MIAKA SABA KAMILI
iliyopita,Kimbunga Katrina(unaweza kuita Catherine au
Katarina),kiliyakumba maeneo ya Pwani ya Ghuba yenye utajiri wa
nishati,nchini Marekani.
Ilikuwa Jumapili,Alasiri
majira ya saa 10. Ilikuwa siku ya Agosti 28. Mamlaka ya Hali ya
Hewa(National Weather Services) ikaonya raia wan chi hiyo juu ya
janga la Kimbunga Katrina kuvuruga eneo hilo,hususan New Orleans.
Agosti 30; saa 7:30 usiku,
tayari maji ya Ziwa yakisombwa na kimbunga kikali,yalishavuka kingo
na kuingia mitaani, ambako yaligharikisha watu.
Barabara Kuu ya
London(London Avenue) hapo New Orleans, zilipokuwa kingo zenye kimo
cha futi 300 zikagharikishwa na mawimbi yenye kubeba maji,yaliacha
makazi yake ya kawaida na kuhamia mjini.
Miundombinu kama umeme
ikaharibiwa vibaya,kukawa kiza totolo. Mawimbi ya maji yenye kina cha
futi hadi 10 yakagharikisha mji, wakazi wengi wakakwea katika mapaa
ya nyumba zao ili kujiokoa,wakisubiri msaada.
Msomaji, piga picha ya
Gharika ya Nuhu mwaka wa BC 4000,kasha tazama kilichotokea miaka saba
kamili iliyopita huko New Orleans.
Ilikuwa Agosti 28 hadi 30,
mwaka 2005.
Katrina, iliwafanya raia
25,000 wa New Orleans kuwa wakimbizi katika mji wao
wenyewe,wakalazimika kukwea katika mapaa ya nyumba zao,kusubiri
uokozi.Maji yenye kimo cha futi hadi 10 yalikuwa yakiotea maisha yao.
Hiki ni kiama cha Katrina
ama ‘Katarina’. Jumanne, Agosti 28 mwaka huu, Historia ikajirudia
wakati na mahali pale pale, safari hii wanakabiliwa na kimbunga
Isaac.
Nataka kukwambia
msomaji,zamani vimbunga vikibatizwa majina ya akina mama, Hellen,
Katrina,Katarina,Mitch n.k. Akina mama wa Haki za Wanawake wakaja juu
sana,kusema kwanini majanga yanabatizwa majina ya wanawake?
Ndiposa, utasikia kuna
Hurricane Isaac, Robert, Andrew ,Charles n.k
Sasa huko Louisiana na New
Orleans, tunasikia kuna Kimbunga Isaka. Hili ni eneo la njia ya
tufani na vimbunga,eneo la Kusini na Mashariki mwa Marekani.
Ni eneo lenye mito mikubwa
duniani,kama Mississippi, ambao ni wa kwanza kwa ukubwa hapa Duniani.
Unafuatiwa na Nile,unaoanzia Owen Falls, Jinja nchini Uganda,
unasafiri kilomita 6,900 hivi hadi Misri.
Naam,kufuatia
Katrina,visiwa jirani na New Orleans vilizama penye kinamansi.Maeneo
oevu ya ya Ghuba hii ya Pwani ya Marekani,yakazamishwa na kina cha
maji cha futi 30 hivi.
Mto Mississippi,
ukatapika maji, na Ziwa Pontchartrain,Kaskazini mwa mji likamwaga
gharika mjini. New Orleans uko chini ya usawa wa Bahari.
Tufani ama kimbunga chenye
kasi ya maili hadi 165 kwa saa,hadi kufika Agosti 31 mwaka huo 2005
kilishabeba mawimbi ya maji yenye futi hadi 29,mji ukazamishwa,uchumi
na biashara vikatiwa kiharusi.
Bidhaa zikapanda bei
kupindukia. Paketi ya sigara iliuzwa sasa kwa Dola 10(sawa na
shilingi 16,000 za Tanzania),magereza yakasombwa na maji,malango
yakafunguka,wafungwa na mahabusu wakajiendea zao.
Wahalifu walianza kutamba
mitaani. Sasa,kama maofisi ya serikali,polisi na mahakama
yaligharikishwa maji,mafaili yakasombwa na mafuriko,hata kama
ukikutana na kibaka au jambazi aliyetoroka jela,ungemkamata tena ili
ukamshitaki kwa ushahidi upi,midhali vielelezo vilishasombwa na
mafuriko?
Wahalifu walipotoroka
gerezani, wakasomba silaha zilizoachwa nyuma na skari, wakaanza
kufanya vitu vyao! Askari na raia wote walitoroka.
