TAI NI
NDEGE, anayeruka juu angani, umbali wa futi 10,000 ambazo hakuna ndege mwingine
aweza kufika.
Kwa sababu
hiyo, ndege tai ana uwezo wa kuona mbali kiasi cha kushangaza.Aweza kuona
mawindo akiwa mbali huko angani. Tunafundishwa sisi wanadamu kuona mbali
mithili ya ndege huyu. Tujifunze kufikiri kuliko kusema na kusoma, lengo ni
kupima faida na hasara ya kila jambo katika maisha.
Watanzania,
tumefika hapa tulipo kwa sababu hatuwezi kuona mbali kwa faida yetu.
Tumewaachia wafadhili na watu wengine kufikiri kwa niaba yetu-makosa makubwa.
Jicho la mtu halikuoneshi wewe hatari inayokukabili.
Sasa,
wasomaji wataniuliza:Wawezaje kuona mbali mithili ya ndege tai? Jibu ni rahisi.
Unatazama jana ili kujua ya kesho. Unatazama historia. Historia hutuonesha
kesho kuna nini?
Historia,
hutuonesha kesho kutatokea nini. Historia ni muhimu katika maisha. Historia
hutuambia siri za siku za usoni.
Mwandishi wa Kiingereza, George Orwell,ambaye
jina lake halisi ni Eric Arthur Blair, aliwahi kuandika hivi:
“He, who
controls the past, controls the future. He who controls the future, controls
the Present”
Tafsiri
yangu isiyo rasmi ni kwamba George Orwell,Yule mwandishi wa kejeli(satire) ya
SHAMBA LA WANYAMA, alisema hivi:
“Anayetawala
Historia,hutawala pia siku za usoni; na atawalaye siku za usoni hutawala hata
leo”.
Anaongeza kusema, “Today was Yesterday’s Tomorrow”-leo ni jana ya kesho!!
Anaongeza kusema, “Today was Yesterday’s Tomorrow”-leo ni jana ya kesho!!
Ndicho
kichwa cha makala haya,kutuonesha kwamba leo ni jana ya siku za usoni. Usione
leo ukadhani utakuwa hivi hivi kesho,leo itapita na itakuja kesho usiyodhani.
Ukitaka kujua ya kesho,tazama jana na leo-tafakari,jifunze kufikiri kwa kina.
Naam, leo
ilikuwa jana ya kesho.Ninapotazama historia nawaona watu wanaorejea tabia na
makosa ya jana.
Dola ya Rumi,
ilipinduliwa zamani kwa sababu ya ulevi,kukosa uzalendo,rushwa,ufisadi, raia
kupenda starehe na anasa, na hata leo Tanzania tunarejea yale yale tu.
Watu
wanafanya makosa yaliyowahi kutendwa katika historia, watu huchagua kufanya
yale yale yaliyofanywa katika historia,na hata kesho haina tofauti kubwa. Vita
vilikuwepo na hata sasa na kesho vitakuwepo,kwa sababu watu huyarejea yale
yaliyotendwa katika historia.
Historia
haiwarogi watu hata wayatende yale ya kale. Hatutaki kujifunza Historia,hatujui
na hatujui kuwa hatujui,ndiyo maana tunafanya makosa yaliyofanywa katika
historia.
Laiti tungejifunza Historian a kubaini makosa
ya wenzetu wa juzi na jana,leo tungetenda tofauti na kwa umakini na hekima.
Jumatano,
Agosti 22 mwaka huu, nilikuwa nikitazama kipindi cha STRAIGHT TALK AFRICA cha
Sauti ya Amerika(VOA) juu ya kifo cha Rais aliyekuwa Rais wa Ghana, John
Atta-Mills.
Nilitazama
kuapishwa kwa Rais Mpya, John Dramani Mahama, mahojiano kati yake na
Mtayarishaji wa kipindi hicho, Dk. Shaka Ssali, kwamba anaapishwa kumalizia
miezi mine iliyobaki,hadi kufikia Uchaguzi Mkuu.
