Jumanne
usiku, Desemba 4,mwaka huu, wakati nilipokuwa nikitazama kipindi cha
televisheni ya BBC kiitwacho DIRA YA DUNIA,nikaona Salim Kikeke akisoma
'twitter' za jamaa wa TANZANIA waliohoji kwamba habari za mke wa Prince
William sasa kuwa na ujauzito wa majuma 12, ziliwahusu nini Waafrika?
Habari
za mke wa mrithi wa ufalme wa Uingereza kupata himila changa na kulazwa
hozpitalini kwa kichefuchefu, akaanza kutangaziwa Mwafrika,utadhani
zingempa kushiba!
Naam,hii
ndiyo AJENDA YA SIRI ya vyombo vyao vya habari,ili kutulisha kila
upuuzi wa akina malkia na wajukuu zake,utadhani Afrika haina cha
kujifunza kutoka hapa barani.
UINGEREZA, ambayo ilifanikiwa kuzikusanya
nchi nyingi zilizokuwa chini ya Utawala wa Rumi, na kuzifanya makaoloni yake, imekuwa ikitawaliwa na
wafalme tangu mwaka 829 A.D.
Hawa
wafalme, na dada zao na mabinti
zao(malkia) wamewatawala Waingereza tangu karne ya tisa AD. Hakuna
anayeandamana, sisi tunahamasishwa maandamano na kuaana utadhani
wendawazimu!
Hadi leo, na hakuna raia aliyekwisha andamana
kutaka utawala wa kifalme na kisultani uliodumu zaidi mya miaka 1,182 ung’olewe,ili
kupisha demokrasia.
Nchi hii, inayoongoza kuata kumpindua Kiongozi
wa Libya, Kanali Muammar al-Gaddafi, kwamba amedumu uongozini tangu mwaka
1949(umri wa miaka 42) imetawaliwa na wafalme lukuki,tangu Egbert na zama za
Saxons na Danes.
Mwaka 1399,Uingereza ilikuwa chini ya House
of Lancaster, wakitawaliwa na Wafalme na
Duke of Lancaster,hadi miaka ya 1900
wakawa chini ya Mfalme GeorgeV,Edward VIII, George VI baadaye akatawazwa
Malkia Elizabeth II, ambaye ni BINTI mkubwa wa GeorgeVI.
Huyu Malkia Elizabeth II alitawazwa kuwa
Malkia wa Uingereza Feburuari 6,mwaka 1952 hadi leo anatawala Uingereza, na
hakuna wa kuhoji mamlaka yake yaliyotamalaki hata hapa kwetu Tanzania.
Serikali
ya Uingereza inayoongozwa na Mawaziri wakuu,ilianzishwa ,mwaka 1721( karne tisa
baada ya Mfalme wa kwanza, Egbert; wakati huo akaanza kutawala Waziri Mkuu, Sir Robert Walpole.
Sir, ni cheo anachopewa mtu anayeheshimiwa
sana na Familia ya kifalme.Cheo hiki, “Knighthood” ametunukiwa hata Salman
Rushdie. Sir Salman Rushdie alipigwa ‘Fatwa’ na utawala wa Ayatollah
Khomeini,huko Iran,hivyo hutafutwa sana auawe kwa kuikashifu dini ya Kiislam.
Niachane na hayo; hayanihusu.
Kutoka Sir Robert Walpole, hadi sasa David
Cameron, Uingereza yapata mawaziri wakuu takriban 80 vya vyama anuwai, ambavyo
aslani haviwezi kuhoji bungeni mamlaka ya Malkia. Malkia Elizabeth II ANA UMRI
WA MIAKA 84, alizaliwa Aprili 21 mwaka 1926.
Akifa leo, ingawa ametawala Uingereza kwa
jumla ya miaka 59, atatawala mwanaye,Prince Charles, ama wajukuu zake, Prince
William na Harry, hao ambao wake zao wakiwa na himila changa,tunatangaziwa dunia nzima!
Wakiwa
hedhi,wakilazwa hospitalini eti kwa kichefuchefu,sisi tunatangaziwa
upuuzi ule, wakati wake zetu nao wanapata kichefuchefu na kuendelea na
hamsini zao tu,na siyo issue!
Novemba 2008, Malkia na mumewe,Prince Phillip, walikuja
Kampala,Uganda kuburuza mataifa lukuki hapa duniani, katika mkutano wa makoloni
yao ya zamani, wao wanaita Jumuiya ya Madola, The Commonwealth.
Hata Ufaransa imetawaliwa na akina
Charlegne,au Charles Mkuu(742-614 AD) hadi wakati wa Jamhuri ya Tano zama za
Rais Charles Andre J.M. de Gaulle(soma Chalz de Go)aliyeishi 1890-1070. Ni wakati wa akina
Georges Pompidou,Valery Giscard d’ Estaing, Francois Mitterand,Jacqius Chirac
hadi huyu “Mzee wa Vimwana” Nicolas Sarkozy.
