WAZIRI Mkuu wa
Ethiopia,Meles Zenawi, alikufa Ughaibuni mwaka jana,akaisababishia majonzi
makubwa Marekani,kuliko Afrika!
Mwaka 2011
na 2012, Afrika iliondokewa na viongozi wake:Nigeria,Zambia,Malawi na hata Kanali
Muammar al-Qaddafi,aliuliwa na Waasi waliojiita Baraza la Mpito,Libya
waliosaidiwa na Marekani.
Kati ya
Julai na Agosti,mwaka jana,Zenawi na Rais wa Ghana,John Atta-Mills waliaga
Dunia.
Wamarekani
wakaangua kilio kikubwa kwa Zenawi kuliko Atta Mills! Inasemwa Ghana inaongoza
kwa upevu wa demokrasia Kusini mwa Jangwa la Sahara; na inasemwa,Ethiopia ni
miongoni mwa nchi zinazoongoza kwa kubinya demokrasia na uhuru wa watu kusema.
Vyombo vya
habari Uhabeshi vimewekwa rumande,na sauti ya umma haisikiki; la sivyo
waandishi wa habari watakabiliana na mkobo wa chuma na magari ya deraya ya
kijeshi.
Wamarekani
wakamwombolezea sana Zenawi;wakasema:
“Alileta
maendeleo makubwa ya uchumi Ethiopia”, wakabwabwaja!Zenawi alikufa katika umri
wa miaka 57,alitumiwa na Magharibi kama chambo cha kuondoa utawala wa adui
yao,Kanali Mengistu Haile Mariam.
Huyu Meles,
aliongoza Waasi wa Tirgrayan People’s Liberation Front ili kumpindua Mengistu
mwaka 1991 akatimkia “ZIM CONTRY” kwa
Robert Gabriel Mgabe.
Magharibi
wanamsifu sana Meles kwamba alifanya ndege ya uchumi kupaa kwa asilimia 10 kwa
miaka mine mfululizo.
Hata hivyo,
hizi ni takwimu za makaratasi,uhalisia wa mambo huko Addis Ababa, umasikini
umeshamiri miongoni mwa raia wa kawaida,licha ya mabarabara na hospitali
kujengwa katika kipindi cha Meles Zenawi.
Alitawala
Ethiopia kwa mkono wa chuma;vyama vya siasa vilitiwa kabala,watu 200
walipojidai kuandamana na kuunga mkono Upinzani,wakafyekwa kwa risasi!
Chama
chake,Ethiopia People’s Revolutionary Democratic Front(EPRDF)mwaka 2010
kilishinda viti vyote vya Bunge dogo,kasoro viwili. Kilipata viti 547.
Laiti
CUF,NCCR ama CHADEMA wangekuwa Ethiopia zama za jamaa huyu, halafu wakajidai
kuandamana na kumpinga,polisi ama jeshi wangefyatua risasi na kuua waandamanaji
maelfu,Marekani ikiwa kimya!
Naam,
Ethiopia ni miongoni mwa nchi zenye jeshi kubwa sana hapa Afrika;na hutumia
asilimia kubwa sana ya Bajeti yake ya nchi katika shughuli za jeshimkuliko
elimu,afya na huduma za jamii.
Ethiopia,
Meles alishinda uchaguzi kwa asilimia 99 za kura zote,wapinzani wakiwa kimya
mithili ya maji mtungini!
Sijui
kwanini Marekani,Uingereza na Ufaransa hawakumkemea kwa ‘uhuni’ sampuli
hiyo,badala yake wakawa wanambeba kwenye mbeleko na kumfanya ‘msemaji’ wa
Afrika!
Ulinzi
ulikuwa mkali kuwakata ngebe wapinzani wa serikali yake katili. Huyu na Isaias Afwewerk
wa Eritrea(watu wao hutoroka nchi kila siku kukimbilia Ughaibuni),lakini
alikuwa mboni ya jicho la Marekani.
Kama kuna
nchi iliyogawanyika sana kwa misingi ya kikabila,kimajimbo,kikanda,kidini na
kimikoa ndiyo hii Uhabeshi.
Hata
hivyo,Masheikh,Maaskofu,Maimam,Manabii na Mitume kama hawa wa kwetu Tanzania,waliziba
midomo zama za Meles,wasije wakachukuliwa ndani ya ‘Buti’za gari za Usalama na
kupotezwa.
Umewahi
kusikia zama za Amin kwamba kulikuwa na The State Research Bureau? Kwamba waliwahi
kuwapoteza maaskofu ambao siku hizi wana midomo mipana hapa kwetu, kuikosoa
serikali na kuhamasisha migomo na maandamano?
