MWAKA
1970.mfuasi wa siasa za Ki-Marxi, Salvador Allende,alikuwa Mkomunisti wa Mwanzo
huko Latin Amerika kuwa kiongozi wa nchi.
Iliwatisha
mabeberu, Mkomunisti kuwa Rais nchini Chile.Allende alianza kutaifisha mabenki
na viwanda vilivyomilikiwa na mabepari;viwanda vya makaa tam awe na chuma.
Akawapora
makabaila ardhi na kuwagawia wakulima wadogo. Nadhani,msomaji unajua
kilichotokea Zimbabwe, “R.G”Mugabe kuwapora ardhi walowezi na kuwapa wakulima
wadogo wa Zimbabwe.
Kama rais
anataka kuchukiwa na Marekani na Ulaya,ni kuwapora ardhi mabwenyenye na kuwapa
wazawa ardhi hiyo ili walime na kujikimu. Hujuma zikaanza,mfumuko wa bei
ukapanda.
Mabeberu
wakaanzisha vurugu kwa kuwatumia vijana wadogo,Chile ikajaa maasi kila mahali.Jeshi
lililazimishwa kumpindua,Allende akajikuta anazingirwa na wafuasi wake
wakajikuta katikaji ya adui.
Miji yote
mikubwa ya Chile ikajaa uasi, kama ilivyotokea Libya,Misri,Tunisia na Syria.
Mwaka
1973,jeshi likampindua Allende.Jeshi hilo kama kawaida lilisaidiwa na Shirika
la Ujasusi la Marekani(CIA),ALIPOONA KAZINGIRWA kila upande,akaazimu kujimaliza
yeye mwenyewe kuliko kukamatwa na waasi.Alijipiga risasi kwa Bunduki,SMG
aliyopewa na rafikiye, Fidel Alejandro Castro Ruz wa Cuba.
Ndipo
alipoanza kutawala Jenerali Pinochet ambaye tumeona habari zake juma
lililopita.Pinochet, aliwekwa mamlakani Chile kwa msaada wa CIA,yaani rais
aliyechaguliwa na wananchi Kidemokrasia
akapinduliwa na vibaraka wa Marekani,wanajeshi.
Marekani
inapoimba kuleta demokrasia duniani,mbona tena raia wa Chile wamchague rais wao
halafu aje kupinduliwa na jeshi,tena kwa msaada wa CIA?
Nataka msomaji
amaizi kuwa,Marekani na washirika wao wanapojidai kuimba demokrasia,basi huwa
na AJENDA YA SIRI.
Hakuna rais
anayeingia mamlakani katika nchi yeyote yenye rasilimali nyingi,hasa hapa
Afrika,akabinafsisha makampuni ya Wamarekani na mabepari wengine akaachwa,wao
hutaka viongozi kama hawa wa sasa ambao wametkeleza masharti yote ya Benki ya
Dunia na IMF ya kubinafsisha mashirika ya umma na mabenki,hata kama yalikuwa na
faida kubwa.
Ubinafsishaji
ni sera ya kibeberu,na viongozi wa kijamaa walitaifisha makampuni hayo ya
kinyonyaji,na kufanya rasilimali za nchi kama migodi,wanyamapori,ardhi kuwa
mikononi mwa umma husika wan chi hiyo.
Tunajadili,kilichofanya
viongozi wa Uhuru,akina Nyerere,Gamal Abdel Nasser,Ahmed Sekou
Toure,Lumumba,Kwame Nkrumah na wenzao,kuanza kuvutana na mabeberu. Baadhi yao
waliuliwa ama kuondolewa mamlakani kwa njia ya jeshi kuasi na kupindua serikali
za kiraia.
Leo watu
hupiga kelele wakidhani viongozi tulio nao wa vyama vyote wana weza kujiondoa
mikononi mwa ubepari uliorejea duniani kwa njia ya Ubinafsishaji!
