Umoja huo wa OAU, ulianzishwa Mei 25 mwaka 1963 ukiwa na kusudi la kuinua maisha ya
watu wake, baada ya kunyonywa na wakoloni kwa karne nyingi, ambao walichota nguvu na rasilimali zetu ili kujenga kwao.
Kulingana
na viongozi 30 wa Afrika, waliokutana mwaka huo wa 1963 mjini Addis
Ababa, Ethiopia, OAU ilikusudiwa kuondoa mifumo ya aina zote za ukoloni
na pia kupinga ubaguzi wa aina zote, ukiwemo ule ulioendeshwa na
Makaburu wa Afrika Kusini.
Swali la kujiuliza leo, miaka 50 baada ya Umoja huo( kama angezaliwa binadamu angekuwa mtu wa makamo), Waafrika tuko huru leo? Hatuwategemei wakoloni?
Wakoloni
walioitawala Afrika ni pamoja na Wafaransa, Waingereza, Wahispania,
Wareno Wabelgiji, Wajerumani na Waitalia: Tumekoma kusubiri shuruti
kutoka kwao sasa?
Kama bado, kwanini? Kwa sababu gani Afrika yenye umri wa mtu mzima mwenye wajukuu, kuendelea kuwa tegemezi kwa wakoloni tuliofukuza miaka 50 iliyopita, tukisema walitudhoofisha? Kwanini Afrika imeshindwa kusimama yenyewe?
Kama bado, kwanini? Kwa sababu gani Afrika yenye umri wa mtu mzima mwenye wajukuu, kuendelea kuwa tegemezi kwa wakoloni tuliofukuza miaka 50 iliyopita, tukisema walitudhoofisha? Kwanini Afrika imeshindwa kusimama yenyewe?
Kulianzishwa
juhudi za makusudi kuhakikisha
yanaundwa mashirika ya kutukomboa kiuchumi. Mashirika hayo ya kiuchumi
ni pamoja na Jumuia ya Uchumi Afrika Magharibi(ECOWAS), ya Kusini mwa
Afrika(SADC), Jumuia ya Afrika Mashariki inayoharakishwa kuwa Umoja wa
Afrika Mashariki(EAC) n.k.
Julai
9, mwaka 2002 Ukaanzishwa Umoja wa Afrika(AU), lengo likiwa kuona
Afrika inakuwa Nchi moja, pengine yenye nguvu za Kiuchumi, Kijeshi na
Kisiasa kama Marekani, United States of America.
Afrika
yenye utajiri wa rasilimali: Ardhi, mito , maziwa, bahari, milima
mirefu, mabonde, watu wenye nguvu na akili nyingi, madini ya kila aina
na yenye thamani n.k imesalia duni, watu wake ni
fukara, tena hawana chakula, kuna maradhi ya kuangamiza kila ustaarabu
wa Mwafrika, Afrika imesalia Bara la Giza , pasipo tumaini.
Afrika
ina ukubwa wa maili za mraba 11,667,000(kilomita za mraba 30,218,000).
Kuna milima mirefu sana kama Mlima Kilimanjaro wenye urefu wa futi
19,340 sawa na mita 5,895. Mlima Kenya una urefu wa futi 17,058 sawa na
mita 5,199.
Kuna maziwa makubwa kama Victoria,
lenye ukubwa wa maili za mraba 26,418, Tanganyika (maili za mraba
12,700), Nyasa(11,430); kuna mito kama Congo , Limpopo , Zambezi , Niger
, Nile , Orange , Senegal na mingine kama Kagera, Tana, Ruvuma n.k.
Bonde la Mto Nile hujumuisha nchi za
Misri,Sudan,Ethiopia, Kenya, Tanzania, Uganda, J K Congo, Eritrea, Rwanda na Burundi.
Hata
hivyo, Afrika ilikuwa ikikatazwa na mikataba ya kikoloni kama ule wa
mwaka 1929 uliokuwa ukizikataza nchi hizi kutumia maji ya Ziwa Victoria
ama Mto Nile kwa miradi ya kilimo, bila idhini ya Misri na washirika
wake!
Afrika kuna madini: Asilimia 70 ya almasi
yote Duniani hutoka Afrika(J K Congo, Afrika Kusini , Botswana ,
Namibia , Ghana , Angola na Tanzania ). Asilimia 55 ya dhahabu yote
Duniani hutoka Afrika: Afrika Kusini , Ghana , Zimbabwe , J.KCongo, na
Tanzania .
