TUREJEE katika historia, ili kubaini
namna Mtu Mweusi anavyodhalilishwa na kuonekana hafai, na si binadamu,bali
mnyama!
Wanaoendesha vitendo hivyo,ndiyo hao
hao wanaotazamwa leo kama wafadhili wa Afrika,na wenye huruma kwa wananchi
wetu.
Zama za harakati za kupinga ukoloni,Mzungu aliitwa, Wasumwa Makaka!Kwamba zimwi lililowameza waafrika!
Husababisha vita hapa Barani,kwa
madai ya kuwaondoa madikteta ili kujenga demokrasia na Haki za Binadamu.
Hufadhili harakati tele Barani Afrika,zikiwemo Haki za Binadamu,hata mashoga na
wasagaji…hawa si lolote bali wabaguzi wa rangi!
Nitakwambia wewe uliyezaliwa baada
ya mwaka 1970.
MWAKA 1936 Mmarekani mweusi ,James
Cleveland Owens,(aliyezaliwa Septemba 12,1913 na kufariki dunia Machi 31,1980),aliwashinda
Wazungu wabaguzi wa rangi waliokuwa wakiongozwa na Dikteta wa Ujerumani, Adolf
Hitler.
Ni katika uwanja wa Olympic Stadium
ulioko Berlin; ambako ndiko fainali ya Kombe la Dunia zilipohitimishwa Julai
9,mwaka 2006.
Berlin ni kielelezo cha kutokomeza
ubaguzi.Berlin,kabla ya Ukuta wake kuangushwa mwaka 2004,ulikuwa kielelezo cha
ukoloni wa kutisha,ndipo Bara la Afrika lilipogawanywa mwaka 1884.
James Cleveland, ambaye alikuja
kuitwa na Mwalimu wake “J.C”. kama kifupi cha jina lake; ndiyo asili ya jina la
Jesse Owens, aliyeweka rekodi nne za Dunia kwa dakika 45 tu mbele ya Dikteta wa
Ujerumani, Adolf Hitler, aliyetaka kutumia mashindano ya Olimpiki ya Berlin
mwaka huo wa 1936, kuuonyesha ulimwengu kwamba mtu mweusi ni dhalili; tena siyo
binadamu, bali mnyama!
Jesse Owens , aliweka kwanza rekodi
ya mita100, akashinda mita 200, akashinda tena kuruka juu, kabla ya kuongoza
wenzake wane katika mbio za kupokezana vijiti.
Hitler aligoma kutambua
ushindi wa Owens, kwa madai kuwa hakuwa binadamu, sawa na mzungu! Naam, Mzungu
alikuwa binadamu, Mwafrika mnyama!
Unajua Mohammed Ali,yule bingwa wa
mabingwa wa ndondi duniani alikuwa akiitwa, “Clay” yaani udongo mweusi wa
mfinyanzi?
Unajua,Mohammed Ali, alipokataa kwenda
kupigana vita vya Vietnam alipokonywa taji la Ubingwa wa dunia? Ilikuwa miaka
ya 1967-69 hivi.
Hitler, kama wabaguzi wenzake wa
rangi, aliamini kuwa mtu mweusi alikuwa dhalili mbele ya mweupe; na pia kwamba
si binadamu kamili bali myama tu…hivyo Jesse Owen alimshinda Hitler katika
mashindano hayo mjini Berlin , miaka 70 iliyopita. Hitler aliyekuwa Mgeni wa
heshima wa mashindano ya Olimpiki mwaka 1936, aliondoka uwanjani,hakutaka kuona
‘mnyama’ akishinda mbio dhidi ya binadamu,yaani Mtu Mweupe!
Ni uwanja huo huo ulioboreshwa, ambako
mshindi wa mechi ya 61 alikuja kupambana na mshindi wa mechi ya 62 katika mechi
ya mwisho(ya 64); ya mashindano ya Kombe
la Dunia mwaka 2006 huko Berlin.
Matarajio ya weusi wengi Duniani yakiwa kuona
timu kutoka taifa moja liwe la Ulaya, Amerika ya Kusini, au Asia, kama siyo
kutoka Afrika, lakini lenye weusi wengi; likiibuka mshindi wa kombe hilo la
fahari; ili kukata ngebe za masalia ya wabaguzi wa rangi wa Ujerumani, kama
alivyofanya Jesse Owens,MWAKA 1936.
Kama ushindi wa shujaa huyo
aliyemshinda Hitler na wazungu wake akiwa ‘kifua wazi’ katika uwanja huo wa
Berlin ; matokeo yake yangekuwa ukombozi wa mtu mweusi dhidi ya kudharauliwa,
kubaguliwa na kuonywa taka mbele ya wazungu; shime watu weusi waushinde
ulimwengu wa wabaguzi mafashisti kama Adolf Hitler!
