Tuesday, December 11, 2012
HATARI ZIWA VICTORIA
KUTOWEKA KWA SANGARA ZIWA VICTORIA
Watu Milioni zaidi ya 30 wa nchi za Maziwa Makuu hatarini kufa njaa
*mamiloni wengine wamepoteza ajira;ndiyo chanzo cha
maandamano na vurugu Kanda ya Ziwa
Na conges mramba,Mwanza
SAMAKI wa Ziwa Victoria wanazidi
kupungua, kufuatia uchafuzi wa mazingira, uvuvi usioendelevu, na uchoyo wa watu
wa Magharibi na mawakala wao Wahindi,
kuhakikisha wanasomba hata
vifaranga,hadi ziwa litakapokauka!
Taasisi ya Globefish iliyo chini ya Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja
wa Mataifa (FAO), imesema athari zilizoletwa na filamu ya Darwin’s Nightmare katika masoko ya
minofu ya sangara Ulaya, zilidunu kwa muda mfupi tu.
Lakini sasa, Tanzania,Kenya na
Uganda wametindikiwa samaki wa kupeleka
katika masoko ya Umoja wa Ulaya,EU.
Kulingana
na ripoti ya mwezi Agosti,mwaka 2006, iliyosainiwa na Helga Josupit;
inayopatikana katika mtandao wa Kompyuta (Internet), soko la minofu ya sangara
liliathiriwa haraka kiasi cha kutosha, mara baada ya filamu ya Darwin’s
Nightmare kuonyeshwa katika televisheni, lakini athari hizo zilikoma baada ya
kitambo kifupi.
Ripoti hiyo ilisema, sababu za kushuka
kwa mauzo ya minofu ya sangara katika masoko ya Umoja wa Ulaya (EU) kuanzia miaka mitano liyopita, ni uzalishaji
kupungua kulinganisha na miaka ya 2000,2003, na 2004.
Katika nchi
zote tatu za Afrika Mashariki, Kenya ,Uganda na Tanzania, sangara walioagizwa
Ulaya walipungua kutoka tani 56,000 (mwaka 2004 )hadi 52,800 (mwaka 2005);
ingawa thamani ya minofu hiyo iliongezeka.
Hadi mwezi huu wa Desemba,mwaka 2012
bei ya samaki katika viwanda imeporomoka kwa kasi,hata kama hakuna sangara tena
ziwa Victoria,kulinganisha na miaka 10 iliyopita.
Ongezeko lilikuwa
kutoka euro milioni 192 hadi milioni 210 kufuatia matatizo katika usambazaji,
yaliyosababisha ongezeko la euro 3.43 kwa kilo mwaka juzi, hadi yuro 4.00 kwa
kilo mwaka 2005.
Hata hivyo, bei hiyo haikufikia
,rekodi ya yuro 5.00 kwa kilo; iliyofikiwa mwaka 2002, muda mfupi baada ya
Umoja wa Ulaya kuanza tena kuagiza samaki, baada ya kufungiwa.
Umoja wa Ulaya ulisusa kuagiza
sangara kyoka Afrika Mashariki,kufuatia tetesi za uvuvi wa sumu.
Kulingana
na FAO, kupungua kwa sangara waliopandikizwa ziwa Victoria miaka ya 60, sasa kumeletwa na kupungua kwa kina cha maji
ya ziwa Victoria; na kwamba hali hiyo huenda ikawasababishia maelfu ya
wafanyabiashara ya samaki na wavuvi kukosa kazi.
Sangara wanapopungua Ziwa Victoria,
makambi ya uvuvi hufungwa na kuwakosesha watu ajira na kipato, hali
inayowafanya kuingia katika uhalifu na vurugu,hususan katika mikoa ya Mwanza.
Jiji la Mwanza,halijasahau fujo
za mwaka 2011,zilizosababisha
wahuni kuvamia maduka ya Wahindi,huku wakiwataka waondoke!
Mali nyingi ziliporwa na vijana
waliojidai Wamachinga.
sangara
Hivi sasa wavuvi hulazimika kuvua
mbali, lakini mahitaji bado ni makubwa kulinganisha na kiasi kinachopatikana;
hali inayowafanya wavuvi kugharimia fedha nyingi ili kumudu gharama za
uendeshaji.
Mwaka
2006,wakati huo Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara, Jaka Mwambi,alipokuwa akitoa
tamko la chama kuiunga mkono kauli ya serikali kuilaani filamu ya Darwin’s
Nightmare, iliyobatizwa jina “mapanki” akasema ndiyo chanzo cha kupungua kwa ulaji wa
minofu ya sangara katika nchi filamu hiyo ilikoonyeshwa.
Wakati huo,Chama cha Mapinduzi
kilitazama hasara ya viwanda vya samaki na haikutazama athari za baadaye ambazo
sasa zinaonekana kwa fujo na maandamano kila mara ya wamachinga hapa Jijini
Mwanza.
Kauli hiyo
ya CCM juu ya athari za Darwin’s Nightmare ilitafsiriwa kuwa ya kisiasa zaidi,
kwa kuwa imeacha kuainisha matatizo mengine yanayoikumba sekta ya samaki, hadi
kusababisha mauzo kupungua, kufuatia samaki wa aina nyingi kutoweka ziwa
Victoria.
Hata hivyo,
ripoti ya FAO inaonyesha kupingana na kauli hiyo ya CCM, ikionyesha dhahiri
kuwa kushuka kwa mauzo ya samaki Ulaya sasa kunatokana na matatizo ya
kimazingira, na wala siyo filamu ya Darwin’s Nightmare.Samaki wametoweka
takriban aina 300 walioliwa na sangara ambaye pia ametoweka.
“Madhara iliyopata minofu ya sangara mwaka jana(2005) yalitokea haraka katika
nchi filamu hiyo (documentary) ilikoonyeshwa katika televisheni, hali hiyo
ikasababisha upungufu wa kutosha; lakini kwa bahati athari hizo zilidumu
kwa muda mfupi,”Imesema ripoti hiyo, ya
FAO kwenye mtandao huo wa Internet, na kuongeza kwamba juhudi zinafanywa
kuhakikisha hali hiyo inarekebishwa, ikiwemo kutafuta mazingira ya haki ya
biashara hiyo ya minofu ya sangara ,katika masoko ya Ulaya.
Kulingana na ripoti
hiyo, kupungua kwa samaki katika ziwa Victoria hakujaifanya Tanzania isiwe nchi
inayoongoza kwa mauzo ya sangara Ulaya.Kenya pia imeripotiwa mauzo yake
kupungua, wakati Uganda mauzo yao yameongezeka kwa tani 5,000 na kuifanya nchi
hiyo ‘kuikalia kooni’ Tanzania kwa mauzo hayo ya sangara katika masoko ya Umoja
wa Ulaya mwaka huo wa 2005.
