MANDELA ‘alimzimia sana’ Oprah Winfrey
Na
Conges Mramba
SHUJAA wa Afrika,ambaye sasa yu mahututi hospitalini mjini Pretoria,Nelson
Mandela, alimhusudu sana nyota wa Marekani mwenye asili ya Afrika, Oprah Winfrey.
Katika makala yake fupi iliyochapishwa Mei 14,mwaka 2007
katika Orodha ya watu mashuhuri 100 wa Gazeti maarufu la TIME(The TIME 100
List),Mandela alisema Oprah alikuwa nguzo ya kimataifa yenye kuumba upya njozi
za wasichana wadogo wa Afrika Kusini waliokata tamaa.
‘Tata’Madiba, alimueleza Oprah alimueleza Oprah katika
makala hiyo kuwa miongoni mwa mwatu mashuhuri sana duniani. Makala hiyo ilikuwa
miongoni mwa nyingine zilizoonyesha wasifu wa watu mashuhuri duniani, makala
ambazo pia ziliandikwa na watu mashuhuri.
Makala hiyo ya Mandela ilimweka Oprah miongoni mwa watu
wengine mashuri sana walioandikwa katika jarida hilo la TIME, ambao ni pamoja
na Papa Benedict XVI aliyejiuzulu, Hillary Clinton, Sonia Gandhi, Hu Jintao,Ayatolla
Khamenei,Angela Merkel, Arnold Schwarzenegger, Thierry Henry, Barack Obama na
wengine.
Mandela alimtaja Oprah mwanamitindo tajiri,anayemiliki
gazeti na kuendesha kipindi cha televisheni, ‘Oprah Winfrey Show’ kama nguzo
muhimu sana katika kuwaondolea vikwazo watu wenye shida kote duniani.
Oprah, alizaliwa Januari 29,mwaka 1954 huko
Kosciusko,Marekani, sasa tajiri aliyeorodheshwa na jarida maarufu la Forbes
miaka michache tu iliyopita kama ‘tycoon’ miongoni mwa Wamarekani Weusi.
Ameanzisha shule ya wasichana Afrika Kusini-The Oprah
Winfrey Leadership Academy for Girls- iliyoko jijini ,Johannesburg.
Shule hiyo huchukua watoto wa kike kuanzia elimu sawa na darasa
la saba hivi hadi kidato cha nne,na ilifunguliwa na Mandela.
Katika hotuba ya ufunguzi,Madiba akasema ingeangaza ‘Future’
ya wasichana Afrika ya Kusini.
Oprah(59) amekuwa akitazamwa na Mandela kama ‘Potential
Figure’ katika kuwasaidia wasichana na akina mama kujinasua katika hali duni ya maisha.
“Wasichana wanakabiliwa na laana ya matarajio duni ya
kimaisha na fursa zisizo sawa na wanaume”,aliandika Tata Mandela katika makala
hiyo katika gazeti la TIME,akifafanua kuwa Oprah ni “A Model for all of them and for all of us”
Tata Mandela alimwita Oprah kuwa shujaa wa kizazi
chetu.Katika orodha hiyo ya gazeti la
TIME(The 100 TIME List)Rais Barack Obama alikuwa nambari Moja,kufuatia TUMAINI
LA KUPENDEZA njozi aliyoota tangu akiwa seneta huko Illinois,aliikopa kwa
mchungaji wake wa Kanisa la Kilokole analoabudu, The Trinity United Church of
Christ, huko Chicago.
Katika orodha hiyo ya TIME La Mei 14, mwaka 2007 ya watu
maarufu walikuwemo pia akina Condoleezza Rice ‘Condi’,Raul Castro,Osama bin
Laden,Omar Hassan Ahmed al Bashir, Malikia Elizabeth II, Warren Buffet na David
Rockefeller.
Wengine ni George Soros,Al Gore na Leonardo
DiCaprio,aliyecheza filamu ya BLOOD DIAMOND inayosimulia vita vya almasi za
damu huko Sierra Leone wakati wa Charles Taylor na Waasi wa RUF.
Taylor sasa amefungwa Uingereza na kiongozi wa Waasi,Fodday ‘Poppay’Sankoh
alifia rumande huko The Hague,Uholanzi.
No comments:
Post a Comment