MISRI, hamkani si shwari tena!
Ni mapinduzi juu ya mapinduzi.Watu wajinga sana watasema
sababu za vurugu Misri hutokana na siasa mbaya za Bara la Afrika.
Huu ni umajununi kuifananisha Misri na siasa za
Uganda,Zimbabwe,Kenya,Sudan ama Somali.Tunapaswa kuitazama Misri.
Ina watu takriban milioni 90 wanaosongamana(watu 181 katika
maili moja ya mraba);Mabedui na Waberiberi ambao ni asilimia 99 ya Wamisri
wote;wanaozungumza Kiarabu,baadhi yao Kiingereza na Kifaransa.
Misri, ni taifa la mchanganyiko wa watu wengi,ambalo baada
ya kupinduliwa Mohammed Mursi,sasa yupo Adly Mansour.
Wengi wao,(asilimia 94) ni Waislam wa Madhehebu ya
Sunni,Wakristo wa Madhehebu ya Coptic ni asilimia sita tu.Sasa angalia kwamba
Washia na Sunni hugombana, halafu Wakristo wa Misri hawajawahi
kukubaliana,hususan chaguzi za kura zinapokuja.
Hawa Sunni na Washia wamehasimiana tangu Irak,Iran hadi
Misri haiko salama. Hosni Mubarak aliyezaliwa Mei 4,mwaka 1928 akaingia Ikulu
ya mjini Cairo Oktoba 14, mwaka 1981,tayari alishapinduliwa kwa maandamano ya
medani ya Tahrir,na yuko nyuma ya nondo za gereza.Alikuwa mshirika wa madola
makubwa ya Magharibi.
Hili ni taifa la kijeshi tangu zama za Farao mwaka kwa takriban miaka 5000 sasa.Ina wanajeshi
448,500.Hata Nabii Musa(1500 BC) alifundishwa kuwa kiongozi wa jeshi la
Misri,ambalo aghalabu ndilo lenye mamlaka makubwa katika nchi.
Bila jeshi Misri hakuna Misri,taifa kubwa kando ya Mto Nile
unaotiririka kutoka Afrika Mashariki na kuweka uhai Misri.Nchi ya uchumi wa
pamba,mpunga,maharage na matunda yanayostawishwa kwa umwagiliaji wa maji ya Mto
Nile.
Misri ni nchi ya uchumi wa mafuta,nchi yenye akiba ya
mafuta,mapipa takriban bilioni tatu.Haimo kwenye Umoja wa Nchi zinazosafirisha
mafuta kwa wingi Duniani( Organization of Petroleum Exporting Countries),ambazo
ni Algeria,Libya,Nigeria(hapa Afrika),Indonesia,Iran,Irak,Kuwait,Qatar,Saudia
na Umoja wa Falme za Kiarabu(UAE) na nchi ya Nicolas Maduro, Venezuela.
Tazama hali ya kisiasa na kiusalama ya nchi hizi zenye
mafuta mengi;linganisha uchumi wake na hali za watu,kasha angalia kama
wanaelewana na nchi za Magharibi-nyingi ni shida tupu,vita vya wenyewe kwa
wenyewe na uadui mkubwa na Marekani na Ulaya.
Nikusaidie msomaji.Makampuni makubwa ya mafuta duniani,
Major Oil Companies,ni mali ya Wamarekani,Waingereza,Wafaransa,China na sasa
Warusi na wabia wao wa biashara na washirika wa kijeshi.
Mafuta ni siasa, ‘Oil Politics’ na mafuta ni vita vya
kiuchumi na kijeshi mahali popote yanapopatikana na kuonekana yanatosha
kutumika katika nchi zenye viwanda vikubwa.
