Na conges mramba,Mwanza
NI JANUARI mwaka huu wa 2013, huko Uwanja wa ndege wa Mwanza.
NI JANUARI mwaka huu wa 2013, huko Uwanja wa ndege wa Mwanza.
Magufuli anafika
huko kukagua miradi ya ujenzi na kuanza kuwachambua wazembe kama ilivyo kawaida
yake!
WAZIRI WA UJENZI,John Pombe Magufuli, ‘alimgonga’kiaina Waziri wa Uchukuzi,Dk.Harrison Mwakyembe,kuhusu mkandarasi kuchelewesha ujenzi wa uwanja wa ndege wa Mwanza.
WAZIRI WA UJENZI,John Pombe Magufuli, ‘alimgonga’kiaina Waziri wa Uchukuzi,Dk.Harrison Mwakyembe,kuhusu mkandarasi kuchelewesha ujenzi wa uwanja wa ndege wa Mwanza.
Dk.Magufuli, alifika
Mwanza Januari 10 mwaka huu, na kukagua barabara ya kutoka Nyakato National
kwenda Buswelu,itakayotumika baada ya ujenzi wa uwanja wa ndege wa Mwanza
kuanza.
Ijumaa,Januari 11, mwaka
huu 2013,Dk.Magufuli akafika uwanja wa ndege wa Mwanza,ili kukagua barabara
iendayo Igombe,inayopita mita chache kutoka unapoanzia uwanja huo na kukuta
mkandarasi hajaanza ujenzi; na wala hakukuwa na vifaa vilivyoletwa kuanza
ujenzi huo.
Awali,kulikuwa na
malalamiko kutoka kwa mkandarasi kwamba,Wizara ya Ujenzi ilikuwa ikikwamisha
kuanza kwa ujenzi wa uwanja wa ndege,kwa kushindwa kuifunga barabara hiyo ya
Igombe inayopita eneo ambalo limo ndani ya ramani mpya ya uwanja huo.
Magufuli, alipoona
hakuna dalili za kuanza kwa ujenzi wa uwanja huo,wakati tayari wizara yake
ikilalamikiwa kwa kushindwa kuifunga barabara ipitayo ndani ya eneo la mradi wa
ujenzi, akaja juu:
“Kwani barabara hii ya
kwenda Igombe inamzuia nini Mkandarasi huyu kuanza ujenzi wa uwanja?
Mkandarasi huyu tayari amelipwa malipo ya awali shilingi bilioni 8; angekwisha ‘clear site’ lakini hakuna alichofanya, wala hajaanza kupanua zile mita 500 za runway inayopanuliwa; na anasingizia kufungwa barabara!” Magufuli alisema.
Mkandarasi huyu tayari amelipwa malipo ya awali shilingi bilioni 8; angekwisha ‘clear site’ lakini hakuna alichofanya, wala hajaanza kupanua zile mita 500 za runway inayopanuliwa; na anasingizia kufungwa barabara!” Magufuli alisema.
Akasisitiza kuwa hawezi
kuifunga barabara ya Igombe hadi mkandarasi huyo aanze kujenga uwanja huo.
Barabara itokayo
katikati ya Jiji hili kwenda Igombe,hupita kandoni mwa uwanja wa ndege
unaopanuliwa ili kufikia viwango wa kimataifa.Habari zilizolifikia gazeti hili
zinasema,Mkandarasi anayejenga uwanja huo, Beijing Construction Engineering
Group(BCEG) alikuwa amesaini mkataba tangu mwezi Juni mwaka jana,na muda wa
kusafirisha vifaa(mobilizing period) wa miezi mitatu ulipita bila kuleta vifaa
eneo la mradi, kwa sababu vifaa vilikuwa vingali kisiwani Zanzibar.
Kufuatia hali
hiyo,Dk.Magufuli akataka maelezo kutoka BRELA,ikiwa BCEG walikuwa
wamesajiliwa,na kama walikuwa na uzoefu.
Mwakilishi kutoka
BRELA,akamwambia Dk.Magufuli kuwa kampuni hiyo kutoka Uchina ilisajiliwa miaka
mine iliyopita,na ilikuwa imejenga uwanja wa Taifa,Dar es salaam.