Nataka nikwambie msomaji.
Serikali ya Rais George
W.Bush ililaumiwa sana kwa kushindwa kuokoa maisha ya Watu Weusi
wengi. Helkopta za uokozi zilipofika eneo lile zikawatupia kamba
Wazungu kwanza,Weusi masikini wakaachwa!
Mji wenye wakazi 500,000
zoezi la uokozi likafanywa kwa misingi ya ubaguzi wa rangi, ambao
hata sasa ungalipo.Waliuanza akina Adolf Hitler, wakaja makaburu wa
Afrika ya Kusini,hata sasa akina Samuel Eto’o Fils wanaushuhudia
huko Ulaya,na Olimpiki huko London kulikuwepo hali hiyo.
Uhalifu ulikuwa
mkubwa,magenge ya wakora yakanyatia polisi na kuwapokonya
silaha,bunduki na vilipuzi.Polisi nao waliasi kazi yao wakaanza
kupora kilichoachwa na Katrina-wengine walikwenda kuangalia majumba
yao na familia zao. Kumbe, wewe siku ya kiama utakumbuka kazi?
Nimesema,wafungwa
magerezani walitoroka wakaingia mjini,mafaili na vielelezo vya
ushahidi vilishasombwa na maji.
Makao Makuu ya Jeshi la
Marekani(The Pentagon) yalikuwa chini ya Ronald Rumsfeld wakati huo.
Yakalaumiwa kwa uzembe wa
kushindwa kuokoa watu na mali zao.
Huko Marekani, unapotaja,”
Hollywood” unazungumsa burudani; ukisema Wall Street unasema Pesa,
sasa ukisema eneo lililokumbwa na Katrina, maana yake ni mahali
inapopatikana nishati.
Katrina,ilileta kiharusi
kwa uchumi wa Marekani.Takriban asilimia 60 ya mafuta yanayoingizwa
Marekani,huingilia maeneo haya ya Ghuba ya Marekani.
Viwanda vya kusafisha
mafuta viko huko,uchumi wa taifa hilo ukatikiswa Agosti 28-31 mwaka
2005.
Niandikapo hapa,leo ni
Agosti 29,miaka saba kamili baada ya Katrina. Leo katika eneo
hilo,tarehe kama ya mwaka huo, kimbunga kingine sasa kilichobatizwa
jina la mwanaume, Isaka, kinalikumba eneo hilo!
Agosti 28-31 kimbunga
Katrina kikalikumba eneo hilo, leo tarehe hizo hizo,kimbunga Isaac
kinarejea nyuma kupitia njia yake.
Nataka kusema kwamba,
Historia inakawaida ya kujirudia-rudia.Yaliyotokea zamani, siku
huenda na kupita,hujirudia tena, nataka tujifunze Historia.
Nimerejea jambo hili,ili
msomaji wangu abaini kwamba mambo ya usoni yalishatokea huko
nyuma.Hata wanasiasa ghiliba tupu walishakuwepo huko nyuma,
yaliyowapata,yalitokea kutufundisha sisi wa sasa.
Ndiyo maana kichwa cha
makala haya hiutwa, “LEO NI JANA YA KESHO!”.Hakuna jambo jipya
hapa duniani. Suruwali za kubana zilikuwepo zamani, vijana wakora
walikuwepo,tabia mbaya ya kutoheshimu serikali na mamlaka ilikuwepo
tangu zama za Kaini!
Kaini, ndiye mwanzilishi
wa wakora na magangwe.Biblia,katika kitabu cha Kohelethi au Mhubiri
husema kwamba:
“Pepo huyarudia
mazunguko yake na mito hurejea inakotoka; wala hakuna jambo jipya
chini yajua”, Mhubiri 1:6-10.
Huyu Mhubiri, ambaye ni
Mfalme Suleiman mwana wa Mfalme Daudi wa Yese,(Tazama Mhubiri
1:12),aliishi kati ya mwaka 965-926 BC.
Msomaji mmoja ananiandikia
kwamba nirahisishe lugha ili wasome watu wa kawaida pia.
Hata hivyo, hiyo miaka ya
Kabla ya Kristo(Before Chris) inapungua na AD inaongezeka. Tujifunze
historia.
Kiwango cha elimu cha huyu
mtu aitwaye Suleiman, au nimwite Prof. Solomon, kilikuwa cha juu
sana, Falsafa yake ni kwamba mambo mengi hapa duniani hujirudia rudia
sana,yalikuwepo na yatakuwepo,ndiyo maana Leo ni jana ya kesho!
Tawala katili sana leo
duniani,zilishakuwepo hapo zamani sana,zikatoweka zitakuja nyingine
na kutoweka kama upepo.