Mwaka 2005, Uganda
iliuza tani 23,793 ambazo ni tani 87 tu nyuma ya Tanzania iliyouza minofu yenye
uzito wa tani 23,880.
Kenya mwaka 2005 iliuza tani 5,176.
Hata hivyo, Uganda ilinufaika zaidi
kwa kupata yuro milioni 101,318; wakati Tanzania ikipata yuro milioni 87,723.
Kenya ilipata yuro milioni19,087 mwaka 2005 kutokana na mauzo yake.
Nchi zilizoongoza kwa manunuzi
ya sangara katika masoko ya Ulaya
ni Hispania, ikifuatia Ufaransa, na Italia.Wakati huo ndege 10 za Ukraine
na Urusi zikisomba tani 50 za sangara kila siku kupeleka Ulaya,wakati wananchi
walipokula mapanki.
Uholanzi na Ubelgiji ndiyo kituo cha
kwanza cha kusambazia sangara katika masoko ya Ulaya; wakati Ufaransa na Italia
siku za karibuni zilianza kuagiza sangara moja kwa moja toka Afrika Mashariki.
Mbunge wa
Ukerewe,wakati huo akiwa Rais wa Bunge
la Afrika, na Mwenyekiti wa Chama cha
Wavuvi (TAFU) na Mwenyekiti wa Wabunge wa Mwanza,Gertrude Ibengwe Mongella,
aliwahi kusema kwamba, kama hatua za
dharura hazitachukuliwa, samaki watakwisha katika ziwa hili la pili kwa ukubwa
duniani.
Ni la kwanza Afrika lenye maji
baridi.
sangara
Lina ukubwa wa
eneo; kilometa za mraba 68,800.Kina chake ni wastani wa mita 40 chini, na juu
mita 80; lina ujazo wa maji wa kilomita 2,760. Linachangiwa na nchi tatu za
Tanzania inayomiliki kilomita za mraba 34,488 sawa na asilimia 51; Uganda
kilomita 27,484 sawa na asilimia 43 na Kenya kilomita 6,828 sawa na
asilimia sita.
Mongella
aliwahi kusema katika vikao vya Kamati ya Ushauri ya mkoa wa Mwanza kuwa, kuna
madai ya wavuvi kutoka nchi jirani kuvua upande wa Tanzania, kwa kutumia zana
bora zaidi, zinazowawezesha ‘kuchota’ mali asili hii na kujipatia faida
wakati watu wetu wakiendelea kuwa masikini!
Inakisiwa kuwa
watu zaidi ya milioni 50 wa nchi za
Maziwa Makuu wanategemea ziwa hili kwa chakula chao, uchumi wao na hata maisha
yao yote.Sasa samaki husafirishwa hadi Zambia,Afrika Kusini na Msumbiji,licha
ya minofu ya sangara kusafirishwa Ulaya.
Hivyo kwamba taarifa za kupungua kwa
kina cha maji cha ziwa hili; na kupungua kwa samaki kunakoletwa pia na
uharibifu wa mazingira, ni kitisho kikubwa kwa uhai katika Ukanda wa Maziwa
Makuu.
Mjadala kuhusu filamu ya mapanki, Darwin’s Nightmare, kwamba nchi za
Kaskazini zimeanza kutumia ukoloni Mamboleo kunyonya rasilimali za nchi za
Kusini, hapa katika kuanza kupungua kwa samaki wetu, lazima kutafakari kwa
kina!
Kwamba, kwa
sababu ya umasikini, ujanja-ujanja, uroho, ujinga na kukurupukia soko huria
katika utandawazi, tunauza mamilioni ya tani za samaki (chakula bora na chanzo
cha uhai wetu) ili kupata vijisenti; kisha baadaye watakapokwisha
kabisa,tujitoe kwa hiari kuwa makoloni ya kudumu, na watumwa wa nchi za
Kaskazini ya Dunia, ambao sasa hivi wanalinda sana na kuhifadhi rasilimali zao!
Kwamba, kwa
kuuza sana rasilimali zetu tena bila kusindikwa ili kuongeza thamani; au kwa
kukabidhi kila tulichonacho kikiwa ghafi, kwa hao wageni, tunakubali kunyonywa
sana, na hao hao tuliowahi kuwakataa miaka 40 tu iliyopita, na sasa wananyonya
kwa mrija, bila jasho! Tusijivunie kuuza sana nje, tujiulize: Tunapata nini na
wao wananufaikaje?
Hawalazimiki kutumia mitaji mikubwa kutunyonya! Mashirika makubwa ya
kinyonyaji, kama Benki ya Dunia (WB), Fuko la Fedha la Kimataifa (IMF) na
Shirika la Biashara la Kimataifa (WTO) yamekwisha andaa sera,masharti na
mikataba ya kuchota kwa mara nyingine rasilimali zetu, zaidi ya ilivyokuwa enzi
za ukoloni.
Safari hii, hawa wanawatumia
viongozi wetu kuwapigia debe kusomba kila tulicho nacho…mwisho wa siku
tutasalia jangwa!
Maziwa, mito na mabwawa yatakauka! Misitu
itafyekwa yote, ardhi yote yenye rutuba itauzwa; mbuga za wanyama zitauzwa,
sangara waliokwisha kumeza samaki wengine wote zaidi ya aina 300 nao watakwisha
ziwani…hata mapanki hayatakuwepo!
Kutakuwa kilio na kusaga meno!
Naam, madini yote
yatakuwa yameuzwa yakiwa ghafi; ili faida kwetu iwe kiasi kidogo sana. Lengo
ni kutufanya tusijekuinuka na kuwa ‘super
powers’ tukaanza kushindana nao kama Japan, China, India , Malaysia na
mataifa mengine ambayo miaka 40 tu nyuma yalikuwa makoloni yao! Tutasaliwa na
mashimo na sumu mbaya katika maziwa yetu yatakayokuwa yamekauka kiasi cha
kutisha.
Kwa sababu
ya uharibifu huu wa kutisha, tutaendelea kuathiriwa na sumu zinazosafiri kwa
maji ya mvua toka migodini hadi katika vyanzo vya maji.
Bila shaka wataanza kuzaliwa watoto
wasio na pua au mimba zilizotungiwa nje ya nyumba ya uzazi n.k! Tutamlaumu
nani?