“Okay,sitaifunga
barabara hii,kwani inawahudumia hata akina mama wanaotaka kujifungua
hospitalini.Nitafungaje barabara halafu akina mama wajifungulie barabarani hapa
eti kwa sababu barabara imefungwa,wakati hata vifaa,hata toroli halijaletwa
hapa ili kuanza ujenzi?”,Magufuli alisaili.
Ujenzi wa Uwanja wa
Ndege wa Mwanza uko chini ya Wizara ya Uchukuzi ya Dk.Harrison Mwakyembe,lakini
Magufuli akamwambia Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi,Eng.Omar Chambo, “Miezi
mitatu ya ‘mobilization’ imepita,mkataba ulisainiwa Juni mwaka jana,leo ni
miezi saba hakuna kinachoendelea hapa, halafu anasema kinachomkwamisha kuanza
ujenzi ni barabara hii! Sasa niifunge basi,tuone kama ataanza ujenzi wakati
hana vifaa,hakuna hata tingatinga, hata toroli!” alisema Magufuli,huku
akiuliza, “Injinia Mshauri(consultant) yupo wapi?”
Akatokea mbele
zake.
Magufuli akampiga maswali kama alikuwa na uzoefu wa kazi. Consultant huyo
toka Zambia, akajaribu kujitetea. Magufuli akamwambia kwa kimombo: “Make sure
not to compromise with that bogus Contractor… message has sent and delivered!”,
Kwamba huyo injinia toka
Zambia aangalie asikubaliane na uzembe huo, akasema tena kwa umombo, “You may
have a bogus contractor, but you must be very tough, otherwise this may be the
last job in East Africa”,
kwamba awe makini la sivyo hii ndiyo itakuwa mara ya mwisho kufanya kazi hapa
Afrika ya Mashariki!
Wakati Magufuli
akimcharukia Mkandarasi huyo na mshauri wake toka Zambia, akatangaza kufungwa
barabara hiyo pindi ujenzi wa uwanja ukianza.
Akasema,serikali tangu
mwaka 2008 imewatimua makandarasi wazembe wanaoshindwa kuzingatia masharti ya
mikataba.
Uwanja wa ndege wa
Mwanza unapanuliwa kufika viwango vya kimabara kwa gharama ya shilingi bilioni
105 zinazotolewa na serikali pamoja na Benki ya Waarabu ya Maendeleo(The Arab
Bank for Economic Development of Africa, BADEA).
Hatua hiyo ya Magufuli
kumcharukia mkandarasi huyo imetafsiriwa kuwa ilikuwaa ‘kugongana’ na waziri
Mwakyembe hadharani.
Utakapopanuliwa,uwanja
huo utakuwa na njia ya kurukia yenye urefu wa mita 3,700 badala ya ilivyo sasa
mita 3,300.
Utakuwa na jingo jipya
la kuongozea ndege jirani na kilima(Traffic control tower),jingo jipya la
abiria,maegesho na maeneo mengine muhimu pamoja na sehemu ya mafuta ya
ndege,ili ndege zinazotoka Mwanza kwenda Ulaya au Asia,zisilazimike kupitia Dar
es salaam kunywa mafuta.
NILIMPIGIA kura Mgombea wa chama
fulani, ili awe rais wa Jamhuri ya Muungano wa Jamhuri ya
Muungano,katika uchaguzi uliopita, 2010.
Lakini, nimepata mashaka moyoni mwangu!
Lakini, nimepata mashaka moyoni mwangu!
Sioni mgombea wa kupigia kura mwaka
2015.
Wagombea wengi,hawana ‘a certain
unique qualities’ ni kelele tu.
Rais wa NCHI YANGU ubongoni mwangu
mimi, anatakiwa asiwe na mke au mume, awe hivi muda wote awapo Ikulu, na asiwe
na watoto wala jamaa,rafiki,mashemeji.
Rais Dikteta,mwenye akili nyingi kama Magufuli; na
hana jamaa,lakini jamaa zake na watoto wake ni sisi raia wake.
