LEO,kuna mjadala mkali wa kwanini Bara la Afrika ni tajiri,lakini watu wake masikini?
Lawama zinakwenda kwa vyama vilivyoko madarakani, ama na watawala.
Inawezekana
vyama hivi huchangia,lakini tatizo kubwa ni ujinga wa kutekeleza
masharti ya wakoloni yanayoletwa kupitia ubinabsishaji.
Vyama
vya ukombozi na viongozi wa Ukombozi walitaifisha makampuni ya mabepari
kwa manufaa ya nchi.sasa hawapo na wameondoka kwa vifo na wengine
kuhujumiwa kama tulivyomwona Lumumba.
SAFARI ya Bara la Afrika kutoka Uhuru kurejea
Utumwani,ilianza kushika kasi mara baada ya viongozi waliopigania uhuru
kuondoka.
Ahmed Sokou
Toure,Kwame Nkrumah, Gamal Abdel Nasser,Julis Nyerere, Patrice Emery
Lumumba,n.k walioondoka madarakani wengine kwa hujuma za mabeberu,Afrika
ikarudi kule ilikotoka.
Fikra huru za kuendeleza Afrika kwa maliasili zake nyingi
zilihafifsishwa, ama na Madola
makubwa kwa njia za vikwazo,au fikra hizi pevu ziliyeyushwa na kutiwa kiza hadi
tukakubaliana na utumwa na kuwategea wakoloni na mashirika yao waliyoanzisha
baada ya Vita Vikuu vya pili vya Dunia, kwamba ndiyo utakaokuwa ufumbuzi wa
matatizo ya maendeleo yetu.
Abdul Rahman Mohamed
Babu,katika kitabu kiitwacho,
“African Socialism or Socialist Africa?”(Tanzania
Publishing House,1981), anasema katika ukurasa wa 35 kwamba, kuwategemea
wafadhili hawa kulikuwa kujiingiza kichwa-kichwa katika ukoloni mamboleo,
neo-colonialism.
Wapo viongozi wa Afrika waliogoma kunyoosha mikono ya
urafiki kwa hawa wakiloni:Agostino Neto, Cabral, do Santos, Samora Machel na wenzao wakadhaniwa
ni wajamaa wa Ki-Marx, waliopinga ukoloni na kutaka kueneza siasa hatarishi za
kijamaa kwa madola ya Magharibi.
Walihujumiwa, hawapo na mawazo na njozi zao zilishapotezwa
na hawa viongozi wa leoambao hawana jipya,sispokuwa kutenda kama
mawakala wa ukoloni.
Afrika, haina tena
njozi za kuendelea kwa kutumia maliasili zake au rasilimali zake. Bali, ni
kutegemea misaada ya tashtiti(myth of aid) kutoka Ulaya,Marekani kwa upande
mmoja, na Japan,Uchina ama Urusi,kwa upande wa pili.
Tumewekewa akilini
kasumba na wakoloni,kwamba, “If no Aid, No Development” sasa, tunadhani misaada
yao ni Haki
Yetu, kumbe ni utumwa kwetu.
Nimewahi kuwasikia
viongozi wa Tanzania
wakijisifu mno kwa ‘kusaidiwa’ sana
na kufutiwa misaada, badala ya kujisifu kwa kuwaendeleza wananchi kwa kutumia
fursa zetu na rasilimali zetu wenyewe.
Hawa vigogo wetu,
wanaona kiongozi anayesaidiwa sana
kupita wenzake, ndiye ‘kipenzi’ cha Mabwana Wakubwa,kumbe ndiyo “Uchangudoa”
mamboleo unaowauza Waafrika, kwa
kutumia utajiri na mitaji wakoloni waliyopora kwetu zama za Ukoloni mkongwe.
Misaada kwa Bara hili
ina makusudi mahsusi: Kwa njia za moja kwa moja au kupitia kwingine,misaada na
hisani,huwanufaisha zaidi hawa wafadhili na wahisani,wakiloni mamboleo,kuliko
sisi.