Nikamaizi kuwa, Rais Mpya wa Ghana, John
Mahama, anafanana sana na wenzake waliomtangulia katika Ikulu ya mjini Accra.
Marais wote
waliapa kuiongoza vema Ghana;wote waliapa kuwajali raia,kuiendeleza nchi kwa
usawa na kutokuwa na upendeleo.
Naam, akina
Jerry John Rowrings ,John Kufour,John
Atta=Mills, na sasa John Dramani Mahama-naam,ni Ghana na utawala wa akina John!
Majina ni yale yale, watu walewale,kasoro ni
mbwembe za kuapishwa,suti walizovaa na wapambe waliowazunguka-maisha yale
yale,mambo yale yale tu,hakuna jipya.
Tujifunze
kuchungulia nyuma katika historia. Wanasiasa wakubwa siyo watu wa
kutegemea,kutumaini na kuegemea. Tunapaswa kuwatii,kuwaheshimu na kuwanyenyekea
kwa sababu wanashikilia mamlaka ambayo ni mithili ya upanga. Lakini siyo
kuwatumaini.
Mwanamuziki,
Roger Whittaker, alishaimba kwamba wanasiasa ni mithili ya ndizi mbivu katika
chane: Wote ni njano, wameshikilia pamoja,wanakula pamoja,wana rangi
moja,lakini hakuna aliyenyooka hata mmoja!
Nataka kuwaonya Watanzania wanaodhani
wanasiasa ni “Truvada” (dawa mpya ya Ukimwi iliyovumbuliwa),kwamba watamaliza
matatizo yao,wanajidanganya kuliko kawaida.
Watu wakubwa
wengi wamepinda mithili ya ndizi, hawana maadili. Wakisemacho hawakitendi na
wakitendacho sirini,hawakisemi. Wanapoapishwa,husema wataitii sheria na Katiba
ya Nchi, mara waingiapo madarakani,hujikuta wakitenda tofauti na walivyoapa.
Sasa, utaona watu wakivuja jasho jingi
kusukuma magari yao,kutandika mavazi yao chini,ili hawa mashujaa wao, “Role
Models” wapiti juu yake. Wengine wamefariki dunia kwa kukinzana na mamlaka kwa
sababu hao mashujaa wao wameagiza wafe!
Maisha yako ni ya thamani kuliko ya mwenzako.
Wanasiasa hawa watakuja na kuondoka,lakini
shida zetu zitabaki ikiwa sisi wenyewe hatuwezi kukaa na kutazama namna ya
kuziondoa.Wanasiasa wana kiu ya madaraka,na wala hawana nia ya kututumikia
mithili ya mshumaa. Mshumaa, hujiteketeza wenyewe kwa nia ya kuwaangaza
wengine. Nani mwanasiasa mshumaa?
Akiwepo
kiongozi mshumaa(na hayupo) huzimika mara kunako tufani. Elton John aliimba
kwamba , “Candle in Wind” mshumaa kunako upepo, wakati wa mazishi ya Princess
Diana, unakumbuka?
Naam, Candle in the Jungle!
Mshumaa mwituni,
utawaka,kunako tufani? Hata Princess Diana hajawahi kuwa mwema mithili ya
mshumaa,kujiteketeza wenyewe kwa nia ya kuwaangaza wengine? Huu ni Upendo wa
Agape.
Wanasiasa hawana upendo wa Agape.
Wanaweza
kuwaona raia wao mithili ya familia zao ama watoto wao wa kuzaa. Huu ni upendo
uitwao kwa Kigiriki, Philos,Phileo ama Philia.
Wengine wana
upendo wa kitoto,Storge, na wengine wana tamaa na ashiki za kimwili,Eros ama
Erao ambazo huzitumia kupora wake za raia wao na kuondoka!