Hizi kampuni za mafuta za mataifa
makubwa-SUPERMAJORS-hufuatiliwa kwa karibu mno na Ikulu kama Kremlin, White
House, Number 10 Downing Street, n.k
Marekani hutumia mafuta mara 20 zaidi ya wastani wa matumizi
ya dunia nzima.Mafuta ni sawa na damu katika mishipa ya mwili wa mwanadamu.Mafuta
ni oxygen;ni uhai wa n chi.Marekani wana
mafuta yao.
Lakini,ni watumiaji wa mafuta kuliko Afrika nzima;wanaongoza
duniani kutafuta na kuagiza mafuta na nishati nyingine hata kwenye sayari ya
Mars ama mwezini!
Safari za anga lengo lake ni kusaka nishati huko.Marekani
huagiza mafuta ambayo ni zaidi sana ya nusu ya kiasi kinachoagizwa na kutumiwa
na dunia nzima kila siku.Ukiwanyima mafuta wanakutoa roho.Ni rafiki hata wa
Shetani,mradi kakubali kuwapa mafuta,gesi,Uranium ama nishati nyingine muhimu
kwa ajili ya mitambo yao.
Nataka kukwambia kwamba,mafuta yanapotindika hapa
duniani,nchi inayogunduliwa ina akiba ya mafuta mengi inageuka eneo lenye
hatari kubwa zaidi kijiolojia na kisiasa.
Hapa ndipo penye uchafuzi mkubwa wa mazingira,penye
machafuko,vita vya wenyewe kwa wenyewe na kila aina ya majanga ya
kijamii,kisiasa,kiuchumi na kiafya.Nchi zenye rasilimali nyingi wakati mwingine
watu hugeukia mambo mengine na kusahau elimu ama dini,katika maeneo hayo
haiwezekani kulinda amani kwa kirungu,bali silaha za kivita.
Ili kudhibiti amani katika nchi ya utajiri wa rasilimali
nyingi ni kuwa na jeshi imara sana;na kwenye vita aslani hakuna haki za
binadamu wala demokrasia.Ni unyama unyama,rushwa,ubabe mwenye nguvu ndiye
hustawi-survival of the fittest.
Angalia Congo(DRC) akina Jenerali Kagame na washirika wao
wamekuwa wakijiingiza huko na kuiba
rasilimali za madini(nitajadili hili baadaye),angalia Sudan ya
Kusini,Chad,Libya,Irak ndiyo sasa Misri.
Tanzania bado hatujaanza kufaidika na gesi.lakini mpaka sasa
huwezi kulinda amani Mtwara kwa virungu vya polisi;ni jeshi imara lenye silaha!
Na bado, gesi ikianza kuleta pesa,eneo hilo lazima kulindwa
na jeshi imara sana;na huko hadithi za demokrasia zitakoma maana makampuni
lazima kujilinda dhidi ya majasusi,magaidi ama tuseme piracy kama hao wa
Somali.
Nigeria,Royal/Dutch Shell walitumia jeshi la Je. Sani Abacha
kulinda eneo zima la Niger Delta,la sivyo eneo zima halitatawalika. Hii ndiyo
laana ya rasilimali- the resources curse.
Hali hiyo
haitokani na ‘siasa mbaya za Afrika’ kama wengine walivyokaririshwa bila
kufikiri, ni rasilimali kuvutia majambazi,wahalifu,wachochezi,walafi wa kila
namna duniani.Raia wan chi husika wanapaswa kuufahamu jambo hilo na kujiandaa
kuishi maisha kando na vurugu.
Nataka watu waelewe kwamba kwenye rasilimali ama gesi,mafuta
na madini yanakuja makampuni ya kigeni makubwa na tabia zao,mkizubaa wao haja
yao ni ku- maximize profit, kwa hiyo,
hiyo win win situation inatoweka.
Matokeo yake kunakuwa na uchochezi toka nje,vita,wenye tamaa
wanapokosa wanaona ujanja ni kutumia silaha ama nguvu za kisiasa,uasi na
ushirika na majambazi wan je wenye silaha za kivita,ndiyo hali kama ya Sierra
Leone inazuka.