Taasisi za Breton
Woods,Fuko la Fedha la Kimataifa(IMF)na Benki Kuu ya Dunia(WB) wamegeuka miungu
kwa kutuamria kila kitu. Nasi tunafuata bila kupinga,hata kama
ni kubinafsisha mashirika yaliojiendesha kwa faida,viwanda vilivyoongeza
thamani ya mazao yetu na kutupa ajira, matokeo yake tumefilisika,tunauza mazao
ghafi kwa bei chee bila kuyachakata.
Viwanda vya ngozi
vimegeuka maghala, viwanda vya kusindika mazao vimekufa, na vingine kama Bora Shoe Company,vilivyoleta tija kwa
Watanzania,vilishakwenda kuzimu.
Imekuwa sasa, hawa
wakoloni kwa kutumia IMF na Benki ya Dunia,wamejivika jukumu letu la kufikiri
na kuamua kwa niaba yetu,nasi tumeaachia jukumu hilo la msingi-tumejiuza mithili ya
machangudoa katika soko la matajiri.
Siku hizi tunaitwa, Nchi za Dunia ya
Tatu(Third World Countries) ingawa tuna rasilimali nyingi na muhimu sana, kama tulivyoona
katika sehemu ya kwanza ya makala hii.
Tuna
mafuta,gesi,uranium,dhahabu,almasi,maziwa makubwa,mito,Bahari,milima
mirefu,wanyamapori na misitu isiyopatikana popote duniani ila hapa Afrika.
Naam, Wakoloni
wanafikiri na kuamua chochote watakacho kwa niaba yetu. Hii ni kusema
kwamba,ubongo wetu wa mbele(The Frontal Lobe) umeshindwa kufikiri na kuamua kwa
niaba yetu wenyewe, tumewaachia Marekani na Ulaya waamue mustakabali wetu!
Rasilimali zetu
wanachukua bila sisi kujua, wanauza na kutulipa mrabaha kidogo wanapojisikia,
au wanatukopesha pesa za kununulia chandarua,na ujenzi wa zahanati,
barabara,hospitali n.k huku tukiwashangalia na kuwachezea ngoma!
Afrika tajiri, watu
wake ni masikini, wenye njaa na wanaoingiliwa kisiasa,kiuchumi,kijamii na
kijeshi na Ulaya na Mrekani na Asia.
Mapinduzi,yalishashindwa kwa sababu
wanamapinduzi walishatoweka,wenye fikra huru walishanyofolewa ubongo wa
mbele-Frontal L obe-sasa tumekabidhi maamuzi na hatima yetu kwa Marekani na
washirika wake!
Nyerere, Patrice
Lumumba, wa Congo, Ben Barka wa Morocco, Amilcar Cabral wa Guinea Bissau na
wenzao wametoweka,jua limekuchwa.
Afrika, ime
‘asilishwa’ hadi kubatizwa utoto bandia wa Ulaya na Marekani, wanaita “Africa
Europeanized”.
Kinachoangaliwa siku
hizi,ni maslahi ya Ulaya hapa Afica, na siyo maslahi ya waafrika. Hakunavyama
kama TANU, FRELIMO, M.P.L.A,UNIP na ANC vyenye kupinga utumwa na ubaguzi wa
rangi na matabaka ya watu.
Matokeo yake, Umoja wa Afrika(AU) hauna turufu katika
masoko, hauna maamuzi wa kura moja katika Baraza la Usalama la Umoja wa
Mataifa, hivyo hauna meno waka kauli hata juu ya yanayotokea hapa Barani.
Ikitokea vita Somalia na Darfur,mpaka
Marekani watutume kulinda amani na wanatulipa posho,utadhani wao walituzaa
sisi!
Marekani ndiyo yenye
kusema kwa sababu ya MITAJI YAKE iliyowekeza hapa. Marekani inaweza kusema,
“Gaddafi Must Go!” A.U ikiwa kimya! Ikisema ‘ Kikwete Must Go!” hata hakuna wa
kupinga.
Marekani ikiona aibu
kwa kauli hizi za ubabe katika macho ya kimataifa, basi inajivua gamba,na
kuwaachia washirika wake,hususan Umoja wa Kujihami wa Ulaya Magharibi(NATO),
wanatushambulia tunapojidai kichwa ngumu.
