WAZIRI
wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe, alisema mwaka 2007
kwamba, sangara walioliingizia Taifa mabilioni ya fedha za kigeni, sasa
wametoweka.
" Wanapungua
kwa kasi
sana . Kama hatua za dharura hazitachukuliwa, watakwisha; wananchi
watateseka kwa kukosa kipato. Viwanda wa samaki vitafungwa na kuathiri
mapato ya nchi na ajira muhimu." Alisema Prof Maghembe, mwaka huo 2007
Prof.
Magembe, ambaye alikuwa akifungua kikao-kazi kwa viongozi wa mikoa na
wilaya kuhusu uvuvi endelevu Ziwa Victoria , Juni 11 mwaka 2007 katika
Ukumbi wa Chuo cha Benki Kuu Mwanza, ameonya kuwa maisha bora kwa
Watanzania hawa yanaweza kuwa pwaji, ama porojo tupu.
Lishe
kwa wakazi milioni 30 wanaozunguka ziwa hili, wa Tanzania , Kenya na
Uganda , itaporomoka; wakati fedha nyingi zikiwemo za kigeni,
zitakosekana. Prof. Maghembe aliagiza, angalau ifikapo Juni mwaka 2007
ufanywe mkakati kuhakikisha sangara waliobaki wanazaa japo uzazi mmoja
tu!
Akasema,
kitu kimoja muhimu sana , ambacho ni muktadha wa makala hii leo:
Kwamba, bila kufanya mkakati wa kuepusha sangara ama samaki kutoweka
Ziwa Victoria , Tanzania haitaepuka ‘Hukumu ya Ulimwengu’ kwa kuruhusu
rasilimali zake wakiwemo sangara, kutoweka, na hivyo maisha ya watu wake
kuathiriwa vibaya.
“Hili,
inabidi litimie. Vinginevyo, hatutaepuka hukumu ya Ulimwengu kwa
kuruhusu rasilimali hii kutoweka, na hivyo watu wetu kuathirika vibaya”,
alisema Profesa Maghembe.
Aliweka
kipindi cha nusu mwaka, kuhakikisha taarifa ya kazi inatolewa. Kwamba
jambo hili si muhali; hivyo kushindwa kulitekeleza ili kuondoa kitisho
hiki si chaguo la serikali
yetu.
Kwa
upande mwingine, ‘Hukumu hii ya Ulimwengu’ aliyosema Prof. Maghembe,
ilikwisha tolewa na Hubert Sauper, yule Mtunzi wa Filamu ya tashtiti, ya
Mapanki(The Darwin’s Nightmare), serikali ikabisha!
Kwamba,
sangara wa Ziwa Victoria walikuwa wakiliwa Ulaya, wakati wazalendo wa
nchi hii wakiambulia vijisenti kidogo vya kikunjajamvi, wakati wengine
wakiambulia vichwa na mifupa-mapanki!
Jinamizi la Darwin;Charles Robert Darwin (1809-1882) lililosimuliwa na
Hubert Sauper, kwa njia ya
kejeli, miaka michache iliyopita, kupitia filamu iliyomfedhehesha hata rais wetu, lilikuwa onyo tosha.
Onyo
kwa serikali yetu kuwamaizi Pwagu,(wezi na wadanganyifu), Pwaji(wapiga
porojo) na Pwaguzi(wajanja zaidi kuliko Pwagu), waliokuwa wakikomba
sangara wetu na kutuacha masikini.
Filamu
hii iliwataka Watanzania kuondoka usingizini mara moja na kuepuka
kugombea ubwabwa kidogo katika sufuria chafu, kula mapanki yenye funza,
na kunywa pombe haramu ili kupata tafaraji, baada ya kuvua sana na kuuza
samaki wengi sana kwa Pwagu, yaani wakala wa
Pwaguzi, bila faida!
Watanzania
tulionywa na filamu hiyo kuwa na akili; yaani kuvua kwa tija, badala ya
kuvua sana tukiishi katika makambi mithili ya manamba, ambako wavuvi
huishia kufa kwa Ukimwi, na dada zetu huishia kuwa machangudoa wanaopigwa ‘kipopo’ mithili ya wezi, na Wazungu kwa ujira wa dola dola 10 tu.
