KIMSINGI,tunakubaliana hapa kila mtu kwamba,
sisi tuna matatizo.
Kila mtu ni chimbuko la shida yake mwenyewe,ingawa ziko
shida zinazoletwa na matokeo ya uchaguzi mbaya wa wenzetu.
Mabaya
yaliyotendwa na jirani,matokeo yake yataathiri wengine-tunashiriki dhambi na
matokeo ya dhambi za watu wengine-corporate sins.
Hii ndiyo dunia tuishiyo.
Maisha
yamekuwa magumu, watu tunakata tamaa, si kwa sababu Mungu kapenda; ni tabia
mbaya na uchaguzi wetu wenyewe, wa wenzetu ama sote tunashiriki kuchagua jambo
baya,kwa kujua makusudi,au kwa kutokujua. Mungu halazimishi watu kuchagua jambo
lolote.
Mungu hakutuumba kama treni,lisivyoweza kuamua
pa kupita,hata kama reli imefurikishwa na maji au imebomoka. Mungu hakutuumba
kama misukule ama zombies. Alimuumba Lusifa kama kiumbe mkamilifu, Lusifa
akachagua kuasi-Hii ndiyo tamu- chungu ya demokrasia.
Mmomonyoko wa maasili tunaolilia sasa,
haukujileta wenyewe kama mashine inayojiendesha yenyewe, automatic machines,mabaya
yanaletwa na mimi,na wewe na mwenzetu mjinga Fulani, n.k
Rushwa,
ufisadi,wizi wa mali ya umma,uporaji,ujambazi,ushoga,ulawiti, hata virusi vya
Ukimwi na Ebola, vimefanywa kwa mapenzi ya watu wenzetu,wakapandikiza kwa jamii
ya sokwe-si Mungu aliyeleta Ukimwi,Ebola na Magonjwa ya hatari.
Sisi wenyewe
ndiyo chimbuko la matatizo yetu-kila mtu anachangia kwa kiwango chake,mwisho wa
siku, mawimbi madogo madogo ya uhalifu na dhambi huwa mawimbi makubwa
yanayogharikisha kizazi chote.
Fanya zoezi
hili; nenda baharini inapokuwa tulivu,shwari. Nenda hata ziwani au katika dimbi
la maji tulivu,tupa kijiwe kidogo tu ndani ya maji tulivu. Unaona nini? Mawimbi
madogo madogo yanatembea pole pole,hatimaye huwa makubwa sana na matokeo yake
hatuyajui.
Ukipora mke
wa mtu, matokeo ya dhambi hiyo huyajui. Labda watoto wake waliokosa malezi ya
mama,watakuwa wavuta bangi,wabwia unga na wezi! Sasa, utalalama, ‘matoto ya
siku hizi’ pindi wakikupora mitaani usiku?
Watoto wa
mitaani, wametoka wapi? Kosa ni lao wenyewe au la serikali? Ni kosa la nani
kama siyo la jamii hii ovu?
Naam, dunia
ina shida sasa. Tatizo ni jinsi ya kuondoa shida hizi.Wengine wanapendekeza
tupigane vita kama Rwanda(mwaka 1994) au kama Burundi, Somalia n.k
Wengine
wanapendekeza itumike njia ya mapinduzi ya kijeshi kuondoa mafisadi! Hawa
hawajui, fisadi siyo mtu mmoja-ni mfumo,ni kizazi kiovu,utaondoa huyu, atakuja
mwingine mwovu kupindukia.
Kwamba
wanaojenga matabaka miongoni mwa walionacho na wasionacho, watu wasio wazalendo,
wasiojali utaifa wauawe!
Katika
mfululizo wa makala haya,nimetangulia kueleza namna watu walivyowahi kupinga
dhuluma katika nchi hii, tangu zama za Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Nyerere..
Nimeeleza
ndege ilivyotekwa nyara na vijana waziba viraka vya matairi ya gari,
wakailazimisha kwenda London.
Tukio hilo
la kwanza la aina yake hapa nchini,liliunganishwa na harakati za siasa za
Mkimbizi maarufu wa Tanzania, Oscar Salathiel Kambona.
Kambona,
akiwa London alikanusha kujihusisha na utekaji nyara ndege hiyo. Baadaye,
Kambona alirejea Tanzania wakati wa mfumo wa vyama vingi,mwaka 1992.
Ilisemwa,
Kambona hakuwa raia wa Tanzania, alikuwa raia wan chi ya Joyce Banda, anayekuja
pupa na atavuna pupa.Ameruhusu ushoga, sasa anataka Ziwa Nyasa-Pato la Pupa!
Kambona
hakuzaliwa Malawi. Alizaliwa Agosti 13, mwaka 1928 huko Kwambe,jirani na Mbamba
Bay,Mbinga.Ni Kusini mwa Ziwa
Tanganyika. Alikufa baadaye mjini London mwaka 1997,Julai.
