Tuesday, February 7, 2012

VATICAN CITY NI MSHIRIKA WA UZAYONI KUUMIZA UISLAM?



NAANZA kwa Sahihisho: Kwamba, Yesu hakuzaliwa wakati wa Kaisari Tiberio,bali wakati wa Augusto.
Nataka msomaji ajue urafiki uliokuwepo kati ya Wapalestina, Warusi, Venezuela na Cuba ya  Kamaradi, Field Marshal Fidel Alejandro Castro Ruz.
Warusi, zama hizo USSR  walikuwa milioni 250 sawa na ilivyokuwa Marekani, na walikuwa na Jeshi kubwa lenye vifaa vingi, wakati ule wa Kambi  yao iliyoitwa Nchi za Makataba wa Warsaw(Warsaw Pact) iliyokuwa kambi adui wa NATO. Kasome Military Balance during The Cold War.
Illich Ramirez Sanchez, “Carlos” mwaka 1970 alipokuwa bega kwa bega  na Wapigania Uhuru wa Popular Front for Liberation of Palestine(PFLP),Magazeti ya Ungereza,hususan The Guardian, likambatiza jina hili, “The Jackal” kulingana na alivyowindwa sana na wapelelezi wa Magharibi.
Kulikuwa na kundi la kigaidi liitwalo, Black September, la akina Carlos na Wapalestina,kazi yao ilikuwa kulipa kisasi kwa adui zao wa Magharibi, na wakati mwingine walivamia Taasisi za Fedha za Ulaya na Marekani ili kupata nguvu za kutekeleza Operesheni zao na Harakati za Kupinga Ubeberu.
Septemba 5 mwaka 1972 Black Septemba walijipenyeza katika kijiji cha Olimpiki huko Munich,Ujerumani, wakawateka wanariadha wa Israeli waliokuwa bwenini wakati wa michezo ya Olimpiki ya Majira ya Kiangazi huko Munich.
Carlos, ni mzaliwa wa Venezuela katika mwaka 1949, baba yake alikuwa mwanaharakati,mfuasi wa siasa za Karl Marx. Mama yake alikuwa Mkatoliki. Tunaposema Ukatoliki, tunausema mji wa Rome(Italia) ambao ni mji wa kale zaidi Ulaya,uliojengwa miaka 753 kabla ya kuzaliwa Yesu.
 Carlos, kafanya  harakati nyingi kuzitia hasara nchi za Magharibi za Kibepari, hadi mwaka 1991 alipotiwa mbaroni Mjini Khartoum, Sudan.Sudan hii ya Omar Hassan al Bashir, nayo iko matatani,kuwalea magaidi.
 Ni makachero wa Kifaransa waliomnasa  Carlos The Jackal mjini Khartoum, wakamsafirisha ndani ya gunia hadi mjini Paris. Mwaka 1997, wakati akiwa mahakamani, akasema hivi:
“”Sijawahi kumuua mtu yeyote kwa ajili ya kutaka fedha; nimeua kwa sababu ya ukombozi wa Palestina”. Amesema.
Amefanya harakati nyingi kukiwemo kutaka kuwatia mbaroni mawaziri wan chi za OPEC; hata hawakufanya mkutano tena hadi baada ya miaka 25,
Hata hivyo, Carlos alianza kutiliwa shaka na Chama cha PFLP kwa kushindwa kuwakamata hao mawaziri wa Fedha wa  Saudia na Iran(zama za Shah), kabla ya Ayatollah Ruhollah  Khomeini kumpindua kibaraka, Shah.
Amekuwa ‘gaidi’ wa kukodishwa mahali pengi duniani.Wakati mwingine alishirikiana na Shirika la Ujasusi la Urusi(KGB),wakati huo aliwindwa sana na Shirika la Ujasusi la Marekani, Central Intelligence Agence, na polisi wa Kifaransa.
                                                   “ KUKAUSHWA” KWA MTO FRATI  (Ufunuo 16:12) 
Kuangushwa kwa ukuta wa Berlin mwaka 1991 ndiko kunakoashiria mwisho wa Vita baridi duniani.Dola la Urusi(USSR) ,liliposambaratishwa, basi Carlos akakosa pa kujificha, akakosa hifadhi.
Saddam Hussein aliuawa mwaka 2006 mwishoni,”Mto Frati” ukakaushwa ili kupisha njia kwa mataifa ya Mashariki, China,India na Japan kujiunga na Soko la Pamoja la Ulaya  ili kufanya biashara pamoja.