Walikuwepo akina Julius
Caesar,Augustus(27BC-14 AD),Caligula(AD 37-41), hata watu wakawaabudu
kama miungu, akina Tiberius, wakati ule wa sensa, wakati Yesu
anazaliwa.
Sensa ipo hata sasa, na
watu wanasusa kwamba ni kinyume cha dini! Hata Yesu alihesabiwa,
maana Mariam mamaye alihesabiwa akiwa mjamzito wa kujifungua.
Tiberius alikusanya kodi
kubwa Rome hadi kufikia kama dola za Marekani1,700,000 katika mji
mmoja.
Walikuwepo akina Kaisari
Nero waliowakata vichwa mitume wa Yesu, watakuwepo wengine wakatili
kama hao. Gidion M. anatwambia jambo hili kwa kina.
Mathayo alichunwa ngozi
akiwa hai, Thomas alichomwa mkuki huko India, Marko alifia Ethiopia,
Mathayo alifia Alexandria,Misri,Luka akafia Ugiriki, Yohana
alichemshwa katika pipa la mafuta,Petro alisulubiwa kichwa
chini-miguu juu! Hapa ni mjini Rome.Yakobo alifia mjini Yerusalem n.k
Wamekuwepo hapa duniani
akina Farao,Nebchadnezzar, akina Malkia Cleopatra wa Misri.Hata sasa
kuna hadithi za kuhusu huyu mwanamama mrembo sana labda kuliko wote
duniani.
Historia inasema Malkia
Cleopatra aliwachanganya wanaume wawili wakuu sana-Julius Caesar na
Marc Anthony.Alitumia udhaifu wa ngono wa wanaume kuwamaliza,halafu
yeye akajiimarisha madarakani.
Kuhusu ngono, akina baba
wenye misuli na maarifa katika medani ya vita kama Julius Caesar, ni
dhaifu kwa wanawake- Strongest But Weak!
Cleopatra alikufa mwaka wa
BC 30,hakuacha hata maandishi yake. Cleopatra, “The Last Queen of
Egypt” ilidhaniwa kifo chake kingekuwa mwisho wa Misri?
Hata leo, wametoka akina
Gamal, akina Hosni Mubarak wako kolokoloni wakiwa mahututi,lakini
akina Mohamed Mursi, wapo!
Watu hutoweka na wengine
huja-hakuna mtu wa kudhaniwa mungu hapa duniani.
Cleopatra, alitumia mwili
wake kwa ghiliba ya ngono,kama silaha mithili ya misaili.
Hata leo wapo akina Joyce
Banda,leo ni kama jana.Wamekuja akina Joyce BANDA wanatumiwa na
madola makubwa kwa kisingizio cha demokrasia. Wameruhusu ushoga, sasa
wanataka kuchukua ziwa Nyasa lote ili makampuni ya Marekani,Uingereza
na Ufaransa wachote mafuta na gesi humo. Watu kama yeye wamekuwepo
zamani!
Namwonya Rais Jakaya
Kikwete, asiwasikilize sana hawa wakoloni,ni laghai na wasaliti,
wanajifanya rafiki,kumbe wafitini na wana hila.Tumkumbuke Julis
Caesar eti aliuliwa sababu ya udhaifu wa hila za mwanamke.
Nawaonya wanasiasa wa
Afrika. Wakiloni leo wanajidai kupromoti Demokrasia,kumbe leongo lao
ni kuchochea vurugu na vita Afrika, nchi inaposalia katika miali
mikali ya moto na mtutu wa bunduki,wao wachote rasilimali na
kuondoka!
Shime, wanasiasa hata wa
upinsani wasidhani wanatafuta haki na demokrasia,kumbe wanasababisha
nchi zetu zisitawalike.Wakoloni wametoka Libya, walikowachanganya
vichwa vijana wasio na ajira, wametoka Irak, sasa wako Syria baadaye
watakwenda Iran.
Wanaharakati wanalipwa
hela eti kuhamasisha demokrasia na haki za mashoga, wajiulize Yule
wanayemtumikia kwa yakini. Harakati siyo mbaya,ujira wa kufanya hivyo
wanatoa wapi?
Baadaye, watalipa nini?
Haya ya njama za akina Cleopatra kwa akina Julius Caesar na Marc
Athony yalishakuwepo mahali pengi duniani. Tuitazame historia.
Leo ni kama jana tu-Leo
ni jana ya kesho,leo na jana havina tofauti.
TAMATI
0786 324 074
Naomba coments zenu na nitaziheshimu kwa ajili ya wasomaji wengine
ReplyDelete