Imethibitishwa na Ikulu ya Marekani kwamba
Obama na mkewe,Michelle,
watakuwa na ziara ya siku nane Afrika,katika nchi za Senegal,Afrika Kusini na
Tanzania.
Obama atafika DAR Julai Mosi
Amesita kwenda nyumbani Kwao,Kenya,kwa sababu huko kuna kilio cha makovu ya ukoloni waliofanya washirika wa Marekani,Uingereza, yaani Kenya imedai ilipwe fidia ya ukoloni.
babaye Obama(OBAMA sr) alifariki dunia Novemba 24,1982 kwa ajali ya gari.
HII SI MARA YA KWANZA Mwafrika kudai fidia ya ukoloni.
Amesita kwenda nyumbani Kwao,Kenya,kwa sababu huko kuna kilio cha makovu ya ukoloni waliofanya washirika wa Marekani,Uingereza, yaani Kenya imedai ilipwe fidia ya ukoloni.
babaye Obama(OBAMA sr) alifariki dunia Novemba 24,1982 kwa ajali ya gari.
HII SI MARA YA KWANZA Mwafrika kudai fidia ya ukoloni.
OMUKAMA(Mfalme) Solomon
I wa Bunyoro, Magharibi wa Uganda , alitishia kuidai serikali ya Uingereza
Pauni Trilioni 3.7; kama fidia ya mali iliyoporwa wakati wa ukoloni.
Mali hiyo,
ni pamoja na mifugo iliyoporwa miaka ya 1890 wakati wa utawala wa babu yake,
yaani Omukama Kabarega II.
Naam, wakati wa
vita vya miaka mitano.
Kama Mfalme
Solomon angefungua kesi hiyo, na mahakama ikampa ushindi, akalipwa hiyo fidia
‘nzito’ ya Pauni trilioni 3.7, miaka tisa iliyopita, serikali ya Uingereza
ingefilisiwa.
Raia
takriban 800,000 wa Bunyoro wangejipatia kitita cha pauni milioni 4.63
kila mmoja. Kiasi hiki mwaka 2004 kilikuwa sawa na shilingi za Uganda
bilioni 15.2. Siku hizi nikama shilingi za Tanzania bilioni 6.3 kila mmoja
Omukama Solomon alisema, kamwe hajawasamehe Waingereza waliomwandoa
madarakani babu yake, Omukama Kabarega II wa Bunyoro.
Alisema, waliiba ng’ombe wakati huo wa vita dhidi ya babu yake, walichoma moto
nyumba, waliharibu mazao na kuambukiza wanawake kaswende.
“Wanawajibika kwa
vifo vya watu milioni 2.4; zaidi sana waliiba ng’ombe wa babu yangu na pembe za
ndovu”, Mfalme Solomon alisistiza miaka michache iliyopita.
“Ni unyama ambao tusingetegemea ungefanywa na watu wanaojidai kustaarabika sana
. Walichofanya, hakina tofauti sana na wanavyotenda magaidi kama al
shabaab ama al-Qaeda leo”, akafafanua.
Alikuwa
amepata wanasheria ndani ya Uganda na Uingereza kwenyewe; akatarajia kesi
hiyo ya madai kuanza kusikilizwa mjini London mwaka huo wa 2004. Kiasi cha
pauni trilioni 3.7 za fidia kilibuniwa baada ya Katibu wa Mfalme huyo, Yolamu
Nsamba, aliyesoma uchumi katika Chuo Kikuu cha Hull , kufanya tathmini.
Mwaka 2004,
pato lote la Taifa(GDP) Uingereza, lilikuwa takriban pauni trilioni moja
kwa mwaka. Hivyo, fidia ya pauni trilioni 3.7 isingekosa kuifanya Uingereza
Muflis. Kama Ufalme wa Bunyoro ungeshinda ‘dili’ hiyo, kila raia wa Uingereza
angelazimika kukamuliwa pauni 60,000 ambazo ni zaidi ya milioni 144 za hapa.
Mchumi huyo
wa Ufalme wa Bunyoro alisema, kiasi hicho kilihusisha mali ya Mfalme iliyoporwa
na Wakoloni wa Kiingereza,mifugo, chakula, pembe za ndovu na akiba ya chumvi
iliyochukuliwa katika nyumba ya Mfalme.
