MWAKA 2012 umepita, umefika mwaka
mpya 2013. Hurree!
Lakini…cha moto tutakiona!
shida ni zile zile,matazizo yale yale ya miaka
yote. Katika jiji hili kuna hatari kubwa kiuchumi.
Ripoti iliyotolewa na Serikali ya
Jamhuri ya Muungano kuhusu Umasikini na Maendeleo ya Watu,mwaka 2011(Poverty
and Human Development Report 2011) iliyotolewa Mei mwaka jana 2012, imesema sekta ya uvuvi
nchini imeporomoka kwa kiwango cha kutisha.
Wakazi wa Mwanza ni wavuvi; naam
wafanyabiashara wa samaki.Asilimia kubwa ya wakazi wa mji hupata kipato chao
kutokana na samaki.
Sasa, “ Poverty and Human Development Report 2011”
inasema, nchini Tanzania sekta ya uvuvi
imeporomoka kutoka asilimia 6.7 mwaka 2004 hadi asilimia 1.5 mwaka 2010.
Ripoti hiyo inasema, hiki ni
kiwango cha chini sana kulinganisha na kingine chochote katika muongo mmoja
uliopita.
Sababu za sekta hii ya
uvuvi,hususan katika Ziwa Victoria kuporomoka ni uvuvi haramu:makokolo,uvuvi wa
sumu hata dawa za kuoshea maiti,vilipuzi majini na usafirishaji wa magendo ya samaki na mazao yake nje ya
nchi.
Uvuvi wa sangara wadogo umekuwa
ukifanywa hata na viwanda vya kusindika samaki,hadi wakati Fulani,John Pombe
Magufuli aliwaposimama kidete,wakaogopa kidogo. Nyavu haramu yakiwemo makokolo
hukamatwa hapa na kuuzwa pengine na hao maofisa uvuvi.
Wakenya waliwahi kukamatwa wakivua
samaki katika visiwa vya Mwanza na Sengerema.Walipovua walisafirisha samaki
pasipo kulipa ushuru na tozo nyingine.Wazawa wa eneo hili hutozwa tozo anuwai,
hadi wamefilisika na kushindwa kushindana na wageni hawa katika soko.Weshindwa
kurejesha mikopo katika taasisi za fedha,wamefilisika.
Matokeo yake, wageni kutoka
Shirikisho la Afrika Mashariki(EAC)sasa wanamiliki soko la samaki,wana mitaji
mikubwa,nao kufuatia ulegelege wa Mamlaka za serikali,wanavua visiwani na
kusafirisha samaki nje,pasipo kulipa kodi na ushuru.
Wakazi wa Mwanza wanafukuzwa pole
pole katika soko,wanashindwa kushindana kwa sababu ya mitaji yao kuwa midogo.
Hiki ndicho kilichosemwa katika Ripoti hiyo.
Tanzania,kipato cha familia
kimeporomoka,kutoka asilimia 18.7 hadi asilimia 16.6. Inasemwa kwamba Pato la
Mkazi wa Mwanza ni shilingi 800,000 kwa mwaka.Ni kama shilingi 2,200 tu kwa siku.
Hii ni kusema kwamba,familia
nyingi katika Jiji hili,hushindia chai,andazi moja la mitaani ama hupa mlo
mmoja kwa siku.Maisha ni magumu katika Jiji hili,kuashiria
maangamizi-Financial Doom!
Vijijini, kilimo hususan cha pamba
kimekufa,tunaposema, “Mtikisiko wa Uchumi(Global Economic Crisis) sasa ndiyo
huonekana Mwanza.Majogoo yameshindwa kuwika alfajiri,mbwa hawabwekei tena adui.
Mfumuko wa bei umepanda kutoka
“Single Digit” yaani kutoka asilimia chini ya 10(mwaka 2008) hadi asilimia 12.1
mwaka 2009. Hata leo hakuna nafuu ya maisha.
Chakula huuzwa bei ghali.Mwanza
huletwa ndizi kutoka Uganda(za Bukoba zimepatwa Ukimwi wa migomba!)Mchele
unauzwa kwa zaidi ya shilingi 2,000 kwa kilo,nao mwingine feki,umechanganywa na
viazi mviringo!
Mwanza, viazi mviringo huletwa
kutoka Molo, kule Misitu ya Mao,Jamhuri ya Kenya.Huku walishafyeka misitu hadi
mvua zimekoma kunyesha.
Leo, katika kila familia kuna
nakisi(deficit) ya Bajeti. Utaona Siku kuu za Noeli na Mwaka Mpya watoto
wakiishia kula maembe.Mwanza,Shinyanga na Mara, Desemba uliopita, ni msimu wa
maembe.
Tanzania Bara ina eneo la kilomita
za mraba 881,000. Hatuitumii ipasavyo,badala yake tumeanza kuiuza kwa
wawekezaji,ili walime sisi tununue kwao!
Watani zangu Wahaya,wameuza ardhi
huko Bukoba na huzidi kuingia Jijini Mwanza na kununua Pikipiki,ili kufanya
biashara ya ‘Bodaboda’.Kila mahali ni pikipiki,ni kelele za ving’ora,ni
fujo.Mwanza ni Jiji la kelele utadhani,Rome,Italia.
Umeme unakatika kila wakati. Maji
yamepungua Mtera,sijui Kihansi. Biashara za vinywaji baridi ziko mashakani.Watu
wamefyeka misitu ili kuchoma mkaa. Jangwa la Kalahari,lililopo Kusini,na lile
Sahara lililoko Kaskazini,limekuja kukutana huku Ziwa Victoria,sasa mvua
imekoma kunyesha jangwani-Njaa!