Nakwambia
ukweli msomaji,amini usiamini. Usiwaamini wanasiasa hata ukajitoa mhanga
.Usifanywe ngazi ya kupandia ama kukwelea mamlakani,usigeuze mabega yako kubeba
wanasiasa hawa-heri kubeba zege,ili upate mlo wa usiku, sembuse wanasiasa hawa?
Watakuja na kuondoka,dhiki zetu zitabaki. Tena
wengine watakuja na kupandikiza chuki na ukabila kama Kenya,watawaachia
wananchi vita,umwagaji damu na visasi vya kurithi.
Mwanafalsafa
wa Athens,Ugiriki,Salon anasema hivi:
“The law is
like spider’s web. The small are caught ,but the great tear it up!”
Tafsiri
yangu:Sheria ni mithili ya utando(mtego) wa buibui,wadogo hunaswa
humo(wanyama,wadudu n.k)
Lakini,
wakubwa huutatulia mbali na kujiendea zao pasipo madhara yoyote! Nataka nikwambie
msomaji,watu wakubwa mnaowategemea(mnasukuma magari yao na kutandaza mashati na
khanga za akina mama ili wapiti juu yake) ni wahalifu sana. Hawana maadili
myoyoni mwao bali midomoni.
Wakubwa,
hujidai kuwapenda raia wao. Raia wako tayari kuwafia wanasiasa wao,lakini
wanasiasa ni nadra kufa kwa ajili ya raia.Wanakubali wafe kwa sababu ya tamaa
ya madaraka,na aslani siyo kwa ajili ya kuwapenda raia.
Kwa
wanasiasa,wanapokuwa akigombea uongozi,raia ni ngazi zao za kukwea uongozini.
Pindi wanapopata madaraka,raia hugeuka shubiri,mizigo ya kuwahoji kutimiza
ahadi. Raia hugeuka ‘adui’ za wenye mamlaka.
Sasa, nani
alikufa kwa ajili ya adui zake. Labda tusome Warumi sura ya 5,kwamba ni Yesu
aliyekufa kwa ajili ya adui zake!
Viongozi wengi wanaponyatia madaraka,hujidai
wema mithili ya mishumaa.Lakini pindi waingiapo mamlakani,hugeuka
mangimeza-hutawala kwa kutoa amri na
shuruti wakiwa mezani,kuliko kusikia kilio cha wananchi.
Uadilifu
hauji kwa maneno ya mdomoni,bali matendo yatokayo moyoni(Mathayo 21:23-32) hii
ni kusema, “To walk the talk”.
Watu wakubwa
sana duniani ni dhaifu kupindukia-Strongest but weak.
Nakusudia
kuchungulia historia ya watu wakubwa duniani kama Julius Caesar, Pharao wa
Misri,Malkia Cleopatra wa Misri, Kaisari Nero, Mfalme Herode,George Washington n.k
Hawa wote
walikuwa wavunja sheria,ambao kama umma ungemaizi, walistahili kukatwa vichwa
kwa uhaini, lakini kwa sababu ya wapambe, walishangiliwa sana.
Leo, nawashauri wasomaji wangu kuwaheshimu
wenye mamlaka(Warumi 13) ili ujiongezee uhai. Ni upumbavu wewe mwenye mawe
kujibizana na polisi wenye SMG zenye risasi za moto,ukijidai Mfalme Daudi kwa
Goriathi. Usijidanganye mwanaharakati kumtupia jiwe polisi mwenye silaha.
Mwanamuziki
Muhiddin Gurumo, na wenzake waliimba hivi zama za Ndekule:
“Usimkaribie
chatu, ooh chatu wee; gongo usimtupie utaukosa ushindi! Natoa onyo kwa yeyote
anayemchezea chatu, ni hatari, atakuja askikose lolote la manufaa na ajali
imkute bila ya kutegemea, atakuja adhirika ajute na duniaaa!”