Aliyekuwa Mbunge
wa Ukerewe, Gertrude Mongella, aliwahi kuonya juu ya hatari hii ya wawekezaji,
hususan wa sekta ya samaki, kuachwa kuendelea kusomba samaki ziwani bila
kuhakikiwa…samaki ni kama dhahabu, almasi, tanzanite, wanyamapori,misitu,
rutuba, mito, maziwa, theluji ya milima:
Hufika muda vyote hivi vikatoweka!
Kizazi kijacho tutakiambia nini?
Kwamba tuliwahi kuwa na madini kama
tanzanite yasiyopatikana popote ulimwenguni, samaki wengi kuliko ukimwengu
wote, wanyama pori, vyura wa Kihansi, misitu, milima mirefu na kila kitu
kizuri; lakini vikatoweka baada ya kuuzwa kama wazee wa Mwadui walivyopewa
shanga za kuvaa kiunoni badala ya utajiri wa almasi?
Ni hayo
hayo aliyosema mtunzi wa Darwin’s
Nightmare, Hubert Sauper, kwamba rasilimali zetu zitakwenda Ulaya kwa ujira
kidogo; sisi tutafanywa walinzi, vibarua: Tutalipwa kiduchu…Wahindi, Wazungu,
na wageni wengine watalipwa fedha nyingi. Sisi tutakanywa, “Acheni wivu wa
kijinga!”
Watachota mali yote..watabeba hata
mchanga na kupeleka Japan.
Dada zetu watageuzwa malaya; na hata
watoto wetu wa kiume watageuzwa ‘wake’ ili kujinusuru kwa njaa!
Naam, baadhi ya
madini na rutuba vitahamia hata Mashariki ya Mbali. Kwa kuwa baadhi ya
wanaharakati wataanza kupinga madhara haya ya utandawizi, ndugu zetu
walioajiliwa kazi ya ulinzi wataendelea kuwapiga risasi, ili kutetea maslahi ya
bwana zao. Mwisho wa siku, tutabaki kusutana, pengine hata tutaanza kuumizana
wakati wengine wakipiga hatua mbele ya maendeleo.
Ukitazama kiasi
kinachopatikana sasa kama mrahaba wa rasilimali zetu, hakilingani na kile
wanachobeba hawa wawekezaji-mawakala wa wakoloni mamboleo. Huu ubishi haupo
hapa Tanzania.
Hata jimbo la Ogoni, Nigeria, Waijaw
hawajakoma kudai mapato zaidi ya mafuta yao
yanayochimbwa na kuuzwa Ulaya, wakati wao hawana shule, zahanati, barabara na
hata mafuta yenyewe! Kitu kama hiki kuitwa ni laana ya rasilimali, The Resources Curse!
Hali ya Niger
Delta, haiko tofauti sana na wilaya ya Kishapu; ambako watu hawana maji ya
kunywa au kunywesha mifugo, hawana nyumba za kuishi.
Itaendelea
0754 324 074
AFRIKA KIZIMBANI
TUREJEE katika historia, ili kubaini
namna Mtu Mweusi anavyodhalilishwa na kuonekana hafai, na si binadamu,bali
mnyama!
Wanaoendesha vitendo hivyo,ndiyo hao
hao wanaotazamwa leo kama wafadhili wa Afrika,na wenye huruma kwa wananchi
wetu.
Zama za harakati za kupinga ukoloni,Mzungu aliitwa, Wasumwa Makaka!Kwamba zimwi lililowameza waafrika!
Husababisha vita hapa Barani,kwa
madai ya kuwaondoa madikteta ili kujenga demokrasia na Haki za Binadamu.
Hufadhili harakati tele Barani Afrika,zikiwemo Haki za Binadamu,hata mashoga na
wasagaji…hawa si lolote bali wabaguzi wa rangi!
Nitakwambia wewe uliyezaliwa baada
ya mwaka 1970.
MWAKA 1936 Mmarekani mweusi ,James
Cleveland Owens,(aliyezaliwa Septemba 12,1913 na kufariki dunia Machi 31,1980),aliwashinda
Wazungu wabaguzi wa rangi waliokuwa wakiongozwa na Dikteta wa Ujerumani, Adolf
Hitler.
Ni katika uwanja wa Olympic Stadium
ulioko Berlin; ambako ndiko fainali ya Kombe la Dunia zilipohitimishwa Julai
9,mwaka 2006.
Berlin ni kielelezo cha kutokomeza
ubaguzi.Berlin,kabla ya Ukuta wake kuangushwa mwaka 2004,ulikuwa kielelezo cha
ukoloni wa kutisha,ndipo Bara la Afrika lilipogawanywa mwaka 1884.
James Cleveland, ambaye alikuja
kuitwa na Mwalimu wake “J.C”. kama kifupi cha jina lake; ndiyo asili ya jina la
Jesse Owens, aliyeweka rekodi nne za Dunia kwa dakika 45 tu mbele ya Dikteta wa
Ujerumani, Adolf Hitler, aliyetaka kutumia mashindano ya Olimpiki ya Berlin
mwaka huo wa 1936, kuuonyesha ulimwengu kwamba mtu mweusi ni dhalili; tena siyo
binadamu, bali mnyama!
Jesse Owens , aliweka kwanza rekodi
ya mita100, akashinda mita 200, akashinda tena kuruka juu, kabla ya kuongoza
wenzake wane katika mbio za kupokezana vijiti.
Hitler aligoma kutambua
ushindi wa Owens, kwa madai kuwa hakuwa binadamu, sawa na mzungu! Naam, Mzungu
alikuwa binadamu, Mwafrika mnyama!
Unajua Mohammed Ali,yule bingwa wa
mabingwa wa ndondi duniani alikuwa akiitwa, “Clay” yaani udongo mweusi wa
mfinyanzi?
Unajua,Mohammed Ali, alipokataa kwenda
kupigana vita vya Vietnam alipokonywa taji la Ubingwa wa dunia? Ilikuwa miaka
ya 1967-69 hivi.
Hitler, kama wabaguzi wenzake wa
rangi, aliamini kuwa mtu mweusi alikuwa dhalili mbele ya mweupe; na pia kwamba
si binadamu kamili bali myama tu…hivyo Jesse Owen alimshinda Hitler katika
mashindano hayo mjini Berlin , miaka 70 iliyopita. Hitler aliyekuwa Mgeni wa
heshima wa mashindano ya Olimpiki mwaka 1936, aliondoka uwanjani,hakutaka kuona
‘mnyama’ akishinda mbio dhidi ya binadamu,yaani Mtu Mweupe!
