Naam, niliona katika katuni ile Obama na Michelle wakiteremka katika dege lile la Air Force One,huku kukiwa na maandishi, "Obama to visit Africa" huku wakipokelewa na wawekezaji wa kichina!
Utadhani Afrika, isipokuwa mali ya Mzungu,basi itaangukia katika ushawishi wa wageni hususan Wachina!
Wachina, wanafanya biashara Afrika,na wametujengea ofisi za Makao Makuu ya Umoja wa Afrika,AU, kule Addis Ababa.
Ni hapa naanza kutafakari ujio wa wakubwa hawa wa dunia hapa Afrika,hususan Tanzania yetu kama ifuatavyo:
UJIO wa Rais George Walker Bush Afrika, hapa Tanzania mwaka 2008 ulifanya mfumo wa kawaida wa maisha ya watu kusimama.
Ni
kawaida kusimama. Kila kinakokwenda kivuli cha Bush,
Clinton,Obama,Malkia Elizabeth na watoto ama wake zao, mfumo wa maisha
ya kila siku husimama hasa wanapokaa takriban wiki nzima.
Ni
jua tu ndilo halisimami; yaani ni dunia tu ndiyo huendelea kulizunguka
jua na kutufanya tuone kwamba dunia ingali inazunguka.Wakati mwingine
tunapumua kwa shida. Bush, ni kama Mungu ama malaika, sijui.
Bush, alikuja Tanzania miezi kama
kumi tu kabla ya Uchaguzi Mkuu wa nchi hiyo mwaka 2008. Naam, miezi 11kabla ya kuiacha White House kwa Rais mpya atakapoapishwa Januari 20 mwaka 2009.
Rais
wa Marekani alikuja mara ya pili hapa, baada ya miaka minane. Rais
Bill Clinton alikuja Arusha, Jumatatu Agosti 27 mwaka 2000. Alialikwa
na Msuluhishi wa Mgogoro wa Burundi wakati wa utiaji saini mkataba wa
amani, Nelson Mandela.
Kilichotokea
wakati Clinton anashuka uwanja wa Kimataifa wa Ndege wa Kilimanjaro,
ni kivuli cha mtu mkubwa kukanyaga ardhi ya watu wanyonge.
Wamekuja
hapa akina Madeleine K. Albright mwaka 1999 mfumo wetu wa maisha
ukasimama ili kupisha wa Kimarekani kutandaa nchi masikini.Bendera ya
nyota 50 ikapepea
anga lote la Mtu Mweusi.
Jumatano,
Julai 13, 2005 mke wa Bush, Laura Welch Bush alitua Dar es salaam kwa
ziara ya siku mbili.Julai 2003 Laura alikuwa Nairobi.
Mama huyu amekuja Dar es salaam tena na mumewe, kwake ikiwa ziara ya tatu Afrika Mashariki, na mara kama tano hapa Afrika.
Mama huyu amekuja Dar es salaam tena na mumewe, kwake ikiwa ziara ya tatu Afrika Mashariki, na mara kama tano hapa Afrika.
Luteni
Usu, na Rubani wa dege la Jeshi(US Army) anapokuja Tanzania, wengine
tunadhani kaja kutafuta namna ya kusimika jeshi la nchi hiyo ili
kudhibiti ugaidi na magaidi.Na akina Obama wanakuja hapa kujipendekeza
kwetu ili tuwaone rafiki,kumbe ni kuona Wachina wanapata ushawishi
mkubwa Afrika,na wanapewa kandarasi,huenda wakatufundisha kichina.
Wapo wanaodhani kivuli cha ‘kichaka’-Bush ni kutafuta kushawishi serikali za Afrika
Mashariki kuwanyanyasa Waislamu…lakini magaidi hawatambuliki kwa dini moja,
Marekani wapo Wazungu na Wachina Magaidi. Hata Ulaya, wapo magaidi kama Red Brigade, waliomuua Aldo Moro Waziri Mkuu wa Italia, Mafia, na wengine wengi.