Wakati huu Carlos akabadili sura na majina, akabadili makazi kila mara hadi alipokamatwa. Mwaka 1997 alikutwa na hatia ya kuua na akafungwa jela kifungo cha maisha huko  Clairvax. Kukaushwa Mto Frati ni kuondoa kizuizi kilichotenga mataifa ya Magharibi na Mashariki.
Carlos, aliingia Uislam akamuoa mwanasheria wake Isabelle Coutant-Peyre, mwaka 2001. Ameandika kitabu kiitwacho Revolutionary Islam ambamo anatetea matumizi ya nguvu dhidi ubeberu wa Kimagharibi.
Amechukia sana baada ya tangazo la Rais Obama la kuuawa kwa Osama bin Laden, ambaye alisema angekuwa ‘Mrithi’ wake, baada ya yeye kuwa amefungwa maisha.
Rais wa Venezuela, Hugo Chavez(aliwahi kumtukana Bush Umoja wa Mataifa)mwaka 2009 alisema Carlos hakuwa gaidi,bali ‘Mpigania Uhuru’ wakati wa harakati za kupinga ubeberu.Aliwahi kushirikiana na Saddam,Muammar Gaddafi,Fidel Castro na mashujaa wengine wanamapinduzi wa zama hizo za Vita Baridi,
Wasomaji wakatafute kitabu kiitwacho, Days of the Jackal cha Frederick Forsth,ili kutazama harakati za akina Carlos wakati wa vita baridi. Usiniulize utakipata wapi; maktaba?
Mwisho wa Vita Baridi,Kuanguka kwa Ukuta wa Berlin,Kusambaratika kwa Dola la Urusi(USSR)maana yake ni kwamba Ukomunisti umekwisha; na Ukomunisti unapokwisha,kinachoshika nafasi ni  mfumo wa kidini ambao Vatican City wanakuwa na nguvu,na tutaeleza kwa undani katika makala hizi.
Hakuna atakayewazuia Magharibi na Washirika wao(Allied Forces of The West)  na Freemasons, kuikomesha nchi yoyote kwa kuwekewa vikwazo vya kiuchumi(Ufunuo 13:11-18).
Yemen,Libya,Syria na Irak na Oman, Mauritania,Jordan wanajisalimisha baada ya mbinyo wa kila namna. Qatar,Kuwait,UAE,Lebanon, Bahrain wanajipeleka wenyewe kwenye muungano wa dini, siasa na uchumi wa dunia.
Watakao kataa kutii sheria hiyo ya Ulimwengu-New World Order-inajulikana wazi watafungwa jela,kuuliwa,kuwekewa vikwazo n.k Gaddafi, Osama, Saddam ni mfano mzuri.
 Mwezi huu,tumeona China na Urusi zikipiga kura ya Veto kupinga Syria kushambuliwa kijeshi na Umoja wa Mataifa,kwa madai kuwa inaua raia wanaoandamana. Unatafutwa mkakati mwingine,lazima mtawala wa Syria aachie ngazi.
Zamani, NATO(Northern Atlantic Treaty Organization) walikuwa nchi  chache tu za Ulaya na Marekani, ambazo zilikuwa Kaskazini mwa Bahari ya Atlantic, sasa kuna nchi 27; ambazo zinafuata kila Marekani na Uingereza wanakokwenda kupindua serikali.
Umoja wa Mataifa ulioanzishwa eti kutuliza vita, umegeuka kuwa Umoja wa Mataifa wa Marekani! Waziri wa Ulinzi wa Marekani,Leon Panetta, anasauti kuliko nchi nyingine yoyote.
Tumjadili kidogo Marehemu Muammar al Gaddafi.
 Ati alikuwa dikteta? Ati Wanachama wa Kudumu wa Baraza la Usalama Umoja wa Mataifa,Marekani, Uchina, Urusi,Ufaransa na Uingereza waliunga mkono apinduliwe kisha akauliwa kwa risasi kwa kukiuka haki za Binadamu.
 Angalia: Libya ya Gaddafi, maji yalikuwa ya kutosha kwa raia tena  ya bure, umeme buree kabisa,nyumba ya kuishi bure,mimi huku ninaongezewa kodi na mwenye nyumba ili apate pa kuponea haya maisha magumu! Kwa Gaddafi nyumba ilikuwa kuishi bure.
Kabla ya kupata ajira unapewa posho ya kujikimu bwana! Libya haikuwa na madeni nje. Akiba yao nje ilikuwa dola za Marekani Bilioni 150.Ukiwauliza hata wapinzani wa Rais KIKWETE hapa kwamba kati ya Kikwete na Gaddafi nani zaidi? Gaddafi angepata kura za Ndiyo!!