Ni uwanja huo huo ulioboreshwa, ambako
mshindi wa mechi ya 61 alikuja kupambana na mshindi wa mechi ya 62 katika mechi
ya mwisho(ya 64); ya mashindano ya Kombe
la Dunia mwaka 2006 huko Berlin.
Matarajio ya weusi wengi Duniani yakiwa kuona
timu kutoka taifa moja liwe la Ulaya, Amerika ya Kusini, au Asia, kama siyo
kutoka Afrika, lakini lenye weusi wengi; likiibuka mshindi wa kombe hilo la
fahari; ili kukata ngebe za masalia ya wabaguzi wa rangi wa Ujerumani, kama
alivyofanya Jesse Owens,MWAKA 1936.
Kama ushindi wa shujaa huyo
aliyemshinda Hitler na wazungu wake akiwa ‘kifua wazi’ katika uwanja huo wa
Berlin ; matokeo yake yangekuwa ukombozi wa mtu mweusi dhidi ya kudharauliwa,
kubaguliwa na kuonywa taka mbele ya wazungu; shime watu weusi waushinde
ulimwengu wa wabaguzi mafashisti kama Adolf Hitler!
Kutokana na ushindi wa Kaka Jesse
Owens,mwaka 1936, mwaka 1976 alikuja kutuzwa medali ya Rais, ya Uhuru (Presidential Medal of Freedom)na Rais
Gerald Ford wa Marekani; akatuzwa tena medali ya Dhahabu ya Congess (Congressional Gold Medal) na rais
mwingine wa nchi hiyo, George Herbert Walker Bush (Bush Baba), mnamo
Machi 28, mwaka 1990; yaani miaka 10 baada ya kifo chake.
Mwaka 1984 mtaa mmoja wa Berlin
ukapewa jina la Jesse Owens kwa heshima yake.
Owens alikufa akiwa na miaka 66
mjini Tucson , Arizona kwa ugonjwa wa Kansa ya mapafu, kufuatia uvutaji wa sigara
uliokubuhu, wa pakiti moja kwa siku.
Hakika, ushindi wa Kaka Owens wa
majira ya joto ya mwaka 1936, majeshi ya Nazi Yalipokuwa yakijiandaa kwa vita
ya Pili ya Dunia, katika uwanja uleule lipochezwa fainali ya Kombe la Dunia, kati ya Italia na Ufaransa,mwaka 2006, ni
alama ya mapambano dhidi ya ubaguzi na dharau za weupe dhidi ya mtu mweusi
anayeishi katika mabara yote.
.Uwanja huo ulijengwa mwaka 1936 kwa
ajili ya mashindano hayo ya Olimpiki; bado ni kielelezo cha kuzikwa ubaguzi na
udhalilishaji wa weusi kama ule wa enzi ya Hitler.
Shime weusi washinde Kombe la
Dunia huko Brazil mwaka 2014.
Katika fainali hiyo, Ufaransa
ilifungwa na Italia,ikajakusemwa kwamba Ufaransa ilifungwa kwa sababu iliwaweka
Weusi wengi kwenye kikosi-Weusi eti waliitia mkosi Ufaransa!
Timu zote za Afrika zijapofungwa na
kufungishwa virago katika raundi ya awali huko Brazil,bado Afrika itashangilia
timu ya kutoka Bara lolote linalojali utu,na timu itakayojumuisha wachezaji
Weusi.
Moja wapo ya timu hizo ni Ufaransa,
Uswisi na Uingereza, ukiwaacha kaka zetu wa Brazil, Saudi Arabia, Ecuador,
Costa Rica, Trinidad na Tobago n.k.
Shime timu zinazojumuisha weusi
ziibuke washindi nchini Brazil mwaka 2014, baada ya aibu ya Zenedine Zidabe
Zizou,kutukanwa matusi ya kibaguzi huko Berlin mwaka 2006 na ndiko liliko chimbuko la ubaguzi wa rangi wa tangu
enzi za akina Dikteta Hitler, ili ukombozi kamili katika nyanja zote upatikane.
Natambua na nijajivcunia mchango wa weusi katika nyanja
nyingine kama masumbwi na siasa: Wapo akina Mohamed Ali , Leon Spinks, Evander
Holyfield, Mike Iron Tyson, Caster Semenya, na mabingwa wengine weusi waliowahi
kuushinda ulimwengu wa ubaguzi; kama Martin Luther King Jr. Kaka Andrew Jackson
Young nk.
Bila kujali mipaka ya nchi za
ulimwengu,Kombe la Dunia linalochezwa katika viwanja vya Brazil safari hii, lazima mtu mweusi audhihirishie
ulimwengu kwa mara nyingine, kwamba ni binadamu kamili mwenye uwezo na akili
timamu; na kamwe si dhalili au hayawani, kama alivyodhani Hitler.
Mashindano ya Kombe la Dunia ni
zaidi ya kutafuta heshima katika nyanya moja ya michezo, bali hata kisiasa,
kiuchumi,kijamii, kiteknolojia n.k.
Kwangu mimi, naam mtu mweusi mmoja
anapopiga mkwaju unaoingia kimiani, na kumwacha mlinda mlango, Mzungu, akigaa-gaa
sakafuni,ni ushindi pia kisiasa na kiuchumi, maarifa, ufundi, uwezo ,akili
nyingi na kila kitu, kuwazidi wazungu!
Weupe walidhani ni bora kuliko weusi.Akina Hitler wa Ujerumani,
Dk. Balthazar Johannes Voster wa Afrika Kusini, akina Ian Smith wa Rhodesia ya
zamani sasa Zimbabwe na wengineo, walijiona wao watu sisi nyani.
Popote alipo mtu mweusi katika
mataifa yote yanayoshiriki kombe hilo la
Dunia nchini Brazil,mwaka 2014 ; shime ashangiliwe na kutiwa moyo kwa kazi
kubwa ya kuushinda ubaguzi wa rangi..chenga moja ya mweusi dhidi ya mweupe ni
ishara ya maarifa na uwezo.
Kwamba, mtu mweusi ni bora kama
alivyo mweupe;ni makini, ni ghali; na kwamba siku si nyingi weusi watautawala
ulimwengu katika nyanja zoote kama wanavyotawala sasa katika dimba katika timu
nyingi na hususan katika ligi za Ulaya,kama Uingereza.
Kama nilivyokwisha sema, Afrika inayatazama mashindano hayo ya Kombe la Dunia, ama Olimpiki, kama
maandamano makubwa ya Dunia ya kupinga ubaguzi wa rangi(Anti-racist Demonstration).
