Monday, January 30, 2012

Dola ipi ya Kiislam itazishinda Ulaya na Marekani?


 
*Saddam, Gaddafi, Osama wameuliwa, sembuse ma-Ayatollah wa Iran?
* Carlos The Jackal alishafungwa jela Ufaransa kwa ‘uzalendo’ wa kuwapinga mabeberu
*Hugo Chavez, Mugabe,Fidel Castro na wenzao waliowapinga Wazungu wamezeeka, falme za Kiarabu za Misri, Yemen,Tunisia, Sysia, nazo  hoi
 
OTTOMAN EMPIRE, ni dola la Kituruki lililokaribia kuitawala Dunia, lilitamalaki Afrika Kaskazini, Asia na Ulaya.
  
Ndiyo dola ya Kiislam iliyoinuka kwa nguvu nyingi na kuzikalia nchi zilizkuwa milki ya Wakristo, zikiwemo zile za Ulaya kwa takriban miaka 150. Tunajua hata Misri ilikuwa nchi ya Wakristo, ila ikatekwa katika karne ya 12 hivi.
 Afrika Kaskazini, ilitekwa na Uislam na falme zake nyingi ziliangushwa kwa ‘Majambia’ ya Waarabu,yaliyong’ata mithili ya mikia ya nge wenye sumu(scorpion stings) zama hizo za vita vya kuwatoa kamasi Wakristo waliokengeuka na kuanza ngula nyama za nguruwe huku wakiabudu sanamu na kutambikia mizimu.
  Dola hii ya Uislam, maarufu sana kama, “Ottoman Empire” ama dola ya Othman, ilikoma Agosti 11 mwaka 1840 AD, kwa hiari yao wenyewe, wakawaachia Wakristo wa Ulaya na Washirika wao(Allied Powers of Europe) wakaukalia mji mkuu wa dola hii wa Constantinople.
Ottoman waliinuka mnamo karne moja na nusu baada ya kifo cha Mtume Mohammed ASW, mwaka 632 AD. Hadi mwaka 1453Waislam hawa(Saracens) walioupinga kwa ‘Jihad’Ukristo(Crusades)ilishapoteza mwelekeo wake wa kuitawala Mashariki mwa iliyokuwa dola ya Rumi-The Roman Empire.
Mapigano baina ya Ukristo uliokengeuka na kumwacha Mungu na Mabedui wa Kiarabu,yalitabiriwa na Mtume Yohana katika Ufunuo wa Yohana 9:1-11.
Ushindi wa vikosi vya wanamgambo wa Kiarabu wenye majambia, waliopanda farasi huko jangwani, ulitabiriwa kuendelea kwa jumla ya miezi mitano ya kiunabii, ambayo ina jumla ya siku 150 ukichukulia ukweli kwamba Kalenda ya kale mwezi mmoja ulikuwa na siku 30 tu.
Miezi mitano ya unabii(Ufunuo 9:5,10) hivyo vikosi vya wapanda farasi vya Waarabu waliotumia majambia makali(mikia ya nge) viliwashambulia Wakristo walioacha imani(kukosa mhuri wa Mungu) na kuanza kuabudu masanamu waliyoyaleta hata makanisani, wakala nyama za nguruwe na kufuata ibada za miungu.(Tazama Ufunuo 9:4)  Walishikishwa adabu kwa ruhusa ya Mungu mwenyewe.
Kulingana na unabii wa Biblia, siku moja ya kiunabii ni sawa na mwaka mmoja(Ezekieli 4:6, na Hesabu 14:34). Kwa sababu hiyo, unabii unashabihiana na Historia kwamba dola ya Ottoman ilikoma baada ya miaka 150.
Leo,Uturuki ilikokuwa hiyo dola ya Ottoman, ilishajifutika yenyewe chini ya mvungu wa miguu ya Umoja wa Kujihami Ulaya Magharibi(NATO) ambao wakigeuza ubavu wanaitwa Soko la Pamoja la Ulaya(European Common Market). Kuna mbio nyingi za mataifa yaliyoupinga ubeberu wa Magharibi sasa kujiunga NATO na Umoja wa Ulaya(EU).