Kutokana na ushindi wa Kaka Jesse
Owens,mwaka 1936, mwaka 1976 alikuja kutuzwa medali ya Rais, ya Uhuru (Presidential Medal of Freedom)na Rais
Gerald Ford wa Marekani; akatuzwa tena medali ya Dhahabu ya Congess (Congressional Gold Medal) na rais
mwingine wa nchi hiyo, George Herbert Walker Bush (Bush Baba), mnamo
Machi 28, mwaka 1990; yaani miaka 10 baada ya kifo chake.
Mwaka 1984 mtaa mmoja wa Berlin
ukapewa jina la Jesse Owens kwa heshima yake.
Owens alikufa akiwa na miaka 66
mjini Tucson , Arizona kwa ugonjwa wa Kansa ya mapafu, kufuatia uvutaji wa sigara
uliokubuhu, wa pakiti moja kwa siku.
Hakika, ushindi wa Kaka Owens wa
majira ya joto ya mwaka 1936, majeshi ya Nazi Yalipokuwa yakijiandaa kwa vita
ya Pili ya Dunia, katika uwanja uleule lipochezwa fainali ya Kombe la Dunia, kati ya Italia na Ufaransa,mwaka 2006, ni
alama ya mapambano dhidi ya ubaguzi na dharau za weupe dhidi ya mtu mweusi
anayeishi katika mabara yote.
.Uwanja huo ulijengwa mwaka 1936 kwa
ajili ya mashindano hayo ya Olimpiki; bado ni kielelezo cha kuzikwa ubaguzi na
udhalilishaji wa weusi kama ule wa enzi ya Hitler.
Shime weusi washinde Kombe la
Dunia huko Brazil mwaka 2014.
Katika fainali hiyo, Ufaransa
ilifungwa na Italia,ikajakusemwa kwamba Ufaransa ilifungwa kwa sababu iliwaweka
Weusi wengi kwenye kikosi-Weusi eti waliitia mkosi Ufaransa!
Timu zote za Afrika zijapofungwa na
kufungishwa virago katika raundi ya awali huko Brazil,bado Afrika itashangilia
timu ya kutoka Bara lolote linalojali utu,na timu itakayojumuisha wachezaji
Weusi.
Moja wapo ya timu hizo ni Ufaransa,
Uswisi na Uingereza, ukiwaacha kaka zetu wa Brazil, Saudi Arabia, Ecuador,
Costa Rica, Trinidad na Tobago n.k.
Shime timu zinazojumuisha weusi
ziibuke washindi nchini Brazil mwaka 2014, baada ya aibu ya Zenedine Zidabe
Zizou,kutukanwa matusi ya kibaguzi huko Berlin mwaka 2006 na ndiko liliko chimbuko la ubaguzi wa rangi wa tangu
enzi za akina Dikteta Hitler, ili ukombozi kamili katika nyanja zote upatikane.
Natambua na nijajivcunia mchango wa weusi katika nyanja
nyingine kama masumbwi na siasa: Wapo akina Mohamed Ali , Leon Spinks, Evander
Holyfield, Mike Iron Tyson, Caster Semenya, na mabingwa wengine weusi waliowahi
kuushinda ulimwengu wa ubaguzi; kama Martin Luther King Jr. Kaka Andrew Jackson
Young nk.
Bila kujali mipaka ya nchi za
ulimwengu,Kombe la Dunia linalochezwa katika viwanja vya Brazil safari hii, lazima mtu mweusi audhihirishie
ulimwengu kwa mara nyingine, kwamba ni binadamu kamili mwenye uwezo na akili
timamu; na kamwe si dhalili au hayawani, kama alivyodhani Hitler.
Mashindano ya Kombe la Dunia ni
zaidi ya kutafuta heshima katika nyanya moja ya michezo, bali hata kisiasa,
kiuchumi,kijamii, kiteknolojia n.k.
Kwangu mimi, naam mtu mweusi mmoja
anapopiga mkwaju unaoingia kimiani, na kumwacha mlinda mlango, Mzungu, akigaa-gaa
sakafuni,ni ushindi pia kisiasa na kiuchumi, maarifa, ufundi, uwezo ,akili
nyingi na kila kitu, kuwazidi wazungu!
Weupe walidhani ni bora kuliko weusi.Akina Hitler wa Ujerumani,
Dk. Balthazar Johannes Voster wa Afrika Kusini, akina Ian Smith wa Rhodesia ya
zamani sasa Zimbabwe na wengineo, walijiona wao watu sisi nyani.
Popote alipo mtu mweusi katika
mataifa yote yanayoshiriki kombe hilo la
Dunia nchini Brazil,mwaka 2014 ; shime ashangiliwe na kutiwa moyo kwa kazi
kubwa ya kuushinda ubaguzi wa rangi..chenga moja ya mweusi dhidi ya mweupe ni
ishara ya maarifa na uwezo.