Marekani wapo Wazungu na Wachina Magaidi. Hata Ulaya, wapo magaidi kama Red Brigade, waliomuua Aldo Moro Waziri Mkuu wa Italia, Mafia, na wengine wengi.
Hata
kabla ya Osama kulikuwa na magaidi kama Black September waliowaua na
kuwateka nyara wanariadha wa Israeli katika mashindano ya riadha ya
Olimpiki mjini Munich, mwaka 1972.
Magaidi hawana rangi moja, dini moja ama ukoo.
Magaidi hawana rangi moja, dini moja ama ukoo.
Bush,
kaja Tanzania, Benin, Rwanda, Ghana na Liberia; na mraba huu haudhani
kaja kuumiza watu wa dini Fulani ambao walitaka kuandamana kupinga
asije!
Naam, sisimizi kupinga tembo asije, kwake kibarua!
Yawezekana, Bush na Obama wakaja kuhakikisha maslahi ya Marekani yanalindwa Afrika hii hata kabla Obama hajaondoka mamlakani.
Maslahi ya Marekani ni pamoja na makampuni ya uchimbaji madini ya (Kimarekani) hapa, na yale ya uchimbaji mafuta kwingineko Afrika.
Maslahi ya Marekani ni pamoja na makampuni ya uchimbaji madini ya (Kimarekani) hapa, na yale ya uchimbaji mafuta kwingineko Afrika.
Ukiacha
siasa, Bush ni mfanyabiashara wa mafuta na madini. Kampuni yake ya
kwanza iliyoanzishwa Midland iliitwa, Arbusto Energy. Arbusto ni neno
la Kihispania lenye kumaanisha ‘kichaka’yaani Bush.
Baadaye,
Arbusto ikabadilishwa na kuitwa, Bush Exploration. Ilifilisika mwaka
1980, wakaanzisha nyingine, Spectrum 7; baadaye Harken Energy
Corporation. Bush ni mwekezaji pia katika michezo.
Yeye na matajiri wenzake walinunua timu ya Baseball, ‘Texas Rangers’ kwa dola milioni 75.
Hii
ni kusema, katika ziara yake hapa, akikumbuka kumuuliza Rais Kikwete
juu ya michezo waipendayo Watanzania, Kikwete atasema Mpira wa miguu.
Anaweza kumshawishi yeye Bush na Wamarekani wenzake kununua hisa katika
vilabu vyetu maarufu hapa, kama Yanga!
Kwa
kuwa Bush ni mfanyabiasha wa madini, yawezekana sasa baada ya kuondoka
Ikulu, akataka kuwekeza zaidi katika dhahabu, almasi, makaa ya mawe, mafuta, gesi tanzanite, shaba n.k
Atataka pengine kuwekeza katika utalii ama sekta ya wanyamapori. Shahada yake ya Uzamili katika Biashara
anaweza kuitumia kuchota rasilimali zetu hapa.
Wengine wanasema Bush ni mabepari walewale wanaitangazia Dunia utawala
bora, demokrasia na haki, wakati makampuni yao yanaongoza duniani kwa
unyonyaji.
Makampuni
ya mafuta kama Chevron, au Chevron Texaco, Conoco Phillips na Exxon
Mobil, ni makubwa sana duniani yanayokomba mafuta ya dunia na
kutengeneza faida ya zaidi ya dola bilioni 80 kila mwaka.Haya yako
Nigeria na popote.
Hivyo, Marekani hufika sehemu zote kuliko mafuta
ili kushinikiza mambo. Ikitokea nchi ikakatalia mafuta au madini yake,
mambo kadhaa, kama ugomvi na vita( kama Iran na Irak) huanza kutokea.
Na watawala wa nchi
hizo wanaokubali kuipa
Marekani rasilimali au mafuta, huwa ‘watoto wazuri’ na rafiki kama
Marehemu Mohamed Reza, ama Shah(wa Iran) ama Mobutu hadi
wanapotimuliwa, au wanapofariki. Usiombe kuchukiwa na akina Bush na
Obama.