Kwa faida ya wasomaji, iko siku nitasimulia
kisa cha ugomvi wa Kambona na Nyerere. Kwanini alikuwa Waziri wa kwanza wa
Mambo ya Nje kama Mzee Bernard Membe leo, halafu akaja kusemwa siyo raia?!!
Msomaji,unapaswa
kufikiri. Usiwe kama dodoki; unalishwa kila jambo,unakubali na kuanza
kulalama,hujui ukweli ni upi.
Jifunze kufikiri,usijifunze kusema na kusoma!
Tunajadili
chimbuko la shida,ufisadi,unyama,rushwa,madaraja kati ya walionacho na
makabwela-watoto wa masikini, ambao mwisho ni watawaliwa na watumwa wa milele.
Haya hayako
Tanzania tu. Wanaotaka kujitoa mhanga, wasubiri kidogo tuwaambie. Chanzo ni
watu kuukataa ukweli,na haki. Nimejadili sana ukweli ni nini,kulingana na
mwanafalsafa mkuu wa pili duniani, Aristotle.
Mwingereza,
George Orwell, alishaandika kabla sijazaliwa kejeli(satire) iitwayo SHAMBA LA
WANYAMA.Aliandika kuhusu viongozi waliochaguliwa kuanza kujiona wao ni bora
kuliko wananchi wanaoongozwa. Kumbuka aliandika yaliyotokea Uingereza, siyo
Tanzania.
George
Orwell, aliandika namna viongozi wa SHAMBA LA WANYAMA, akina Mzee Nguruwe,
walivyoanza kukiuka AMRI,Katiba,makubaliano waliyojiwekea, wakaanza kushibisha
matumbo yao, bila kujali raia.
Hizo Amri
zilizomo katika Animal Farm ya George Orwell,ndiyo MAADILI tunayosema
yameporomoka.
Nani hutaka kufuata sheria pasipo
kushurutishwa?
Asilimia 30 ya watu hufuata sheria kwa sababu polisi,wapo na
mahakama zipo na sheria ni kali. Asilimia 65 ya watu hawataki kutii sheria hata
mahakama zikiwepo na polisi wakiwepo.
Ni asilimia 5 tu ya watu walio tayari kuishi
maisha adili hapa duniani hata kama mahakama na polisi wasipokuwepo. Mtu hakulipi
haki yako hadi umburuze kortini?
Yooo! Mawe!!
Halafu mnasema maadili! Kutii bila shuruti. Kutii taratibu,kanuni za maisha,kufuata
sheria-bila shuruti, unazifuata?
Maadili ni
nini?
Maadili,kwa Kiingereza, “ETHICS” katika Uandishi wa Habari kwa mfano,ni
Kiwango cha ubora wa Tabia kilichowekwa ili jamii ifuate na kuishi hivyo.
Kwa
Kiingereza, Ethics is a Standard of Behavior. Maadili ni tabia njema.Sasa
jifunze kufikiri vizuri kwa kichwa, siyo kwa tumbo. Maadili mtu huzaliwa nayo?
Kila mtu ana
kiwango bora cha tabia? Unakuwa na kiwango bora cha tabia kutoka wapi?
Viongozi wa
dini wanataka viongozi wa serikali wawe waadilifu; wawe na kiwango bora cha
tabia njema-A high standard of Behavior!
Viongozi wa
dini,ni waadilifu?
Wanataka watu wengine wawe waadilifu sana, wakati wao sasa
ni kituko,ni waovu sana,wako chini ya kiwango cha ubora wa tabia njema.
Wanataka mtu
mwingine ashike maadili, sheria,kanuni ambazo wao wamezihalifu sana. Huu ni
unafiki, Ufarisayo,ushetani na upofu-soma Mathayo 23:13-36.
Maadili
mema,huletwa na mtu kujitambua kati ya mema na mabaya.”
To distinguish between Right and
Wrong, or in some cases, between two wrongs”
Sasa,nani
atakuwa tayari kusema ubaya kwa jina lake halisi na ukweli kwa jina lake
halisi?
Si ndiyo
siasa hizi? Mnatambua makosa,mbona mwatetea watoto kuwa mashoga? Nani
anawajibika kwa makosa yake?
Maadili,maanayeke
ni kila mtu kuwajibika kwa kosa lake.Wajibu ni deni.Wajibu ni kila mtu kuwa na
deni-Under Obligation-Wanaoongoza kulaumu wenzao, hawatambui wajibu wao,ila
kusukumia wenzao lawama. Mtu mzembe,fisadi, ni mwepesi na fundi wa
kukosoa-Criticism.
Alhamisi,Aprili
Mosi mwaka 2010,gazeti la Rai liliandika makala yenye kichwa, “Matendo ya ‘kishetani’
yalichafua Kanisa Katoliki”.
Makala hiyo
iliandika tabia ya makasisi wa Kanisa Katoliki kulawiti watoto wa
kiume,wanaosoma katika shule za kikatoliki duniani.
