Utawala wa
Makaburu(Boers)ulikumbatiwa na Uingereza na Marekani;wakati watu zaidi ya
14,000 (Weusi)walipouliwa huko Zulu,katika miaka ya 1980.
Tumeona
Mobutu akisaidiwa na mataifa haya ambayo siku hizi hujidai ‘Masihi’ hapa
duniani,na huimba demokrasia na Haki za Binadamu kwa midomo bila vitendo.
Mobutu,na
hawa,waliwasaidia Waasi wa Angola kukipinga Chama cha Ukombozi, Popular
Movement for the Liberation of Angola(MPLA),uhuru usipatikane kutoka kwa
Wareno,hadi nchi ikabaki vitani kwa muda mrefu.
Mobutu na
hawa rafiki zake, Ungereza na Marekani, walimsaidia Jonas Malheiro Savimbi na
Chama chake cha Unita, kilichopinga uhuru wa Angola.
Tumeona
harakati za uhuru nchini Afrika ya Kusini chini ya African National Congress (ANC)
zikiwa zimeharamishwa na utawala dhalimu sana wa Makaburu hadi Rais De Clerk
alipokuja kuondoa marufuku hiyo Feburuari 1990
“Tata”Mandela
aliachiwa huru kutoka Greza la Victor Verster, lililopo Paarl Feburuari 11
mwaka 1990. Ni tukio la kihistoria kuachiwa kwa Mandela; ni kama Afrika ilipata
uhuru mwaka 199
Mtu huyu, “Tata”
Mandela,alitangaza msamaha kwa Makaburu waliomtesa; ikaunfdwa Tume ya Ukweli na
Maridhiano(THE TRUTH COMMISSION) iliyoongozwa na Askofu Desmond Tutu.
Mandela alikiri
chama chake (ANC) kuunda tawi la jeshi(Umkontho we Sizwe) kwa nia ya kujilinda
na kujihami dhidi ya siasa za ubaguzi wa rangi; siasa zilizoandamana na dhuluma
na mauaji ya kinyama dhidi ya wazalendo na harakati za ukombozi.
Mandela na
De Clerk walitunukiwa baadaye tuzo ya Nobel ya Amani,mwaka 1993.Aprili mwaka
huo 1993 ndipo Mpigania uhuru Chris Hanni alipouliwa na utawala wa
Makaburu,rafiki wa Uingereza na Marekani.
Mandela,
ameishi siku zote kama Mwafrika halisi; akachaguliwa kuwa rais mwaka 1994 akiwa na umri wa miaka 77-na alistaafu mwaka
1999 akamwachia kiti Thabo Mvuyelwa Mbeki,mmoja wa wana wa mashujaa wa
mapambano dhidi ya Kaburu jeuri.
ANC
kilishinda uchaguzi wa 1994 kwa asilimia 62 ya kura.Mandela aliapishwa kuwa
rais wa Kwanza Mweusi Mei 10,mwaka 1994,wakati Kiongozi wa National Party, de
Clerk akiambulia Umakamu wa Kwanza wa rais;wakati Thabo Mbeki alipopewa Umakamu
wa Pili katika serikali ya Umoja wa Kitaifa.
Naam,
tunamkumbuka ‘Tata’Mandela kwa mashati yake ya Batiki. Ama ‘Mandela Shirts’
yanayovaliwa siku hizi hata na akina Rais Jakaya Kikwete.
Uchaguzi wa
kwanza huru Afrika ya Kusini ulifanyika Aprili 26-29,mwaka 1994,ANC kikapata
asilimia 62,National Party cha Makaburu kikapata asilimia 20.4.Inkhata Freedom
Party cha Chifu Mangusuthu Butelezi kilipata asilimia 10.5.
‘Tata’
Mandela alipata kuoa mara tatu; ni baba wa watoto sita,wajukuu 22 na vitukuu
vingi. Mmoja wa wajukuu zake ni Chifu Mandla Mandela.
Mzee huyu
kipenzi cha Afrika alifunga ndoa ya kwanza na Evelyn Ntoko Mase kutoka kwao
Mandela huko Transkei.Walikutana Johannesburg-walizaa wavulana
wawili,Thembikile ama Thembi mwaka 1946,Magkatho alizaliwa 1950 na wasichana
wawwili waliopewa jina moja,Makaziwe, “Maki” mmoja alizaliwa 1947 na mwingine
1953.Mwingine alifariki dunia kabla ya kufikisha umri wa mwaka mmoja.
Ndoa ya
Mandela na Evelyn Mase ilivunjika baada ya miaka 13(mwaka 1957),Mandela alikuwa
haonekani nyumbani kwa muda mrefu,akiwa ‘Msituni’katika harakati za
Ukombozi,mama huyo na imani yake ya kilokole ya Mashahidi wa Jehova, aliamua
kwenda zake,akaachana na Mandela.
