Tuesday, December 11, 2012

Mbona Uingereza walimuua Princess Diana?

TUHUMA za Ufalme wa Uingereza kumuua Princess Diana zilipowafika kooni,wakaunda Tume ya Uchunguzi wa kifo hicho.
 Mkuu wa zamani wa Scotland Yard, Lord Stevens alitoa kwa waandishi wa habari ripoti ya uchunguzi wake juu ya kifo cha Princess Diana.
   Katika ripoti hiyo ya kurasa 832, Lord Stevens amebaini kuwa Princess Diana alikufa kwa ajali ya kawaida ya kibinadamu; au ‘Ajali ya Mungu’(Tragic Accident); na si kwamba aliualiwa kijanja na serikali ya Uingereza, ama ukoo wa kifalme.
   Ripoti hiyo inapingwa vikali na na Bilionea mwenye asili ya Misri, Mohamed al Fayed, ambaye ni baba wa Dodi al Fayed mpenzi wa wa Diana ambaye pia alikufa katika ajali hiyo ya gari Agosti 31, mwaka 1997.
  Serikali ya Uingereza inasisitiza, Diana alikufa katika ajali ya gari, kwa kuwa dereva alikuwa amelewa, na aliendesha kasi zaidi ili kuwatoroka mapaparazzi waliokuwa wakiwafuatilia. Pia hawakuwa wamefunga mikanda.
    “Siamini ushahidi wowote uliopo sasa unaweza kuthibitisha kuwa Dana aliuawa”, anasema Lord John Steven’s, Kamishna wa zamani wa polisi aliyeongoza Operesheni, Paget Probe. Wapelelezi 15 wa Scotland Yard wametumia Dola milioni saba kuhoji mashahidi 300.
  Watoto wa Diana, Prince Willam na Prince Harry, Kakayem Lord Charles Spencer na dada zake wawili wanaonekana kukubaliana na Lord Stevens kwamba Diana alikufa kwa ajali ya kawaida ya kibinadamu.
  Ripoti hiyo ya Lord Stevens wa Kirkwhelpington’s Investigation, juu ya Diana ilitolwa kwanza Desemba 13 mwaka huu kwa watoto hao wa Diana; yaani siku moja kabla ya kutangazwa kwa umma.
  Kwamba, Princess Diana aliyekuwa na umri wa miaka 36 na Dodi Fayed(42) walikufa hiyo Agosti 31 mwaka 1997 baada ya gari lao kugonga nguzo katika barabara mjini Paris .
            Wapelelezi wa Ufaransa walimlaumu dereva, Henri Paul kuwa aliweka ‘kinywaji’ kuzidi kawaida; akawa nakwenda mwendo mkali. Msingi wa upelelezi wa Lord Stevens ulikuwa kufuatilia madai kwamba aliuliwa.
  Ripoti hiyo ilitolewa  katika mkutano na waandishi wa habari, katikati ya jiji la London .
Hata hivyo, vipimo vya damu kavu vya vinasaba(DNA) vilionyesha kuwa Diana alikuwa kalewa. Ripoti hiyo inakubaliana na upelelezi wa Wafaransa kwamba Princess Diana alikufa kwa ajali iliyosababishwa na mwendo mkali, baada ya dereva kushindwa kumiliki gari, Mercedes Benz. Pia ripoti hiyo inayaweka pembeni madai kuwa uhusiano wa Dodi na Diana ulikwisha zaa matunda ya himila changa.
   Ilidaiwa kuwa himila  changa ilichonchea hasira ama wivu mkali miongoni mwa Waingereza, hadi wakaamua kumwondolea mbali, kuondoa aibu.
Wanadai waliuawa na vikosi vya majasusi wa MI5. Haya ni madai yaliyowahi kutolewa pia na baba wa Dodi, Mohamed al Fayed. Kwamba Diana na Dodi waliuliwa pale katika nja ya ardhini, Pont de I’Alma mjini Paris .
 Prince William na Harry, wanaandaa misa ya kumbukumbu ya miaka 10 ya kifo hicho kwenye uwanja mpya wa Wembley, Julai Mosi mwakani, ili kusherehekea miaka 46 ya  “Birthday’ ya Diana, itakayohudhuriwa pia na maonyesho ya wanamuziki nyota kama Sir Eltonh John, aliyeimba Candle in The Wind katika mazishi yake. John amesema hatauimba wimbo huo mpaka aombwe.
  Kundi lingine litakaloshiriki ni Duran Duran, Jose Stone na rapa mashuhuri Pharrel William, na kundi la Halaiki la Taifa.
  Gazeti la Mail on Sunday  lilisema Lord Stevens alipokuwa Kamishna wa Metropolitan, alipanga kuchunguza ujauzito wa Daiana kwa kuchukua sampuli za damu kavu katika Mercedes Benz walilokuwa wakisafiria siku hiyo ya ajali, jijini Paris .
   Fayed anasisitiza, Dodi na Diana wangeoana; na kwamba alikuwa mjamzito. Anasema waliuawa na vikosi vya usalama vya Uingereza kwa sababu familia ya Kifalme isingevumilia kumwona Diana kapakata kitoto Kiislamu!
  Wanaomjua Diana wanajaribu kukanusha madai kuwa Diana alikuwa na mimba, na wakamhakikishia Lord Stevens kuwa mimba kwa Dodi ilikuwa ndoto. Unajua, ukoo wa Kifalme haukutaka aibu kama Diana angeongoka na kuwa Muislamu! Maana yake ni kwamba Mfalme wa baadaye wa Uingereza(Mtoto wa Diana) ambaye pia angekuwa Mkuu wa Kanisa la Uingereza, angepata baba wa kambo(Dodi) Mwarabu; na kwamba Mfalme wa Uingereza angekuwa na ndugu Mwarabu!
   Hii ndiyo sababu ya kuhisi kifo hicho kilipangwa kuondoa aibu. Kwamba ajali ya Mercedes Benz S280 sedan, iliyogonga nguzo ya 13 ilikuwa geresha, na kwamba dereva, Henry Paul alionwa akizungumza na watu Fulani saa chache kabla ya ajali.
  Marehemu Diana na Prince Charles walikuwa wametengana tangu Desemba 9, mwaka 1992 na wakapeana taraka rasmi Agosti 28 mwaka 1996; ingawa Diana alisalia wa ukoo wa Kifalme.
    Prince Charles alikuwa tayari katika uhusiano wa mapenzi na Camilla Parker Bowles ambaye walikuja kuoana majuzi. Kwa vyovyote kifo cha Princess Diana ni ajali iliyotokana na Mungu. Lakini wengine wanahoji, ni Mungu yupi mzembe aliyesababisha kifo kinacholeta utata hata sasa takriban miaka 10 baada ya kutokea?
 mwandishi hupatikana kwa simu 0754 324 074
 


No comments:

Post a Comment