Hivyo,
Amerika Kusini Mabeberu walimwondoa Allende wakamweka Pinochet,Dikteta ambaye
alitokea kutesa raia wa Chile,akaua zaidi ya watu 2000.Wengine walipotea katika
mazingira ya kutatanisha, hata waandishi wa habari takriban 7,000 walijikuta
wakizuiliwa katika viwanja vya michezo.
Watu
walifungwa pasipo kufikisha mahakamani Sasa shangaa kama madiketa wanaolindwa
na Marekani kama hawa akina Pinochet,ndiyo demokrasia ya Marekani?
Nimeleta
kisa hiki,kumjibu mzungu wa reli mmoja aliyenipigia simu kusema madikteta
hawajawahi kutengenezwa na Marekani na Ulaya,bali hustawishwa na rasilimali za
nchi zetu.
Huu ni ujinga uliopindukia. Hakuna dikteta
atakayedumu bila kulindwa na Ulaya na Marekani.Akina Jean Bedel-Bokassa, Nguema
Mbasongo Teodoro wa Equatorial Guinea, wanalindwa.
Wanalindwa,ili
waibe fedha na kuficha Uswisi ama wapore rasilimali na kupeleka ng’ambo,wanapewa
hisa katika makampuni yaliyobinafsishwa kwa bei chee.Wananchi wanapolia kwa
maisha magumu, makampuni haya hulifadhili jeshi na kulipa hata mishahara ya
polisi kama walivyofanya Nigeria zama za Dikteta Sani Abacha, ambaye alikuwa
mshirika wa makampuni kama Royal / Shell, Chevron,Total n.k
Kuna wajinga
wengi leo,hawajui historian a kwa sababu hiyo hawatajua kesho na leo.Kama hujui
ya jana aslani huweza kujua ya leo na kesho.
Dikteta
Pinochet aliyeingizwa mamlakani na CIA kwa njia ya mapinduzi ya kijeshi,
akapiga marufuku uchaguzi katika nchi hiyo kutoka 1974-1985. Naam, hii ndiyo
demokrasia na Haki za Binadamu za Marekani?
Duniani kuna
mafisadi na madikteta wengi wanaoumbwa na nchi hizi za Magharibi. Juan Peron wa
Argentina,alitawa tangu 1946-55.Akarudi kupindua tena nchi akatawala mwaka
1973,mkewe Isabel,akafanywa kuwa Makamu wa Rais.
Dikteta
Peron alipokufa mwaka 1974 Isabel akawa Rais! Nchi ikamshinda,mfumuko wa bei
ukapanda hadi asilimia 500! Hapa,mfumuko wa bei umefika takriban 20 tunakaribia
kuzimia kwa njaa na kiu.
Hapa Afrika,utawaona
akina Museveni wanaoigeuza Uganda kama kampuni binafsi. Baba,Mama na
Watoto(BMW) ni viongozi wa serikali,lakini kwa kuwa bado wanauhusiano na
wakubwa wa Magharibi,umesikia amri kutoka White House?
Juzi,tumesikia
Rais Barack Hussein Obama akimpigia simu Kagame wa Rwanda kuacha maramoja
kuwasaidia Waasi wa M23 HUKO CONGO.Sasa,kwanini asipige simu kumzuia Museveni
kumchagua Janet na Muhozi kuwa vigogo katika serikali anayoiongoza? Tuwe na
akili jamani,mbona sisi mbumbumbu kiasi hiki?
Noriega wa Panama.
Desemba
1989 George Herbert Walker Bush(Bush Baba) alituma jeshi Panama
City,likampindua Jen. Manuel Noriega na kumfunga pingu kama alivyofungwa Saddam
zama za mwanaye, George W.Bush.
Makampuni
ya Marekani,Uholanzi,Uingereza n.k ya mafuta,yamechochea vita na mauaji mahali
pengi,yametumikisha watu huko Burma ama Myanmar sasa, ukiwapinga Marekani
unakamatwa na kufungwa jela,labda uwe kibaraka wao.