“Hydropower” inayopatikana sasa ni
asilimia 55 tu nchi nzima,Mwanza ni zaidi. Hata mitaa muhimu ya ofisi na viwanda,hakuna umeme. Siyo mgawo,
tuseme ukweli umeme hakuna huku.Unakatika zaidi ya dazeni kutwa.
Matokeo yake,uhalifu
umeongezeka.Kesi 567,288 ziliripotiwa nchi nzima mwaka 2009.Ziwa Victoria
limevamiwa na majambazi wenye silaha.Mwaka 2010 kesi zilikuwa 543,358 nchi
nzima. Hii ni kwa mujibu wa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, alipotoa hotupa
ya Bajeti ya 2011/2012.
Kufuatia hali hii,Mwanza kuna
machangudoa, “Commercial Sex Workers” lukuki,na ukija mgeni
ukawakurupukia,utapeleka habari kwenu.Wengine ni wakwapuzi wa hatari.
Mtunzi wa Filamu ya Darwin’s
Nightmares,Hubert Sauper alisema,machangudoa wa Mwanza hujiuza kwa Dola moja tu
ya Marekani,kwa Wazungu,hasa wale marubani wa madege ya Kirusi waliofika Mwanza
zama hizo kuchukua minofu ya sangara.
Machi 24 mwaka 2005, Ilyushin 76 ya
mizigo, ya Shirika la Air Trans Inc, la Moldova huko Ukraine, ilianguka Ziwa
Victoria, na kuua wafanyakazi saba wa ndege hiyo na rubani
.Wote walikuwa raia wa wa mataifa ambayo zamani iliyokuwa Jamhuri ya Kisovieti: Belarus, Russia, Moldova n.k
.Wote walikuwa raia wa wa mataifa ambayo zamani iliyokuwa Jamhuri ya Kisovieti: Belarus, Russia, Moldova n.k
Ilikuwa ikiruka kutoka Mwanza,
ikiwa na zaidi ya tani 50 za minofu ya sangara,kutoka viwanda vya Mwanza.
Ilikuwa safarini kwenda Croatia,kupitia Benghazi(Libya) na Osijek.
Visanduku vyeusi(Black Box)
Viwili vilipatikana majini:
Cockpit Voice Recorder,kinachonasa
sauti na Flyght Data Recorder,viliandikwa Kirusi,vikawashinda wataalamu wetu
hapa kubaini chanzo cha ajali.
Bado nayakumbuka majina ya
Warusi(waporaji wa minofu yetu ya sangara) waliozama Ziwani na dege lao na
kufariki dunia katika ajali ile: Znak,Kapteni wa ndege na raia wa Belarus,
Nesterenko,Nikolaev, Pabaruyev, Markevich,Liakh,Pulin na Pereglida.
Nataka nikwambie msomaji. Dege
lile lilizidisha uzito wa sangara wetu.
Wenye viwanda walikula njama
kuzidisha uzito ili kuwakwepa maofisa wa serikali wa Forodha ama Mamlaka ya
Mapato(TRA), wasijue ni kiasi gani cha sangara walisafirishwa kwenda Ulaya,ili
tusilipwe mrahaba stahili.
Tanzania inaibiwa sana rasilimali
zake.
Wenye viwanda vya samaki walihaha
pale uwanja wa ndege,wakati wa ajali ile ya Ilyushin 76.
Nilikuwepo wakati Kaimu Mkuu wa Mkoa
wa Mwanza, Peter Toima Keroya, alipowaambia waandishi wa habari kwamba uwanja
wa ndege wa Mwanza haukuwa na tatizo hadi ndege ile itumbukie ziwani wakati
ndege inaanza kupaa.
Hapa kuwa na mvua siku hiyo, maana mvua ikinyesha uwanja huo hujaa maji.
Hapa kuwa na mvua siku hiyo, maana mvua ikinyesha uwanja huo hujaa maji.
“Runway ni nzuri…'standard' ni ya
kimataifa. Ubalozi wa Urusi, wataalamu kutoka Moscow na Moldova wa Air Accident
Commission,watakuja kuchunguza chanzo cha ajali”, alisema Kaimu Mkuu wa mkoa wa
Mwanza wakati huo.
Siyo madege ya Ilyushin 76 tu
yaliyokuwa yakitua Mwanza kusomba samaki,hata BOEING 707, DC-8 ambayo katika
‘documentary’ ya Darwin’s Nightmare marubani walisema walitangulia kushusha
silaha katika nchi za migogoro,kabla ya kutua Mwanza na kupakia sangara,huku
wakizidisha uzito ili kukwepa kutulipa mrabaha.
Kitendo cha Wazungu kuleta silaha na
kuondoka na sangara wetu-Guns For Fish –kilisemwa na marubani hawa kwamba
wakati nyakati za Krismasi na Mwaka Mpya, KAMA HUU, Watoto wa Ulaya
walipelekewa samaki, zabibu,dhahabu na almasi, watoto wa Afrika waliletewa
Automatic Kalashnikov 47(AK-47) ili wauane! Aibu.
Ulaya kuna shibe,kutokana na sangara
za zabibu za hapa kwetu,Afrika kuna njaa,kuna vita,maandamano na migomo!
|
No comments:
Post a Comment