Msomi
wa Nigeria, Dk. Babafeni A.Badejo ameandika kitabu, “An Enigma in
Kenyan Politics” (Utata katika siasa za Kenya) akiufumbua macho umma wa
jamii ya Afrika Mashariki, harakati za mwanasiasa huyo machachari sana,
kuwa alishiriki Mapinduzi ya kijeshi, kutaka kumwondoa madarakani Rais
Mstaafu, Daniel arap Moi, Agosti Mosi 1982.
Katika
kitabu hicho kilichozinduliwa Nairobi zaidi ya wiki mbili
zilizopita,Dk. Badejo amwemweleza Raila kuwa mtu asiyeeleweka katika
siasa za nchi hiyo.Maoni ya
watu katika kitabu hicho humweleza Raila kama mwenye tabia ya kinyonga;
ambaye si rahisi kumtambua
au kumwamini katika harakati za kisiasa.
Raila
ameelezwa kama bingwa wa “michezo michafu” dhidi ya wapinzani wake wa
kisiasa.Baadhi ya wabunge wa Kenya katika kitabu hicho wamemfananisha na
Dikteta wa zamani wa Ujerumani, Adolf Hitler! Kwamba wakati mwingine
huonekana mzalendo,mwenye msimamo mkali ambaye kama babaye, Marehemu
Jaramogi Odinga Oginga, aliwahi kuswekwa kizuizini kwa kile anachoita
yeye kutafuta dira ya Wakenya!
Raila Odinga, anadhihirishwa katika kitabu hicho kama kinyonga, popo, na ‘sungura mjanja’ awezaye kuchochea mabalaa, halafu
akajiweka kando bila umma
kumaizi.
Asubuhi, kwa mara nyingine, miaka michache iliyopita,
Raila alishindwa kukubali au kukanusha madai kwamba alihusika katika
jaribio la mapinduzi ya mwaka 1982. Alikuwa akihojiwa na Idhaa ya
Kiswahili ya Shirika la Utangazi la Uingereza (BBC), kupitia kipindi cha
Wiki Hii.
“Nitaweka mambo yote wazi katika kitabu changu
kitakachotolewa, ili uuma ujue
ukweli”, alisema Raila kajika mahojiano hayo na Tido Mhando wakati akiongoza idhaa hiyo.
Kwa kauli hiyo, bila shaka Raila anajibanza katika pazia la mlango wa madai hayo.Anakiri kuliunga mkono jaribio hilo la mapinduzi kwa madai kuwa, kwa kuwa Kenya ilikwisha piga marufuku vyama vingi nchini, hapakuwa na namna nyingine ya kuuondoa utawala wa Kidikteta wa Moi,isipokuwa njia hiyo pekee ya mapinduzi.
Kwa kauli hiyo, bila shaka Raila anajibanza katika pazia la mlango wa madai hayo.Anakiri kuliunga mkono jaribio hilo la mapinduzi kwa madai kuwa, kwa kuwa Kenya ilikwisha piga marufuku vyama vingi nchini, hapakuwa na namna nyingine ya kuuondoa utawala wa Kidikteta wa Moi,isipokuwa njia hiyo pekee ya mapinduzi.
Kwa
kuwa katika jaribio hilo watu walimwaga damu yao, na wengine wakatiwa
mbaroni na kufunguliwa mashitaka ya uhaini, wapo waoishinikiza serikali
Raila akamatwe sasa na kufunguliwa mashitaka hayo, hata baada ya miaka
24.
Hata hivyo, katika mahojiano na BBC, Raila aliwafananisha
waliohusika katika jaribio hilo la mapinduzi, lililoshindwa, na mashujaa
waliokufa wakipigania haki tangu enzi za uawala wa rais wa kwanza, Mzee
Jomo Kenyatta: J.M. Kariuki, Pio Gama Pinto, Tom Mboya, Dk. Robert Ouko, na wengineo wengi.
Raila
alijitetea katika mahojiano hayo kuwa, anaonekana ‘mpinzani’ mara
nyingi kwa sababu ya kutafuta haki, uhuru, haki na usawa kwa Wakenya.