Na
viongozi wetu wengi ni vibaraka wa Marekani, wanaogopa kukamatwa au
kupinduliwa!
Si
unasikia kwamba hata maandamano ya kupinga serikali wanachochea wao katika nchi
nyingi,kwa kisingizio cha demokrasia?
Nigeria,
Ken Saro-Wiwa, aliuliwa na Jen. Sani Abacha Novemba 10 mwaka 1995 kwa sababu
alilipinga sana kampuni la mafuta la Royal/Dutch Shell la Uingereza na
Uholanzi.
Marekani
wanajidai kuimba demokrasia na haki za binadamu,lakini ukiwapinga wanakuua
wakiwa nyuma ya pazia!
Nataka nikwambie msomaji. Orodha ya watu
waliouliwa na Marekani na washirika wao na Mashirika ya Ujasusi kama CIA,MI6 na
MI5,Mossad , BOSS la Makaburu,na mengine ni kubwa sana.
Sasa, kaangalie huko Mahakama ya Uhalifu wa
Kivita(ICC)The Hague,Uholanzi, wanashitakiwa akina nani?
Orodha ya washitakiwa,kama wale wa
Luis Moreno Ocampo maarufu kama “Ocampo Six” wamo Wakenya tu na Waafrika,na
Wazungu adui zao kama wafuasi wa Adolf Hitler na Dikteta Slobodan Milosevic wa
Serbia!
Bush na Tony Blair hawamo,kuna Fodday
Sankoh, Charles Taylor na ‘Ocampo Six’ kwa sababu hawana maslahi ya Marekani na
washirika wao.
Kanali
Muammar al-Qaddafi wa Libya, alisakwa kama nguruwe-pori,huko Benghazi
na Tripoli,kisa…Marekani na washirika wake wakasema anahatarisha ubinadamu!
Aprili 14 mwaka 1986 mvua ya masika ya mabomu ya madege ya Kimarekani,ilinyesha
Tripoli na Benghazi, wakashambulia kasri la Qaddafi, hakuwemo wakaua wanaye wa
kambo.
Qaddafi,
alikuwa adui yao tangu mwaka 1988,magaidi wake wakiwemo maofisa usalama wake
walipoilipua ndege ya Pan American Airways, Flight 103 huko Lockerbie, Scotland.
Pia alisaidiwa kupindua serikali mwaka 1969 akaja kugeuka.
Akina Abdel Basset Ali Al-Meghri
wakahukumiwa kifo,baadaye wakaachwa huru lakini Qaddafi bado anatafutwa ili
afuate nyazo za ‘waasi’ wenzake kama Noriega,Saddam,Hosni Mubarak, Ben Ali,
Samora Moises Machel,Murtala Mohamed, Patrice Emery Lumumba-ya watu wa kufa, ni
ndefu.
Akiwa Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika(AU),Qaddafi
alitaka Afrika iwe nchi moja(Pan Africanism) ili kupinga ubeberu wa Magharibi.
Visingizio
vya kutaka kumumaliza vilikuwa vingi tu. "Anataka kumrithisha mwanaye urais wa Libya".
Makampuni mengi makubwa ya Marekani yanayochimba
na kusafisha mafuta duniani:Exxon, Mobil,Chevron,Texaco,Conoco,Phillips n.k
yanaongoza kwa mikataba ya wizi na utapeli na mikataba yenye dhuluma duniani.
Nchi nyingine zenye makampuni
makubwa ya kuchimba na kuchakata mafuta ni pamoja na Uingereza,( British
Petroleum au BP), Uholanzi na United Kingdom wanamiliki kampuni kubwa la
Royal/Dutch Shell, Ufaransa na Ubelgiji wanamiliki kampuni la Total,na Urusi
ina makampuni kama Lukoil,Yukos na Sibneft.