Makampuni
hayo ya mafuta ndiyo yanayolalamikiwa sana hata huko Niger Delta, kwa
mikataba ya ovyo ya rushwa kwa viongozi wa Nigeria, kama akina Marehemu
Dikteta Sani Abacha.
Ni
kwa sababu hii Bwana ‘Arbusto’(Bush) ama mrithi wake Obama
wanastahili kuchungwa sana watakapotaka kuwekeza katika rasilimali
zetu.
Aulizwe Obama, kama atakubali kulipa tozo kamili na mrahaba sahihi au wa kinyonyaji kama Niger Delta?Atashinikiza mikataba iwe siri? Utawala bora upi hapo?
Aulizwe Obama, kama atakubali kulipa tozo kamili na mrahaba sahihi au wa kinyonyaji kama Niger Delta?Atashinikiza mikataba iwe siri? Utawala bora upi hapo?
Bush
ni ‘pacha’ wa baba yake, George Herbert Walker Bush(84); ambaye
Desemba 1989 alituma majeshi Panama na kupindua serikali na kumkamata
mateka kiongozi wa nchi hiyo, Jen. Manuel Noriega.
Na Obama ndio wale wale wanaong'ata na kupuliza wakati Gereza la Guantanamo Bay,Cuba linaponyanyasa watu kwa miaka mingi bila kuwafikisha mahakamani,sasa wanasusa kula chakula,dunia kimya!
Na Obama ndio wale wale wanaong'ata na kupuliza wakati Gereza la Guantanamo Bay,Cuba linaponyanyasa watu kwa miaka mingi bila kuwafikisha mahakamani,sasa wanasusa kula chakula,dunia kimya!
Bush Aliingilia
ugomvi wa Irak na Kuwait mwaka 1990, alivuruga uchumi uliokuja
kurekebishwa na Rais Clinton.Alidhoofisha dola la Urusi(USSR) na
kumfanya Mikhail Gorbachev kujisalimisha mikononi mwake mwaka 1989.
Arbusto(Bush
mtoto) aliyewahi kutiwa mbaroni na polisi mwaka 1976 kwa kuendesha
gari akiwa ametutika mtindi, anafanana sana na babaye.
Kasoma
chuo kikuu kilekile
alichosoma babaye, cha Yale; kaendesha madege ya jeshi kama
babaye,anafanya biashara ya mafuta, amewapindua Saddam Hussein na Mullah
Mohamad Omar. Mmoja amenyongwa, mwingine ni mkimbizi asiyefahamika
alikokimbilia.
Kama
muda wake wa kuwepo Ikulu ungeruhusu, haikosi angemaliza kazi kwa
kuwapindua Marehemu Hugo Chavez wa Venezuela na Ahmadinejad wa Iran.
Hawa, wanakiburi cha mafuta, na marekani huhitaji kama asilimia 30 ya mafuta yote duniani.
Hawa, wanakiburi cha mafuta, na marekani huhitaji kama asilimia 30 ya mafuta yote duniani.
Naam, kwa kuwa Arbusto ‘kichaka’ Bush bado anakumbukumbu ya kuvurumisha dege la Jeshi, F-102 Fighter,
kule Texas Air Nation Guard, kwa vyovyote atataka Tanzania kuwa
mshirika wake wa kijeshi kwa kile kiitwacho, African Command; ama
maslahi ya kijeshi na kiuchumi ya Marekani hapa Barani.
Kwa
kuwa Rais
Kikwete ni mwanajeshi; tena wa enzi zile za vita baridi, tunaimani
atakuwa ‘chonjo’ na jamaa huyu, kama ataleta njama zozote za kutaka
kuchukua mwambao wetu kiulinzi, ama maliasili zetu kiuchumi.
Jambo moja tunaomba Rais Kikwete alikatae: Udhalilishaji na nyodo za Wamarekani kwa mataifa anayotembelea rais wao.