Jumatano ,Machi 30 mwaka
2011,nilipokuwa nikitazama kipindi kiitwacho, STRAIGHT TALK AFRIKA kinachorushwa
na luninga Sauti ya Amerika(VoA) nikapatwa kichefuchefu,na kupiga chafya.
Niliaona kwamba
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Hillary Rodham Clinton, alipokuwa
akizungumzia Majuma Sita ya Vita nchini Libya’ hatimaye alisema, “Gaddafi
Must Go!”
Kwamba, Gaddafi
lazima aondoke Libya,utadhani
Marekani ndiye mwamuzi na ofisa
habari wa watu wa Libya!
Lini Walibya walimpa Clinton ubongo wao wa
kufikiri na kutoa maamuzi(Frontal Lobe) ili aamue mustakabali wao kwa niaba yao?
Kudhihirisha kiburi
hiki cha Marekani, Machi 17 mwaka 2011, Marekani chini ya mwamvuli wa Umoja wa
Mataifa(UN) wakatoa Amri ya ndege zote za Libya
kutoruka katika Anga ya Libya,
”No Fly Zone!”
Ati, hii ni Amri ya
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa dhidi ya kiongozi wa Libya,Kanali
Mouammar al-Gaddafi, asiendelee kuwashambulia waasi wan chi hiyo kwa madege ya
kijeshi,ama kusababisha maafa makubwa.
Gaddafi, kawaita
wanaompinga(Waasi) kwamba ni mende, panya,mijusi,pusi-paka nyau!
Ndipo sasa, Umoja wa
Mataifa umeruhusu NATO kuishambulia Libya,utadhani
Libya imetangulia
kuzishambulia nchi wanachama wa Umoja wa Kujihami wa Ulaya Kaskazini mwa Bahari
ya Atlantic, yaani NATO!
Tukubaliane kimsingi,
kwamba Gaddafi kakaa kwenye uongozi tangu mwaka 1969,na kwamba ni Dikteta
anayewaita wapinzani,mende,panya n.k
Tuchukulie kuwa kweli kwamba, Gaddafi nawaburuza raia wa Libya na
wamemchoka.Sasa, Marekani,Ufaransa na Uingereza,ama NATO wamekujaje katika
mgogoro huo?
Ati, Gaddafi
anatishia maisha ya watu na utu? Mbona Umoja wa Mataifa haujachukua hatua
madhubuti za kuondoa vita Cote
d’ Ivoire? Mbona hata huko kuna vita
vinasambaa,na watu wanakufa?
Sasa,kwa
akili tulizonazo na kuomba omba kwetu,kukaribisha Marekani na Ulaya
kuamua lolote na kuingilia Afrika kijeshi,ndiyo Ukooloni tunaokaribisha
Afrika.Afrika haijawahi kulaaniwa,kama wengine wasemavyo,ni kushindwa
kuwa huru kifikra tu.
Mtayarishaji wa
kipindi cha Straight Talk Africa,Dk. Shaka Ssali, Jumatano hiyo alimuuliza
swali mgeni wake studioni, Profesa Dk. Abdul Karim Bangura, ambaye ni
Profesa wa Uhusiano wa Kimataifa katika
Chuo Kikuu cha Howard.
“Kwanini Marekani
ichukue hatua Libya,na siyo Cote d’ Ivoire?”
“ Ni mafuta” Prof.
Abdul Karim Bangura alijibu, kwamba sababu ya Marekani kuiingilia kijeshi Libya kabla ya Cote
d’ Ivoire ni mafuta ya Libya!
Mafuta ya Libya,yanawavuta
kunguru,tai, mainzi ya kijani na nyang’au wengi ili kuja kula mizoga!
Ndivyo nilivyosema
katika makala iliyotangulia,juma lililopita,kwamba mgogoro mmoja unaachwa ili
kuingilia mahali kuliko na ‘uhondo’ wa mafuta.
Wameacha suala la
Laurent Gabagbo, wakaenda Libya,kwa
sababu ya tabia yao ya upendeleo na macho yao yana
makengengeza,ndiyo wanaita ‘double standards’.