Misri,
alikopinduliwa Rais Hosni Mubarak na ambako sasa Mohammed Mursi anakalia moto,,ina rasilimali tele ya
mafuta,gesi,phosphate, matunda n.k
Mwaka 2000,
Misri ilikuwa na akiba ya mafuta kama mapipa bilioni 2.9 hivi, nchi hii ina
ushawishi mkubwa kwa nchi za Kiarabu zenye hazina kubwa ya mafuta kama
ulivyokwishaona hapo juu.
Ni
nchi yenye mfereji wa Suez wenye urefu wa maili 103 unaoziunganisha Bahari za
Shamu(Red Sea)na Mediterranean.
Ulijengwa(ulichimbwa)
kwa ushirika na Ufaransa na Uingereza mwaka 1859-69 kukatokea vita vya
kuumiliki mfereji huo,kwa sababu yanapita mameli makubwa.Julai 28 mwaka 1956
serikali ya Misri ikautaifisha.Lazima Marekani iukodolee mimacho mfereji wa
Suez. Kutaifisha mali za nchi kutoka kwa Mkoloni ndiyo uadui mkubwa kwa mataifa
haya beberu.
Tunakusudia
kuona jinsi nchi za Magharibi zikiongozwa na Marekani zinavyochochea maasi
katika nchi zenye rasilimali nyingi na muhimu sana kama mafuta, gesi,madini
muhimu kama Uranium,almasi,dhahabu, bahari,maziwa makubwa n.k
Je, msomaji,
unaona uhusiano gani kati ya Marekani na washirika wake dhidi ya nchi zenye
mafuta mengi kama Algeria, Iran,Irak, Kuwait.Libya,Venezuela na Misri?
Hapa
Afrika,umeona uhusiano hasi kati ya Marekani na Misri, Algeria,Libya, Guinea ya
Ikweta,Angola n.k hapa Barani Afrika?
Nitashuhudia,ubabe
uchochezi, maandamano, migomo,migogoro ya kutengenezwa na vita ya wenyewe kwa
wenyewe na uasi.
Tumeona ugomvi mkubwa kati ya Marekani na nchi
zinazomgomea kuwa kibaraka wake,kama Iran ya Mahmoud Ahmadnejad(Iran ya Shah
ilikuwa kibaraka wa Marekani,wakaiba mafuta kwa wingi hadi watu walipomkataa
miaka ya mwisho ya 70,akatimkia Marekani), kuna Irak ya Marehemu Saddam
Hussein, Venezuela ya Hugo Chavez na Libya na Kanali Muammar al-Qaddafi.
Ukiyanyima
mataifa haya babe duniani wanachotaka, utaanza kusikia kwamba Hosni Mubarak
anamiliki utajiri wa Dola za Marekani Bilioni 70(Zaidi kumshinda Carlos Slim,
Bill Gates Na Warren Buffet),utasikia baadaye kwamba Rais Yoweri Kaguta
Museveni anamiliki utajiri wa Dola za Marekani Bilioni 10,siku wakikosana.
Ukiwanyanyima
maslahi yao unakuwa adui yao;tena wakimaliza kukutumia kama “kondomu”,kama
Charles Taylor,Fodday Sankoh na Jonas Savimbi,wanakutupa jela au wanakuua!
Osama
bin Laden, alikuwa mtu wao akawaasi, wanamsaka!Siku hizi hawamsemi sana,labda
walishakutana, wakayamaliza!
Rais
Mstaafu wa Afrika ya Kusini, Nelson Mandela,aliwahi kusema kwamba Vita vya
Ghuba vilikuwa vita vya mafuta.
Yaani
vita na migogoro ya Kuwait na Irak ya Saddam Hussein katika miaka ya 90-vita ya
kwanza ya Ghuba na ile ya Pili ya 2003 iliyomsababishia Saddam Hussein
kukamatwa,kufungwa jela na kunyongwa Alfajiri ya Jumamosi, Desemba 30 mwaka
2006,huko jengoni Camp Justice, mjini Baghdad,vilikuwa vita vya mafuta
Itaendelea
0786 324 074
No comments:
Post a Comment