Hili niliache. Unabii unatimia, waliopinga sera za Magharibi sasa wanang’olewa, watu wote wa ule ‘mlengo wa kushoto’ sasa wanalazimishwa kufuata ‘mlengo wa kulia’.
Uislam, ni dini iliyoanzia Mashariki,siyo Ukomunisti. Muislam ni mtu aliyejitoa kimamilifu kwa Allah,Uislam ni kulinda utu,ukweli na uhuru-Jambo hili ni hatari kwa siasa za Magharibi. Hakuna tofauti kubwa na kusema UJAMAA NI UTU,na ubepari ni unyama.
Kukaushwa mto Frati(The dries up process of the River Euphrates) maana yake ni kuzing’oa dola za Mashariki na sera zake kudai usawa na utu hivi; ndiko kupinga ubeberu na maguvu ya mtu mmoja mmoja au mabwenyenye wachache.
Carlos, alikuwa mfuasi wa PFLP na alipewa jina hili kwa ushabiki wa babaye kwa akina Che Guevara na Carlos Merighela-wajamaa, ali ‘Slim’ na kuwa na Msimamo mkali, “Extremisms”.
Nimetumia neno kuwa na msimamo mkali kwa kuwa ni ushupavu tu wa kidini-shahids, martyr ama ujasiri wa kutetea dini. Carlos alitetea Ukomunisti na dini,kama Osama na wenzake.
Mwaka 2009,Hugo Chavez, rais wa Venezuela asiyependwa na Marekani, alisema Carlos hakuwa gaidi ,bali Mwanamapinduzi.
Nirejee Historia ya Uislam(kwa mujibu wa Historia) umeanzishwa mwaka wa AD 622 Mecca katika Peninsula ya Arabia na Mtume Muhammad(570-632 AD)kukataa jambo hili ni kuikana historia n a unabii.
Ndani ya Uislam kuna nguzo tano hasa kulinda UTU,UKWELI na Haki, na itakavyokuwa NATO, na washirika wao wanajidai kutetea jambo hili hili lakini wataondoa haya yote matatu, wataondoa uhuru na demokrasia duniani. Hapa ‘majambia’ hayawezi kupambana nao maana wanasaidiwa na Shetani.
Watakaokataa kutii mamlaka inayokuja duniani, watafungwa jela na kukumbwa na mauti ama dhiki ya vikwazo vya uchumi(UFUNUO 13:15-18).
Napenda kumjibu George Mbilinyi wa Iringa kama ifuatavyo:
Vatican City(The Holy See) mwaka 2004 ulikuwa na watu 870;wengi Waitaliano na wapo Waswisi. Wanaongea Kiitaliano, Kilatini, na wote ni Wakatoliki-Vatican ni nchi ya dini moja. Fedha wanayotumia ni Lira ya Vatican na ile ya Italia ambazo thamani yake ni sawa.
Lira tatu hivi thamani yake ni sawa na dola moja ya Marekani. Vatican inazungukwa na Italy-eneo lake ni ekari 108.7 na mtawala wake ni Papa.(Papal State).
Katika kitabu kiichwacho THE WORLD ALMANAC toleo la 2002,ukurasa wa 863 kuna maelezo kuhusu Vatican.
Kwamba,Feburuari 11 mwaka 1929 ulitiwa saini mkataba kati ya Kadinari Gasparri na Waziri Mkuu,Benito Mussolini; mkataba wa uhuru wa Vatican na ukatoliki kupewa “Special Status” ndani ya Italia.
Mkataba huu unaitwa,  Lateran Agreement(Article 7). Feburuari 10 mwaka 1798 Papa alitiwa mbaroni na akafungwa jela. Nataka kusema kwamba, ‘donda la mauti’ la Ufunuo 13 lilipona baada ya miaka 131 kamili.
Marekani, hawakuwahi kuitambua mamlaka haya ya VATICAN,SABABU zinafahamika, wakati wa vita kati ya Wakatoliki na wanamatengenezo(Christian Reformation) wa Ulaya walitimkia Marekani ili kukwepa vita vya miaka 1260 yaani kutoka 538 hadi 1798 AD.
Mtu anaweza kusoma vitabu vingi akajua haya, hasa kile kiitwacho, Africa Learns about Europe, The Great Controversy n.k
Marekani ilikuja kutambua mamlaka ya Vatican mwaka 1984,ilikuwa baada ya kuondoa uhusiano wa Kidiplomasia katika mwaka 1867.
