TANGU
UHURU,miaka 237 kamili iliyopita,
‘demokrasia-njiwa’ ya Marekani haijawahi kuruhusu mwanamke kuwa Rais.
Hillary
Rodham Clinton, alishindana na Barack Obama katika chama chao cha Democrat,
pasipo kufua dafu; alikuwa akiwania uteuzi wa kugombea urais,Novemba mwaka
2008.
Kuna akina
mama wengi wasomi katika taifa hili, wana uwezo mkubwa labda kushinda wanaume.
Lakini,
hakuna hata mmoja aliyevuka vizingiti na mizengwe katika uteuzi ndani ya vyama
vyao vilivyokithiri kwa mfumo dume.
Condoleezza
Rice(57), utotoni akiitwa, “Condi”, alikuwa Mshauri wa Rais wa Usalama wa
Taifa,kabla ya kuwa ‘Secretary of State’ ama Namba 3 wakati wa Utawala wa
George W.Bush .
Baada ya
Bush kumaliza mhula wake 2008,wengi walidhani angeteuliwa kuwania urais kupitia
chama chao beberu cha Republican.
Wapi bwana!
“CONDI’mwanamke,tena
Mweusi mwenye asili ya Afrika,ateuliwe na Republican kugombea urais?
Thubutu!!
Susan
Rice,Balozi wa Marekani Umoja wa Mataifa(UN) na Mtaalamu wa Usalama wa Taifa,
aliyeteuliwa punde baada ya Barack Obama kuingia mamlakani,ni mwanamke,tena
kama alivyo ‘Condi’ ni Mweusi wa asili ya Afrika; anayemshauri Obama masuala ya
Afrika.
Namkumbuka
Balozi Dk.Jendayi Frazer, alikuwa Msaidizi wa Condoleezza Rice wakati wa
utawala wa Bush;msomi mwenye Shahada ya Uzamivu(PhD);Mjuvi katika masuala ya Bara la Afrika.
Hata
hivyo,kama ilivyo kwa Dk Condoleeza na Susan Rice, hawa ni ‘wanawake’ tena
Weusi wa asili ya AFRIKA;watakuwaje Marais katika macho ya Wamarekani Weupe?!
Hillary
Clinton(64) angeweza kuwa rais wa Marekani na kuweka rekodi ya mke wa Rais
Mstaafu(Bill Clinton) kuwahi kuwa Seneta wa New York, na Rais wa kwanza
mwanamke.
Angeweza
kuwa miongoni mwa viongozi wa nchi;
akina mama kama Angela Merkel wa Ujerumani,Ellen Johnson-Sirlief ama Joyce
Banda hapa Afrika,kama siyo kama Waziri Mkuu wa zamani India,Indira Gandhi, na
wengine wa Brazil,Argentina,Korea Kusini n.k
India,ni
taifa lenye demokrasia pevu duniani kuliko Ulaya na Marekani.Je, Marekani
inaweza kumchagua Rais mwanamama,halafu Mhindu?
Marekani,waweza
kumchagua rais mwanamke asiye na shahada ya chuo kikuu ili kuwaongoza?
Kwa miaka
takriban 240 sasa tangu wapate uhuru kutoka Uingereza, Marekani hawajawahi
kumchagua rais asiye Mkristo!
Sembuse Muislam
kuwa Waziri Mkuu Uingereza
! Ama Bahai
kuwa Mkuu wa nchi hizi,zenye kutangaza sana haki za binadamu,usawa wa jinsia na
demokrasia?
Obama,
kavunja mwiko wa kuchaguliwa Mtu wa asili ya Afrika kuwa Rais wa Marekani.MARAIS
wa Marekani aghalabu huwa wanaume;tena Wazungu kamili!
Walimpinga
sana Obama,wakasema huyu kazaliwa Kenya; Obama naye akamuua Osama Bin
Laden,basi kelele zikazimwa za kumpinga.
Ndiyo
maana,Obama akijua misingi ya Ubaguzi wa rangi na siasa za kimwinyi na
kihafidhina, aliposhinda Urais 2008 akasema, “THE CHANGE HAS COME TO AMERICA”.
Hizi ndizo
siasa za akina Martin Luther King Jr, Malcolm X,Luis Farakhan na wenzao Weusi
wa Marekani zama hizo.
Turejee
India,nchi ya demokrasia pevu duniani.