Watoto wa rais ni nywele za kila
raia wake!
Mwandishi,Mike Royko, wa Chicago
Sun-Times, aliwahi kuandika jambo hili zamani sana, President’s family in
everyone’s hair.
Nilikuwa nikimheshimu Rais Kikwete na hata Dk. Wilbrod Slaa,lakini...
Nilikuwa nikimheshimu Rais Kikwete na hata Dk. Wilbrod Slaa,lakini...
Siyo kwamba, Kikwete ni Rais
mbaya; la hasha. Si kwamba amefanya kazi mbaya.
Nafurahishwa na baadhi ya
mambo na vitu vingi anavyofanya Rais wetu; lakini ningependa Tanzania iongozwe na
Rais mwenye sifa mbadala, ambazo hazijawahi kuwepo.
Nawaheshimu viongozi wa Kambi ya
Upinzani, na kazi njema waliyofanya,ya kuikosoa serikali hii ya Chama cha
Mapinduzi, ambayo ilishaanza kuota mapembe.
Hata hivyo, sijaona mgombea mwenye
sifa za kutosha kuwa Rais wa TANZANIA NINAYOITAKA. Naam, Tanzania ya kesho
niitakayo mimi lazima iongozwe na Rais asiye na watoto, asiye na mke,asiye na
ndugu wala jamaa!
Isipokuwa,ndugu,mke na jamaa
zake tuwe sisi Watanzania kwa ujumla wetu,na Rais atulee mithili ya nywele zake
kichwani!
Ningependa sasa
Tanzania iongozwe na Rais mwenye sifa za pekee, ili kuondokana na majanga kama
haya ya viongozi kuendesha Biashara zao(japo halali) wakiwa Ikulu.
Naam, namtaka Rais ambaye ana sifa
ambazo Kikwete hana!
Hata Slaa na wanasiasa wengine
kama Prof Lipumba hawana sifa ninazotaka!
Nimeorodhesha hapa
baadhi ya sifa ninazotaka Rais mpya baada ya Kikwete awe nazo:
Rais asiwe na mke, yaani awe mseja;
na awe hivyo kipindi chote cha kuwa kwake Ikulu yetu ya Magogoni, Dar es salaam
!
Pili, Rais atakayekuja
baada ya Mhula wa Kikwete kumalizika mwaka 2015, awe yatima. Hatutaki marais wenye wake,watakaojaza mashemeji Ikulu!
Rais asiyekuwa na ndugu na jamaa
wenye madhambi yanayoigubika nchi kwa kashfa; tena kashfa zenyewe kubwa
zinazopamba kurasa za mbele za magazeti. Tumeshochwa na kashfa za wake na
watoto wa vigogo, ambao pengine huua raia kwa risasi,lakini polisi hugwaya
kuwatia mbaroni.
Naam. Rais asiye na mke
anayepenyeza pua yake katika masuala ya uongozi wan chi, wakati hakuna
aliyempigia kura kufanya hivyo!
Rais mwenye mke ambaye anafungua makampuni yanayoendesha biashara pengine bila kulipa kodi.
Mke wa Rais(First Lady) ambaye
atapewa leseni na kukopeshwa fedha na mabenki kwa kasi, ili kufanya biashara
kubwa kubwa, akijidai mjasiliamali.Kumbe,hata kodi halipi?
Rais asiwe na watoto ambao wanatajirika haraka haraka,baba yao anapokuwa Ikulu,wakati sisi raia tunahangaika!
Rais asiwe na watoto ambao wanatajirika haraka haraka,baba yao anapokuwa Ikulu,wakati sisi raia tunahangaika!
Lazima Tanzania
yenye watu kama Milioni 44.9 iwe na Rais mwenye sifa za pekee, kuliko
Benjamin William Mkapa, au Jakaya Kikwete.
Kuliko Dk.Slaa,Mbowe, Prof.Lipumba,
ama wanaotajwa siku hizi,akina Magufuli,Membe,Mwakyembe,Lowassa n.k
Nataka Rais awe Mwenye hekima, mtu
wa haki, mwenye akili.