Kauli hii inalenga kumsafisha na hisia za watu kuwa ni
mbinafsi, anayeendekeza mno
ukabila kwa lengo la kuwapendelea watu wa kabila lake la Waluo. Raila
anatazamwa na wengi kuwa chanzo cha migawanyiko na migogoro tangu KANU,
NARC na hata umoja wao wa Orange Democtatic Movement(ODM)!
Anadaiwa
kuivuruga KANU, kabla ya uchaguzi mkuu wa Desemba 2002,ulioiweka
madarakani serikali legelege ya Narc.Akaivuruga Narc yenyewe. Alianza
kuivuruga Narc mara tu baada ya Baraza jipya la Mawaziri kutangazwa.
Alikuwa amejibanza nyuma ya ndugu zake. Ilikuwa siku mbili tu, kabla ya
baraza jipya kuapishwa.
Januari 4, mwaka huo wa 2002, kakaye Raila, Oburu
Odinga,(Mbunge wa Bondo)akiwa
na wenzake wa chama chao cha Liberal Democratic (LDP), walitangaza kumpinga rais Emillio Mwai Kibaki!
Katibu
mkuu wa LDP,Joseph Kamotho, aliitisha kikao cha wabunge wa LDP mjini
Nairobi.Ilikuwa baada ya Oburu kukutana na waandishi wa habari kutangaza
kutokubaliana na rais Kibaki kuhusu kushindwa kuipa LDP mawaziri wengi
zaidi.
Oburu
alimlaumu rais Kibaki kwamba uteuzi wake wa mawaziri haukuwa wa haki.
Kwamba LDP kilichangia viti 54 vya Bunge kati ya
vyote 125 walivyopata NARC Katika uchaguzi mkuu; hivyo kilistahili
kupewa mawaziri wengi zaidi ya wanane kati ya mawaziri wote 23!
Kama
kawaida yake, Raila ‘alijibanza’ kando ya mgogoro huo ulioanza kufukuta
hata kabla ya serikali mpya ya Narc kuapishwa, baada ya kumtoa
madarakani Moi kwa njia za kidemokrasia, kitu walichokuwa wakililia kwa
miaka mingi!
Akasema,
akiwa mjini Kisumu kwamba yeye alifurahia uteuzi huo;kwa kuwa serikali
ilikuwa makini kuteua watu wenye karama ya kusaidia kupanga mipango ya
kukuza uchumi, kwa lengo la kutimiza ahadi
zake.
Odinga,
na aliyekuwa Wazuri wa Nchi, Christopher Murungaru, wakasisitiza kuwa
Narc kilishiriki uchaguzi kama chama kimoja cha siasa, na siyo vyama
mbalimbali. Kwamba, katika makubaliano yao (Memorandum of Understanding)
waliyotiliana saini kati ya NAK(National Allience Party) na LDP, walizungumza kupeana stahili katika mgawanyo wa nafasi; na siyo mgao sawa.
Tangu
hapo LDP kikaanza kumpinga rais Emilio Mwai Kibaki, hadi majuzi
walipotaka kumwondoa madarakani kwa kura ya kutokuwa na imani
naye.Kampeni kali dhidi ya katiba ikazaa umoja wa Orange
Democratic Movement(ODM).
Aidha,
yaliyotokea Kenya yanafahamika kuwa yameleta seriakali legelege, vigogo
wengi wamefukuzwa serikalini, akiwemo Raila mwenyewe,hivi sasa
kinacosubiriwa kuokoa hali hiyo ni uchaguzi wa mwaka kesho, ambao
kampeni zinaonekana kuanza japo si rasmi.
Wakati
Raila Odinga angali ‘akiuponda’ utawala wa Moi, anasema ulitaka kumbeba
Uhuru Kenyatta. Anasema ni kheri Kibaki dhaifu na legelege anayejali
demokrasia, kuliko utawala wa kiimla wa Moi.
Raila ndiye
aliyeanzisha uasi katika KANU katikati ya mwaka 2001, ukaanzishwa muungano
wa Upinde wa Mvua(NARC), Kibaki akaruhusiwa awe rais, kisha abadili katiba na kumpa Raila Odinga wizara yenye nguvu.
