Dikteta idi Amin Dada(1)
Na conges mramba
ALIPOTIMULIWA na majeshi ya Tanzania Uganda, Aprili 11 mwaka
1979,Amin alitimkia Saudi Arabia.
Aliishi katika gorofa za juu katika Hoteli ya
Novotel,iliyoko Palestine Street ,mjini Jeddah,Saudi Arabia.
Julai 20 mwaka 2003 mmoja wa wake zake,Madina, alitoa
taarifa kwamba Amin alikuwa mahututi hospitalini King Faisal,mjini Jeddah.
Mafigo yalikuwa yakimsumbua;yalishashindwa kufanya kazi.Kwa
sababu hiyo,Madina alimtaka Rais Yoweri Kaguta Museveni kuruhusu Amin arejee
nyumbani na akifa azikwe Uganda.
Serikali ya Museveni iliweka masharti makali kwa Amin,kwamba
kabla hajarejea nyumbani atubu dhambi zake.Agosti 16 mwaka 2003 Amin aliaga
dunia hapo hospitalini mjini Jeddah. Ilibidi azikwe kwenye makaburi ya Ruwais
mjini humo,kwani Museveni alimwekea nguMU Amin hata maiti yake kuzikwa Uganda.
Amin alizaliwa labda mwaka 1925 hivi huko kijiji cha
Koboko.Baba yake alikuwa Andreas Nyabire(1880-1976)na alikuwa wa kabila la
Kakwa.Mwanzoni walikuwa Wakatoliki,wakabadili dini na kuwa Waislam mwaka 1910.
Akaitwa Amin Dada, alipomzaa mtoto naye akamwita jina hilo
hilo la Amin DADA.Kama Adolf Hitler,Amin naye alitelekezwa na babaye,Amin
akakulia ujombani,Kaskazini Magharibi mwa Uganda.
Mama yeke,Assa Aatte(1904-1970) wa kabila la Lugbara,alikuwa
mganga wa miti shamba au tuseme ‘Sangoma’ hivi.Amin akasoma Madrassa, akasoma
Kiingereza kidogo katika shule ya msingi hakumaliza huko Bombo,kilomita 30
Magharibi mwa Kampala .Huo ulikuwa mwaka 1941.
Alipoacha shule akafanya vibarua kama Hitler
alivyokuwa,baadaye akajiunga na jeshi la Kikoloni la Mwingereza, King’s African
Rifles(KAR).
Amin alikuwa mwanajeshi wa KAR tangu mwaka 1946,akianza kama
mpishi msaidizi na baadaye alipanda vyeo kila mwaka hadi kuwa Mkuu wa majeshi
zama za Apollo Milton Obote(PhD).
Aliingia Batalioni ya 21 ya KAR kikosi cha ardhini huko
Gilgil,Kenya ambako walipelekwa KASKAZINI ya Kenya ili kudhibiti
majambazi(magaidi)wa Kisomali.
Mwaka 1952 Amin akapata u corporal na mwaka uliofuata
akapandishwa cheo na kuwa sergeant.Mwaka 1959 Amin alikuwa warrant officer,cheo
ambacho hakuna Mwafrika aliyekuwa nacho katika jeshi la kikoloni.
Amin alirejea Uganda
na mwaka 1961 alipewa cheo cha Luteni,kazi yake ilikuwa kuwafagia wezi wa
mifugo baina ya Karamajong wa Uganda na Turkana ambao ni wafugaji wahamaji wa
Kenya.
Wakati wa Uhuru 1962 Amin alipandishwa cheo na kuwa Captain
na 1963 akawa Major.Mwaka ulipopita akawa Naibu Commander wa jeshi.Watu
walisema huenda alisaidiwa na uchawi wa mamaye ili kupanda vyeo!
Alikuwa mwanariadha.Alikuwa na urefu wa sentimita 193 yaani
futi 6 na inchi 4.Jitu lenye miraba minne na alikuwa Bingwa wa ndondi wa uzito
wa juu mwepesi-light heavy weight.
Mwaka 1951 alikuwa pia mwogeleaji nguli na alicheza rugby
katika nafasi ya ushambuliaji, akichezea timu ya Nile RFC mwaka 1951.
Alishiriki magendo ya pembe za ndovu na shahabu huko
Congo(DRC) inawezekana walidhulumiana na OBOTE chuki zikaanza ingawa
alishampandisha cheo sasa na kuwa Mkuu wa majeshi(CDF) ya Uganda.
Ni Amin aliyemshambulia Kabaka Mutesa akatimkia Uingereza
ambako alifia 1969.Amin alikula fedha za jeshi, alipooNA Rais anakwenda kuhudhuria
Mkutano wa kilele wa Commonwealth huko Singapore,Amin akapindua serikali
Januari 25,mwaka 1971.
Obote akiwa njiani akaambiwa Amin kapindua
serikali,wanajeshi wakatanda tangu uwanja wa ndege wa Entebbe hadi Kampala,
Obote akaenda kutua Tanzania-Dar.Wakati huo kulikuwa na wakimbizi 20,000 wa
Uganda,akina MUseveni.
Itaendelea
No comments:
Post a Comment