Meles,
alikuwa mbabe, na wapinzani wake walikuwa wakikabiliana na mauti ya bunduki
kama ile ya Yoweri Kaguta Museveni(Seven Battalion), inayoitwa ‘Lwitabagomyi”
ama kiboko ya wanaojidai kugomea amri ya mamlaka!!
Meles,
alitoka kikundi cha Tigray, akawakata kauli makundi makubwa ya nchi hiyo, Oromo
na Amhara.
Alitumika
vilivyo kutuliza ghasiaUpembe wa Afrika(The horn of Africa).Majeshi yake
yaliingia Somalia mwaka 2006, ili kuwakata ngbe Waislam wenye msimamo
mkali,al-Shabaab.
Ni Meles huyu aliyetumika kuhakikisha Sudan ya
Kusini inajitenga na Khartoum ya Omar
Hassan al-Bashir ambaye anatakiwa na Mahakama ya mjini Hague kwa makosa ya
mauaji,husuan Darfur.
Mahakama hii
ambayo Umoja wa Afrika umeishutumu kwa kuitazama Afrika kama ‘target’ huku
ikiwaacha wauaji wengine wa Ulaya na MAREKANI,wahalifu wa kivita huko
Irak,Libya n.k
Wenye
mahakama hii iliyoundwa na Wakoloni,waliposikia kwamba Afrika imeanza
kuipinga,wakaona wamwondoe Louis Moreno-Ocampo wa Buenos Aires,wakamweka Fantou
Bensouda wa Gambia,ili kuwafanya Waafrika mbumbumbu waone Waafrika wanajaliwa!
The Hague,ni
mahakama ya kikoloni na yenye malengo ya kibaguzi na makengeza, ‘double
standards’ ndiyo maana Kenya wameamua akina Uhuru Kenyatta,Rutto na Arap Sam
washitakiwe mjini Nairobi, ama imependekezwa hata Tanzania!
Kwani Afrika
hakuna mahakama hadi Ulaya? Acheni ujinga!
Wazungu
wanasema,wakati Afrika ina ombwe(vacuum) la viongozi wenye mvuto, “Charismatic
leadership”,Meles alikuwa kiongozi mwenye mvuto mkubwa,akachaguliwa kuwa ‘Msemaji’
wa Afrika kila jambo!
Alialikwa
mikutano takriban yote ya G 8,G 20 na akatoa kauli katika mikutano hiyo ambayo
madikteta wengine wa Afrika,akina Mugabe,Gaddafi,Obiang Nguema Mbasongo na
wenzao hawakusogea.
Alitazamwa
mshirika mkuu wa Dola za Magharibi
katika medani ya amani duniani. Hata madege yasiyo na rubani ya
Wamarekani-Drones- yalitumia Uwanja wa ndege wowote Ethiopia,kufanya Operesheni
zao.
Sijui
unaelewa msomaji? Yaani,kama mtu angejidai kukiuka matakwa ya maslahi ya
Marekani huko Upembe wa Afrika na Kusini,yangetumwa madege hayo, akamwagiwa
mvua ya risasi na kusambaratishwa kutokea Ethiopia.
Haya madege
yaliipeleleza Afrika ili kujua kama kuna wanaharakati wanaoitwa Magaidi.
Magharibi
walimpenda Meles kiasi kwamba hawakuona makosa,aliwapa kila walichotaka,akaitwa
KIONGOZI WA KIZAZI KIPYA wa Afrika na Bill Clinton mwaka 1998.
Walimwombea
adumu uongozini hata miaka 100!! SIJUI unaelewa nini kuhusu Marekani kumwombea
mtu kudumu miaka 100 katika zama hizi za demokrasia?
Sasa utaona
ni kwanini Marekani inaomboleza baada ya mauti kumpokonya Meles Zenawi katika
umri mdogo wa miaka 57.Mwaka 2012 alipotembelea Washington akazungumza
angeachia madaraka 2015, akafikiria kufundisha katika shule yake ya Uongozi.
Wapinzani
walimwita katili katika masikio kiziwi ya Marekani na washirika wake wanaotetea
demokrasia duniani kwa mauaji ya akina Saddam na Gaddafi huku wakifunga watu
jela Abu-Ghraib na Guantanamo Bay,wakivamia nchi kama Syria na kusambaratisha
utu na amani.
Wazungu
walisema,Meles aliimarisha miundo minu na kuwapa maisha bora masikini wa
Uhabesbi!
Ethiopia ina
watu milioni 90;nchi ya pili kuwa na watu wengi Kusini mwa jangwa la Sahara.
Mwezi mmoja
baada ya Meles kuaga dunia Rais Atta-Mills wa Ghana akaaga dunia.
Hata hivyo
wazungu walimlilia Meles kuliko kiongozi wan chi ya Demokrasia kama Ghana,John
Atta Mills
Itaendelea
0786 324 074
No comments:
Post a Comment