Sonia Gandhi
mwenye asili ya Italia,tena Mkatoliki,mjane wa Rajiv Gandhi,ambaye alihitimu tu
High school-hakuwa na shahada ya Chuo Kikuu!
Miaka 16
tangu kuuawa kwa mumewe,Rajiv,Sonia nee Maino Gandhi,aliongoza Chama cha
Congress,ambacho mwaka 2004 kilishinda;na Sonia angekuwa Waziri Mkuu wa
India,akakataa mwenyewe na kumteua Mchumi,Manmoahan Singh.
UWAZIRI Mkuu
wa Singh ukaletwa Sonia Gandhi ambaye ana watoto:Rahul na Priyanka,ambao waweza
nao kuuata nyayo za ukoo wa Gandhi.
Uingereza,
Mawazari wakuu wote wamekuwa Waanglican kasoro wachache; hawataki watu wenye
mawazo mapya kama Askofu Peter Akinola,Askofu Mkuu wa Nigeria.
Akinola(68)
alipinga kanisa hili la Anglikan Marekani kumchagua shoga-V.Gene Robinson kuwa
askofu huko Hampshire, Marekani mwaka 2003.
Kanisa lenye
waumini takriban milioni 80 duniani(sawa na raia wote wa Misri) sauti lazima
Kutoka kwa Malkia wa Uingereza, ndiyo maana mawaziri wakuu wengi wamekuwa
Waanglikan hata kama kuna Waislam,Budha,Wahindu,Bahai sijui Wasabato n.k
Eti hii
ndiyo demokrasia pevu ya Ulaya na Marekani na Haki za Binadamu tunazoimbiwa
huku,ambayo akina Obama na Bush hujidai kustawisha kwa mabavu huku Afrika!
Tuwe na
akili.Tanzania,INDIA,Malawi,Brazil,Uganda n.k wanajali zaidi haki za akina mama
kuliko hawa.
Hata
Ulaya,Margaret Thatcher wa Uingereza kawa Waziri Mkuu,wakati India tayari akina
Indira walishatawala.
Marekani
hakuna rais au Makamu wa RAIS Mwanamke,Uganda ilishakuwa na Makamu wa Rais
Mwanamke,na Tanzania kuna SPIKA Mwanamama.Rwanda kuna wanawake wengi
wabunge,sasa utatwambia nani anawanyima haki wanawake?
Marekani wanajalije
akina mama wakati miaka takriban 40 hakuna rais au Makamu wa rais mwanamke?
Uingereza,ni
Thatcher tu,Waziri Mkuu mwanamama,wengine wote madume,wakati hata Ghuba ya
Korea sasa kuna rais tena msichana tu sawa na Brazil na Argentina na hata Chile
kwa akina Michelle Bachelet.
Leo,nataka
kuwafumbua macho watu wan chi hii kudhani Ulaya na Marekani kuna demokrasia ya
ajabu sana!
Wakiona
Obama analindwa sana huku hata hawezi kutokeza katika gari la wazi,wanadhani
Marekani ama Uingereza angekwenda disko peke yake bila ulinzi!
Wakati hata
London, magari yangeondolewa barabarani ili Obama apite, na asingethubutu
kukiuka itifaki ya ulinzi kama kawaida.
Itifaki
haichagui Afrika ama Ulaya,hata Papa alichapwa risasi mchana kweupe Ulaya,na
Marais wengi wa Marekani waliuawa ndani ya nchi-tuwe na akili jamani.
Marekani,Oprah
Winfrey hawezi kuwa rais kwani ni mwanamke tena Mwenye asili ya Afrika.
Akina
Mohamed Ali walivuliwa taji la ubingwa wa ndondi duniani kwa sababu
walipolazimishwa kwenda kupigana vita vya Vietnam 1968/69 wakakataa ikawa
shida.
Hapa kinachoitwa
‘demokrasia’ participation of majority na serikali za watu na watu kwa maslahi
ya watu wote ni uongo.
Washington
kuna maslahi ya Wamarekani tena wa sili na si Weusi; Katrina ilipopiga mwaka
2005 Wazungu kwanza waliokolewa kwa helkopita,Weusi wakabaki wanaomboleza juu
na mapaa ya nyumba zao!
Itaendelea
0786 324
074,0713 324 074,0754 324 074
No comments:
Post a Comment