Monday, January 30, 2012

Sababu za vifo vya Saddam,Gaddafi na Osama



UNABII WA BIBLIA umetwambia namna dola za Kiislam zinavyojisalimisha zenyewe kwa adui zake, Mabeberu wa Magharibi, ili kuwarahisishia kutangaza ile Amri ya kuunganisha dini zote duniani-New World Order.
Gideon M. amekuwa akijadili jambo hili kila mara, name ninataka kuonesha kwamba mfumo wa kuunganisha Uislam,Ukristo,Umizimu n.k  kwa kuwatumia hao Freemason,leo ni kitu cha wazi sana, na tunaichambua Historia kwa kulinganisha na Unabii wa Biblia Takatifu.
Tuijadili kidogo Iran, kama itanusurika kupinduliwa na Ulaya na Marekani; ama kama itajisalimisha yenyewe, midhani milki zi Kiislam leo zinagongana zenyewe kujisalimisha Washington,London,Paris na Vatican City.
Washirika wa Ulaya na Marekani, Freemasons wanakamilisha taratibu za kuunga Uislam na Umagharibi, na desturi zile za kishenzi mno,kwa kile kinachoitwa,Uhuru,Demokrasia ama Haki za Binadamu.
Rais Mahmoud Ahmadinejad wa Iran anapingwa mno na Marekani na washirika wake. Sababu hasa siyo msimamo wake mkali wa kidini, bali pia itikadi kali ya kikomunisti. Yeye ni ma-Ayatollah, wanaupinga ubeberu,hasa Magharibikutaka kuimeza nchi yao,kama ilivyotaka kutokea zama za Shah.
Ahmadinejad, amerejea madarakani kupitia uchaguzi Mkuu wa Juni mwaka 2009 kwa mbinde; ni utawala ambao Marekani na washirika wake wanauita, ‘Janga la dunia.’
Mataifa ya Magharibi, kama kawaida yao walishapandikiza vibaraka,kama walivyofanya Irak,Misri, Yemen, Uturuki, Afghanistan na popote wanakotaka kwenda. Ahmadinejad anapingwa tena kwa maandamano makubwa, hasa nbaada ya uchaguzi wa mwaka 2009.
Propaganda za Magharibi zinasema polisi na wanamgambo wanaoogopwa sana mjini Tehran, Baseej, waliwaua raia na wengine walipigwa sana na kuswekwa rumande, baada ya ushindi wa Rais Ahmadinejad.
Unajua hawa viongozi wenye msimamo mkali  walimpindua Shah, ambaye alikaribia kuiuza nchi yenye utajiri wa mafuta kwa Wazungu, akapinduliwa na katimkia Bahamas, Panama, Marekani hata baadaye Misri.
Kiongozi Mkuu wa Iran, Ayatollah Ali Khamenei, na Vikosi vya taifa hili linalojiita Jamhuri ya Kiislam ya Iran, wanajua maandamano katka nchi yao yameletwa na Maadui wa Taifa=Magharibi.
Hawa maadui wa Taifa,NATO na washirika wao, wamesimika vibarama mjini Tehran ili kumng’oa Ayatollah na Rais Ahmadinejad, kwa madai ya kuwatesa wapinzani,kuibaka demokrasia na Haki za Binadamu, ama kwa kuwatoa kolokoloni wapinzani wa serikali.
Vuguvugu la Kijani, “The Green Movement” la Kiongozi wa Upinzani, Mir Hosein Mousavi,lilidhaniwa na washirika wa Nato kwalmba lilishinda uchaguzi wa Juni mwaka 2009. Huyu Mousavi ndiyo wale wale Waarabu wanaolelewa Ulaya kasha wanatumwa kuingia katika nchi zao na kufanya maandamano huku wakitumiwa mishahara kutoka Ulaya na Marekani.
Hii Iran ambayo zamani ilikuwa dola ya Umedi na Uajemi, inatikiswa sasa kwa kutaka Rais ambaye ni Muislam mwenye itikadi kali, na Viongozi wa kidini, ma-Ayatollah waondolewe,ili kupisha mabadiliko, demokrasia na uhuru wa watu kuabudu Mungu,miungu ama nyoka.
Mousavi, ama mpinzani mwenzake Mehdi Karroubi, ambao ingawa ni Waislam hawawezi kuaminiwa na ma-Ayatollah, kama watasimamia maadili ya kidini. Ma ayatollah warichukua uongozi wan chi mwaka 1989 pale Ayatollah Ruhollah Khomeini alipompindua Shah, alipokufa akarithiwa na huyu Ayatollah Ali Khamenei.Zamani walingwa mkono na Urusi kabla ya kuparaganyika mwishoni mwa miaka ya 90.