Hata Afrika ilipoondolewa baada ya
mechi ya Ufaransa na Togo, Ijumaa, Juni 23, mwaka 2006 weusi tulio wengi katika mabara
yote tuliwashangilia weusi wenzetu waliosalia katika kinyang’anyiro cha timu 16
kutafuta nane zilizoingia robo fainali mwaka 2006 huko Berlin.
Ni kwa sababu hii, Fikra Pevu hupata
taabu sana kushabikia timu ya weupe; hata kama inatoka Afrika, inapocheza na
timu ya taifa lenye weusi wengi hata kama ni Ufaransa, Saudi Arabia, Brazil
,Ecuador, Costa Rica, Trinidad na Tobago na nyingine!
Ni kwa sababu hii, Fikra Pevu
zinawaona wachezaji kama Paulo Wanchope wa Costa Rica, Sol Campbell wa
Uingereza, Eric Abidal, Claud Makelele, Zenedine Zidane, Thierry Henry, Gallas,
Louis Saha,na wengineo wa Ufaransa na akina Patrick Mueller wa Uswisi, akina
Ronaldo, Gaucho, Cafu na Wabrazili wot, na wengine woote waliochipukia kama
mabalozi wa mtu mweusi katika mashindano hayo yanayoufundisha ulimwngu kwamba
mtu mweusi siyo mnyama, kama alivyosema Hitler.
Kusema hivi si kuendeleza ubaguzi wa
rangi, ni kuwaenzi wote waliopinga ubaguzi. Kama akina Nelson Mandela, Martin
Luther King Jr,Jesse Owens, Askofu Abel Muzorewa ,Desmond Tutu n.k.
Hata sasa mabalozi wetu
wengine kama Samuel Eto’o Fils wangali wakizomewa na wabaguzi wengine wa
Hispania na kwingineko Ulaya na Asia; na kufananishwa na manyani!.
uwanja wa Olimpiki wa Berlin ungegeuka shimo
la kuuzika ubaguzi wa rangi,lakini Marco Materazzi akaongeza kidonda kwa
kumtukana Zidane,mwenye asili ya Tunisia matusi ya kibaguzi,, hata kuzidi
alivyofanya Kaka Jesse Owens dhidi ya Dikteta Hitler!
Mtu mweusi atatazamwa kama chimbuko
la maarifa, tija, mafanikio katika kila jambo na hata ishara ya kiongozi na
mshindaji wa kila kitu; amini usiamini.
Wapo weusi walioathiriwa na kasumba
ya kikoloni,hata hawajithamini,wanamwona Mzungu kuwa ndiye mtu.Alifika
Afrika,mzungu huhudumiwa haraka kwa kutetemeka,Mweusi anaachwa akafie koridoni.
Natambua watu weusi walivyouzwa
katika mabara mengine kama rasilimali watu.
Kwa hali hiyo, sitaacha
kuwashangilia weusi katika harakati hizi Ujerumani hata kama watapambana na
weupe wa Afrika kusini mwa Jangwa la Sahara , acha Kasikazini!
Afrika ,siyo tena mahali penye vita,
majanga, magonjwa, njaa na machafuko kama Somali, Darfur n.k ni mahali sasa pa
maendeleo makubwa tangu katika soka, uchumi, riadha, ngumi, siasa na kila kitu
kuzidi ulimwengu wa wazungu…kinachotuponza ni kudhani wazungu ni bora kwa kila
kitu!
Nawashangaa waandishi wa habari
wanaowakilisha mashirika ya Magharibi,wanadhani vita,ukimwi na wakimbizi na
njaa ndiyo habari. Kumbe ipo miradi
tele ya maendeleo haitangazwi,na tumebaki ku copy na ku paste habari za akina mke wa Prince William kulazwa
hospitalini kwa kichefuchefu cha himila changa!
Badala ya Muafrika kuandika kwamba
Prince William mkewe ni mvivu tu,sisi huko mama mwenye himila changa, hata awe
na kichefuchefu bado huchapa kazi kama kawaida,tunatangaza kulazwa hospitalini
kwa vichefuchefu vya mimba za wazungu,Shameful!
itaendelea
Shime
watu weusi, wembe ni uleule wa Jesse Owens dhidi ya Hitler!!
Mwandishi anapatikana katika www.congesmrambatoday.blogspot.com
0713 324 074
Mbona Uingereza walimuua Princess Diana?
TUHUMA za Ufalme wa Uingereza kumuua Princess Diana zilipowafika kooni,wakaunda Tume ya Uchunguzi wa kifo hicho.
Mkuu wa zamani wa Scotland Yard, Lord Stevens alitoa kwa waandishi wa habari ripoti ya uchunguzi wake juu ya kifo cha Princess Diana.
Mkuu wa zamani wa Scotland Yard, Lord Stevens alitoa kwa waandishi wa habari ripoti ya uchunguzi wake juu ya kifo cha Princess Diana.
Katika
ripoti hiyo ya kurasa 832, Lord Stevens amebaini kuwa Princess Diana
alikufa kwa ajali ya kawaida ya kibinadamu; au ‘Ajali ya Mungu’(Tragic
Accident); na si kwamba aliualiwa kijanja na serikali ya Uingereza, ama
ukoo wa kifalme.
Ripoti
hiyo inapingwa vikali na na Bilionea mwenye asili ya Misri, Mohamed al
Fayed, ambaye ni baba wa Dodi al Fayed mpenzi wa wa Diana ambaye pia
alikufa katika ajali hiyo ya gari Agosti 31, mwaka 1997.
Serikali ya Uingereza inasisitiza, Diana alikufa katika ajali
ya gari, kwa kuwa dereva alikuwa amelewa, na aliendesha kasi zaidi ili
kuwatoroka mapaparazzi waliokuwa wakiwafuatilia. Pia hawakuwa wamefunga
mikanda.
“Siamini
ushahidi wowote uliopo sasa unaweza kuthibitisha kuwa Dana aliuawa”,
anasema Lord John Steven’s, Kamishna wa zamani wa polisi aliyeongoza
Operesheni, Paget Probe. Wapelelezi 15 wa Scotland Yard wametumia Dola
milioni saba kuhoji mashahidi 300.
Watoto
wa Diana, Prince Willam na Prince Harry, Kakayem Lord Charles Spencer
na dada zake wawili wanaonekana kukubaliana na Lord Stevens kwamba
Diana alikufa kwa ajali ya kawaida ya kibinadamu.
Ripoti hiyo ya Lord Stevens wa
Kirkwhelpington’s Investigation, juu ya Diana ilitolwa kwanza Desemba 13
mwaka huu kwa watoto hao wa Diana; yaani siku moja kabla ya kutangazwa kwa umma.