Mnaletewa silaha ili muuane,mnawapa dhahabu,almasi ama
mafuta na gesi.Turejee Misri ambako taifa ni la tangu mwaka 4000 BC.Tangu zama
za Hawa na Adamu,tangu zama za Nuhu akawazaa watoto wake na Misri(Mizra) ni
mjukuu wa Nuhu.
Tangu zama hizo,Misri ni chi ya jeshi kubwa ili kulinda
maslahi,Mapiramidi,mafuta,Mto Nile n.k
Nchi inakaliwa na watu wengi wa kutokaaa tangu
Syria,Uturuki,Israeli,Irak,Iran na hata Warumi,Wazungu n.k
Uingereza imeitawala Misri tangu 1882;ingawa ilikuwa chini
ya Dola ya Kiislam ya Ottoman(Uturuki) hadi mwaka 1914.
Dola ya Ottoman iligeuza mataifa mengi ya Kaskazini mwa
Afrika kuwa Waislam,zamani walikuwa Wakristo.Jamhuri ya Misri ilitangazwa Juni
18 mwaka 1953.Luteni Kanali Gamal Abdel Nasser alikuwa Waziri Mkuu mwaka 1954;
akaja kuwa rais mwaka 1956 kwa kuchaguliwa.
Nasser,alikufa mwaka 1970,Anwar al Sadat aliyekuwa Makamu wa
Rais akawa RAIS.Oktoba 6, mwaka 1981 Anwar Sadat alilimwa risasi na na KOMANDOO
mmoja wakati akikagua gwaride la kijeshi mjini Cairo,watu wengine saba
waliuawa,28 walijeruhiwa.
Watu wanne walikamatwa wakanyongwa baadaye-nchi ya
mapinduzi,nchi ya jeshi tangu Farao.
Msomaji akumbuke kwamba, aliyemtabiri rais Obama,Martin
Luther King Jr, aliuliwa huko Memphis, Aprili 4,mwaka 1968, akina Robert F
Kennedy wameuliwa kwa risasi huko Marekani,siyo Misri.
NJAMA!Naam, tunazungumza njama za mapinduzi na mauaji
duniani ili kulinda na kutafuta maslahi ya wenye nguvu duniani-unapaswa kujua
yupo atawalaye dunia na marais kama Kikwete ni marais wan chi ndogo-ziko kubwa.
Nitasimulia siku nyingine Marekani inavyopanga kuondoa
demokrasia na haki za watu kama uhuru wa dini(Ufunuo 13:11-18) halafu watu
wataona nchi nyingine zina nafasi gani ya kukubali ama kukataa?
Obama kaja Tanzania ili kuwafanya wajinga wagutuke
kwamba,kumbe Marekani hutawala kila mahali duniani? Kumbe rais wao hutawala
Ulimwengu mzima kasoro mbingunni?
Hosni Mubarak, aliingia mamlakani MISRI baada ya Anwar
al-Sadat,Mubarak naye alishapinduliwa yuko jela na alikuwa akipelekwa
mahakamani akiwa kwenye machela.Mohammed Mursi naye kaingia kichwa-kichwa,sasa
yuko kizuizini,sasa wapo akina Adly.
Hii ni nchi ya ‘tensions’
ambazo huwezi kuziondoa kwa siasa bali jeshi,ndiyo maana watu zaidi ya 50
wamefagiliwa kwa risasi za kijeshi na Marekani haijasema kitu bali kuongeza
misaada kwa Misri.Sasa wapinzani wakahoji,kwa nini kununua silaha za kulinda
raia halafu silaha hizo zikapindua demokrasia na kuua raia mbele ya macho ya
Marekani?
Kwa nini badala ya kuondoa msaada kwa serikali,Obama anasema
ataendelea ku ‘supply’ msaada wa kijeshi? Labda hii nayo ni demokrasia? Wenye
midomo mipana mbona hamlisemi hilo?