Afrika
kuna Nickel au shaba , kuna Tanzanite inayopatikana Tanzania tu(lakini
Kenya inaongoza kwa mauzo Duniani, na Marekani , India , Japan n.k
hufuata). Afrika kuna mafuta, Nigeria , Libya , Algeria na Misri na nchi
nyingine kama Tanzania , Kenya , Uganda , Zanzibar ziko katika mchakato
wa kutaka kuchimba mafuta na gesi.
Kuna
madini mengine kama Ruby na Uranium. Uranium yanaweza kutumiwa kwa
nishati ya umeme, na wala si kutengeneza mabomu ya Nyuklia pekee.
Wamiliki wa madini haya, mafuta, mbuga za wanyama, shughuli za utalii
n.k ni wageni, wakoloni wetu wa zamani, Waafrika, hususan weusi ni
watazamaji na washangaaji wa utandawazi na sera zake za uporaji
rasilimali.
Naam, Afrika bado inawategemea akina Tony Blair
kuunda Tume zao za kuchunguza umasikini wetu, ili ripoti iwasilishwe kwenye Mkutano wa Mataifa makubwa ya viwanda(G-8) ili isaidiwe.
Afrika
bado hakuna utawala wa sheria, hakuna amani, ni vita na machafuko kila
kunapokucha. Rushwa imefanywa kama biashara. Afrika ni kichwa cha
mwendawazimu, kila tapeli hujifunzia kwetu.
Matapeli
wa Ulaya hunufaishwa na rasilimali za Afrika kwa miradi ama bidhaa
feki,tena hewa! Miradi hii ni kama Richmond , IPTL, Rada na mingine
mingi. Afrika ina makovu usoni yanayongoja akina Tony Blair, George W.
Bush pengine na Gordon Brown, ili kuyatatua!
Waafrika,
wanapopigana wao kwa wao, kama J.K
Congo , Sudan , Somalia , Sierra Leon, Rwanda , Burundi n.k Umoja wa
Afrika huwasubiri akina Bush kulinda amani, au kulipa mishahara ya
askari wetu wanaokwenda kulinda amani! Afrika humtegemea Blair na Bush
kutupa silaha ama vifaa kwenda kulinda amani.
Ndio
hawa hawa wakoloni wanaochochea vita Afrika, ili Waafrika wapigane, wao
warejee kutubadilishia bunduki za rashasha
kama A K 47 kwa dhahabu kama si almasi! Juzi, vikosi vya Pakistan vya
Jeshi la Umoja wa Mataifa(UN) nchini Congo , walibabwa wakibadilisha
bunduki kwa dhahabu!
Yaani,
wageni hawa wanachochea Waafrika waendelee kuuana, halafu wao wawauzie
bunduki kwa kubadilishana na madini; dhahabu au almasi! Hali hii si
tofauti sana na Sierra Leone , ambako Waasi wa RUF wakisaidiwa na
Charles Taylor, walikuwa wakibadilisha almasi kwa bunduki. Katika
biashara hii haramu, Marekani haikosi kulaumiwa.
Wakati
wa mjadala mkali wa Filamu ya Mapanki(The Darwin’s Nightmare) ilielezwa
kwamba mabeberu wa Magharibi walikuwa wakibadilisha madini ama sangara
kwa bunduki! Watoto wa Afrika walikuwa wakiletewa bunduki toka Ulaya
ili wauane, wakati Ulaya walipelekewa zabibu, dhahabu, almasi na nyama
toka Afrika.
Naam, miaka 50 baada ya Umoja wa Nchi Huru za Afrika kasha Muungano wa Afrika, bado tunawategemea akina Blair na Bush kutupa fedha za Bajeti ili kuondopa kansa nyusoni mwetu.
Afrika ni Bara pekee fukara
sana Duniani kwa miaka 25 sasa, inajipatia chini ya asilimia moja kutokana na vitega uchumi vyake.
Watoto milioni 44 hawaendi shule; wengine wanakufa kwa njaa na vita vinavyochochewa na wageni ili waendelee kuiba madini.
Watoto milioni 44 hawaendi shule; wengine wanakufa kwa njaa na vita vinavyochochewa na wageni ili waendelee kuiba madini.