Kwamba,
Princess Diana aliyekuwa na umri wa miaka 36 na Dodi Fayed(42)
walikufa hiyo Agosti 31 mwaka 1997 baada ya gari lao kugonga nguzo
katika barabara mjini Paris .
Wapelelezi
wa Ufaransa walimlaumu dereva, Henri Paul kuwa aliweka ‘kinywaji’
kuzidi kawaida; akawa nakwenda mwendo mkali. Msingi wa upelelezi wa
Lord Stevens ulikuwa kufuatilia madai kwamba aliuliwa.
Ripoti hiyo ilitolewa katika mkutano na waandishi wa habari, katikati ya jiji la London .
Hata hivyo, vipimo vya damu kavu vya vinasaba(DNA) vilionyesha kuwa Diana alikuwa kalewa. Ripoti hiyo inakubaliana na upelelezi wa Wafaransa kwamba Princess Diana alikufa kwa ajali iliyosababishwa na mwendo mkali, baada ya dereva kushindwa kumiliki gari, Mercedes Benz. Pia ripoti hiyo inayaweka pembeni madai kuwa uhusiano wa Dodi na Diana ulikwisha zaa matunda ya himila changa.
Hata hivyo, vipimo vya damu kavu vya vinasaba(DNA) vilionyesha kuwa Diana alikuwa kalewa. Ripoti hiyo inakubaliana na upelelezi wa Wafaransa kwamba Princess Diana alikufa kwa ajali iliyosababishwa na mwendo mkali, baada ya dereva kushindwa kumiliki gari, Mercedes Benz. Pia ripoti hiyo inayaweka pembeni madai kuwa uhusiano wa Dodi na Diana ulikwisha zaa matunda ya himila changa.
Ilidaiwa
kuwa himila changa ilichonchea hasira ama wivu mkali miongoni mwa
Waingereza, hadi wakaamua kumwondolea mbali, kuondoa aibu.
Wanadai waliuawa na vikosi vya majasusi wa MI5. Haya ni madai yaliyowahi kutolewa pia na baba wa Dodi, Mohamed al Fayed. Kwamba Diana na Dodi waliuliwa pale katika nja ya ardhini, Pont de I’Alma mjini Paris .
Wanadai waliuawa na vikosi vya majasusi wa MI5. Haya ni madai yaliyowahi kutolewa pia na baba wa Dodi, Mohamed al Fayed. Kwamba Diana na Dodi waliuliwa pale katika nja ya ardhini, Pont de I’Alma mjini Paris .
Prince William na Harry, wanaandaa misa ya kumbukumbu ya miaka 10 ya kifo hicho kwenye uwanja
mpya wa Wembley, Julai Mosi mwakani, ili kusherehekea miaka 46 ya “Birthday’
ya Diana, itakayohudhuriwa pia na maonyesho ya wanamuziki nyota kama
Sir Eltonh John, aliyeimba Candle in The Wind katika mazishi yake. John
amesema hatauimba wimbo huo mpaka aombwe.
Kundi lingine litakaloshiriki ni Duran Duran, Jose Stone na rapa mashuhuri Pharrel William, na kundi la Halaiki la Taifa.
Gazeti
la Mail on Sunday lilisema Lord Stevens alipokuwa Kamishna wa
Metropolitan, alipanga kuchunguza ujauzito wa Daiana kwa kuchukua
sampuli za damu kavu katika Mercedes Benz walilokuwa wakisafiria siku
hiyo ya ajali, jijini Paris .
Fayed
anasisitiza, Dodi na Diana
wangeoana; na kwamba alikuwa mjamzito. Anasema waliuawa na vikosi vya
usalama vya Uingereza kwa sababu familia ya Kifalme isingevumilia
kumwona Diana kapakata kitoto Kiislamu!
Wanaomjua
Diana wanajaribu kukanusha madai kuwa Diana alikuwa na mimba, na
wakamhakikishia Lord Stevens kuwa mimba kwa Dodi ilikuwa ndoto. Unajua,
ukoo wa Kifalme haukutaka aibu kama Diana angeongoka na kuwa Muislamu!
Maana yake ni kwamba Mfalme wa baadaye wa Uingereza(Mtoto wa Diana)
ambaye pia angekuwa Mkuu wa Kanisa la Uingereza, angepata baba wa
kambo(Dodi) Mwarabu; na kwamba Mfalme wa Uingereza angekuwa na ndugu
Mwarabu!
Hii
ndiyo sababu ya kuhisi kifo hicho kilipangwa kuondoa aibu. Kwamba
ajali ya Mercedes Benz S280 sedan, iliyogonga nguzo ya 13 ilikuwa
geresha, na kwamba dereva, Henry Paul alionwa
akizungumza na watu
Fulani saa chache kabla ya ajali.
Marehemu
Diana na Prince Charles walikuwa wametengana tangu Desemba 9, mwaka
1992 na wakapeana taraka rasmi Agosti 28 mwaka 1996; ingawa Diana
alisalia wa ukoo wa Kifalme.
Prince
Charles alikuwa tayari katika uhusiano wa mapenzi na Camilla Parker
Bowles ambaye walikuja kuoana majuzi. Kwa vyovyote kifo cha Princess
Diana ni ajali iliyotokana na Mungu. Lakini wengine wanahoji, ni Mungu
yupi mzembe aliyesababisha kifo kinacholeta utata hata sasa takriban
miaka 10 baada ya kutokea?
mwandishi hupatikana kwa simu 0754 324 074
HAKI ZA BINADAMU UINGEREZA NA MAREKANI?
Jumanne
usiku, Desemba 4,mwaka huu, wakati nilipokuwa nikitazama kipindi cha
televisheni ya BBC kiitwacho DIRA YA DUNIA,nikaona Salim Kikeke akisoma
'twitter' za jamaa wa TANZANIA waliohoji kwamba habari za mke wa Prince
William sasa kuwa na ujauzito wa majuma 12, ziliwahusu nini Waafrika?
Habari
za mke wa mrithi wa ufalme wa Uingereza kupata himila changa na kulazwa
hozpitalini kwa kichefuchefu, akaanza kutangaziwa Mwafrika,utadhani
zingempa kushiba!
Naam,hii
ndiyo AJENDA YA SIRI ya vyombo vyao vya habari,ili kutulisha kila
upuuzi wa akina malkia na wajukuu zake,utadhani Afrika haina cha
kujifunza kutoka hapa barani.
UINGEREZA, ambayo ilifanikiwa kuzikusanya
nchi nyingi zilizokuwa chini ya Utawala wa Rumi, na kuzifanya makaoloni yake, imekuwa ikitawaliwa na
wafalme tangu mwaka 829 A.D.