Fidia hiyo
haikujumuisha fidia ya ardhi ya watu wote, hasa waliouliwa. Ilikisiwa, fidia ya
jumla ingekuwa mara 10 zaidi.
Mwanasheria
mwingine, Ernest Kizza, Spika wa Bunge la Bunyoro, aliingiwa kiwewe kwamba,
kama hawa Waingereza wangeshindwa kesi hiyo na kuamuriwa kulipa fidia, basi
uchumi wa Uingereza ungevurugika mno, kama chumi za Afrika ulivyovurugwa.
Kama
wasingeuchafua ufalme wa Bunyoro, Kizza alisema, basi leo ungekuwa taifa kubwa
duniani(Super Power); na kwamba wangekuwa na ubavu wa kuikemea Marekani
ikaufyata!
Mfalme Kabarega, alitekwa na Waingereza katika mapigano ya 1899, akapelekwa
uhamishoni, Seychelles , alikoishi kwa miaka 24. Wafungwa wenzake huko walikuwa
wafalme wa Ashanti ( Ghana ) na Bahrain .Siku hizi Ashanti ni kampuni ya
Mzungu.
Aliachwa
huru 1923, lakini akafia njiani wakati akirejea nyumbani Uganda , kabla ya
kufika jirani na mpaka wa Bunyoro. Ufalme wa Bunyoro uliharibiwa baadaye na
Rais Milton Apollo Obote katika miaka ya 60, ukarejeshwa na Rais wa sasa,
Yoweri Kaguta Museveni mwaka 1993.
Mfalme Solomon I alikuwa amekaa mamlakani miaka 14 tangu atawazwe, na
Wabunyoro wanalaani wizi wa Waingereza wa ng’ombe na mbuzi wao wakati wa
ukoloni; wanaona ndiyo chimbuko la ufukara wao.
Naam,
nimetangulia kueleza kisa hiki cha miaka minne iliyopita, kufuatia Kasisi mmoja
kuniandikia ujumbe kwa njia ya simu ya mkononi, kwamba niliwasingizia Wazungu
kuhusika na vita na umasikini wa Waafrika, hususan katika vita vya 1999 nchini
Sierra Leone .
Kwamba,
kama ni tamaa ya mali, watu wa mataifa yote, bila kujali kabila na rangi
walipenda mali na si Wazungu peke yao.
Alikuwa
akiilalamikia makala yangu iliyotokana na Filamu, “Blood Diamond”,
inayowashushua Wazungu kuchochea vita na machafuko Afrika, ili waendelee
kusomba rasilimali; mafuta, pembe za ndovu, almasi(kama ya Sierra Leone ),
dhahabu, samaki , ardhi kama ya Zimbabwe n.k
Hadithi ya Mfalme Kabalega wa Bunyoro na tishio la mjukuu wake kufungua kesi ya
madai mjini London , ni kielelezo cha namna ukoloni ulivyoidhalilisha Afrika;
na bado wageni hawa hawajatosheka kuinyonya Afrika, wanachochea vita,
fujo na mauaji, ili Waafrika tuuane, wao wakisomba utajiri wetu. Mafisadi,
madikteta na magaidi kama Osama bin Laden, wanawaandaa wao!
Juzi,Uingereza imekiri kuilipa serikali ya Museveni fedha hizi ambazo zilikuwa hazijafika Bunyoro,Uingereza ilikubali yaishe nje ya mahakama,na Kenya imerudia kutaka Uingereza kuwalipa Wakenya fidia ya utumwa.
Juzi,Uingereza imekiri kuilipa serikali ya Museveni fedha hizi ambazo zilikuwa hazijafika Bunyoro,Uingereza ilikubali yaishe nje ya mahakama,na Kenya imerudia kutaka Uingereza kuwalipa Wakenya fidia ya utumwa.
Ni
kwa sababu hii, tunamuunga mkono kwa dhati Omukama Solomon I wa Bunyoro, kuona
kwamba umasikini wa mtu mweusi haukujileta wenyewe; kuna mkono wa mtu,
anayestahili kufunguliwa mashitaka.Anastahili kulipa fidia, tena kufikishwa The
Hague kujibu mashitaka, sambamba na Taylor, Sankoh, Hitler, Milosevic n.k
Vita
vya Sierra Leone , vinavyosimuliwa katika filamu, ‘Blood Diamond’ vinaonyesha
mtu mweupe akifanya uchochezi ili viendelee.
