‘mungu’ wa Equatorial Guinea anayekula
‘nyeti’ za wapinzani wa serikali yake!
TEODORO OBIANG
NGUEMA MBASONGO, alitawazwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Guinea ya Ikweta Agosti 3,
mwaka 1979,kufuatia mapinduzi dhidi ya mjomba wake,Marcias Nguema Biyogo.
Nguema Mbasongo,ni
miongoni mwa viongozi wa kiimla hapa Barani Afrika, ambao viongozi wa Magharibi
humfananisha na Robert Gabriel Mugabe wa Zimbambwe, “Zim Country”
Ni mpwa wa Rais wa
Kwanza,Dikteta Fransisco Marcias Nguema Biyogo, alimpindua kupitia jeshi mwaka
1979 ambao hapa Afrika ulikuwa mwaka wa anguko la madikteta.
Baada ya kukanyaga
Ikulu,akatangaza kupitia redio ya taifa kwamba sasa yeye ni ‘mungu’ ambaye anao
uwezo wa kula maini na hata makende(testicles) ya watu wanajitia kichwa ngumu
kumpinga!
Guinea ya Ikweta,ni
taifa dogo la watu kama 500,000 hivi.Ukubwa wan chi hii ni maili za mraba
10,800 katika Ghuba ya Guinea.
Alizaliwa Juni 5,
mwaka 1942; akawa rais Oktoba 10, mwaka 1979 kupitia mapinduzi ya kijeshi
katika taifa hili lililopata uhuru wake Oktoba 12,mwaka 1968.
Huyo mjomba wake,
‘Masie’ alikuwa pia mbabe sana aliyeisababishia nchi kufilisika. Ndipo Agosti
1979 Teodoro Mbasongo akaongoza Mapinduzi ya kijeshi, akapiga marufuku nyama
vya siasa.
Hii
Guinea,huzalisha sana mafuta hapa Afrika; ni kama nchi ya tatu hivi nyuma ya
Nigeria,na Misri.Na Wazungu huitamani hata walitaka kumpindua mwaka 1994
akanusurika.Waliofanya njama ni pamoja na mtoto wa Waziri Mkuu wa zamani
Uingereza, Margaret Thatcher, Sir Mark Thatcher.
Nchi ni tajiri
sana,watu wake ni masikini sana, nadhani msomaji umewahi kusikia ‘laana ya
rasilimali’-The resources curse!
Hata hivyo,Jarida
la Forbes limemtaja Teodoro Nguema miongoni mwa viongozi matajiri sana hapa
duniani;utajiri wake ukifikia Dola za Marekani milioni 700.
Utajiri huo
unafuatiliwa na Shirika la Kupambana na Rushwa, Transparency International ili
kubaini mahali alipouficha Ulaya.
Hivi sasa
inasekemekana anaugua saratani. Katika viwango vya Utawala Bora na Haki za
Binadamu vinavyotolewa na Mo Ibrahim, alipata asilimia 46 kati ya nchi 54 za
Umoja wa Afrika.
Nchi hii haina
uhuru wa habari kama huku kwetu;kuna rushwa kupindukia.
Kuna redio moja tu
ya taifa inayotegemewa na watu kupata habari.Sasa kama hujipendi nenda
ukapeleke maneno huko uone cha mtema kuni!
Unakatwa ‘nyeti’
zako halafu zinawekwa kwenye friji,kabla ya kuliwa baadaye!
Alipata alama 34.7
katika viwango vya Mo Ibrahimu vya Utawala Bora.Mwaka 2003, katika kipindi cha
redio ya taifa kinachoitwa, “Bidze-Nduan” tafsiri yake Kuzika Moto!
Kipindi hiki cha
redio ya taifa huhimiza amani,utulivu na kuheshimu mamlaka katika nchi,
ilitangazwa kwamba Rais Teodoro Obiang Nguema Mbasongo sasa anawasiliana na
Mungu moja kwa moja!!
Kwamba Rais alikuwa
na mawasiliano ya Mung Mwenyezi moja kwa moja.
Radio hiyo ilisema
kwamba rais Teodoro ni kama Mungu wa mbinguni, ambaye anayo mamlaka yote juu ya
wanadamu na viumbe wengine.
“Ana maamuzi ya
kuua chochote,pasipo yeyote kumuuliza,kwa sababu yeye pia yu mungu”,Tangazo la
redio hiyo lilisema.
Mwandishi wa
Shirika la Utangazaji la Uingereza,BBC,Angue Nguema, akasema kwamba redio hiyo
ya taifa husikilizwa na raia wengi kwa kuwa hakuna redio nyingine na hakuna
utitiri wa magazeti kama hapa Tanzania.
Nguema amekuwa
akishinda chaguzi kwa asilimia 100.MHULA WA UCHAGUZI HUKO HUCHUKUA MIAKA
SABA.Mara ya mwisho uchaguzi ulifanyika 2009;na utafanyika tena 2016.
Wasaidizi wa rais
huyu husema kwamba, ana nguvu za miungu ndani yake-redio huwaonya watu
wanaotaka kuondoa amani ya nchi wachukue hadhari-watakiona cha moto, ‘nyeti’
zao zitang’olewa na kuwekwa kwenye friji kasha kuwekwa kwenye sahani za ‘State
House’.
Hivi sasa Obiang
ana umri wa miaka 71; na ametawala kwa jumla ya miaka 32.
Mke wake anaitwa
Constancia,ambaye ni miongoni mwa wake za Marais wa Afrika, “First Ladies”
wanaoponda sana maraha,yeye na Mke wa ‘RG’Mugabe,Grace.
Mugabe alikuwa Rais
Zimbabwe tangu 1987,kabla ya hapo alikuwa Waziri Mkuu.
Gazeti la East
African la Desemba 27 mwaka 2011 likamweka Rais huyu miongoni mwa marais
madikteta watano wabaya Afrika
Wengine
waliorodheshwa chini ya kichwa cha habari, “THE LEAGUE OF EXTRAORDINARY
DICTATORS”ni pamoja na Omar Ahmed Omar Hassan al-Bashir, Mugabe,Isaias Afwerki
wa Eritrea,Laurent Gbagbo sasa yuko rumande The HAGUE.
Nchi zinazoongoza
kwa utawala Bora hapa Barani ni Mauritius,Cape
Verde,Botswana,Ghana,Namibia,Afrika ya Kusini,Seycheles,Sierra Leone,Mali sasa
imetiwa doa na vita ya wenyewe kwa wenyewe na Tanzania.
No comments:
Post a Comment