Suala la Marekani na
Washirika wake kuona kwamba Cote d’ Ivoire
hakuna taabu, wakakimbilia Benghazi na Tripoli ili kukamata visima vya mafuta, kwa visingizio
kwamba Gaddafi ana madege mengi ya kijeshi na vifaru kuliko Gbagbo…ndiyo maana
UN wakatuma NATO kushambulia Libya,ni
uhuni na usanii ulioje?
Kwa sababu gain Amri
ya “No Fly Zone” ITANGAZWE LIBYA
na wala siyo Abidjan
ama Yamoussoukro?
Sasa wako Congo na wanawatumia akina Museveni na Jen.Kagame
Ati,
Libya hakuna
demokrasia,hakuna katiba,kwa hiyo ni vita vya kuleta demokrasia na Haki za
Binadamu. Vita dhidi ya ugaidi….Gaddafi ni gaidi kuliko akina Laurent Koudou
Bagabgo, wanaoshindwa uchaguzi wanagoma kuondoka mamlakani.
Umoja wa Afrika,mjini
Addis Ababa
umeshindwa kusema kwa sauti kubwa. Ulikuwa kimya wakati Hosni Mubarak
akitimuliwa mjini Cairo.
AU hawakusema kitu wakati Zine El Abidine Ben Ali akitimuliwa na wamachinga
huko Tunis, Tunisia.
Sasa, AU
inasema
polepole ikiwa chini ya makomeo ya milango na nondo za madirisha mjini
Addis Ababa,kwamba
Gaddafi anaonewa.Kesho watasema kiongozi mwingine kaonewa. Halafu hii AU
haina chake,imejengewa hata ofisi zake Addis Ababa na Uchina kwa dola
Milioni 200,kwa hiyo China itatazamwa kama Baba yetu,hata kama wachina
wanakosea!
Ni kwa sababu hii,
Marekani inaidhihaki AU,kwamba “Mfalme
wa Wafalme” wa Afrika, GADDAFI alipaswa kutimuliwa tangu Libya hadi Afrika yote.
Gaddafi hakuwa Mfalme wa Afrika,upuuzi tu. Ulaya mbona kuna wafalme na malkia?
Kanali Mouammar
al-Gaddafi, “King of African Kings” kama
wanavyomkebehi, ilikuwa lazima aondoke!
Hii ni Amri ya
Marekani iliyojaa dharau na kiburi dhidi ya Waafrika wa rangi zote(Pan
Africanism) ili Mzungu arudi kutawala?
Gaddafi, “King of
Kings” akiwa Mwenyekiti wa AU alitaka
Afrika iwe dola moja kubwa(UNITED STATES OF AFRICA) ili yeye awe rais
kwa kwanza awatoe kamasi mabeberu,na kuwanyima rasilimali tete wanazotolea
udenda!
Gaddafi, ‘King of
African Kings’ aliwakufuru hawa UNITED STATES OF
AMERICA kwa kutaka kuwe na USA
nyingine Africa?
Mimi najiuliza, haya
mapinduzi yaliyoanzia Tunisia,Misri, sasa Libya,Yemen na Syria zinawaka
moto,yakivuka Jangwa la Sahara na
kufika Kusini, Robert Mugabe atapona kweli?
Ataendelea
kuwanyang’anya walowezi mashamba na kuwagawia Waafrika?
Hili Baraza la
Usalama la Umoja wa Mataifa,lenye wajumbe wa kudumu,Marekani, Ufaransa,Uingereza(wanaoongoza
kuivamia Libya) pamoja na Uchina na Russia, wakimwondoa Gaddafi,wakapora mafuta
watakwenda Cote d’ Ivoire na kutwaa
kakao, kasha watakuja Zanzibar, Uganda,Musumbiji na kwingine kwenya harufu ya
mafuta,na kuleta migogoro!
Ni kwa sababu
hii,tunauona ukoloni na utumwa mpya ukirejea Afrika kwa nguvu za
kijeshi, huku
wakijidai kuleta Haki za Binadamu na demokrasia,kumbe ni ‘Militarization
and
Human Right Abuses!”.MZUKA WA GADDAFI utazidi kuitafuta Afarika,na kifo
chake na kufungwa kwa baadhi ya viongozi madikteta hapa Barani,siyo
kheri ni mwanzo wa utumwa mpya
Waafrika tuamke.
0754/0786-324 074
No comments:
Post a Comment