Wakati
katika sura nyingine, Mataifa yenye viwanda(G8) ambayo yaliwahi kuigawana
Afrika mwaka 1884, yakijidai kuweka vizuizi eti almasi ya nchi hiyo
isiingizwe katika nchi zao…nikasema unafiki mtupu! Hivi, vitendo vya RUF,
al-Qaeda, na vile vya Waingereza dhidi ya Ufalme wa Bunyoro , Ashanti n.k, vina
tofauti gani?
Kasisi, alitaka kusema ufukara wa Afrika ni shauri yao wenyewe na upumbavu wao,
wakati makovu yapo yanaonekana; yalitokana na utumwa, ukoloni, vita
vilivyoletwa na hawa, wakavuruga tawala zetu, wakawateka viongozi wetu wa Falme
kama Ashanti na Bunyoro, wakawakata vichwa viongozi wetu kama Mkwawa na wengine.
Waliiba dhahabu, almasi, mifugo mingi….walibaka akina mama na kuwaambukiza
maradhi ya zinaa.
Walifanya
mengi yanayofanana sana na na yale ya Saddam Hussein aliyenyongwa,
magaidi kama al-Qaeda, au kuzidi. Baadaye, walikuja wakafungua ‘dirisha
dogo’ la misaada, wanawalazimisha viongozi wetu wa leo, wawapigie goti, ili eti
watupe msaada!
Afrika, madikteta
wengi wana mizizi yao kwa Wazungu. Jean-Bedel Bokassa, alikuwa na mizizi yake
kwa Wafaransa, kama alivyo Kanali Mohamed Bacar, aliyetaka kupora Anjouan.
Wafaransa haohao bado wana makoloni Afrika.Wamejificha katika vivuli vya hawa
vibaraka wao. Akina Dikteta Augusto Pinachet wa Chile walikuwa na mizizi
yao kwa wakubwa hawa.
Marehemu
Foday Sankoh, kiongozi wa waasi wa RUF wa Sierra Leone , waliokuwa wakikata
wananchi mikono, midomo na miguu kwa mashoka, alikuwa na mizizi yake kwa
Wazungu. Amini usiamini.
Charles Taylor, kiongozi wa zamani wa Liberia aliyekilea kikundi hiki nchini
mwake, alikuwa akifanya biashara haramu ya kutorosha almasi za Sierra
Leone hadi kwa Wazungu, huku mapigano makali yakiendelea.
Popay
Sankoh, aliyezaliwa Oktoba 17, mwaka 1937 alifariki Julai 2003, akiwa mahabusu
alikokuwa akisubiri hukumu ya kesi yake ya mashitaka 17 ya uhalifu wa kivita.
Alitiwa mbaroni mwaka 2000.
Hakuzaliwa akiwa katili na shetani. Alipata mafunzo ya vita vya msituni Libya ,
ambako alikutana na Charles Ghankay Taylor, aliyekuwa pia akiendesha vita vya
msituni dhidi ya utawala wa Liberia .
Wakati huo Rais wa Libya,Gaddafi alikuwa Mtu wao na walimtuma kuwafundisha jeshi Taylof na Sankoh,nadhani unajua Taylor alitoroshwa jela na CIA huko Boston.
Wakati huo Rais wa Libya,Gaddafi alikuwa Mtu wao na walimtuma kuwafundisha jeshi Taylof na Sankoh,nadhani unajua Taylor alitoroshwa jela na CIA huko Boston.
Baada
ya kupata mafunzo ya kijeshi na harakati za kijeshi nchini Libya , walirejea
Liberia mwaka 1990, wakafanya walivyofanya hadi Taylor akawa rais Liberia .
Baadaye, wakisaidiwa na Taylor, waliunda RUF kwa msaada wa biashara haramu ya
almasi walizouzia Wazungu, huku wakibadilisha almasi kwa bunduki.
Umoja wa
Mataifa, na Guinea kwa msaada wa hao Waingereza, wakaingilia kati mgogoro
wa Sierra Leone , ndipo vita vikakoma mwaka 2002.
Revolutionary
United Front(RUF) walijigeuza chama cha siasa kilichoitwa, RUFP, na kushiriki
uchaguzi uliofanyika miezi michache baadaye.
Popay
Sankoh, akiwa tayari katupwa kolokoloni, Almamy Pallo Bangura ndiye aliyegombea
urais kupitia chama hicho, wakaambulia asilimia 1.7 ya kura, wala hawakushinda
hata kiti kimoja cha Bunge.
