UWANJA WAAA NDEGE wa Mwanza, unapanuliwa uweze kufikia viwango vya kimataifa,ili kuweza kuhudumia nchi zote za Maziwa Makuu.
Njia ya kurukia inapanuliwa ili kuwezesha ndege kubwa kuuruka na kutua,bila matatizo,na mnara wa kuongozea ndege unawekewa vifaa vya kisasa.
Miaka michache iliyopita,uwanja huu umekuwa gomzo kwa ajali za ndege,na ni mahali ambapo ndege ya kwanza ilitekwa hapa Tanzania.
Siku moja, saa 10:15 hivi jioni, ndege ndogo, F06 Cessna
iliyokuwa na marubani wawili, iliparamia mlima; ikaugonga na kuwaka
moto, dakika chache tu baada ya kuruka kutoka uwanja wa ndege wa Mwanza.
Ndege
hiyo ya Shirika
la Auric Air Services, yenye uwezo wa kubeba abiria kama wanane,
ilianguka na kuwaka moto; ikasababisha watu wawili ambao ni marubani,
Chris Marley mwenye uraia wa Uingereza na Mathew Smith, Mwanaanga wa
Australia kufariki dunia.
Ndege hiyo ilidaiwa kutengenezwa Marekani miaka michache iliyopita, na ilikuwa
ikikodishwa migodini na kusafirisha watalii.
Ajali iliyotokea ilitokana na kugonga mlima ulioko jirani na uwanja wa ndege wa Mwanza, marubani hao walipokuwa wakifanya mazoezi.
Ajali iliyotokea ilitokana na kugonga mlima ulioko jirani na uwanja wa ndege wa Mwanza, marubani hao walipokuwa wakifanya mazoezi.
Ilipoparamia
mlima, ikaanguka na kuanza kuwaka moto, kitendo kilichofanya maofisa wa
uwanja wa ndege na maofisa wa Jeshi la wananchi(JWTZ) kwenda kuzima
moto huo na kujaribu kufanya uokozi.
Hii ni ajali kama ya sita katika uwanja huo katika muda usiozidi miaka 10.
Uwanja wa ndege wa Mwanza ni muhimu sana katika nchi za Maziwa Makuu, lakini unaandamwa na mikosi ya kila mara.
Uwanja wa ndege wa Mwanza ni muhimu sana katika nchi za Maziwa Makuu, lakini unaandamwa na mikosi ya kila mara.
Licha
ya kuwa kandoni mwa Ziwa kubwa kuliko yote Afrika, Ziwa
Victoria , au kuwa jirani na Rwanda , Uganda , Burundi , Kenya na
Jamhuri ya Congo(DRC); uwanja wa ndege wa Mwanza, upo maeneo
yanayozalisha pamba, kahawa, samaki, dhahabu, almasi na mbuga za wanyama
maarufu sana Duniani; Serengeti.Mbuga za Serengeti ziko kilomita 100 tu
kutoka Mwanza.
Mkurugenzi
Mkuu wa Viwanja vya Ndege nchini(TAA), Prosper Tesha, aliwahi kusema
kuwa sasa uwanja huo utafanyiwa matengenezo ili kuboresha miundombinu
yake.
Mwaka 2003 uwanja huo ulisafirisha jumla ya abiria 5,344 tu wa kimataifa;wakati abiria wa
ndani walioutumia uwanja huo hawakuzidi 125,499 kwa sababu anuwai, ukiwemo uduni wa usalama na miundombinu.
Minofu ya sangara iliyosafirishwa mwaka huo kutoka katika viwanda vya kusindika minofu ilikuwa tani 13,426.
Kulingana
na rekodi za habari za viwanja vya ndege duniani, uwanja huo umegubikwa
na ‘mikosi’ ama ‘pepo wachafu’ kufuatia ndege kama sita sasa kuanguka
uwanjani hapo.
Ukiacha ajali hiyo ya Alhamisi, Aprili 3,Ajari nyingine ni ya Machi 24 mwaka 2005 wakati Ilyushin 76 ya mizigo ya Shirika la Air Trans Inc. la Moldova , Ukraine , ilipoanguka Ziwani na kuua wafanyakazi saba na rubani, wote raia wa iliyokuwa Jamhuri ya Urusi , USSR .