Sadat alipigwa risasi Oktoba 6 mwaka huo 1981 kufuatia hiyo
mivutano iliyoenea nchi nzima.Misri ni nchi ya maadui wengi,mikataba ya amani
kama ya Camp David Marekani zama za Jimmy Carter,ndiyo inayofanya Misri
isipigane na Israeli n.k
Vita vimekuwa vikipamba moto tangu Gaza, Sinai ,Milima ya
Goran n.k
Hii ni nchi ya Mfereji wa Suez;nchi iliyowahi kuwa mshirika
mkubwa wa Urusi(Ukomunisti) sasa utaona kwa nini itazamwe sana na
Magharibi.Mfereji wa Suez wenye urefu wa maili 103 unaunganisha Bahari ya
Mediterranean na Red Sea ndiyo bahari ya Sham waliyovuka Waisraeli bila boti,baada
ya utumwa wa miaka 400.
Mfereji wa SUEZ unaiunganisha Ulaya na Bahari ya Hindi;na
ulijengwa na Wafaransa mwaka 1859-1869
tazama ramani uone umuhimu wake.Mwaka 1875 Waingereza wakajipenyeza na kuanza
kuumiliki,ukawa unalindwa na vikosi vya Kiingereza.
Mameli ya Ulaya na Marekani hupita hapo yakiwa na shehena ya
mabilioni ya Dola,kutoka Mashariki mwa dunia.Vikosi hivyo vya Uingereza
viliondolewa katika mfereji huo Juni 13, mwaka 1956,na ilipofika Julai 26 mwaka
huo serikali ya Misri ikautaifisha.
Kutaifisha Mfereji wa SUEZ uliojengwa ama kuchimbwa na
wafaransa kwa miaka 10,kuna maana gani kwako? Fikiri. Tunazungumza umuhimu wa
mfereji huu na mafuta ya Misri, tazama kuunganisha bahari za Sham,Mediterranean
na Hindi kupitia hapo SUEZ.
Mpaka hapa umeona umuhimu wa Misri kisiasa,kijografia na
kiuchumi.Unaona mataifa makubwa wakija Misri ili kuweka mambo sawa huko
Mashariki ya Kati-hata Obama alikanyaga Cairo mara tu baada ya kuapishwa.
Sasa tunaona nguvu za Misri kisiasa zinashikiliwa na jeshi,
wapo vijana wanaoota ndoto za kufanikiwa
siku moja na mapinduzi kutoka Nasser aliyekuwa mshirika wa akina Nyerere,Kwame
Nkrumah(Nkrumah wa Ghana alioa kwa Nasser yupo mtoto anaitwa Gamal Nkrumah)akaja Sadat na Osni
Mubarak waliolelewa katika mbeleko za Magharibi.
Demokrasia ya kura imepinduliwa miguu juu kichwa chini huko
Misri mbele ya Wamarekani, Muslim Brotherhood wanapaswa kutambua wamepinduliwa
na nani? Labda walitaka Misri iwe kwa maslahi ya WAMISRI-KOSA KUBWA!
Dola hii ya Farao inakwenda mikononi mwa Magharibi kama
ilivyo Irak na mataifa mengine ya Mashariki kwa kutumia minyukano ya medani ya
TAHRIR na jeshi. Mapinduzi ya kijeshi na maandamano ya vijana wamachinga,ni
mkono msaidizi wa Marekani na washirika wao, amini usiamini.
Akina Mohammed El-Baradei, waliokuwa juzi wakuu wa
International Atomic Agency ni washirika wakubwa wa Magharibi,sasa
watakabidhiwa nchi hii,Waislam wenye msimamo mkali walie tu!
Nchi nyingine kama Korea Kaskazini,Iran n.k zikae mkao wa
kunyolewa kavu-kavu
Itaendelea toleo lijalo
0713 324 074
No comments:
Post a Comment