Vyombo
vya ulinzi vya nchi anakotua hugeuka ‘mdoli’ ama sanamu.Ombaomba
huwekwa kizuizini ili wasionekane mabarabarani wakitangatanga, barabara
hupigwa deki usiku kwa magari ya zimamoto, na viongozi wetu wakuu ama
hukatazwa kumkaribia, na pengine magari ya viongozi wetu hunuswa na mijibwa ya Marekani yanayokuja kwa dege maalum kabla ya Air Force One, kutua.
Hawa jamaa
huja na magari yao ‘Bullet Proof’ ili rais wao asishambuliwe kwa
namna yoyote na magaidi na wenye msimamo mkali wanaojitoa mhanga, kama walivyomuua Benazir Bhutto huko Pakistan.
Arbusto
‘kichaka’ na Obama wanapokuwa Dar es salaam pilika pilika huwa nyingi;
ni karibia kama Amri ya hatari huwa imetangazwa.
Usafi
huwa wa hali ya juu, ulinzi wa polisi na usalama barabarani wenye vyeo
vikubwa; hapana tuseme FBI na makachero wengine huwa kila sehemu, kila
mahali kusikiliza na kuchunguza chochote kisemwacho kumhusu jamaa
huyu, Arbusto.
Marekani inajidai sana kusemea demokrasia na haki za binadamu.
Bush aliwahi kudaiwa kumwibia kura Al(bert) Gore mwaka 2000 hadi kesi ilipohamia mahakamani, baadaye AlGore akakubali kushindwa, kwa maslahi ya Marekani.
Bush aliwahi kudaiwa kumwibia kura Al(bert) Gore mwaka 2000 hadi kesi ilipohamia mahakamani, baadaye AlGore akakubali kushindwa, kwa maslahi ya Marekani.
Kuhusu haki za binadamu, Arbusto hana cha kusema kwa sababu
anadaiwa kumiliki jela Abu-Ghraibu, mjini Baghdad na Guntanamo nchini
Cuba. Juzi tumewaona wafungwa wakichechemea na kugomea chakula, lakini
nani aseme?
Huko watuhumiwa wa ugaidi huteswa bila kupelekwa mahakamani….hiki nacho ni kivuli cha kichaka kinachotisha wanyonge.
Huko watuhumiwa wa ugaidi huteswa bila kupelekwa mahakamani….hiki nacho ni kivuli cha kichaka kinachotisha wanyonge.
Digrii
yake ya Uzamili katika Usimamizi wa Biashara aliyopata katika Chuo
Kikuu cha Harvard mwaka 1975, kama ataitumia vema kumshauri Rais wetu
kutowatumia akina ‘Karamagi’ katika mikataba… Buzwagi na Richmond;
tutampongeza sana.
Lengo
ni kutaka wanyonge wa nchi hii kupata mgawo katika ‘kasungura’ kadogo
kanakoishia mikononi mwa wajanja.Kumbuka, mfisadi huficha fedha zetu
katika mabenki hata ya Marekani, baadaye hukimbilia huko, Bush akiwa
kimya.
Bush, ni wa pili kwa watoto wa Marais kutawala Marekani. Mwingine
ni John Quincy Adams, mwaka 1824.Asigeuke somo hapa kwa watoto wa wakubwa kuhamia NEC ya CCM kila unapofika msimu wa uchaguzi ili kusaka madaraka.Watoto wa wachungaji huwarithi baba zao.
Ni
kwa sababu hii, tunamtaka Bush na Obama wakifika Washington, wakemee
mabepari wanatunyonya kwa kutumia makampuni yao ya uwekezaji hapa na
kuwanyima watu ajira. Mengine hewa.
Bila
shaka, atawaona watu maskini na wenye Ukimwi hapa; atawaona ombaomba,
pengine atasikia habari za machangudoa, atatembelea mbuga zetu na
kutamani kujenga hoteli la nyota sita(six star hotel), afikirie kutupa
ajira sisi, na si Wamarekani.