Dola nyingine za kale sana duniani ni Babeli,uliojengwa na Nimrodi(Mwanzo10:8-10). Mnara wa Babeli ulikuwa na kimo cha futi 75 hivi, wakati kulikuwa na hekalu la kuabudia miungu lenye kimo cha futi 600 kwenda angani.
Babeli inayosimuliwa katika kitabu cha Danieli zama za Dikteta Nebuchadnezzar, ilitawala dunia mwaka 606 BC.
Umedi na Uajemi(leo Iran)ilitawala dunia kuanzia mwaka 536 BCbaada ya kuishinda Babeli.
Tutajadili hapa chini, kama Iran ya sasa chini ya ma-Ayatollah na Mujahidina kama Mahmoud Ahmadnejad, wanaweza kuzishinda dola za Magharibi, ambazo zinajiandaa kuishambulia Iran hii kwa kitisho cha Nyuklia!
 Iskanda(Alexander) Mkuu wa Ugiriki, aliwashinda Wamedi na Waperizi ama Waajemi hawa wa Iran ya sasa kati ya mwaka 336 na 323 BC akatawala milki yoote ya hawa. Ugiriki ya sasa imesalia nchi ndogo ya vilima,wakazi wake ni wavuvi masikini tu ambao nao wako European Common Market.
 Ugiriki ingali  inakumbukwa kwa kuasisi michezo kama Olimpiki itakayochezwa mwaka huu mjini London, mwezi Juni.Wanakumbukwa kwa kuanzisha mbio za Marathon, na maarifa ya sayansi,kasha kwa wana falsafa wake mahiri kama Plato, Aristotle na Socrates.
Warumi waliwashinda Wagiriki kuanzia mwaka 168 BC.
  Na eneo lote hili ambalo lilikuwa milki ya Rumi leo ndilo European Union na Soko la Pamoja(Common Market) nchi hizi zimeungana na Marekani; milki hii inatanuka kuelekea Mashariki kulikokuwa na milki za Waarabu wa Ottoman.
 Rumi inakumbukwa kwa watawala wake kama Kaisari Gaius Julius Ceasar aliyechaguliwa kutawala Rumi BC 46, Augustus, Tiberius na Claudius. Hawa wapo katika Biblia.Yesu alizaliwa wakati wa Kaisari Tiberius ama Tiberio aliyetoa amri ya sensa, na alianza kutawala AD 14.
Dola ya Rumi ilishambuliwa na kuvunjwa kabisa ikatawanyika katika vipande vidogo ambavyo ni nchi kubwa za Ulaya siku hizi. Hizi ni nchi 10.
Mamlaka ya Rumi yalirithiwa na Upapa(Papacy Power) huu Upapa ulipigana vita na kuzing’oa falme zifuatazo huko Ulaya.
Vandali(mwaka AD 454), Heruli (AD 493) na Ostrogoths(AD 538), huu ndiyo mwaka Upapa ulianza kuitawala dunia rasmi. Ulikuja kukoma Feburuali 10 mwaka 1798 wakati Jenerali wa Kifaransa, Berthier, alipomtia mbaroni Papa, akamfunga jela ambako alifia.
 Mwaka 1929 Mussolini alitiliana saini mkataba(Literan treaty) ambao ni makubaliano ya kisiasa kwamba sasa mji wa Vatican ingekuwa taifa jipya huru duniani, na mtawala wake angekuwa Baba Mtakatifu-Papa.
Nimeleta kisa hiki hapa, kuwajibu wasomaji wangu Waislam wanaoniuliza kila mara, ‘Kwa nini Papa apigiwe mizinga 21 anapozuru nchi mbalimbali? Kwanini awe na mabalozi? Kwa nini  VATICAN wawe na kiti Umoja wa Mataifa; wakati Waislam hawana?”
 