Lakini, hana familia, hana jamaa wa
kumharibu akili awapo Ikulu pale.Hana mashemeji.
Rais ambaye familia yake ni sisi Watanzania, na awe anatutunza mithili ya mboni ya jicho lake.
Rais ambaye familia yake ni sisi Watanzania, na awe anatutunza mithili ya mboni ya jicho lake.
Nimewahi kusikia tetesi
za wake za Marais wastaafu, jamaa zao na watoto wao kuitumia vibaya ikulu
kufanya biashara.
Nakiri, sijawahi kusikia tetesi za
Mjane wa Hayati Mwalimu, Mama Maria Nyerere kutumia Ikulu kufanya biashara.
Hata hivyo, simpendi Rais kama Nyerere,najua familia yake haiwezi kuwa
waadilifu na wajamaa tena.
Tetesi kwamba
Benjamin Mkapa na Mama Anna Mkapa waliendesha kampuni yao , ANBEN wakiwa Ikulu,
zinanivuruga akili.
Biashara hiyo ya Mkapa na Mama Anna,
iwe halali au haramu, si hoja kwangu.
Lakini, napendekeza Tanzania isiwe
na Marais wenye familia zinazowasukuma kufanya biashara mapema wakiwa Ikulu,
ili kukimbia umasikini!
Nimesikia tetesi za utajiri wa watoto wa mararais kama Kikwete, na Mkapa! umepatikana haraka!
Nimesikia tetesi za utajiri wa watoto wa mararais kama Kikwete, na Mkapa! umepatikana haraka!
Wapo marais
waaminifu na ndugu zao na watoto wao ni waaminifu; hawaitumii vibaya Ikulu.
Lakini, hatuhitaji sasa Rais mwenye
mke,watoto,ndugu na jamaa na familia.
Kadhalika, wapo wake
wabaya wa marais wenye wapambe, ndugu na jamaa wanaowashauri vibaya ili
kujinufaisha na Ikulu. Wake, jamaa, wapambe na ndugu hawa nao hujigeuza maofisa
wa serikali.
Nani aliyewachagua
kufanya chochote?
Nani aliwateua kuwa na sauti hadi
kuwafokea mawaziri?
Unakumbuka Kenya, Lucy Kibaki
aliwahi kuwachapa makonde maofisa wa serikali na kubomoa makompyuta na
magazeti?
Kama ni hivyo, basi tungepewa nafasi
ya kuwapigia kura hawa jamaa za marais, na wake zao kabla hawajaingia
Ikulu.
Au, kwa sababu ndugu
yao anapoingia Ikulu, wao hujigeuza ‘Mabalozi’ ama ‘Wabunge’ Fulani, basi
wangepelekwa kula kiapo mahakamani, kwamba hawataitumia Ikulu kwa maslahi
binafsi kipindi chote cha Bwana, Bibi, Mjomba au Shemeji yao, anapokuwa Ikulu.
Leo, tunashuhudia mbio
kali za watoto wa vigogo kutaka kuwania madaraka. Sisemi kwamba watoto wa
wakubwa hawana haki ya kuwania madaraka, la hasha!
Wawe watoto wa wakubwa wenye Visheni; waachane na hadithi za kurithi damu za uchifu wenye falsafa ya kurithishana madaraka.
Wawe watoto wa wakubwa wenye Visheni; waachane na hadithi za kurithi damu za uchifu wenye falsafa ya kurithishana madaraka.
Siasa si maneno
matupu majukwaani.
Ni kuzifanya sera zizae maendeleo ya watu. Je, watoto wa vigogo wanaosaka madaraka kwa udi na uvumba, kupitia vyama Tawala, wanayo Visheni hii?
Ni kuzifanya sera zizae maendeleo ya watu. Je, watoto wa vigogo wanaosaka madaraka kwa udi na uvumba, kupitia vyama Tawala, wanayo Visheni hii?
Au,wanawania
madaraka ‘kutetea’ madhambi ya baba zao pindi wanapomaliza mhula wao,
baada ya kushindwa kubadili Katiba ili kurefusha muda wa kusalia madarakani?