Kwamba, mtu mweusi ni bora kama
alivyo mweupe;ni makini, ni ghali; na kwamba siku si nyingi weusi watautawala
ulimwengu katika nyanja zoote kama wanavyotawala sasa katika dimba katika timu
nyingi na hususan katika ligi za Ulaya,kama Uingereza.
Kama nilivyokwisha sema, Afrika inayatazama mashindano hayo ya Kombe la Dunia, ama Olimpiki, kama
maandamano makubwa ya Dunia ya kupinga ubaguzi wa rangi(Anti-racist Demonstration).
Hata Afrika ilipoondolewa baada ya
mechi ya Ufaransa na Togo, Ijumaa, Juni 23, mwaka 2006 weusi tulio wengi katika mabara
yote tuliwashangilia weusi wenzetu waliosalia katika kinyang’anyiro cha timu 16
kutafuta nane zilizoingia robo fainali mwaka 2006 huko Berlin.
Ni kwa sababu hii, Fikra Pevu hupata
taabu sana kushabikia timu ya weupe; hata kama inatoka Afrika, inapocheza na
timu ya taifa lenye weusi wengi hata kama ni Ufaransa, Saudi Arabia, Brazil
,Ecuador, Costa Rica, Trinidad na Tobago na nyingine!
Ni kwa sababu hii, Fikra Pevu
zinawaona wachezaji kama Paulo Wanchope wa Costa Rica, Sol Campbell wa
Uingereza, Eric Abidal, Claud Makelele, Zenedine Zidane, Thierry Henry, Gallas,
Louis Saha,na wengineo wa Ufaransa na akina Patrick Mueller wa Uswisi, akina
Ronaldo, Gaucho, Cafu na Wabrazili wot, na wengine woote waliochipukia kama
mabalozi wa mtu mweusi katika mashindano hayo yanayoufundisha ulimwngu kwamba
mtu mweusi siyo mnyama, kama alivyosema Hitler.
Kusema hivi si kuendeleza ubaguzi wa
rangi, ni kuwaenzi wote waliopinga ubaguzi. Kama akina Nelson Mandela, Martin
Luther King Jr,Jesse Owens, Askofu Abel Muzorewa ,Desmond Tutu n.k.
Hata sasa mabalozi wetu
wengine kama Samuel Eto’o Fils wangali wakizomewa na wabaguzi wengine wa
Hispania na kwingineko Ulaya na Asia; na kufananishwa na manyani!.
uwanja wa Olimpiki wa Berlin ungegeuka shimo
la kuuzika ubaguzi wa rangi,lakini Marco Materazzi akaongeza kidonda kwa
kumtukana Zidane,mwenye asili ya Tunisia matusi ya kibaguzi,, hata kuzidi
alivyofanya Kaka Jesse Owens dhidi ya Dikteta Hitler!
Mtu mweusi atatazamwa kama chimbuko
la maarifa, tija, mafanikio katika kila jambo na hata ishara ya kiongozi na
mshindaji wa kila kitu; amini usiamini.
Wapo weusi walioathiriwa na kasumba
ya kikoloni,hata hawajithamini,wanamwona Mzungu kuwa ndiye mtu.Alifika
Afrika,mzungu huhudumiwa haraka kwa kutetemeka,Mweusi anaachwa akafie koridoni.
Natambua watu weusi walivyouzwa
katika mabara mengine kama rasilimali watu.
Kwa hali hiyo, sitaacha
kuwashangilia weusi katika harakati hizi Ujerumani hata kama watapambana na
weupe wa Afrika kusini mwa Jangwa la Sahara , acha Kasikazini!
Afrika ,siyo tena mahali penye vita,
majanga, magonjwa, njaa na machafuko kama Somali, Darfur n.k ni mahali sasa pa
maendeleo makubwa tangu katika soka, uchumi, riadha, ngumi, siasa na kila kitu
kuzidi ulimwengu wa wazungu…kinachotuponza ni kudhani wazungu ni bora kwa kila
kitu!
Nawashangaa waandishi wa habari
wanaowakilisha mashirika ya Magharibi,wanadhani vita,ukimwi na wakimbizi na
njaa ndiyo habari. Kumbe ipo miradi
tele ya maendeleo haitangazwi,na tumebaki ku copy na ku paste habari za akina mke wa Prince William kulazwa
hospitalini kwa kichefuchefu cha himila changa!
Badala ya Muafrika kuandika kwamba
Prince William mkewe ni mvivu tu,sisi huko mama mwenye himila changa, hata awe
na kichefuchefu bado huchapa kazi kama kawaida,tunatangaza kulazwa hospitalini
kwa vichefuchefu vya mimba za wazungu,Shameful!
itaendelea
Shime
watu weusi, wembe ni uleule wa Jesse Owens dhidi ya Hitler!!
Mwandishi anapatikana katika www.congesmrambatoday.blogspot.com
0713 324 074
No comments:
Post a Comment