Nataka kusema kwamba, hizi dola kuu zilitoka
mbali,kwenye tawala za kifalme,hadi leo kinachoitwa demokrasia halisi hakuna.
Isipokuwa, wao wanataka wafalme wa
Afrika(Gaddafi anaitwa , ‘King of Afrcan Kings’) watokomezwe.
Ili, akina Malkia
na wajukuu zake Harry na Prince William wabaki wakitutawala huku,kwenye
Commonwealth.
Malkia huyu, bado anaburuza mataifa mengi tu
kama Canada, Austria, New Zealand,Jamaica,Barbados, Bahamas kwa kuyataja
machache.
Tena, Marekani ndiko walikoiba kura katika
uchaguzi wa mwaka 2000 pale Al Gore alikaribia kushinda, wakamwibia kura.
Mashabiki wake na chama chake cha Democrat walikuwa wataarabu tu,ingekuwa kwetu
huku,ingekuwa kama Cote d’ Ivoire.
Hata mwaka huu Democratic walishaanza kuiba kura,wakastuka.Ukimpigia Obama,kura zilikwenda kwa Romney,hukusikia?
Dola iliyodumu kwa jumla ya miaka 235
wakahesabu kura kwa mashine kisha kwa mikono, wakamnyang’anya kura AlGore,
wakampa Bush. Kesi ikaenda mahakamani, mahakama ikachakachua matokeo na kumpa
Bush mhula wa kwanza wa utawala.
Tunajua
kura za Palm Beach na Miami-Dude zilileta shida, mwezi mzima ukapita bila
kujulikana mshindi. Algore alipata kura za watu wote51,000,894wakati Bush
alipata 50,495,211 akaongoza Florida na kujipatia kura za ushindi za electoral
271.
Nataka kuwagutua wanaoshabikia
Uingereza,Marekani,UfaransamUjerumani n.k kwamba kuna demokrasia pevu,kuna
uhuru na haki za binadamu(zipi?) wanazofanya hapa duniani?
Mwaka 1936, Uwanja wa
Olimpiki wa Berlin ulijengwa na Dikteta Adolf Hitler. Michezo ya Olimpiki
ilifanywa hapo Berlun, na Hitler akawa mgeni wa heshima.
Julai 9 mwaka 1936 Mwamerika Mweusi, Jesse
Owens akawatioa kamasi Wazungu wote
kwenye mbio na riadha. Akajipatia nishani nne za dhahabu kwa muda wa dakika 45
tu. Hitler akakasirika kuona Mweusi akishinda kila mara, wakati Wazungu
hawakumwona. Yeye alijua mtu mweusi ni mnyama, kwahiyo akasusia mashindano ya Olimpiki
kwa sababu mnyama, Owen, salishinda!
Miaka 70 baadaye,
mwaka 2006,uwanja huohuo wa Olimpiki wa Berlin,ndiko fainali za Kombe la Dunia
zilikofanyika, Michael Materazzi wa Italia akamtukana Zenedine Zidane Zizou,matusi
ya kibaguzi.
Chukua tabia hii ya
akina Hitler na Materazzi halafu uchanganye na ubaguzi wa rangi huko Afrika ya
Kusini zama za Makaburu.
Angalia, ubaguzi wa rangi dhidi ya akina Samuel Eto’o Fills wanaoitwa nyani, ama kawaulize
akina Eric Abidal Claud Makelele,Zidane, Thiery Henry, William Gallas,Louis
Saha,Patrick Vieira na wenzao waliposhindwa kuipa Ufaransa ubingwa, ilisemwa
kwamba ni rangi yao Nyeusi ya mkosi!
Hapa, msomaji, unaona haki gani za binadamu
huko Ulaya?Agosti 2009 huko Berlin,Ujerumani,
Caster Semenya(19) wa Afrika Kusini akawatoa kamasi Wazungu katika mbio za mita
800, wakamnyima ushindi, kwa madai kuwa yeye ni ‘Dume-Jike,’ Wazungu bwana!
Kwa Muingereza, eti neno uhuru ni mzaha
linapofika kwa Mwafrika. Mwaka 1787 mji Mkuu wa Sierra Leone, Freetown(MJI ULIO
HURU)ulijengwa na Muingereza huyu kama kituo huru cha watumwa! Watumwa
walijengewa mji huru wa Freetown?! Ajabu.
KIFO CHA DIANA AIBU TUPU
Kifo cha Princess
Diana mwaka 1997,na kuundwa kwa tume ya uchunguzi wa kifo chake, The Paget
Probe, ni kielelezo kwamba Uingereza hakuna uhuru,hakuna demokrasia na haki za
binadamu. Kuna ubaguzi wa rangi na ukaburu uliotamalaki.