Hawa
wafalme, na dada zao na mabinti
zao(malkia) wamewatawala Waingereza tangu karne ya tisa AD. Hakuna
anayeandamana, sisi tunahamasishwa maandamano na kuaana utadhani
wendawazimu!
Hadi leo, na hakuna raia aliyekwisha andamana
kutaka utawala wa kifalme na kisultani uliodumu zaidi mya miaka 1,182 ung’olewe,ili
kupisha demokrasia.
Nchi hii, inayoongoza kuata kumpindua Kiongozi
wa Libya, Kanali Muammar al-Gaddafi, kwamba amedumu uongozini tangu mwaka
1949(umri wa miaka 42) imetawaliwa na wafalme lukuki,tangu Egbert na zama za
Saxons na Danes.
Mwaka 1399,Uingereza ilikuwa chini ya House
of Lancaster, wakitawaliwa na Wafalme na
Duke of Lancaster,hadi miaka ya 1900
wakawa chini ya Mfalme GeorgeV,Edward VIII, George VI baadaye akatawazwa
Malkia Elizabeth II, ambaye ni BINTI mkubwa wa GeorgeVI.
Huyu Malkia Elizabeth II alitawazwa kuwa
Malkia wa Uingereza Feburuari 6,mwaka 1952 hadi leo anatawala Uingereza, na
hakuna wa kuhoji mamlaka yake yaliyotamalaki hata hapa kwetu Tanzania.
Serikali
ya Uingereza inayoongozwa na Mawaziri wakuu,ilianzishwa ,mwaka 1721( karne tisa
baada ya Mfalme wa kwanza, Egbert; wakati huo akaanza kutawala Waziri Mkuu, Sir Robert Walpole.
Sir, ni cheo anachopewa mtu anayeheshimiwa
sana na Familia ya kifalme.Cheo hiki, “Knighthood” ametunukiwa hata Salman
Rushdie. Sir Salman Rushdie alipigwa ‘Fatwa’ na utawala wa Ayatollah
Khomeini,huko Iran,hivyo hutafutwa sana auawe kwa kuikashifu dini ya Kiislam.
Niachane na hayo; hayanihusu.
Kutoka Sir Robert Walpole, hadi sasa David
Cameron, Uingereza yapata mawaziri wakuu takriban 80 vya vyama anuwai, ambavyo
aslani haviwezi kuhoji bungeni mamlaka ya Malkia. Malkia Elizabeth II ANA UMRI
WA MIAKA 84, alizaliwa Aprili 21 mwaka 1926.
Akifa leo, ingawa ametawala Uingereza kwa
jumla ya miaka 59, atatawala mwanaye,Prince Charles, ama wajukuu zake, Prince
William na Harry, hao ambao wake zao wakiwa na himila changa,tunatangaziwa dunia nzima!
Wakiwa
hedhi,wakilazwa hospitalini eti kwa kichefuchefu,sisi tunatangaziwa
upuuzi ule, wakati wake zetu nao wanapata kichefuchefu na kuendelea na
hamsini zao tu,na siyo issue!
Novemba 2008, Malkia na mumewe,Prince Phillip, walikuja
Kampala,Uganda kuburuza mataifa lukuki hapa duniani, katika mkutano wa makoloni
yao ya zamani, wao wanaita Jumuiya ya Madola, The Commonwealth.
Hata Ufaransa imetawaliwa na akina
Charlegne,au Charles Mkuu(742-614 AD) hadi wakati wa Jamhuri ya Tano zama za
Rais Charles Andre J.M. de Gaulle(soma Chalz de Go)aliyeishi 1890-1070. Ni wakati wa akina
Georges Pompidou,Valery Giscard d’ Estaing, Francois Mitterand,Jacqius Chirac
hadi huyu “Mzee wa Vimwana” Nicolas Sarkozy.
Nataka kusema kwamba, hizi dola kuu zilitoka
mbali,kwenye tawala za kifalme,hadi leo kinachoitwa demokrasia halisi hakuna.
Isipokuwa, wao wanataka wafalme wa
Afrika(Gaddafi anaitwa , ‘King of Afrcan Kings’) watokomezwe.
Ili, akina Malkia
na wajukuu zake Harry na Prince William wabaki wakitutawala huku,kwenye
Commonwealth.
Malkia huyu, bado anaburuza mataifa mengi tu
kama Canada, Austria, New Zealand,Jamaica,Barbados, Bahamas kwa kuyataja
machache.
Tena, Marekani ndiko walikoiba kura katika
uchaguzi wa mwaka 2000 pale Al Gore alikaribia kushinda, wakamwibia kura.
Mashabiki wake na chama chake cha Democrat walikuwa wataarabu tu,ingekuwa kwetu
huku,ingekuwa kama Cote d’ Ivoire.
Hata mwaka huu Democratic walishaanza kuiba kura,wakastuka.Ukimpigia Obama,kura zilikwenda kwa Romney,hukusikia?
Dola iliyodumu kwa jumla ya miaka 235
wakahesabu kura kwa mashine kisha kwa mikono, wakamnyang’anya kura AlGore,
wakampa Bush. Kesi ikaenda mahakamani, mahakama ikachakachua matokeo na kumpa
Bush mhula wa kwanza wa utawala.
Tunajua
kura za Palm Beach na Miami-Dude zilileta shida, mwezi mzima ukapita bila
kujulikana mshindi. Algore alipata kura za watu wote51,000,894wakati Bush
alipata 50,495,211 akaongoza Florida na kujipatia kura za ushindi za electoral
271.
Nataka kuwagutua wanaoshabikia
Uingereza,Marekani,UfaransamUjerumani n.k kwamba kuna demokrasia pevu,kuna
uhuru na haki za binadamu(zipi?) wanazofanya hapa duniani?
Mwaka 1936, Uwanja wa
Olimpiki wa Berlin ulijengwa na Dikteta Adolf Hitler. Michezo ya Olimpiki
ilifanywa hapo Berlun, na Hitler akawa mgeni wa heshima.
Julai 9 mwaka 1936 Mwamerika Mweusi, Jesse
Owens akawatioa kamasi Wazungu wote
kwenye mbio na riadha. Akajipatia nishani nne za dhahabu kwa muda wa dakika 45
tu. Hitler akakasirika kuona Mweusi akishinda kila mara, wakati Wazungu
hawakumwona. Yeye alijua mtu mweusi ni mnyama, kwahiyo akasusia mashindano ya Olimpiki
kwa sababu mnyama, Owen, salishinda!
