NILIPOWAONA, naam katika televisheni, Mke wa Rais Mama Salma
Kikwete na Mke wa Rais wa Marekani, Laura Welch Bush, Jumanne Septemba 25 jijini New York, nikajisaili kimoyomoyo: Hawa,
wana nini cha kufanana?
Salma Kikwete
alikuwa na mumewe jijiiini New York, Rais Jakaya Kikwete aliyekuwa akihudhuria
Mkutano wa Umoja wa Mataifa, .
Laura Bush ni
mpole; si mwenye harara. Ni mtulivu; mvumilivu dhidi ya mabaya. Ni mwenye
upendo kwa watu wenye dhiki, hususan wagonjwa.
Alipofika Tanzania
mwaka 2005, aliwatembelea wagonjwa wa Ukimwi; akawaona yatima na kuahidi kupoza
madhila yaliyowakabili.
Jumapili, Novemba
4 mwaka huu, Laura Welch Bush atakuwa anatimiza miaka 58. tangu azaliwe huko
Midland, Texas. Alizaliwa katika familia ya kidini. Amesoma shahada ya kwanza
Chuo Kikuu cha Southern Methodist, Dallas.
Alisoma ya
pili(Masters) ya Sayansi na Ukutubi katika Chuo Kikuu cha Texas. Alikuwa mwalimu na mkutubi Texas, kabla ya kuolewa
na George Walker Bush, Novemba 5, mwaka 1977.
Kwa hakika, picha
niliyoiona ya Mama Salma Kikwete na Laura Bush, katika Maktaba ya Pierpont
Morgan, jijini New York, ilinikumbusha kwamba
Laura ni Mkutubi na pia mwalimu kama Mama
Salma. Nikajiuliza: Hawa, wanashahiana nini?
Sijui walizungumza
nini wanawake hawa wawili, walipokutana hapo Maktaba jijini New York?
Nadhani, bila
shaka Mama Salma hakusahau kumwalika Laura nyumbani Tanzania, ili aje tena kutembelea
Serengeti, Mlima Kilimanjaro, Oldonyo Lengai Pengine kukagua miradi ya harakati za
kupambana na Ukimwi na kupunguza umasikini.
Laura Welch
Bush(58) amefika Afrika Mashariki mara mbili. Julai 2003 alikuwa Nairobi. Na aliwasili
katika Uwanja wa Ndege wa Dar es
salaam, DIA(sasa wa Mwalimu Nyerere) Jumatano Julai
13, mwaka 2005.
Alikuwa katika
ziara ya siku mbili chini.
Alipokelewa na Mke
wa Rais, Mama Anna Mkapa(wakati huo) na Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na
Watoto, Dk. Asha-Rose Migiro, ambaye sasa ni Msaidizi wa Katibu Mkuu wa Umoja
wa Mataifa.
Laura Bush
alipowasili Da es salaam mwaka huo, alilindwa sana na makachero wa Marekani. Alikuja na
mmoja wa mabinti zake mapacha, Jenna. Walikuwa wakitokea Gaborone, Botswana.
Aliandamana na ujumbe wa watu zaidi ya 30, wakiwemo waandishi wa habari 12 na
maofisa wengine.
Kufuatia
‘protokali’ ya mikogo ya Kimarekani, hakupanda gari aliloandaliwa na mwenyeji
wake, Mama Anna Mkapa. Alikwea moja la gharama sana-naambiwa MAREHEMU Michael Jackson alikuwa akitumia
magari kama haya ya bei mbaya kuendea na kutoka mahakamani, wakati wa kesi yake
ya kulawiti. Wamarekani wana ‘nyodo’…
Naam, Mama Laura
alikwea Limousine, lenye milango sita.
Alilindwa na mbwa maalum wa kubaini mabomu ama milipuko. Si unajua tena kitisho
cha al-Qaeda? Mama Anna Mkapa alijitutumua na Mercedes Benz.
Mbwa wa Marekani
walinusa kila kitu uwanja wa ndege, saa mbili kabla ya Laura kutua. Hata
mawasiliano yote ya simu yalikatika mama huyu alipokuwa akitua kwa mbwembwe za
kitajiri.
Nikakumbuka ulinzi wa Wamarekani hawa kwa
Waziri wao wa Mambo ya Nje, Madeleine K. Albright, alipofika Dar sa salaam
kuhudhuria maziko ya Hayati Mwalimu mwaka 1999. Leo ni miaka minane tangu
Mwalimu aage Dunia St. Thomas jijini London.
Nikakumbuka pia
‘nyodo’ za Makachero- Wamarekani- alipokuja Rais William(Bill) Jefferson
Clinton mjini Arusha, Jumatatu Agosti 27 mwaka 2000.
Clinton
alitua uwanja wa ndege wa Kilimanjaro(KIA) ili kushiriki utiaji saini
makubaliano ya kurejesha amani ya Burundi. Alialikwa na Msuluhishi wa
mgogoro huo, Rais Mstaafu wa Afrika Kusini, Nelson Rolihlahla Mandela, ambaye
wapenzi wake humwita, Madiba.