Marekani walipata uhuru Julai mwaka 1776,kwa muda wote hawakuitambua Vatican hadi mwaka huo wa 1984.
 Vatican na Israeli walitiliana saini makubaliano ya uhusiano wa kibalozi Desemba 30 mwaka 1993. Msomaji mmoja aliniuliza uhusiano wa Israeli na Vatican, na anapaswa kujua kwamba Israeli maana yake ni dini ya Kiyahudi, ‘Judaism’ na Ukatoliki wa Vatican kuanza kuhusiana, maana yake ni kuondoa kizingiti kati ya Uzayoni na Ukatoliki.Sasa bado Waislam?
Turejee katika unabii wa Ufunuo wa Yohana 13.
Marekani ni mamlaka inayosemwa katika fungu la kuanzia 11 kwamba ina pembe mbili mfano wa kondoo-yaani UHURU WA DINI na Uhuru wa kisiasa, lakini sasa unabii unasema Marekani wataondoa demokrasia duniani, itapindua serikali nyingi kwa kushirikiana na Vatican, Israeli, Ulaya na mataifa ya Kiarabu yaliyojisalimisha na kushirikiana, na watakuwa chini ya maelekezo ya Freemasons na Ibilisi.
Marekani itashirikiana na VATICAN(Donda la mauti lililopona Feburuari 11 mwaka 1929-Ufunuo 13:12) ili kulazimisha dunia nzima kumsujudu,kumwabudu Mfalme,badala ya Mungu wa Mbinguni. Rejea Danieli sura ya 3.
Waislam, walioniandikia SMS kunipinga wanaweza kusoma Danieli sura ya 3. Jeraha la mauti lilipona wakati wa kutiliana saini ule mkataba(Article 7) wa Lateran Agreement.
Mbilinyi kutoka Iringa, alipenda kujua,Vatican kuna jeshi lipi?
 Papa ni miongoni mwa viongozi wanaolindwa sana hapa duniani. Analindwa na askari wa Kiswisi. Baba Mtakatifu ana maadui pia,lazima alindwe. Papa Pius VI alitiwa mbaroni na Jenerali Berthier wa Ufaransa,Feburuari 11 mwaka 1798.
 Papa John Paul II alipigwa risasi. Novemba 27 mwaka 1970 Papa Paulo VI alishambuliwa kwa kisu(hakuumia) katika Uwanja wa Ndege wa Manila, Ufilipino.
 Mwaka 1981 Papa Paulo II na watu wengine wawili waliokuwa jirani naye walipigwa risasi. Ilikuwa Mei 23, mwaka huo wa 1981 Mahmet Ali Agca, akafumua risasi akamjeruhi Papa. Huyu jamaa Mahmet Ali Agca, ni  Mturuki, ambaye alitekeleza tendo hilo la kigaidi wakati Papa akihutubia St. Peter’s Square ,Rome.
Huyu Papa alikufa mwaka 2005 kwa ugonjwa wa kutetemeka.
Mei 12 mwaka 1982  Papa John PauloII ALINYATIWA na muuaji mwenye kisu,walinzi wake wakamnyang’anya kisu huyo jamaa huko Fatima,Ureno.
Papa ni Askofu wa Rome; ni Mwakilishi wa Yesu-THE VICAR OF JESUS CHRIST-NI Mrithi wa Mtume Petro, ni Mkuu wa Mitume wote,ni Mkuu wa Kanisa lote la Kikristo Duniani. Papa ni Mamlaka.
Kasela wa Mbeya, msomaji wa kila siku wa gazeti hili ameniuliza uhalali wa kueneza dini kwa mfumo wa maguvu,vita na majambia?
Ujumbe wa Biblia ni huu(Yohana 18:10-11)Petro alimkata sikio adui yao aitwaye Malko kwa jambia kali.Yesu akaona tukio hilo na kuanza kumkemea, “Rejesha panga  lako Alani mwake!” Hata mimi nasema, “Rudisheni mapanga yenu mahali pake” ndiyo Amri pekee ya kudumisha Amani Duniani.
 Mpigania haki za Weusi Marekani, Martin Luther King Jr. aliwahi kuwakataza Wamarekani Weusi zama za Ubaguzi wa rangi kupinga unyanyasaji bila vita-Non Violence Resistance- ndivyo walivyowahi kufanya wanamapinduzi kama Mahtma Gandhi wa India,uhuru ukapatikana!
0786-324 074




No comments:

Post a Comment