Dk.Milton
Apollo Obote, alikuwa akihudhuria Mkutano wa kilele wa Commonwealth,huko
Singapore alipopinduliwa na Amin.
Vikosi
vilivyomtii Amin Dada,vilikamata uwanja wa ndege wa Entebbe,na jiji la Kampala
likawekwa chini ya Ulinzi mkali,Makazi ya Obote yakazingirwa na jeshi,kasha mabarabara
makubwa yaliwekewa vizuizi.
Radio
Uganda,ikamlaumu Obote na serikali yake kwamba ilijaa upendeleo hususan kwa
kabila lake la Acholi na Lango.
Raia nao
hawakai mbali kwa viherehere,walishangilia majeshi kuipindua serikali ya mjini
Kampala,wakidhani Amin angekuja na jipya,labda kuwapikia chai ya asubuhi!
Amin
akatangaza kwamba yeye si mwanasiasa,nia skari;hivyo jeshi likashika hatamu
hadi hapo siku ya uchaguzi mkuu ingetangazwa,baada ya hali kuwa shwari.
Haikutangazwa.Ila,wafungwa
wa kisiasa waliachwa huru,ni wale ambao serikali ya Obote iliwasweka jela ama
kizuizini.
Wakati huo
msafara wa Obote uliokuwa Singapore ulilazimika kutua Dar es salaam,Obote akawa
mkimbizi wa kisiasa kwa rafikiye, Hayati Mwalimu Nyerere. Obote aliungana na
Waganda wenzake hapa Tanzania.
Mwaka 1972
hawa wakimbizi walijaribu kuipindua serikali ya Nduli Iddi Amin.Hawakujipanga
vizuri;walishindwa vibaya.Amin akitaka kujikosha, akawaachia huru wafungwa wa
kisiasa na akampa mazishi ya kitaifa Sir Edward Mutesa,aliyefia
uhamishoni.Mazishi hayo yalifanywa Aprili, mwaka 1971.
Feburuali
Pili, mwaka 1971 Amin alijitangaza mwenyewe kuwa Rais,Mkuu wa Majeshi,Mnadhimu
Mkuu na Mkuu wa Vikosai vya Anga na akawa kila kitu.
Baadhi ya
vipengele katika katiba ya Uganda vilibadilishwa vikaondolewa kabisa,Baraza la
Kijeshi likaongoza nchi,wanajeshi wakaongoza Mahakama,serikali, Ikulu ya
Kampala ikawa ‘Command Post’.
Amin
aligeuza kikosi cha General Service Unit(GSU) kuwa kikosi cha kupeleleza
wanaomsema vibaya The State Research Bureau,na ole wako ukutwe unaisema vibaya
serikali ama Amin mwenyewe!
Unapelekwa
Nakasero,unateswa kinyama hadi unakufa kasha maiti yako wanapewa mamba wa Mto
Nile.
Tafuta
filamu ya Whittaker, THE LAST KING OF
SCOTLAND, utajua Amin alikuwa nani?
Polisi nao
walipewa ruhusa kukamata wenye midomo mirefu vijiweni asubuhi-subuhi,na
kulikuwa na ma ‘MP’ wa jeshi na kikosi cha usalama wa Raia(PSU) kikitanda kila
sehemu kubaini wapinzani wa serikali.
Ndugu zake
Obote,Acholi na Lango waliteswa sana maana walihusishwa na jaribio la mapinduzi
la 1972.
Kambi za
Mbarara na Jinja zilifanya mauaji ya wapinzani wa serikali hii ya kiimla.Askari
5000 Waacholi na Lango waliuliwa kinyama sana,inakisiwa raia 10,000
walipotezwa!
Hawa walikuwa
wa makabila hayo ya Obote na wale viongozi wa dini waliojitia kugeuza madhabahu
kuwa kijiwe cha siasa za kumpinga Amin.Wanahabari pia walichinjwa ‘wakapotezwa’,wasanii
waliokosoa serikali,majaji,wasomi,wanasheria na wanazuoni na raia wa kigeni,miili
yao ilikuja kugunduliwa ikiliwa na mamba Mto Nile.
Utawala wa
Amin(1971-1979) uliua watu wengi wasiofahamika idadi.Inakisiwa labda watu
80,000 walikufa ama labda 300,000.Amnesty International walisema Amin aliua
watu 500,000.
Miongoni mwa
watu maarufu waliouawa ni Benedicto Kiwanuka,Waziri Mkuu wa zamani na Jaji
Mkuu,mwingine Askofu Mkuu wa Anglikan,Janani Luwum,Joseph Mubiru,Frank
Kalimuzo,BYRON Kawadwa,na mawaziri,Erinayo Wilson Oryema na Charles Oboth
Otumbi-unakutwa asubuhi nyumbani kwako na maofisa wa SRB unachukuliwa ndani ya
buti ya gari,kisha mke wako hakuoni tena-umeliwa na mamba wa Mto Nile.
Amin
aliwalisha mamba wa Nile kwa maiti za wapinzani wa serikali yake,mwaka 1972
ilikuwa Agosti,Amin akatangaza vita vya kiuchumi. Aliwatimua Waasia 80,000
walioishi Kampala huku wakiwa na passport za Uingereza,maduka yake walipewa
nduguze Amin.
Hawa Wahindi
wengine walizaliwa Uganda zama za ukoloni,wakajidai kutojipambanua kama
raia,wakafanya biashara na passport za kigeni mkononi,walitimuliwa wakaacha
maduka yao nyuma,magari na mali nyingine.
Walijifanya
si wazalendo wa nchi, wakijidai kuthamini uraia wa Uingereza,Canada,Marekani na
mahali pengine.Amin alivunja uhusiano na Uingereza, akataifisha biashara 85 za
Waingereza.
Uhusiano wa
Uganda na Israeli nao ulikufa,ingawa Waisraeli walishajenga miradi kadhaa
pamoja na uwanja wa Entebbe.Israeli iliwauzia Waganda silaha. Walikuwa washauri
wa kijeshi lakini Amin akawatimua akajenga uhusiano na Kanali Muammar al
Qaddafi na Warusi.
Mwaka 1976
Juni,likatokea tukio la Wapalestina(PFLP-EO) na Wajarumani wa Revolutionare
Zellen kuteka Waisraeli hadi Entebbe,watu 156 ambao hawakuwa na passport za
Israeli waliachwa huru ndege hiyo ilipotua Entebbe.
Watu 83 na
wengine 20 wakiwemo wafanyakazi wa ndege walishikiliwa na wateka nyara hao hapo
uwanja wa Entebbe.
Umewahi
kusikia Operation Thunderbolt? Ama umewahi kusoma 90 Minutes at Entebbe?
Umewahi kutazama filamu ya Raid on Entebbe? Nitakupa full stori katika matoleo
yajayo juu ya Waisraeli kukomboa mateka wao hapo Entebbe, usikose toleo lijalo
0713 324 074
No comments:
Post a Comment