Bila
shaka ilitegemewa kuwa kama katiba ingerekebishwa, ili kupunguza
madaraka ya rais(Kibaki) ili kumpa madaraka makubwa Waziri mkuu ambaye
angekuwa Raila!Baada ya Rais kukataa kutekeleza ahadi hiyo,uasi dhidi
yake uliowatupa akina Raila nje ya serikali ukatokea.Hapa
kilinachodhaniwa ni kwamba Waluo walitaka kunufaika zaidi, ingawa Raila
amekanusha katika mahojiano na BBC, kuwa siyo mbinafsi kiasi hicho.
Kama Ofisi ya Waziri mkuu ingeundwa, yaani kama mapendekezo ya katiba mpya
iliyoahidiwa wakati wa kampeni
ingekubaliwa, basi
wizara nyeti kama Usalama,Utawala wa mikoa au majimbo na Utumishi wa umma zingekuwa chini yake.
Hata
hivyo, katika mahojiano na BBC, Raila Odinga amesema siyo mtu hatari.Si
mbinafsi wala mkabila. Anasema ni mwanaharakati na mpambanaji. Kwa kuwa
mapambano ya kudai haki hayana kikomo, ndiyo maana Raila anaonekana
mvurugaji wa mambo kila wakati. Harakati zake za kudai haki, uhuru na
usawa, huzifanya wakati wowote, mahali popote dhidi ya adui au rafiki
anayetaka kuweka vizuizi barabarani mwa demokrasia, haki na uhuru!
Hakika hii ni njozi njema aliyonayo Raila…nakubaliana na kiongozi kama
huyu!
Hata
hivyo, sikubaliani kabisa na tabia ya Raila kutaka kuitawala Kenya kwa
sababu za kikabila. Kwamba kwa kuwa Wakikuyu na Wakalenjin
wamekwishatawala, sasa ni zamu ya Waluo.Hili ni doa baya linaloweza
kuifanya Kenya kama Somalia, Congo na penginepo penye machafuko.
Baadhi
ya vigogo kutoka Magharibi ya Kenya waliokuwa maarufu mni pamoja na Tom
Mboya, James Gichuru, Jaramogi Oginga Odinga, Chiedo Moa Gem
Arwings-Kodhek, J.D. Otiende, Achieng Oneko,na aliyekuwa Waziri wa Mambo
ya Nchi za Nje “Mr. Clean”,Dk. Robert Ouko.
Ouko alidaiwa kuondoka nyumbani
kwake Asubuhi ya Feburuari 13 mwaka 1990,
hakurudi; mwili wake ulikuja kugunduliwa kichakani akiwa Marehemu, huko
Got Alila, takriban kilometa sita toka kwake, Koru, Nyanza, Magharibi
mwa Kenya.
Baba
yake Raila, pia aligombana na wenzake akaanzisha Kenya Peoples Union,
baada ya kuhitilafiana na Kenyatta. Hali hii huleta maoni ya kuwepo
katika ubinafsi miomgoni mwa Waluo, lakini Raila anasema wengi wao ni
wanaharakati wasiochoka kudai haki siku zote, ndiyo maana wamekuwa watoa
dhabihu maisha yao, kama Marehemu, Dk. Ouko.
Kufuatia
hali hiyo, sitaki Raila awatumie akina Ouko kama mtaji wa kuendea
madarakani Kenya…sitaki wanasiasa wa Nyanza wamnufaishe Raila katika
harakati zake za Urais Kenya, kwa kuwa ataigawanya nchi hiyo zaidi ya
kuleta umoja na kuondoa ukabila.
Kwa
upande mwingine, navutiwa mno na harakati za Raila, kuwa tayari hata
kumpinga rafiki yake anapokwenda kinyume na matakwa ya Wakenya…ni kwa
sababu hii nami nakuwa na utata dhidi ya mwanasiasa huyu kama anastahili
kuongoza au la! Utata huo ndio chanzo cha kisebusebu na kiroho…
“Sitaki-nataka”(half reluctance) dhidi ya Raila, sawa na utata
aliosema Dk. Babafemi A.Badeja!
itaendelea
itaendelea
Want to be your own boss? Learn how on Yahoo! Small Business.
No comments:
Post a Comment