Licha ya wake za marais
kudaiwa kufanya biashara ama kufungua vikampuni visivyotozwa kodi wakiwa Ikulu,
watoto wao wamekuwa wakiwasaidia baba au mama zao kutawala kwa mabavu.
Wamekuwa wakishiriki kuwatesa raia na kukiuka Haki za Binadamu.
Rais wa zamani wa
Liberia, Charles Ghankay Taylor ambaye juzi amefungwa London miaka 50 kufuatia
mashtaka ya Uhalifu wa kivita huko The Hague, Uholanzi, mtoto wake,
Charles Mc Arthur Emmanuel, au Charles Taylor Jr; ambaye Liberia alifahamika
sana kama, Roy Belfast Jr, alitiwa mbaroni Desemba 15 mwaka 2005, akafunguliwa
kesi mbili.
Alitiwa mbaroni huko
Miami , Marekani kwa kosa la kuwatesa kinyama waliompinga baba yake, na pia
alikuwa na kesi ya kughushi Hati ya kusafiria.
Ghankay Taylor, ambaye
sasa amefungwa jela, na mahakama ya The Hague, alishirikiana na rafikiye,
Foday Sankoh, wa kikundi cha RUF kufanya unyama Sierra Leone na kuwauzia waasi
hao silaha kwa kubadilishana na almasi.
Licha ya kuwepo
kwa tetesi za wake za marais kuingilia mambo ya serikali, kuwafokea mawaziri na
hata kuwatwanga makofi waandishi wa habari hapa Afrika, watoto wa Marais pia
wanatuhumiwa kuhusika na kashfa nzito.
Wanakuwa matajiri upesi bila kujua mitaji ya biashara walipata wapi?
Wanakuwa matajiri upesi bila kujua mitaji ya biashara walipata wapi?
Gideon Moi, mtoto
wa Rais wa zamani wa Kenya , Mzee Moi, alikuwa na tuhuma za kuhusika katika
kashfa anuai za ufisadi nchini humo. Wengine, wakiwemo watoto wa wakubwa wa
Dunia hii, wanatuhumiwa kubwia unga, kuuza ama kuvuta bangi na kuendesha
biashara haramu hata katika Vyuo vikuu, lakini kwa sababu ya upendeleo, woga au
kujikomba, vyombo vya Usalama hujikuta vikishindwa kuwachukulia hatua.
Mtoto wa Makamu wa Rais wa Marekani,
AlGore, aliwahi kutiwa mbaroni kwa tuhuma za madawa ya kulevya.
Hata kama watoto
hawa wa wakubwa waliua, au hata kama walijeruhi ama kutaharukisha umma,
huachiwa mara moja, wasiyaone magereza!
Mtoto wa Waziri Mkuu wa
zamani wa Uingereza, Bi Margaret Thatcher(86), Mark Thatcher(60) lituhumiwa
kuendesha biashara haramu na kufanya uhaini.
Sir Mark Thatcher,
mwenye vituko vya “Front Page” katika magazeti, aliwahi kupotea katika Jangwa
la Sahara . Alipotea kwa siku kadhaa, wakati akishiriki Mashindano ya
Paris-Dakar( Senegal ) Rally, akasababisha Bi Thatcher kuangua kilio hadharani,
wakati akiwa Waziri Mkuu!
Margaret
Thatcher, alikuwa Waziri Mkuu wa Uingereza tangu mwaka 1979 hadi 1990. Lakini
mtoto wake huyo aliwahi kutiwa mbaroni na polisi wa Afrika Kusini kwa tuhuma za
kuongoza njama za kupindua serikali ya Guinea ya Ikweta.
Ametiwa mbaroni
na vikosi vya usalama mahali pengi Afrika; hata Zimbabwe . Polisi wa Afrika
Kusini walisema, walikuwa na ushahidi wa kutumainiwa, kwamba Mark Thatcher
aliwapa fedha waasi wa Guinea ya Ikweta, ili wampindue Brigedia Jenerali
Mstaafu, Teodoro Nguema Mbosongo, Rais wa Baraza la Kijeshi la nchi hiyo,
aliyedaiwa kuvunja Haki za Binadamu.