Wakati kesi yake ilipokuwa ikiendelea mwaka 2002, Sankoh aliangua kicheko
mahakamani, bila sababu dhahiri na kusema: “Ninashangaa kuona nahukumiwa, kwani
mimi kiongozi wa dunia?”
Ni
kweli kwamba alikuwa na ugonjwa wa kiharusi, alikuwa akipelekwa mahakamani
kwenye kiti cha magurudumu. Alikuwa tayari dhaifu wa mwili na akili. Lakini,
kauli yake hii, ilikuwa aikihoji mambo Fulani yaliyohusiana na mashitaka yake
na Wazungu wanaojifanya viongozi wa dunia.Kwamba, yeye alikuwa nani kufanya
biashara hiyo bila Wazungu kuikubali?
Charles
Ghankay Taylor aliyewekwa kolokoloni mjini Freetown kwa miaka mitatu kabla ya
kupelekwa, The Hague Uholanzi, aliwahi kusema kauli kama hii, “Adui yako
anapokuwa ndiye Bosi wako(Marekani), basi wewe umekwisha”.Hawa jamaa, walikuwa
wakishangaa Wazungu kuwatosa, wakati walikuwa pamoja msituni.
Miongoni mwa mashitaka 11 yaliyomkabili Taylor katika Mahakama hiyo ya The
Hague, ni kushiriki vita Sierra Leone sambamba na waasi wa RUF, waliotuhumiwa
kubaka, kuua na kufyeka watu miguu, midomo na mikono kwa mashoka.
Tayari Taylor kafungwa Uingereza ili anyamaze kimya!
Tayari Taylor kafungwa Uingereza ili anyamaze kimya!
Lakini, kwa vyovyote, Ghankay Taylor na Popay Sankoh, walikuwa na sababu ya
kutaka kuwahusisha wakubwa wa dunia(Wazungu) na vita walivyopigana Sierra Leone
, unyama wao, mauaji na biashara haramu ya silaha, na almasi.Sina sababu ya kuchochea
ukabila, naweka mambo hadharani.
Waziri wa Sheria wa Sierra Leone , Frederick Carew, alisema: “Ushahidi tulio
nao ni kwamba Taylor alitumia almasi kuchochea vita na kuleta dhiki isiyosemeka
katika nchi yetu”.
Je, almasi aliiuza
wapi kama si alishirikiana na hawa Wazungu, waliompa hata silaha ili yeye na
rafikiye, Foday Sankoh, waendelee kuua watu? Hawa jamaa walibadilisha silaha
kwa almasi-na ndivyo filamu ile, ‘Blood Diamond’ inavyosema, kwamba Wazungu
walifuata silaha hata Afrika Kusini, wakaziuza katika makambi ya waasi,
wakachukua wanachi mateka na kuwalazimisha kuchimba almasi waliyouza Ulaya na
kuendesha vita. Kasisi, aliyenitumia ujumbe wa SMS ananiona mzushi, nawazushiwa
Wazungu!
Charles Taylor,aliyezaliwa Feburuali 28, mwaka 1948, alitokana na waliokuwa
watumwa wa Marekani, walioachwa huru. Mwaka 1997 raia wa Liberia walimpigia
kura kwa woga, akashinda
Juni 2003
waasi wa Lurds waliingia mjini Monrovia , Taylor akatimka. Alikamatwa Mashariki
mwa Nigeria , baada ya kutoweka kijijini, Calabao, alipokuwa akishikiliwa tangu
Agosti mwaka 2003.
Alitaka
kutimkia Cameroon na Chad , akashindwa. Alitiwa mbaroni Machi, mwaka 2006
akapelekwa The Hague.
Uingereza
ilishapiga ‘ndogondogo’ kwamba akatumikie kifungo nchini humo. Ikawa
hivyo.
Hii haina tofauti sana na Ufaransa kujidai kumpeleka Kanali Mohamed Bacar mahakamani, wakati ni mshirika wao wa karibu,- waafrika wanapigwa ‘changa la macho’.
Hii haina tofauti sana na Ufaransa kujidai kumpeleka Kanali Mohamed Bacar mahakamani, wakati ni mshirika wao wa karibu,- waafrika wanapigwa ‘changa la macho’.