Athari
hasi za utandawazi, muktadha wake ni pamoja na kugombea maisha(struggle
for existance); ni harakati zinazowafanya viumbe dhaifu kushindwa
mapambano; na hivyo
kuishia kuliwa mithili ya mchwa, panzi na kumbikumbi.
Falsafa
ya ya Charles Robert Darwin, mwanasayansi maarufu sana wa
Kiingereza(alizaliwa Feburuali 12 mwaka 1802 na kufa Aprili 19, mwaka
1882) iitwayo Darwinism, huonya kwamba, katika maisha viumbe dhaifu
ikiwemo mimea, abadan havishindani na vyenye nguvu.
Katika zama hizi za utandawazi, mataifa dhaifu kama Tanzania , hujikuta yakinyang’anwa chakula, maji, hewa na mwanga wa jua, ili kuyapisha yenye nguvu kustawi.
Tanzania kama mmea, itanyauka baada
ya kuzongwa na magugu(Super powers), au baada ya kutafunwa kama sangara
anavyowatafuna samaki wadogo, ama kama simba anavyowatafuna swala,pofu,
nyumbu na palahala porini.
Kitu hiki, ndicho Darwinism; yaani kwamba wenye kupona ni wenye nguvu tu(survival of the fittest).
Kitendo cha sangara wetu kuuzwa Ughaibuni kwa vijisenti kidogo na
kuwalisha Wazungu na Wahindi huku Watanzania wakihangaika kwa njaa kali,
ni athari yakinifu za
utandawazi unaoruhusu wakubwa kuwatafuna wadogo.
Yesu
wa Nazareti aliwalisha watu zaidi ya 5,000 katika kijiji cha Bethsaida
kama miaka 2010 iliyopita, kwa visamaki viwali vidogo, ukilinganisha na
sangara wa Ziwa Victoria, na mikate mitano.
Katika Darwin’s Nightmare, muujiza huu unaosimuliwa katika Injili ya Mtakatifu Luka 9:10-11 na Marko 6:34-44 umeonyeshwa.
Bila
shaka, muujiza uliwekwa ili kuwakumbusha Watanzania
kwamba,
kama Yesu aliwalisha watu hao(walihesabiwa wanaume pekee, bila wanawake
na watoto) kwa visamaki viwili; wakala hadi wakasaza vikapu12,
Watanzania hushindwaje kujilisha kwa mabilioni ya sangara, dhahabu,
almasi, tanzanite, ruby, wanyamapori, misitu,shaba, pamba, kahawa, katani, korosho na rasilimali zingine anuwai?
Kwa
upande mwingine, hofu ya Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Maghembe,
kwamba samaki wetu(si visamaki) watatoweka na kuwafanya wananchi
kuathiriwa vibaya, ni sawa na kilio cha uchungu kuashiria maombolezo ya
taifa.
Sauper,
alitaka kuwasagua Watanzania, tena kuwagutua kwamba umasikini na njaa
yetu wakati sangara mabilioni wakitoroshwa Ulaya na akina Pwagu,
bazazi, dumizi na pwaguzi kwa mrabaha kidogo, ulikuwa umbumbumbu.
Hata
rasilimazi nyingine kama madini, wanyamapori na mazao ya kilimo
hutoroshwa hivihivi na ma-Pwagu, Pwajizi na mapwaguzi, pasipo sisi
kunufaika na chochote. Sisi ni ng’ombe wa maziwa-watu wa kukamuliwa hadi tone la mwisho la damu.
Pwagu, Bazazi na Pwaguzi wanavyowanyonya wavuvi. Wanasomba
sangara kwa ujira kidogo.
Hushirikiana na Maofisa uvuvi,polisi, maofisa wa Forodha, TRA, na hata baadhi ya Mawaziri husafirisha sangara kwa magendo!
Kama Profesa Maghembe na aliyekuwa Mkurugenzi wa Uvuvi,Geoffrey Nanyaro walikuwa hawajui, shime wamaizi kuwa sangara wetu hukombwa na'pwaguzi’ kwa ujira kidogo wanaolipwa akina Pwagu!