Princess Diana(36) na
Dodi al Fayed(42) walikufa Agosti 31 mwaka 1997 katika Ponto de I’Alma
Park,mjini Paris, Ufaransa, mahali penye njia ya chini kwa chini.
Ilikuficha tetesi kwamba ‘wivu’ wa Malkia na
familia yake dhidi ya Diana aliyekuwa amevuka mipaka na kutaka kuolewa na
Mwarabu, Dodi, na ikasemekana alikuwa na himila changa ya miezi miwili, ndicho
kitu kilichomsababishia mauti ya tashtiti.
Vyombo vya usalama mjini Paris, baada ya
ajali yakupangwa, vikamsingizia dereva,Henri Paul kwamba aliendesha gari kwa
kasi sana, ili kuwatoroka ma-Paparazzi.
Kwamba, Dodi na Diana
waliutia mtindi kwa sana, hawakufunga mikanda wakati Mercedes Benz S-280 SEDAN,
ilipogonga nguzo ya 13 hapo barabara ya chini na kusababisha vifo vya Diana na
Dodi!
Maneno yalipokuwa mengi, ikaundwa tume ya
kuchunguza vifo hivi, Paget Probe iliyokuwa na wapelelezi 15 kutoka Scotland
Yard, wakatumia Dola za Marekani 7,000,000 kuwahoji mashuhuda 300.
Hata hivyo,Mkuu wa Paget Probe, zamani alikuwa
Mkuu wa Scotland Yard, Lord John Stevens alishia kukaa ‘kama kamati’ na watoto
wa Diana, Harry na William na kakaye,Lord Charles Spencer na dadaze wawili,
wakasema haikuwa ajali ya kupangwa.ilikuwa ajali ya kibinadamu-tragic accident!
Ripoti ya uchunguzi yenye jumla ya kurasa 832
haikuwa na jipya. Baba wa Dodi, Bilionea wa Kimisri, Mohammed al-Fayed
akaipinga vikali tume hiyo, na kusema hadharani kwamba majasusi wa Uingereza
waliwaua Dodi na Diana kwa sababu ya wivu,kuona Daiana angeolewa na Dodi.
Diana na Prince Charles walishatengana tangu Desenba 9 mwaka 1992 wakapeana talaka
rasmi Agosti 28 mwaka 1996.
Prince Charles
alishaoa kimwana mwingine, Camilla Parker Bowless, lakini Diana alifungwa
kuolewa na mtu kwa sababu alikuwa wa familia ya ufalme!
Mtu wa ‘Royal Family’ kama yeye hakuruhusiwa
kuolewa na mtu,tena Muislam, sasa sijui kama kweli alikuwa na mimba, sasa kama
Diana angezaa Mwarabu, anaye angekuwa
anakuja Makao Makuu ya Malkia-Buckingham Palace, kuwasalimia nduguze, Harry na
Prince William?
Waingereza, walimuua
Diana na Dodi,ili kutupilia mbali udhia na aibu ya warithi wa Ufalme kuwa na
ndugu Mwarabu halafu Muislam.
Si unajua dini ya Anglikana ndiyo dini yao na
Malkia ndiye mkuu wa dini hii ya Uingereza? Sasa, hawakutaka Mwarabu azae na
mke wa mwana wa Malkia, sasa tunajua Diana aliuawa kwa sababu ‘aliasi’ na
kutaka kuolewa na Dodi na alikwisha kuwa na mimba changa ya miezi
miwili,ikaleta taabu.
Unaweza kumuuliza Mohammed al Fayed, Yule tajiri
wa Kimisri, babaye Dodi,kama nasema uongo kwamba Diana aliuawa na majasusi wa
Uingereza huko Paris.
Ndiyo maana tunasema Uingereza hakuna
demokrasia,uhuru wala Haki za Binadamu. Labda uhuru uko kwa mashoga kuvua nguo
na kuandamana hadi bungeni wakiwa uchi, kuna uhuru wa wanaume kuoa na kuolewa
kama Sir Elton John na David Furnish.
Kuna uhuru wa maaskofu na wachungaji wa dini
ya Malkia kuoana wanaume na wanawake, na wanaweza kwenda baa na vimwana na
kuuchapa mtindi, halafu waumini wanapoandamana kupinga wazinzi kuwa wachungaji,
maaskofu wanawatetea!
Huu
ndiyo uhuru ulioko Uingereza,Marekani na
Ufaransa..uhuru wa kumomonyoa maadili na sheria za Bwana Mungu. Uhuru wa
kutwambia hata habari za mama mjamzito na hata anapokuwa hedhi!
itaendelea
0786/0754-324 074
No comments:
Post a Comment