Shime, Bush afikirie
maslahi ya mtu mweusi wakati huu anapojitayarisha kuipisha
White House.
Tanzania
ni taifa dogo la watu milioni 46 kulinganisha na Marekani yenye
milioni 250.Bila shaka Obama atajifunza namna tunavyopambana na akina
‘Karamagi’ huku bila kupigana ngeu, kama ‘nyumba’ ya jirani.Fujo
zimeanza,lakini angalau tuna amani.
Shime, aambiwe kutusaidia kuwatia mbaroni akina Ballali , pindi wanapotimkia huko, baada ya kutu ‘richmond’ huku!
Mwisho,
kwakuwa Marehemu Osama Bin Laden hajawahi kukimbilia huku kwetu, na
kwa kuwa watuhumiwa wa ugaidi wengi si wa dini, rangi ama ukoo Fulani
tu.Obama asitufanye sisi magaidi.
Basi, Wamarekani wanapokuja Dar es salaam(Bandarisalama),
waepuke nyodo zao za ulinzi, utadhani sisi nyau –wakombamboga.
Watuamini kuwa sisi ni rafiki tu…tafadhali Rais mwingine wa Marekani akija hapa kwetu, asiigeuze Tanzania
Jehanum:
Moja,
kwa itifaki na mikogo ya ulinzi, pili kwa kuzuia mfumo wa kawaida wa
maisha. Tatu, kwa kupandisha bei hata za mafuta, kukata na kuingilia
mawasiliano yetu, kusumbua ombaomba wetu, machangu na kunyanyapaa
viongozi, waandishi wetu na makachero.
Mwisho, mikogo na utajiri wa Marais wa Marekani usiowaongoze katika tamaa mbaya vigogo wetu kwa fahari na utajiri wao.
Unajua Rais Bush, mbali na biashara zake za madini na mafuta alikuwa anapokea mshahara wa dola 400,000(zinazotozwa kodi) kwa mwaka. Alilipwa alawansi ya matumizi dola 50,000(hazitozwi kodi) kwa mwaka, kwa kazi za kiofisi.
Unajua Rais Bush, mbali na biashara zake za madini na mafuta alikuwa anapokea mshahara wa dola 400,000(zinazotozwa kodi) kwa mwaka. Alilipwa alawansi ya matumizi dola 50,000(hazitozwi kodi) kwa mwaka, kwa kazi za kiofisi.
Rais Mwai Kibaki wa Kenya alikataa kulipwa mshahara kama huo wa dola za Marekani 500,000 kwa mwaka, wakati raia
wake wakingali masikini.
Bush,
alililipwa pia masurufu ya safari kama dola 100,000(hazikatwi kodi)
kwa mwaka; na pia hupewa dola 19,000 za viburudisho ama burudani.
Anuani yake ya barua pepe ni president@whitehouse.gov mtu yeyote aweza kumwandikia na hata kumkosoa ijapokuwa ni mbabe tu kama madikteta wengine.
Hata hivyo,Rais wa zamani Venezuela, Hugo Chavez alipomtukana wakati wa Mkutano wa Umoja wa Mataifa(UN) mwaka 2007,akapewa saa chache awe ameondoka jijini New York. Nitafuatilia mshahara wa Obama na Michelle.
Siku hizi Venezuela 'Jembe' limelala, anatawala Nicolas Maduro,nchi imeanza kuwaka moto kwa ushawishi wa hawa jamaa.Sasa Obama yuaja hapa Afrika Mashariki, atatufanyia nini kama si kuja kuleta nyodo na shinikizo hapa?
Itaendelea
Siku hizi Venezuela 'Jembe' limelala, anatawala Nicolas Maduro,nchi imeanza kuwaka moto kwa ushawishi wa hawa jamaa.Sasa Obama yuaja hapa Afrika Mashariki, atatufanyia nini kama si kuja kuleta nyodo na shinikizo hapa?
Itaendelea
0754/0785 324 074
No comments:
Post a Comment