Guinea ya Ikweta ni ya
tatu Afrika kwa kuzalisha mafuta kwa wingi. Pengine, Mark anayetuhumiwa hata
kuhusika katika biashara haramu ya silaha, alitaka mafuta ya nchi hiyo. Naam,
hao ndiyo watoto wa wakubwa.
Hata hivyo, wapo watoto
wa viongozi waliopata kuwa viongozi wazuri. Waziri Mkuu wa zamani wa India ,
Indira Ghandhi, alikuwa Binti wa Waziri Mkuu wa Kwanza wa India , Jawaharlal
Nehru. Baadaye, Sanjay na Marehemu Rajiv Ghandi nao wakafuata nyayo.
John Quincy Adams
aliyekuwa Rais wa Marekani 1825-1829, alikuwa mtoto wa Rais John Adams
aliyetawala Marekani mwaka 1791 hadi 1801. Adams alikuwa Rais wa pili baada ya
George Washington.
Yupo George
W.Bush ambaye baba yake George Herbert Walker Bush, alikuwa rais miaka ya
90.
Nduguze, kama Jeb Bush ni viongozi;
ni wanasiasa maarufu. Hata hivyo, katika orodha, wapo wengi viongozi watoto wa
viongozi kama akina Sir Mark Thatcher wenye tuhuma kama wahaini, wezi,
wauza unga na wahujumu uchumi, wao na wapambe wao, lakini hawakamatwi wala
kuhojiwa!
Wako akina Roy
Belfast Jr. wanaoghushi hati mbalimbali na kufanya biashara haramu na
halali, wanaotesa wapinzani wa serikali za baba zao, ambao pia hugeuza Ikulu
kuwa ‘mapango’ ya wanyang’anyi ama ‘Mungiki’ wanao ifanyia jamii ugaidi mkubwa.
Hayati Mwalimu Nyerere
aliwahi kuwaonya watu kuiogopa Ikulu. Ikulu ni mahali Patakatifu. Si mahali pa
kufanyia biashara hata ziwe halali na nyeupe kama sufi.
Rais anapoboronga, ama mkewe, jamaa
au shemeji zake wanapoendesha magendo ikulu(Doing Business from Ikulu), ndipo
harakati za kutafuta warithi huanza!
Akina Umaru Yar’
Adua wa Nigeria wametafutwa na akina Obasanjo mara nyingi sana kupitia kitu
ambacho si Uchaguzi, bali unyafuzi na Uchafuzi Mkuu wa Haki, Demokrasia na
Uhuru Afrika!
Ni kwa sababu
hii, ningependekeza wakati wa Kampeni za Uchaguzi Mkuu, angetazamwa Mgombea
ambaye jamaa, wapambe, rafiki, mke na watoto wake hawataiabisha ikulu kwa
magendo, vituko, skandali na biashara zisizolipiwa kodi.
Kama
watoto, wake na wapambe wa Rais wangepelekwa Bungeni kwanza kuthibitishwa na
kula viapo mahakamani, basi hofu kama ya Rais Jakaya Kikwete ya kumchunguza mtangulizi
wake, isingekuwepo. Hofu ya kutafuta kubadili katiba isingekuwepo, kama wake,
watoto na jamaa wa Rais wangedhibitiwa na Bunge au Mahakama.
Lakini, pamoja na
haya yote, ili kuepuka Marais kufanya Biashara Ikulu, napendekeza Tanzania
ingekuwa na Rais Mseja, lakini asiye mzinzi wa kukwapua wake za raia wake;
asiyekaribisha machangudoa Ikulu na kuitia unajisi nchi, rais mjane asiye na
familia ya kumtia majaribuni; na yatima ambaye baba, mama na watoto wake ni
sisi raia wake.
Nikijadili, agenda 2015 katika
televisheni ya Star, nikamfananisha mtu Dikteta ninayemtaka kama
Magufuli,kidogo!!
Kosa lake aliwahi kujitia doa katika nyumba za serikali wakati wa Awamu ya tatu,lakini Magufuli 'Jembe' kali Bwana!!
0713 324 074
www.congesmrambatoday.blogspot,com
No comments:
Post a Comment