Madiktea wengi Afrika walioleta vita na kuwaburuza raia ni vibaraka wa hawa
Wazungu. Amin Dada, kwanza alikuwa kibaraka wa Wazungu, wakamtema. Mobutu
alikuwa kibaraka wao-alipoiba mabilioni ya fedha, akazificha kwao, wakati nchi
ikikauka.
Hata leo, hawa Wazungu wanafanya ufisadi mwingi hapa Afrika. Mikataba ‘hewa’
kama ya rada mbovu inayowaweka akina Waziri Andrew Chenge matatani
leo, imehasisiwa na hawa jamaa.
Wanangoja siku
,wakikosana, ndipo waseme kuwa kuna fedha katika mabenki yao . Kwanini
wasingesema mapema, wakati zinapelekwa huko kufichwa?Fedha chafu
zinafichwa kwao-ndiyo biashara hata ya baadhi ya Wahindi matapeli hapa.
Hata fedha
zinafichwa na vigogo wetu katika mabenki yao.Zinajenga uchumi wao.
Hawa na
mafisadi, lao moja! Ni walewale, kasoro tarehe ya kuzaliwa!
Watajibaraguza hivi na vile, lakini hakuna hatua zaidi itakayochukuliwa.Mafisadi
wataachwa watambe, kwa sababu wana mizizi mirefu Uingereza, Ufaransa, Marekani,
Uswisi, Ujerumani , Canada n.k
Migogoro ya kisiasa Afrika huletwa na Wazungu, ili wachukue mafuta, almasi,
dhahabu, samaki, mazao ya misitu, wanyamapori, mazao ya kilimo, ardhi n.k.
Tangu shambulio la magaidi la Septemba 11, mwaka 2001 hawa jamaa wanapunguza
utegemezi wa mafuta na rasilimali nyingine Mashariki ya Kati. Huko, kunawaka
moto.
Wako
katika Pwani ya Bahari za Atlantic , na Hindi, wanachukua mafuta na madini
hapa; wanachochea migogoro mahali ambapo hawapokelewi kwa urahisi. Wanauza
bunduki kwa vikundi vya waasi wanaopewa mafunzo ya msituni katika nchi
tajiri, kama tulivyoona, Sankoh na Taylor wakiwa Libya .
Wangalipo watuhumiwa wengi wa uhalifu wa kivita Afrika…hawa wanatawala katika
mbawa za wakubwa Wazungu, bila wasiwasi. Pindi akina Bush wanapokuja huku,
hutandikiwa zulia jekundu na kuondoka pasipo kuhoji Demokrasia kwa hao ‘rafiki
zao’ ambao situ ni madikteta, bali wahalifu wa kivita kama Taylor,
Sankoh, Milosevic, Hitler, Mohamed Bacar n.k
Hawa
vibaraka wa Wazungu, badala ya kusubiri kuchaguliwa na wananchi, wao ndio
wanaochagua watu watakaowaweka madarakani-Nazungumzia Tume zisizohuru za
Uchaguzi…kila kiongozi mshirika wa hawa Wazungu, ana tume yake
inayomweka madarakani. Wazungu wako kimya. Wanampigia kelele yule
anayewasaliti.
Marekani na Wazungu wengine wanaruhusiwa kujenga ‘base’ zao katika Pwani ya
nchi tajiri za mafuta, madini na rasilimali zenye thamani kubwa. Wanashirikiana
na watawala mafisadi kuhamisha utajiri wa Afrika hadi huko Ughaibuni.
Waafrika
huendelea kuteseka na kulia njaa…ndipo Wazungu wanapofungua vidirisha
vidogo vya misaada ya kinafiki. Hawa na mafisadi, magaidi kama Bob Dinard,
madikteta kama Bokassa na Mobutu, na wezi wa mali ya umma, lao moja. Amini
usiamini…
Juzi Uingereza ikakimbia kuilipa fidia Uganda kufuatia madai ya Ufalme wa Bunyoro nje ya mahakama,maana waliona wanaaibika. Wamelipa Pauni milioni 700 lakini hazijafika, bado Ufalme huo unadai
Itaendelea
Juzi Uingereza ikakimbia kuilipa fidia Uganda kufuatia madai ya Ufalme wa Bunyoro nje ya mahakama,maana waliona wanaaibika. Wamelipa Pauni milioni 700 lakini hazijafika, bado Ufalme huo unadai
Itaendelea
0786\0754-324 074
www.congesmrambatoday.blogspot.com
No comments:
Post a Comment