Iran ni miongoni mwa nchi zinazozalisha sana mafuta duniani. Na wameanza kurutubisha uranium, kitu ambacho sasa kinazidisha joto la vizingizio vya Magharibi kutaka kufanya mapinduzi nchini humo.
Zamani, Russia na China ambao ni wanachama wa kudumu katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, wangeweza kupinga uvamizi wowote dhidi ya Iran. Siku hizi hawa ni wafanya biashara na wabia wa Ulaya na Marekani.
Vita ndani ya Misri ama Libya, imeyanufaisha mno makampuni ya mafuta ya Urusi, na wakati vita vya kumpindua Gaddafi vinapamba moto, wao walikuwa wakiuza mafuta kimya kimya. Urusi na China, sasa ni wafanya biashara, siyo tena Dola zenye nguvu kijeshi.
Kufuatia hali hiyo, Iran inaweza kushambuliwa wakati wowote kuanzia sasa,kwa kisingizio cha Nyuklia ama kubaka demokrasia na uhuru wa watu.
Kwa upande mmoja ni kwamba, watu wanaweza kuwa na muda mchache sana wa kuamua kuwa Wakristo,lakini hali hii itadumu kwa kipindi kifupi mno kabla ya Amri ya Marekani kulazimisha watu kuabudu Shetani na Freemasons katika hiyo Amri ya NEW WORLD ORDER!
Tumeshuhudia nchi za KIISLAM kama Misri,Tunisia,Syria,Yemen na Libya zikikumbwa na vuguvugu la Kijani-Green Movement, na anayepinga hukumu yake ni kifo-kwa hiyo Syria na Yemen wataishia kujisalimisha wenyewe Washington, tumeona dalili za upendeleo ama ‘double standards’ siyo kama alivyofanyiwa Muammar Gaddafi,kuuawa.
Iran ndiyo ‘target’ la Wazungu. Iran ni adui mkubwa wa Israeli, wakati Marekani na washirika wake ni ‘wajomba’ wa Israeli na “Uzayoni”.
Na kama Iran itapinduliwa, kama tulivyoeleza katika makala iliyotangulia, basi dola za Kiislam zenye nguvu zitakuwa zimepinduliwa, na kwa sababu hiyo, “Mto Frati” (Euphrates) utakuwa ‘umekaushwa’ ili kuruhusu njia kwa mataifa yaliyo Mashariki-India, Uchina na Japan, kuvuka na kwenda kuungana na Umoja wa Ulaya na Soko lake, European Common Market, ili kuwawekea vikwazo vya uchumi wale vichwa maji wasiotaka kuunganisha dunia nzima!
Ni hapa,unabii wa Biblia unaosema kwamba Dola za Kiislam zilizokuwa zikiwang’ata adui zake kwa  ‘mikia ya nge wenye sumu kali’ wakati wa Jihad, sasa zitakomeshwa.Ukristo uliochanganywa na upagani na umizimu na Freemasons utatamba duniani-dini zote zimeanza kumezwa na ushenzi-dini za wanawake kubatizwa wakiwa uchi huko Uganda, biashara ya maji ya Baraka huko Kenya na Tanzania na ushenzi mwingi katika Ukristo ambao zamani uliruhusiwa kupigwa na mabedui wa KIARABU(Ufunuo sura ya 9).
Mabaki ya dola ya Ottoman eti yameungana na NATO, nchi za Kikomunisti zilikokuwa katika mkataba wa Warsaw,Poland, zilishajisalimisha NATO.
Sasa,Marekanina Soko la Pamoja Common Market ni zamu yao kulazimisha kila mtu,kila nchi kuamini mfumo wanaotaka wa kuabudiwa, na watakaopinga watauliwa kama Gaddafi, Osama na Saddam na wengine watawekewa vikwazo vya kiuchumi kama Iran,Cuba, Zimbabwe,Venezuela n.k
Hakuna tena taifa la Kiarabu ama la Kiislam litakalong’ata kama mikia ya nge(sting in the dragon’s tail),muda huo umepita(Ufunuo 13:15-18) na muda wa Marekani na washirika wake wa Kikristo kutamba.
Marekani sasa wako nyuma ya upinzani wa kijani kila mahali ili kutaka mabadiliko ya sheria,kuwe na uhuru watu kuamua hata wanaume na wanaume kuoana=kama hutaki hakuna msaada!