Afrika,
licha ya utajiri wa rasilimali zake, imeshindwa kabisa kuinua hali ya
maisha ya watu wake.Kupitia sera za ubinafsishaji katika mchakato wa
ukoloni mamboleo uitwao utandawazi, fursa zote wanarejeshewa
wakoloni.Afrika inasubiri kupangiwa kila kitu na Taasisi za Breton
Woods, kama IMF na Benki ya Dunia. Benki ya Maendeleo Afrika(ADF)
haijaweza kuwakopesha watu wa Bara hili kufanya miradi ya maendeleo, ili
kuondokana
na utumwa wa Taasisi zilizoundwa na Wazungu, kuwarejesha Waafrika
utumwani.
Kwa upande mwingine, miaka 50
baada ya Umoja wa Afrika, bado Waafrika hawana makazi, hawana maji,
hawana shule, barabara, hospitali na hata hawana tumaini kutokana na
biashara kusimamiwa na wageni kote Barani.Je, umoja huu ni mtego ama
mkataba wa faida?
Mbona dhahabu, almasi, tanzanite, sangara, wanyamapori wetu na misitu, havituletei neema?
Mbona wanaturoga kwa takwimu tu kwamba tunauza nje madini?
Misamaha ya kodi, mrahaba wa asilimia karibu na bure katika madini yetu, samaki na rasilimali zingine, vitatuepusha kula nyama za mbwa ili tusife njaa
Tanzania pekee miaka ya nyuma ilikuwa ikipoteza Dola milioni 200 kutokana na misamaha ya kodi kwenye dhahabu. Afrika inadanganyika kupakwa wanja wa mdomo, wakati ina kansa ya uso?
Mbona wanaturoga kwa takwimu tu kwamba tunauza nje madini?
Misamaha ya kodi, mrahaba wa asilimia karibu na bure katika madini yetu, samaki na rasilimali zingine, vitatuepusha kula nyama za mbwa ili tusife njaa
Tanzania pekee miaka ya nyuma ilikuwa ikipoteza Dola milioni 200 kutokana na misamaha ya kodi kwenye dhahabu. Afrika inadanganyika kupakwa wanja wa mdomo, wakati ina kansa ya uso?
Afrika
ipo miradi mingi ya wazungu ya Ukimwi, viwanda vya pombe, miradi ya
wakimbizi n.k ili isifike siku sisi wenyewe tusimame kujisimamia. Kauli
mbiu ya Afrika inahusu kuisimika Afrika kwa nguvu katika nafasi ya Dunia
kupitia mkakati bora wa Umoja wenye nguvu.
Juni
25 hadi Julai6 mwaka 2007, Wakuu wa
Afrika chini ya Mwenyekiti wao , Rais John Kufour(Mstaafu) wa Ghana ,
walikaa mjini Accra , kujadili serikali ya Afrika, yaani United State of
Afrika.
Itaweza kuondoa migogoro Afrika? Serikali mpya ya Afrika, itawakemea mafisadi, wala rushwa, madikteta, wezi wa kura na wanaokaidi Haki za Binadamu?
Baadaye, Kanali Muammar al Qaddafi naye aliiongoza AU kutaka Afrika iwe na serikali moja na taifa moja, United States of Africa, leo Qaddafi amewindwa na NATO na akapinduliwa na kukamatwa kisha kuuliwa kama Osama bin Laden.
Itaweza kuondoa migogoro Afrika? Serikali mpya ya Afrika, itawakemea mafisadi, wala rushwa, madikteta, wezi wa kura na wanaokaidi Haki za Binadamu?
Baadaye, Kanali Muammar al Qaddafi naye aliiongoza AU kutaka Afrika iwe na serikali moja na taifa moja, United States of Africa, leo Qaddafi amewindwa na NATO na akapinduliwa na kukamatwa kisha kuuliwa kama Osama bin Laden.
Serikali Mpya Afrika, inalenga kuikomboa Afrika mara ya pili kutoka utumwa wa utegemezi na
wizi wa rasilimali zetu?
Wapiga kelele wa Afrika, wazungumze juu ya ukombozi wa mara ya pili kutoka Ukoloni mambpleo,lakini wanaingia katika mtego ule ule wa ugomvi na kufarakana,fujo na mauaji sisi kwa sisi.
Wapiga kelele wa Afrika, wazungumze juu ya ukombozi wa mara ya pili kutoka Ukoloni mambpleo,lakini wanaingia katika mtego ule ule wa ugomvi na kufarakana,fujo na mauaji sisi kwa sisi.
Mwandishi wa makala hii hupatikana kwa simu 0754 324 074, 0786- 324
www.congesmrambatoday.blogspot.com
www.congesmrambatoday.blogspot.com
No comments:
Post a Comment