambui kwamba Mungu alituumba huru na tuko sawa na Mzungu au Mchina?
Lakini watu wako radhi kuitwa ‘dog’ la Mzungu ama Mchina,na nywele
tumebadili,rangi ya Afrika tumeitupa,hakuna Mwafrika siku hizi, nywele za
Mzungu,makalio ya Kichina!
Sikiliza
vinyimbo vya vijiredio vyetu..upuuzi. Ndiyo vile Mungu alimwambia Nabii Amosi, “Keep away the noise of your songs”
peleka mbali nyimbo za kipuuzi(Amosi 5:23).
Akili za
Mtanzania zimelala,zimelevywa na mvinyo wa Magharibi hadi uzalendo kwa nyi yetu
umekwisha.Mafisadi huiba ili kuficha mali Ulaya,wanatamani wakaishi Ulaya.Wanaota
Ulaya.
Ukiona
habari. “The Most Influential People in The World” hakuna Mweusi hata
mmoja,utaona wavuta bangi,wabwia unga wa Ulaya humo,hakuna kitu Afrika,na
hakuna watu wenye mvuto!
Nijadili
kidogo kuhusu uandishi wa habari Tanzania.Mwandishi sharti kuwa na “A Professional
Attitude”Mtazamo wa kitaaluma kuhusu unachotaka kufikisha kwa
wasomaji,watazamaji ama wasikilizaji.
Kwa kuwa
hatuna chetu ila kushabikia upuuzi wa Marekani na Ulaya,basi watu wetu
wanageuzwa kuwa Mzungu anavyotaka!
Kauli ya
weledi na taaluma katika habari zinazotangazwa na vyombo vyetu vya habari
hakuna.Kwanza waandishi humaliza miezi 10 bila kulipwa-wamedhulumiwa nao
hufikiri kuitoroka nchi ama kuisaliti kama wanavyosalitiwa!
BBC,VoA,DW,CNN
n.k wanachotangaza siku hizi ndicho kinachoingia akilini mwa watu na
kushabikiwa katika mijadala ya vijiredio vingi,Watanzania wameporwa
sauti,Mzungu amepewa sauti Afrika.Wakisema, Afrika hakuna fikra ni njaa na
ukimwi na vita kutoka Cairo hadi Cape Town,tunakubali.Wakisema Dar hadi
Accra hakuna maarifa,tunasema ndiyoo!
Hamnazo??
Kuna
dhuluma,ufisadi na ushoga wa kifikra, sauti kapewa Mzungu hapa kwetu.Juzi
tumeona Venezuela wabunge wakikunjana ngumi bungeni, tusubiri hapa akina Tundu
Lissu wetu na akina Stephen Wassira na Lukuvi!
Watanzania
tumegeuka watoto.Tunalalamika kama watoto.Tuna akili za kitoto,tunaidai
serikali itufanyie kila kitu kama watoto: Itununulie maziwa, itupe nguo na
chakula…hatudai kusimama na kufanya mambo mengi kama watu wazima.
Mwisho wa
siku,Bunge hili, serikali na wanasiasa hawa wanatuona sisi kama watoto
wadogo;wanatudanganya, “Takununulia pipi,peremende,chips’wakati wa chaguzi
kumbe tunadanganywa huku tukisema,’sidanganyiki!’Chizi??!
Niimbe wimbo
wangu uliotungwa na rafiki,
“Each time we blame the government
for failing to keep us safe, and the government goes back to treat us like
children!”
Leo,tunasukuma
gari la mwanasiasa huyu, kesho serikali inakuja kumwaga peremende na
chips,tunahamia huko na kuimba nyimbo za shangwe; hatuna akili,tunahadaika na
wanasiasa wanajua sisi ni watoto wadogo,ndiyo maana serikali imechelea
kutwambia kwamba ni ujinga kila kitu kuandamana na kuchoma matairi barabarani!
Watu wa aina
hii hakuna kuwakataza,ni kuja na staili ya kuwadanganya maana ni watoto,kila
mwenye hadaa huwateka akili.Siku hizi wanawafuata wenye ahadi, “Takununulia
kaptula enhee!” Wanasema Hureee! Chizi?
Tujikinge na
propaganda,tuamke,tusidanganyike kwa upuuzi wa kutumiwa ili nchi yetu iwake
moto wa matairi na maguruneti bure.
Tunahitaji
Mtazamo Mpya, “New Attitude’ ili kujilinda na chachu ya Mafarisayo wa siku
hizi.Busara Tanzania imekwisha, akili zimelala,uzalendo uko ICU’’Tumekwisha,tunahitaji
dose dhidi ya ukoloni
wa akili- mental decolonization.
Bila
hivi,Waliowaua J.F Kennedy na Abraham Lincoln wanaivuruga nchi yetu, kwa
kutumia makanisa,misikiti,majukwaa ya siasa n.k
TAMATI
0786 324 074
No comments:
Post a Comment