Ukiacha ajali hiyo ya Alhamisi, Aprili 3,Ajari nyingine ni ya Machi 24 mwaka 2005 wakati Ilyushin 76 ya mizigo ya Shirika la Air Trans Inc. la Moldova , Ukraine , ilipoanguka Ziwani na kuua wafanyakazi saba na rubani, wote raia wa iliyokuwa Jamhuri ya Urusi , USSR .
Ilikuwa
ikiruka kutoka uwanjani hapo, ikiwa na tani 50 za minofu ya sangara
kutoka viwanda vya kusindika samaki vya jijini Mwanza; na ilikuwa
safarini kwenda Croatia kupitia Benghazi na Osijek .
Hata
hivyo, mkosi wa kwanza uwanjani hapo ulitokea Feburuari 26 mwaka 1982,
siku ndege ya Shirika la Ndege la Tanzania(ATC), Boeing 737 ‘Tango
Charlie 207’ iliyokuwa na jina Kilimanjaro mbavuni, ilipotekwa nyara na
kulazimishwa kwenda London.
Ilikuwa
na abiria 74 na wafanyakazi watano; ikiendeshwa na Kapteni Deo
Mazula, wakati Yassin Membar(21), Mohamed Tahir Ahmed(21),Abdallah Ali
Abdallah(22), Mohamed Ali Abdallah(26) na kiongozi wao Musa Membar(25)
walipoiteka nyara ndege hiyo na kuunajisi uwanja huo kwa mara ya kwanza
kabisa.
Walikuwa
na silaha ‘mwanasesere,’ kufuatia usalama dhalili uwanjani hapo,
wakazipenyeza ndegeni, ambamo baada ya kuwatisha abiria na wafanyakazi
wa ndege, walipata ‘Revolver’ katika chumba cha rubani.
Pia,
walipata bastola nyingine yenye risasi, baada ya kuwapekua abiria.
Tena, walipata Shotgun mbili zisizokuwa na risasi, mali ya abiria ambazo
hazikuwa zimehifadhiwa vizuri.
Ndege
hiyo ilirejeshwa nchini na abiria wake 74 Machi 4 mwaka
huo wa 1982 wakapokelewa kishujaa, wakati Membar na wenzake walifungwa
jela kati ya miaka minane na mitatu kwa makosa hayo ya kigaidi.
Oktoba
Pili, mwaka 2001 ndege nyingine yenye shehena ya silaha, ikazuiliwa
uwanjani hapo kwa saa 30; ikajakuachiliwa baadaye kwa maagizo ya
kiusalama kutoka Dar es salaam.
Ndege hiyo ilitokea Batislava, Jamhuri ya Slovak; ikipitia Israeli hadi Misri, kabla ya kutua jijini Mwanza.
Mkuu
wa Mkoa, Stephen Mashishanga, wakati huo akasema mwanzoni walidhani
vifaa, kumbe zilikuwa silaha zilizokuwa zikienda nchi zenye migogoro.
‘Laana’ hiyo ilitua Bungeni baadaye, Mbunge wa Shinyanga
mjini, Leonard Derefa, akamtaka Waziri wa Mambo ya Ndani ajiuzulu.
Laana
hiyo ikaongezwa na Mtunzi wa Filamu ya Mapanki(The Darwin’s Nightmare),
Hubert Sauper, aliyeutangazia Ulimwengu kwamba, ndege zinazofika Mwanza
kuchukua minofu ya sangara, huja na shehena ya silaha zinazorutubisha
vita na machafuko nchi za Maziwa Makuu.
Mfaransa
huyo,akasema kupitia filamu hiyo iliyorushwa Dunia nzima, kwamba madege
yanayotua Mwanza huja na bunduki kabla ya kupakia samaki; yaani
hubadilisha samaki kwa silaha-“Guns For Fish”!
Watu
waliohojiwa na mtunzi huyo wa filamu ya tashtiti walidai, madege,
Ilyushin-76, Boeing 707 na DC8 yaliyokuwa yakija Mwanza kuchukua samaki,
yalikuwa yakishusha silaha katika nchi za migogoro, kabla ya kupakia
samaki Mwanza.
Mkurugenzi
Mkuu wa
Mamlaka ya Viwanja vya Ndege nchini(TAA), Prosper Tesha, alikanusha
madai ya filamu hiyo ya kizandiki, akasema mambo yalikuwa shwari
uwanjani hapo, kulingana na viwango vya kimataifa vilivyowekwa na
Shirika la Usafiri wa Anga Duniani, ICAO.