Wanasiasa ni
chatu,hasa wawapo mamlakani. Ukitumwa kuwatupia gongo,ukinaswa na chatu mwenye
kiu ya damu,umejitoa kafara mwenyewe.
Najua watu
wajinga wapo wengi wenye kuchochea wenzao wafe ili wapige kelele nyingi kwamba
Haki za Binadamu zinavunjwa. Kila mtu atazame haki yake ya uhai kwanza.
Mara
nyingi,hawa wapiga domo wanaoitwa wa Haki za Mashoga, haki za akina mama, haki
sijui za Binadamu,huwavisha ngozi za kondoo raia wanaopenda kukaa-kaa vijiweni
saa za kazi, ili wakararuriwe na wanyama wakali!
Nawashauri watu kuwa ‘Busy’ na mambo yao na
kazi zao,tuachane na Politiki saa za kazi,maana hakuna mtawala atayekuja
kutugawia sembe na maziwa kila nyumba,bila kufanya kazi
Kanali
Muammar Gaddafi, alikaribia kuwagawia maziwa raia wake kila subuhi,lakini wapo
waliomkana, akauzwa kwa Wamarekani, na sasa yuko Kaburini, mtoto wake,Saif
al-Islam anakabiliwa na kitanzi.tazama historia ili kujua kesho.
George
Orwell anawafananisha nguruwewa SHAMBA LA WANYAMA na viongozi na unyama wao dhidi ya raia waliojidai
kuwapenda sana.
Mwanafalsafa
wa Ugiriki, Salon amewafananisha viongozi ho na wanyama wakubwa
wanaoichanachana sheria na katiba ya nchi na kujiendea zao wanakofuata maslahi
yao.
Sisi wadogo
ndiyo tunaswao na sheria. Usidanganywe kuvunja sheria na watu wakubwa-utanaswa
wewe wao watabaki. Utazame utando wa buibui ujifunze somo hili,wanaonaswa humo
ni akina nzi,mbu,sisimizi n.k Lakini,wakubwa hujiendea na kuuchana utando huo
wa bui bui. Tembo atanaswa katika ‘spider’s
web’?
Wakubwa
hukiuka maadili,na kwao si hoja.Hawnaswi na mkono wa sheria,hujiendea zao
salama. Usipoteze muda kuhoji jambo hilo,kafanye kazi zako, maana ni
historia,,bishana nayo upoteze muda na maisha bure!
Nawe wataka
kuvunja sheria za nchi?Wewe ni nzi, utanaswa katika mtedo wa
buibui(sheria),katika tawala za dhuluma, sheria wamewekewa wanyonge-wewe na
mimi, kutii ni njia ya kuokoa maisha,amini usiamini.
Tunisha
misuli uone,kesho utakuwa mshumaa katika tufani-Candle in Wind!
Usifuate
maoni ya watu wengi wajinga, Public Opinion. Jihadhari na maneno ya kijiweni.
Usimtupie fimbo chatu,utajuta. Utaumia. Usiwatupie polisi mawe wakiwa na
bunduki,utavuja damu puani. Usitumiwe kama kinyangarika.
Duniani,viongozi
wenye upendo na raia wao wanapokuwa madarakani,siyo wengi. Kiongozi hupenda
enzi na mamlaka yake kuliko raia,kuliko mke na wanaye. Sembuse wewe?
Nikupe
mfano. Karibia miaka 2,500 iliyopita,Mwanafalsafa aitwaye Euripides wa Ugiriki
aliandika kisa cha Admetus mfalme wa Thesaly kukabiliwa na mauti,hadi apatikane
mtu wa kujitoa mhanga ili afe badala yake.
Ndugu
zake,marafiki na baba na mama yake walikataa kufa kwa ajili yake. Ni msichana
mzuri,mpenzi wake aliyeitwa, Alcestis aliyekubali kufa badala ya Admetus.
Itaendelea
0786 324 074
No comments:
Post a Comment