Mussolini ndiye aliyempa Papa nchi ya Vatican yenye ukubwa wa kama ekari 100.7 hivi; na ni miongoni mwa nchi ndogo sana hapa duniani.
Ni huyu Mussolini aliyeponya ‘donda la mauti’ ama “Jeraha la Mauti” la miaka mingi, Vatican ukawa mamlaka takatifu inayotawaliwa na Papa ambaye pia ni kiongozi wa Katoliki duniani-Papa, ni kiongozi wa dini na siasa.
Ulikuwa mwaka huo wa 1929, Papa Gaspari na Mussolini walipotiliana saini mkataba huo wa kuliponya donda la miaka mingi(Tazama Ufunuo wa Yohana 13:3,12). Kulingana na Biblia,’Mnyama’ siyo mtu,bali ni mamlaka ama falme(Danieli 7:23) Tunajadili falme na mamlaka za dunia. Tangu zama zile hadi leo, tunatafuta kujua yajayo baada ya sasa.
 Nataka kusema kwamba, mapinduzi yaliyoanza mwaka jana huko Tunisia,Misri,Libya na sasa Yemen na vuguvugu limepamba moto Syria na hata Iran ili kuziangusha dola za Uislam wenye itikadi kali duniani, ni kutafuta mabaki ya Ukomunisti, yaani Uislam(nitajadili hili katika makala zitakazofuatia,kwa sababu hata Illich Ramirez Sanchez yaani Carlos The Jackal amegusia hili)
 Uislam, ulianzishwa na Mtume Muhammad AWS, kati ya mwaka 622 AD na ukapinga kwa nguvu Ukristo wa kifisadi(kuacha Amri 10 za Mungu)na ubeberu, baadaye vita hivyo vya Jihad vimetafsiriwa ‘ugaidi’ kwa sababu vinanyang’anya watu maisha.
  Vita vya kigaidi havina tofauti kubwa na mapambano ya kudai uhuru ama haki Fulani,kama nitakavyobainisha baadaye katika makala hii kama alivyosema Carlos The Jackal anayetumikia kifungo cha maisha huko Ufaransa.
                  
 Saddam, Gaddafi na Osama wamekufa ili kutimiza Unabii wa Biblia
 
Kuanguka kwa Saddam Hussein huko Irak(Babeli ya zamani)mwaka 2003 na kasha kunyongwa kwa kamba nene shingoni usiku wa kuamkia Jumamosi, Desemba 30 mwaka 2006 huko Baghdad, na kuangushwa kasha kuuawa kwa Muammar al-Gaddafi huko Sirte,Libya Alhamisi, Oktoba 20 mwaka 2011 ni dalili za wazi kwamba dola za Waislam
  Kuanguka kwa dola za Mashariki dhidi ya Marekani na Washirika wake wa Ulaya ni kutimia kwa unabii kwamba sasa mataifa haya ya Magharibi yanainuka kuitawala dunia kwa pamoja, na yatanena na kutenda kama shetani(Ufunuo 13:11-18).
   Ottoma walisalimisha mamlaka yake NATO, na mataifa haya hususan Uturuki yamejiunga Nato, juma la jana nilimwona Mfalme wa Jordan akiwa katinga suti safi nyeusi jijini Washington,pale ikulu ya White House, alipokutana na Rais Barack Obama. Sijui kwa nini televisheni hazikumwonyesha vizuri, wapo pia wafalme wa Saudia, Falme za Kiarabu na wengi wengine, na hawaipendi Iran ili kujikosha kwa Marekani na washirika wake wa Ulaya.
 Huu Umoja wa Ulaya(EU) na Soko lake la Pamoja, Common Market, na kwa kutumia nguvu za kijeshi NATO, wanajiandaa kutunga sheria kali(kuondoa demokrasia) kwa kutunga sheria kali-NEW WORLD ORDER-ili mtu au nchi itakayojifaragua kuwapinga, wawekewe vikwazo vya kiuchumi(Ufunuo 13:14-18).
 Kwa kutumia ushawishi hata wa Freemasons, watauteka uchumi wa dunia na kuvuruga chumi za mataifa yote mengine na kuwalazimisha kuabudu dini wanayotaka wao, Mungu wanayemtaka wao(zaidi sana teknolojia,sayansi na mizimu) watakaogoma watawekewa vikwazo vya uchumi ili wasiuze wala kununua.
 Iran iko mbioni kuwekewa vikwazo vya uchumi ili wasiuze mafuta yao Ulaya na Marekani,kwa sababu eti wanashupaza shingo kurutubisha Uranium.
 Kumbuka dola ya Afghanistan ya kina Mullah Muhammad Omar ilishapinduliwa kitambo. Katika toleo lijalo nitajadili kuhusu Iran halafu nitazungumzia habari za Carlos The Jackal na Uislam.
   0786 324 074
 
 

No comments:

Post a Comment