Protokali ya
ulinzi na mbwembe za Wamarekani zilifanya mawasiliano ya Dar es salaam na
Arusha kukatika; mbwa wakanusa magari hata ya viongozi wa juu wa serikali,
wakati askari wetu wa Usalama Barabarani, makachero na waandishi wa habari
walitimuliwa wasikaribie kwa wakubwa hao!
Ombaomba na wakoma
waliondolewa mitaani, kisha magari ya Zimamoto tuliyozoea kuyaona yakizima moto,
yakapiga ‘deki’ barabara! Kwa hakika, napendekeza Mama Salma Kikwete ayaige
yote mazuri kutoka kwa Laura Bush, lakini kamwe asiendekeze ‘nyodo’ za namna
hii. Aendelee kuwa mtu wa watu na mlezi wa Taifa letu.
Wake wengine wa
Marais wa Marekani ni pamoja na Jacqueline Lee Bouvier(mke wa Rais Kennedy),
Claudia ‘Lady Bird’ Alta Taylor Johnson, Thelmacathy Patricia Ryan Nixon, na
Elizabeth Bloomer Warren Ford, mke wa Gerald Ford.
Wengine ni Anne
Frances ‘Nancy’
Robbin Davis Reagan, Barbara Pierce Bush(mama mzazi wa George W. Bush, Hillary
Rodham Clinton na Laura ‘rafikiye’ Mama Salma.
Laura ana mabinti
wawili; Barbara(alipewa jina la mama yake Bush) na Jenna, jina la mamaye Laura.
Ni mapacha waliozaliwa mwaka 1981. Mama huyu hujishaghulisha na masuala ya Afya
ya akina mama, hususan vita dhidi ya saratani ya matiti.
Ni changamoto kwa
Mama Salma kuepuka biashara zote awapo Ikulu, ili akazanie elimu na Afya(mama
Salma pia ni Mwalimu kama Laura Bush), lengo likiwa kupunguza umasikini wa watu,
magonjwa kama Ukimwi na umasikini, bila kusahau maendeleo ya akina mama.
Wapo wake wengi wa
Marais walioacha ulezi kwa taifa wakaanza kufanya hata biashara za magendo
wakiwa Ikulu(si Tanzania),
wapo waliowahi kuwapiga ngumi hata mawaziri na waandishi wa habari.
Wapo wanaoishi
maisha ya anasa sana
kwa pesa za walipakodi, bila kulifanyia taifa kitu chochote, ia\sipokuwa nyodo
na anasa!
Pia, wapo wanaotibiwa mafua Paris,
Washington na Geneva, wakati akina mama wetu hapa wakilazwa
wanne kitanda kimoja, hususan wakati wa kujifungua… Mama Salma Kikwete asije
kuwa miongoni mwa hawa.
Mke wa Rais wa
Maisha, Dikteta Jean-Bedel Bokassa, alilazimisha wanafunzi wote wa shule
kununua sare katika moja ya duka lake! Walipogoma na kufanya maandamano, waliuawa
si chini ya 100!
Mama Salma asiache kuwa kama mkewe Pilato Mrumi,
alivyomtetea Yesu wa Nazareth kuwambwa msalabani..
Tanzania ipo mifuko kama
Fursa sawa kwa Wote(EOTF) ambayo haijulikani ipo kwa manufaa ya nani? Mama
Salma Kikwete hastahili kufanya biashara hizo, isipokuwa awe na Taasisi ya Malezi
ya Taifa(TMT).
Salma Kikwete(kama mwalimu na mlezi wa Taifa) angeanzisha Taasisi ya
Malezi ya Taifa itakayonusuru vijana katika maangamizi ya Ukimwi, umaskini,
biashara ya ukahaba, madawa ya kulevya, ujinga na mmomonyoko wa maadili na Afya
ya mwili na kili.
Katika Dunia ya
Utandawazi, Mama Salma Kikwete akimshirikisha Laura Bush, watawaokoa vijana
dhidi ya majanga haya ya madawa ya kulevya, Ukimwi na biashara ya ngono
inayofanywa sasa ili kujitafutia kipato.
Nahisi, Mkataba wa
Ushuru wa pamoja wa Afrika Mashariki(East African Customs Union Treaty)
ulishaleta soko la pamoja hata la makahaba katika Afrika Mashariki. Makahaba,
wakiwemo watoto wadogo kutoka hata Rwanda,
Burundi, Somali na Afrika
Kusini, wananyatia soko hilo
ili kuendesha biashara ya ngono(sex trade) na kumomonyoa maadili licha ya janga
la Ukimwi.