Papa Benedicto
XVI amekuwa akienda kila mahali duniani na kuomba radhi kwa matendo hayo.
Kuomba radhi hutokana na kukiri makosa-yapo yanatendeka kweli,na amewaomba
msamaha waathirika, siyo wahanga.
Sasa,
wasikie makasisi wa Kanisa hilo wanavyomkosoa sana Rais Kikwete na serikali
yake kwa ufisadi,utadhani ufisadi ni kupora fedha za umma tu,kumbe na kulawiti
watoto chekechea ni kitu gani? Soma Wagalatia sura ya 5.
Siyo Kanisa
Katoliki tu,takriban viongozi wa dini zote,wengine hujiita Manabii na
Mitume,wachungaji sijui watumishi,masheikh,maimam- miongoni mwao ni wakora,
matapeli na mawakala wa shetani.
Ni waporaji
wa zaka na sadaka za waumini,wanajilisha na kondoo wa Bwana wao, wanachagua
kondoo walionona, wanakula polepole, wamevunja ndoa za watu n.k
Juzi,
nikisikiliza highlights za magazeti,nikasikia Kiongozi mmoja machachari anayefanya
miujiza hadi anafananishwa na Mungu, anashitakiwa na waumini wake kufakamia
mali ya kanisa kama yake binagsi!!
Jamani,
anaikosoa serikali huyu hadi anataka ipinduliwe! Sasa unajiuliza: Hini ‘Unethical
Practices” ni nini kama siyo wizi,utapeli, ulawiti,uzinzi,uporaji wa zaka na
sadaka za waumini n.k?
Nadhani, hata viongozi wa kidini akina
Vibwetere hawa,hawajui Dhambi ni nini? Hawajui kwamba Dhambi ni Uasi wa Sheria
ya Mungu(Amri 10 zinazokataza uongo,wizi,uzinzi na ufiraji).
Gidion M. anaandika kwamba hawa jamaa wa dini
hutumiwa na Freemasons,halafu wanakuwa wakali kama pilipili.
Sijasema
wasiikosoe serikali. Nasema hawa wanajidai kuujua ukweli,mbona kuna kashfa hizo
hadu juzi BBC wametangaza Vatican inamburuza jamaa mahakamani kwa kuvujisha
siri za wizi! Naam, ufisadi Vatican?
Ukitazama
kwa jicho la tatu, sasa utaona si viongozi wa dini, siyo wanasiasa wala jamii
sote tumeoza-mafisadi tu-Soma Wagalatia sura ya tano.
Waandishi wa
habari na wahariri wao ni matapeli,iko siku nitasema ukweli.Manabii na Mitume
wa siku hizi ni wezi kuliko Yule wa Msalabani. Jamii imechafuka sasa.
Robert Charles Darwin, alisema kila mwenye
nguvu ndiye anayekula leo,wengine tunanyauka. Mbuzi hula kulingana na urefu wa
kamba yake;kamba ni madaraka,cheo hata cha kanisani na msikitini-ni uporaji
tu,kila Nyanja.
Hii Falsafa
ya Darwin ya Survival of the Fittest, inawafanya watu maskini kugeuka mbolea ya
kuwastawisha wakubwa na matajiri hapa duniani.
Siku hizi
hata makanisani na misikitini,ni kugombea madaraka-supremacy struggle-hakuna
anayekubali alichosema Mungu, Amri za Mungu, maadili,uzalendo,upendo,unyoofu
n.k Sisi sote tu waovu,wachafu,hakuna wa kujigamba.
Hakuna wa
kumcheka mwenzie,tujisahihishe,tumeacha MAADILI.
Maadili ni
Ethics kwa Kiingereza. Waingereza wanasema,
Ethics is a system of principles that guides your conduct and helps you to
distinguish between Right and Wrong.
Nguvu
inayomtambulisha mtu mazuri na mema,ni ya Roho Mtakatifu, sasa hawa jamaa wa
dini hawana Roho Mtakatifu,bali Roho Mtakavitu!
Kutambua mema na mabaya huja kwa njia ya
SHERIA YA MUNGU,sheria ya Mungu, Amri 10 za Mungu ni kioo cha kutuonesha
tongotongo!
Tumekataa
Amri 10 za Mungu tangu ngazi ya familia,tutakuwaje raia wema,viongozi wema au
tukapa rais mwema?
Sisi ni
waovu, hatutaki ukweli na haki. Nani atunza sheria ya Mungu moyoni?
Tumebaki kulalama,na kutafuta kugombana kwa
vita ili kuondoa shida miongoni mwetu. Hii wanafalsafa wanasema ni kutafuta
njia ya kumkimbia Shetani kwa kuomba hifadhi ya ukimbizi kwa Lusifa!
“Looking a way from Satan, and seeking refuge from the
Devil!”
Itaendelea
0713 324 074
No comments:
Post a Comment