Hata
hivyo, wakazi wa jiji la Mwanza waliofanya mahojiano na mwandishi wa
makala hii, mwishoni mwa wiki, walishauri matengenezo yatakayofanwa
yaende sambamba na uboreshaji wa ulinzi na miundombinu itakayoepusha
ajali, ili kuondoa mikosi inayouandama uwanja huo.
Miundombinu inayoshauriwa kuimarishwa ni pamoja na vifaa vya uchunguzi mkali, security check point na mitambo maalum yenye kubaini silaha na mabomu, metal detector.
Sauper, alidai, wakati akipiga picha za filamu yake
kwamba, alipenya uwanjani hapo kwa kuwahonga baadhi ya watu hadi akafanikiwa kupiga picha katika chumba cha kuongozea ndege, traffic control tower, ambako
mwangoza ndege mmoja alipigwa picha akiacha kuongoza ndege na kuanza
kuwaua nyuki waliokuwa wakirandaranda katika vioo vya madirisha!
Wamesema,
kama Mwanza ni kitovu cha Biashara kama vilivyo viwanja kama John F.
Kennedy International, New York city na Newark(New Jersey), Sauper
asingepata upenyo wa kupigapiga picha hata maeneo ya kijeshi na
kuonyesha mabaki ya ndege zilizokwisha anguka uwanjani hapo.
“Je, viwanja vikubwa kama Mirabel , Canada , Honolulu , Charles De Gaulle, Fiumicino, Palma de Majorca n.k wanaruhusu watu
kama Sauper kupiga mapicha ovyo na kudhalilisha ?” wananchi hao waliozungumza na Mtanzania Jumapili wamehoji.
Ajali
ya Alhamisi ya ndege hiyo, Cessna, iliyoua watu wawili ni mfuatano wa
majanga mengine yasiyopungua saba katika uwanja huo tangu mwaka 2000.
Ajali nyingine iliyohusisha ndege za aina hii duniani, ni ile ya Septemba 25, mwaka 1978, ambapo Cessna 172 iligongana na Boeing 727 angani huko San Diego na kuua watu 150.
Ajali nyingine iliyohusisha ndege za aina hii duniani, ni ile ya Septemba 25, mwaka 1978, ambapo Cessna 172 iligongana na Boeing 727 angani huko San Diego na kuua watu 150.
Kulingana
na matukio haya, baadhi ya wananchi hapa wanadhani uwanja wa ndege wa
Mwanza kuna mikosi ama ‘bundi’ wanaofanya ughubikwe na ajali za kila
mara ama matukio ya kupakwa matope. Katika Filamu ya Darwin’s Nightmare,
iliyozua mtafaruku hapa nchini,
mabaki ya baadhi ya ndege zilizowahi kuanguka uwanjani hapo
yanaonekana.
Hata ajali ya miaka michache iliyopita, mabaki ya ndege hii ya Cessna huenda
yakahifadhiwa uwanjani hapo, kitu kinachofanya baadhi ya watu kuhofu
kwamba wasafiri wanaweza kudhani uwanja huo si salama na ni eneo la
ukanda wa ajali za ndege, kwa sababu kila afikaye uwanjani hapo, lazima
ataona mabaki ya ndege zilizowahi kuanguka jirani na uwanja huo.
Hata hivyo, sasa serikali inauboresha uwanja huo kwa kupanua njia ya kurukia,running way, majengo ya ofisi na miundo mbinu mingine.
Hivi sasa,uwanja huo huhudumia ndege za ATCL,Precision,54O,Kenya Airways n.k
Mwanzaoni uwanja huu ulijengwa ili kuhudumia ndege za kijeshi,ukapanuliwa hata kuwa wa ndege za abiria na mizigo kama sangara, na husafirisha pia madini na mizigo mingine
Hata hivyo, sasa serikali inauboresha uwanja huo kwa kupanua njia ya kurukia,running way, majengo ya ofisi na miundo mbinu mingine.
Hivi sasa,uwanja huo huhudumia ndege za ATCL,Precision,54O,Kenya Airways n.k
Mwanzaoni uwanja huu ulijengwa ili kuhudumia ndege za kijeshi,ukapanuliwa hata kuwa wa ndege za abiria na mizigo kama sangara, na husafirisha pia madini na mizigo mingine
Mwisho.
No comments:
Post a Comment