Miaka 70 baadaye,
mwaka 2006,uwanja huohuo wa Olimpiki wa Berlin,ndiko fainali za Kombe la Dunia
zilikofanyika, Michael Materazzi wa Italia akamtukana Zenedine Zidane Zizou,matusi
ya kibaguzi.
Chukua tabia hii ya
akina Hitler na Materazzi halafu uchanganye na ubaguzi wa rangi huko Afrika ya
Kusini zama za Makaburu.
Angalia, ubaguzi wa rangi dhidi ya akina Samuel Eto’o Fills wanaoitwa nyani, ama kawaulize
akina Eric Abidal Claud Makelele,Zidane, Thiery Henry, William Gallas,Louis
Saha,Patrick Vieira na wenzao waliposhindwa kuipa Ufaransa ubingwa, ilisemwa
kwamba ni rangi yao Nyeusi ya mkosi!
Hapa, msomaji, unaona haki gani za binadamu
huko Ulaya?Agosti 2009 huko Berlin,Ujerumani,
Caster Semenya(19) wa Afrika Kusini akawatoa kamasi Wazungu katika mbio za mita
800, wakamnyima ushindi, kwa madai kuwa yeye ni ‘Dume-Jike,’ Wazungu bwana!
Kwa Muingereza, eti neno uhuru ni mzaha
linapofika kwa Mwafrika. Mwaka 1787 mji Mkuu wa Sierra Leone, Freetown(MJI ULIO
HURU)ulijengwa na Muingereza huyu kama kituo huru cha watumwa! Watumwa
walijengewa mji huru wa Freetown?! Ajabu.
KIFO CHA DIANA AIBU TUPU
Kifo cha Princess
Diana mwaka 1997,na kuundwa kwa tume ya uchunguzi wa kifo chake, The Paget
Probe, ni kielelezo kwamba Uingereza hakuna uhuru,hakuna demokrasia na haki za
binadamu. Kuna ubaguzi wa rangi na ukaburu uliotamalaki.
Princess Diana(36) na
Dodi al Fayed(42) walikufa Agosti 31 mwaka 1997 katika Ponto de I’Alma
Park,mjini Paris, Ufaransa, mahali penye njia ya chini kwa chini.
Ilikuficha tetesi kwamba ‘wivu’ wa Malkia na
familia yake dhidi ya Diana aliyekuwa amevuka mipaka na kutaka kuolewa na
Mwarabu, Dodi, na ikasemekana alikuwa na himila changa ya miezi miwili, ndicho
kitu kilichomsababishia mauti ya tashtiti.
Vyombo vya usalama mjini Paris, baada ya
ajali yakupangwa, vikamsingizia dereva,Henri Paul kwamba aliendesha gari kwa
kasi sana, ili kuwatoroka ma-Paparazzi.
Kwamba, Dodi na Diana
waliutia mtindi kwa sana, hawakufunga mikanda wakati Mercedes Benz S-280 SEDAN,
ilipogonga nguzo ya 13 hapo barabara ya chini na kusababisha vifo vya Diana na
Dodi!
Maneno yalipokuwa mengi, ikaundwa tume ya
kuchunguza vifo hivi, Paget Probe iliyokuwa na wapelelezi 15 kutoka Scotland
Yard, wakatumia Dola za Marekani 7,000,000 kuwahoji mashuhuda 300.
Hata hivyo,Mkuu wa Paget Probe, zamani alikuwa
Mkuu wa Scotland Yard, Lord John Stevens alishia kukaa ‘kama kamati’ na watoto
wa Diana, Harry na William na kakaye,Lord Charles Spencer na dadaze wawili,
wakasema haikuwa ajali ya kupangwa.ilikuwa ajali ya kibinadamu-tragic accident!
Ripoti ya uchunguzi yenye jumla ya kurasa 832
haikuwa na jipya. Baba wa Dodi, Bilionea wa Kimisri, Mohammed al-Fayed
akaipinga vikali tume hiyo, na kusema hadharani kwamba majasusi wa Uingereza
waliwaua Dodi na Diana kwa sababu ya wivu,kuona Daiana angeolewa na Dodi.
Diana na Prince Charles walishatengana tangu Desenba 9 mwaka 1992 wakapeana talaka
rasmi Agosti 28 mwaka 1996.
Prince Charles
alishaoa kimwana mwingine, Camilla Parker Bowless, lakini Diana alifungwa
kuolewa na mtu kwa sababu alikuwa wa familia ya ufalme!
Mtu wa ‘Royal Family’ kama yeye hakuruhusiwa
kuolewa na mtu,tena Muislam, sasa sijui kama kweli alikuwa na mimba, sasa kama
Diana angezaa Mwarabu, anaye angekuwa
anakuja Makao Makuu ya Malkia-Buckingham Palace, kuwasalimia nduguze, Harry na
Prince William?
Waingereza, walimuua
Diana na Dodi,ili kutupilia mbali udhia na aibu ya warithi wa Ufalme kuwa na
ndugu Mwarabu halafu Muislam.
Si unajua dini ya Anglikana ndiyo dini yao na
Malkia ndiye mkuu wa dini hii ya Uingereza? Sasa, hawakutaka Mwarabu azae na
mke wa mwana wa Malkia, sasa tunajua Diana aliuawa kwa sababu ‘aliasi’ na
kutaka kuolewa na Dodi na alikwisha kuwa na mimba changa ya miezi
miwili,ikaleta taabu.
Unaweza kumuuliza Mohammed al Fayed, Yule tajiri
wa Kimisri, babaye Dodi,kama nasema uongo kwamba Diana aliuawa na majasusi wa
Uingereza huko Paris.
Ndiyo maana tunasema Uingereza hakuna
demokrasia,uhuru wala Haki za Binadamu. Labda uhuru uko kwa mashoga kuvua nguo
na kuandamana hadi bungeni wakiwa uchi, kuna uhuru wa wanaume kuoa na kuolewa
kama Sir Elton John na David Furnish.
Kuna uhuru wa maaskofu na wachungaji wa dini
ya Malkia kuoana wanaume na wanawake, na wanaweza kwenda baa na vimwana na
kuuchapa mtindi, halafu waumini wanapoandamana kupinga wazinzi kuwa wachungaji,
maaskofu wanawatetea!
Huu
ndiyo uhuru ulioko Uingereza,Marekani na
Ufaransa..uhuru wa kumomonyoa maadili na sheria za Bwana Mungu. Uhuru wa
kutwambia hata habari za mama mjamzito na hata anapokuwa hedhi!
itaendelea
0786/0754-324 074
Subscribe to:
Posts (Atom)