Thembi,
alifariki katika ajali ya gari mwaka
1969 akiwa na miaka 25 wakati huo Mandela alikuwa selo, Robben Kisiwani.Hawa
watoto walisoma shule moja,baadaye Evelyn alifariki dunia 2004.
Ndoa ya pili
ya Mandela ni ya Winnie Madikizela-Mandela, huyu ‘Iron Lady’ kutoka
Transkei.Watoto wa Mandela na Winnie ni wasichana wawili:Zenani au
Zeni(Feburuari 4,1958) na Zindzishwa ama Zindzi aliyezaliwa 1960.
Walitengana
Aprili 1992; mwaka 1996 waliachana kabisa.Juzi, Winnie alikwenda
kumtembelea Mandela hospitalini
anakolazwa.
Kaka mkubwa
wa Mfalme wa Swaziland,Mswati III,Prince Thumbumuzi Dlamini alimuoan Zenani
mwaka 1973,na wanaisti Boston,Marekani.
Mwaka 1998,Mandela
alimuoa Graca Machel nee Simbine wakati alipokuwa akiadhimisha ‘Birth Day’ ya
80.
Mwaka
2003,Cable News Network(CNN) walitangaza tanzia ya Mandela.Mwaka 2007 pia ‘wasela’walitangaza
kifo cha Mandela,wakiwataka Wazungu kwenda kwao,la sivyo wangechinjwa!
Mtu huyu, ‘Tata’
Nelson Mandela ni kielelezo cha Mzalendo wa kweli,Mwanahalisi wa Afrika
aliyeitwa ‘Gaidi’ na utawala wa Makaburu wa Waziri Mkuu PW Botha, aliyejiuzulu
Agosti 14, mwaka 1989 ndipo akaingia De Clerk aliyemwachia huru Mandela.
Utawala wa Makaburu uliua watu wengi,si Afrika
Kusini tu bali hata Msumbiji walifanya njama na kumuua Samora Machel mwaka
1986.
Naam,namkumbuka
‘Tata’Mandela, ambaye namba yake ya jela ilikuwa 46664. Tunawakumbuka
wanamapinduzi wa Afrika ambao wamemwaga damu wakipigania uhuru wa watu wao, si
ulaji wa matumbo yao kama watu wengine
wanavyotaka kuitwa leo.
Namkumbuka
Samora Mises Machel,John Garang de Mabior ‘ Chris Hani na wenzao.
Obama
anapokuwa Dar es salaam wakati huu makala hii inapachapwa gazetini,nataka
kumwambia kwamba aslani asiweze kusahau hujuma kama hizi na zile za Kanisa la
Aglican,za kuwaweka mhuri wa moto mgongoni Waafrika wenzetu waliofanywa
watumwa-The Transafrica Slave Trade-waliobandika mihuri ya society migongoni!
Napenda
kumwambia Barak Hussein Onyango Obama,kwamba urais wake Marekani umekuja baada
ya harakati za ukombozi za akina Mandela, Malcom X,Martin Luther King Jr, na
wenzao ambao walijikuta wakiuliwa na Pentagon ama kufungwa maisha kwa uhaini.
Wakati Obama
anapojitia kushutumu tawala za kiimla, Authoritarian regimes, asisahau kwamba
serikali ya nchi yake imekiuka haki za msingi za Weusi kwa kuwaunga mkono
majambazi kama Savimbi,majeshi ya Makaburu,Wareno na makampuni ya kifisadi
kuihujumu Afrika.
Nigeria kwa
mfano, inasemwa Boko Haram wameua watu 1000 wakati ukweli ni kwamba hata
makampuni ya mafuta ya Magharibi kama Elf,Agip, Royal/Dutch Shell,Chevron n.k
wamehujumu raia wa Niger Delta,waliodai haki zao zama za utawala wa Dikteta
Sani Abacha,ambaye wao walibeba sana kwenye mbeleko hadi akawaua akina Ken
Saro-Wiwa.
Makampuni ya
Marekani,Ufaransa na Uingereza yameua watu wangapi Kusini mwa Nigeria
kulinganisha na Boko Haram? Zaidi ya dola bilioni 400 za mafuta zimeporwa na
makampuni hayo tangu zama za uhuru hata sasa huko kwa Waogoni,Igbo,(Biafra) na
Yoruba.
Obama,
anapozungumza utawala bora na demokrasia ana maana gani kama makampuni ya
Magharibi yanashiriki unyonyaji, na dhuluma hapa Afrika?
Itaendelea
0713 324 07
www.congesmrambatoday.blogspot.com
No comments:
Post a Comment