Kama Profesa Maghembe na aliyekuwa Mkurugenzi wa Uvuvi,Geoffrey Nanyaro walikuwa hawajui, shime wamaizi kuwa sangara wetu hukombwa na'pwaguzi’ kwa ujira kidogo wanaolipwa akina Pwagu!
Katika biashara hii, wamo bazazi na dumizi wanaojipendekeza kwa Pwagu, ili kujipatia makombo!
Naam. Hapa, Tanzania inaliwa na kubakizwa mifupa mitupu-mapanki.
Mapanki nayo huuzwa nje yakaliwe na kuku, wakati Watanzania wakibaki kugombea fadhila na chakula cha wahisani.
Masikini
wavuvi wanapofikisha sangara kiwandani, huambiwa na Mapwaguzi kwamba ni
‘reject’ kisha huambulia kipeto na kuondoka na njaa yao.
Kitengo cha samaki (Globefish)cha Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja
wa Mataifa(FAO), Agosti mwaka jana kilisema kwamba sangara walikuwa
wakitoweka kwa kasi Ziwa
Victoria.
Ni
taathira kwa Watanzania watakaobaki hawana chakula, wakiomba msaada
Ulaya na Marekani, ili kujiepusha kupotea katika uso wa dunia.
Tunaambiwa Watanzania huambulia milioni 500 kwa siku kutokana na
biashara ya samaki kila siku
Kwamba kila mwaka wavuvi na wachuuzi wa samaki hupata sh. Trilioni176.
Kwa mwaka Wazungu hutafuna minofu maelfu ya tani kutoka Tanzania , wakati samaki wao wakiachwa akiba.
Vya walevi huliwa na mgema.
Kwa mwaka Wazungu hutafuna minofu maelfu ya tani kutoka Tanzania , wakati samaki wao wakiachwa akiba.
Vya walevi huliwa na mgema.
Wavuvi
wadogo leo husukumiwa laana ya kusababisha sangara kutoweka; kwamba
wanavua kwa kutumia nyavu haramu. Hizi nyavu haramu hukamatwa hapa na
maofisa uvuvi, kisha huuzwa pale, baada ya kuchoma moto chache tu,
mbele ya polisi na waandishi wa habari!
Nyavu au makokoro hayo ya polisi na maofisa uvuvi ndiyo yanayoharibu mazingira ya ziwa na mazalia ya samaki.
Leo,Maofisa wanadanganywa kwamba wavuvi haramu ni wananchi vijijini! Wakale wapi sasa?
Samaki wawili wa kitoweo wanapunguza samaki?
Leo,Maofisa wanadanganywa kwamba wavuvi haramu ni wananchi vijijini! Wakale wapi sasa?
Samaki wawili wa kitoweo wanapunguza samaki?
Sangara wadogo wanaosafirishwa nje ya
nchi, wanavuliwa na nani kama si na hao maofisa uvuvi na ndugu zao?
Kwanini
wasikamatwe? Watanzania masikini wanaovua bila leseni, huvua tani ngapi
kama si kitoweo? Wanayuga-yuga kuepuka mhali, ama njaa inayowakabili.
Kwanini akina Pwagu na Pwaguzi wanaachwa kuvua na kusafirisha mamilioni ya sangara kwa magendo?
Tatizo
si wavuvi wadogo, ni mapwagu, mabazazi,dumizi na pwaguzi wanaokomba
samaki Ziwa Victoria na kuwauza nje kwa magendo, lakini
hawakamatwi. Vigogo, wakiwemo hata baadhi ya Mawaziri wana vikampuni
hewa, wanapewa mgawo wao na akina Pwagu na Pwaguzi.
Waziri
Maghembe anawataka wabadilike! Waache kuimumucha Tanzania ? Hizi ni
porojo, pwaji na soga! Waondolewe katika madaraka, tena wafilisiwe. Je,
viongozi watazinduka? Wataweza? Shime wawafunge mikatale ili kuinusuru
Tanzania.
Wanao ubavu wa kuwakomesha akina Bazazi, pwajizi, pwagu na pwaguzi wasilikaushe ziwa Viktoria? Labda.
0754 324 074
0715 324 074.
No comments:
Post a Comment