Mwishoni mwa
Desemba mwaka 2003, polisi wa Kenya
waliwatia mbaroni wasichana wasomi wa vyuo vikuu, wakiuza mapenzi katika mitaa
ya Nairobi,
hususan Koinange, wao huita, ‘K-Street’! Hapa Tanzania
mitaa kama hiyo huitwa Uwanja wa Fisi!
Si muda mrefu
kuanzia sasa, wasomi wa vyuo vikuu watanyatia soko hilo la biashara ya ngono; wataacha
kulihudumia Taifa ili kujipatia kipato kutokana na ngono
Hivyo, kunahitajika
Taasisi yenye nguvu ya kutoa nasaha kuzuia hali hii.
Kadiri siku
zinavyokwenda, ukahaba unatazamwa kama biashara ya kawaida, inayowavutia wasomi
na watu wengine, hadi wamebadili majina kutoka ‘changudoa’, ‘wauza kuku’ au
makahaba na kuwa Wafanya Biashara wa Ngono, Commercial Sex Workers(CSW)!
Ni kwa sababu hiyo,
Itifaki ya Ushuru wa pamoja(EACU) itawaleta pia wauza madawa ya kulevya, ‘dada
poa’ na ‘kaka poa’ wengi kutoka nchi zote za Afrika Mashariki, pengine kutoka Afrika Kusini na Ulaya.
Watasababisha
mmonyoko mkubwa kabisa wa maadili na
gharika kwa vijana, ambao wataingilia biashara hiyo kama
wafanyabiashara wa ngono, Commercial Sex Sellers!
Ni kwa sababu hiyo,
Taasisi ya Malezi anayoweza kuanzisha Mama Salma kwa kushirikiana na Lura Bush,
na Michelle Obama, itapambana na biashara hiyo kwa kutoa mafunzo na
ushauri-nasaha, ili kuwaokoa wasichana
wetu wakiwemo wanafunzi kuwa, Sex Seller Girls(SSG)!
Taasisi kama hii
inaweza kuendeshwa kwa msaada mkubwa wa watu kama Mama Laura Bush; yumkini
ikafanikiwa kuwarejesha wasichana na wavulana masomoni, baada ya kukatisha
masomo kwa mimba, au kuolewa, na wavulana
bangi na madawa ya kulevya.
Taasisi ikianzishwa na Laura Bush na Mama Salma,
inaweza kufadhiliwa na watu maarufu sana hapa Duniani, kama Bill Clinton,
Nelson Mandela, Tony Blair, n.k. Mama
Salma atakuwa mke wa kwanza wa Rais atakayejitofautisha na wenzake kwa kuokoa
kizazi katika maangamizi ya Ukimwi, madawa ya kulevya na ukahaba katika zama
hizi za utandawazi.
inaweza kuwa Taasisi itakayolea na kufufua
vipaji vya vijana. Badala ya biashara ya ukahaba kubadili maendeleo ya watoto
kielimu, watazaliwa hapa akina Venus na Serena Williams, akina Didier Drogba,
watakaoiletea Tanzania
medali za heshima, badala ya hawa kugeukia biashara ya ngono kwa wageni na
wawekezaji wa migodi na kubwia unga.
Zamani, ilidhaniwa
jamii na madhehebu ya dini yangeweza kuifanya kazi hii. Sasa, imegundulika,
vijana na watoto hawako salama katika madhehebu ya dini, kwa kuwa hata wachungaji, masheikh na mapadri wameripotiwa kumomonyoa maadili
kwa kiwango cha kutisha. Tunahitaji Taasisi ya Malezi.
Hivyo, Mama Salma
na Laura Bush ama Michelle wakianzisha
Taasisi ya Malezi Tanzania, wataliokoa Taifa katika maangamizi. Bila shaka Mama
Salma ataibuka Shujaa wa Taifa atakayetoka pasipojulikana(from Zero to Hero) na
kutoa mwanga namna Taifa linavyoweza kuokoa maisha ya watoto na vijana wake kwa
kuwaandaa kuwa wazalendo na raia waaminifu.
Taasisi hiyo pia
itakemea unyanyasaji na udhalilishaji kama wa akina Mfalme Mswati III wa Swaziland,
wanaooa vigoli kila mwaka, bila kujali Ukimwi na Haki za Msingi za Wanawake.
Kwa kuwa kuna
habari kuwa Michelle na mumewe walikwisha alikwa hapa nchini, t tunawakaribisha
kwa moyo mkunjufu,ikiwezekana wafike kabla ya kumaliza Mhula wao mwakani.
Naungana na Mama
Salma na Watanzania wengine kumkaribisha Laura na George W. Bush, Obama na
Michelle kwa wimbo, ‘Welcome to Tanzania’
ulioimbwa na Hayati Pepe Kalle na wenzake, Djuna Bileku Mpasi, Papy Tex, Ikomo
Djodjo, Lofombo na wengine wote wa Empire Bakuba… Welcome to Tanzania!!
Itaendelea
0754 324 074
0713 324 074
www.congesmramba.blogspot.com
No comments:
Post a Comment