Marais, kama Mahmoud Ahmadinejad wanapopata fursa kuhutubia Umoja wa Mataifa(UN General Assembly)wanasema unyama huo dhidi ya taifa lao,lakini nani awasikilize? Marekani wanatetea demokrasia na uhuru wa dini,wakati huo huo wataondoa uhuru huo wa kuabudu kwa mkono mwingine.
Novemba, Barack Obama anaweza kurejea White House kwa mhula wa pili wa uongozi mwaka 2012. Na yumkini,Obama atatangaza hii amri ya New World Order.
Wakati wa uchaguzi wa 2008,gazeti la The New Yorker lilichapisha katuni, Michelle Obama na mtindo wake wa nywele wa ‘Afro’ akibadilishana na mumewe ‘Jambia’ lenye ncha kali la magaidi wa Kiarabu kwa bunduki, Machine Gun!!
Tafsiri yake ni kutimia kwa unabii. Osama Bin Laden ameuliwa-na juzi nikitazama televisheni,nikaona Obama akijisifu kwa kumuua Osama,kwamba kwa kipindi chake Marekani imekuwa mahali salama pa kuishi-hii ndiyo silaha yakekubwa ya kampeni za Novemba mwaka huu.
Marekani, zama za Obama huyu, amefanikiwa kuwanyang’anya Waarabu, tena Waislam “uwezo” uliokuwa katika mikia ya nge yaani katika majambia ya wafuasi wa vita vya Jihad. Tusome historia.
  Osama, Saddam,Gaddafi na Carlos The Jackal walikuwa Wakomunisti
Wote hawa walikuwa Waislam waliopata kupinga ubeberu wa Kimagharibi,kila mtu kwa staili yake na kwa mchango tofauti.
Osama Bin Laden alianza kuwapinga Warusi mwaka 1979 walipoivamia Afghanistan=alisaidiwa na Marekani. Osama alikosana na Marekani. Ni vigumu ukiwa na akili timamu kuwatumikia Marekani. Dikteta wa zamani wa Zaire, Mobutu aliyetimkia Togo baada ya kupinduliwa akaishia kuugua kansa na kufa Morocco, aliwahi kusema hivi, “I’m the latest victim of Cold War, because support for US was nothing” nimekuwa mwathirika wa hivi karibuni wa VITA BARIDI,sabababu(nimemaizi) kuwaunga mkono Marekani,hakuna faida!”
 Hii ni kauli ya majuto ya Mobutu alipokuwa katika kitanda cha mauti. Yuko Charles Taylor anasema, “Adui yako anapukuwa ndiye Bwana wako, wewe umekwisha!” huyu yuko The Hague, anashitakiwa kuleta mauti ambako yeye na Wazungu waliiba almasi za damu, Sierra Leone.
Naam, msimamo wa Saddam, Osama,Gaddafi na Carlos The Jackal ni kuupinga ubeberu kwa dhati. Rais wa Venezuela(nchi alikozaliwa Carlos) Hugo Chavez, anasema, Carlos The Jackal, hajawahi  kuwa gaidi,bali ni ‘Mpigania Uhuru’ wa zama za Vita Baridi, aliua watu lakini wengi wao mabeberu!,
Tumjadili kidogo Carlos The Jackal. Wakati huo wa Vita Baridi, Carlos The Jackal aliitwa Illich Ramirez Sanchez, na aliwapenda sana wanamapinduzi wa Amerika Kusini; akina Che Guevara, Camillo Torres na Carlos Merighella.
Babaye Carlos hakutaka kumpeleka Marekani kusoma ‘uchafu’ wa Magharibi.Alimpeleka kusoma Chuo Kikuu cha Patrice Lumumba huko MOSCOW,Urusi . Huko alikutana na wanamapinduzi wa Chama cha Popular Front for Liberation of Palestine (PFLP), ambao miaka hiyo ya 70 walikuwa wakidai uhuru wa Taifa lao.
Urusi inatajwa katika Biblia kama nchi iliyoko Kaskazini mwa Ulaya inayoitwa Gog(Ezekiel 38:)ni nchi kubwa iliyoenea mabara mawili ya Ulaya na ASIA na ina ukubwa ambao ni 1/6 ya dunia.
Carlos,mbali na kushiriki operesheni za ‘kigaidi’ kama kuwateka mawaziri wa OPEC huko Venna,Austria alikuwa Komando aliyefuzu katika Chuo cha Kijeshi cha Mantanzas,Cuba.
Nataka msomaji ajue urafiki uliokuwepo kati ya Wapalestina, Warusi,Venezuela, na hata Cuba ya Field Marshal Fidel Alejandro Castro Ruz, zama hizo.Wakati huo Urusi iliyoongoza nchi za Mashariki(Warsaw Pact) ilikuwa na watu milioni 250 sawa na Marekani.
 
0786 324 074



No comments:

Post a Comment