Thursday, March 29, 2012

unataka utajiri?


                                                         
                                                          *Lazima kulamba dole gumba la Freemasons
                                                          *Ziara ya Papa Benedict XVI  imezika Ukomunisti Cuba
SHETANI, akampandisha Yesu katika kilele cha Mlima, akamwonesha MILKI zote za Ulimwengu kwa muda wa dakika moja tu.
Akamwambia: “Nitakupa wewe enzi yote hii na fahari yake,kwa kuwa imo mikononi mwangu; name humpa yeyote kadiri nipendavyo. Basi, wewe(Yesu) ukinisujudia tu, vyote vitakuwa vyako”, alisema Ibilisi, Luka 4:5-6.
Naam, kifungu hiki ambacho ni nukuu kutoka kwa Shetani,hudai kuwa Enzi na Milki zote Ulimwenguni,fahari yake yote,vimwana warembo walioacha sehemu ya miili yao ya tashtiti nje-nje, rasilimali muhimu kama mafuta, madini ya thamani,gesi,miji mikubwa yenye majengo ya fahari,ndege,meli za fahari kupita Titanic n.k viko mikononi mwake.
 Akitaka, humpa yeyote kwa kadiri apendavyo. Isipokuwa, shatri ni moja,dogo,lakini matokeo yake huathiri maisha-KUSUJUDU MBELE ZA SHETANI-kumsujudia Ibilisi na rafiki zake,Freemasons,Illuminati, viongozi wakuu duniani,mawakala wa  waganga na wachawi n.k
Nimetumia kifungu cha Luka 4:5-6 ili kumwonesha msomaji kwamba, enzi,mamlaka,utajiri na fahari zake zote, vimo mikononi mwa Ibilii na hao rafiki zake na mawakala wake. Na humgawia kila ampendaye. Usianze kunisumbua kuniuliza namba ya kiganjani ya Shetani…mimi sina! Wengine hunisumbua kwa SMS kuniomba namba za Freemasons, sina na sijui!!
  Turejee milki ya Rumi ya kale. Mji mkuu wa Dola hii yenye nguvu na utukufu mwingi duniani,ulikuwa Rome. Siku hizi ni mji mkuu wa Italia. Biblia,iliutaja Rome wa kale kama Makao Makuu ya Shetani(Ufunuo 2:13).
  Jiji hili,lilijengwa yapata takriban Milenia tatu zilizopita. Rome ulikuwa Makao Makuu ya UCHUMI wa Dunia ya wakati huo. Kila mkazi wa dunia,alitamani kuwa na uhusiano mzuri na Rome,ili kupata mafanikio.
 Nataka kusema kwamba, kama Rome ulikuwa “centre of economic Life of the ancient World”, maana yake ni kwamba, mmiliki wake na mwenye mamlaka na uchumi-IBILISI-aliishi jijini Rome, amini usiamini.
 Kulikuwa na wakazi lukuki jijini Rome,kwa kuwa kilikuwa kituo kikuu cha biashara duniani.
Dola hii ya Rumi ilipokuwa ikishambulia mataifa mengine na kuteka nyara nyingi na mali za kutosha, vyote vilileta neema kwa wakazi wa Rome, hadi wakaishi maisha saafi sana!
 Inakisiwa, kulikuwa na watumwa 650,000 jijini humo katika mwaka wa BC 5, wakati huu ndio Yesu alizaliwa Bethlehem. SIku hizi sisi raia wa dunia ni watumwa wa makao makuu ya Fuko la Fedha la Kimataifa(IMF) na Benki Kuu ya Dunia(WB).
Tuwajadili kidogo Makaisari wa Dola ya Rumi, ili kufahamu vizuri somo lifuatalo kitambo: Tiberius(AD 14-37);Caligula(AD 37-41);Claudius(AD 41-54);Nero(AD 54-68);Vespasian(AD 69-79);Titus(AD79-81);Domitian(AD 81-96) wakati Mtume wa Mwisho wa Yesu wa Nazareti(siku hizi kuna mitume lukuki wa Yesu  hata wa Michungwani),Yohana anaandika kitabu cha Ufunuo huko Patmo kisiwani. Yohana alifariki wakati huo huo.
 Dola ya Rumi iliutawala ulimwengu wa wakati huo.Watu wote wakalipa kodi zao kwa makaisari hawa jijini Rome.      Rome ulitegemea utajiri wa mataifa mengine yaliyokuwa makoloni yake,ili kupata ustawi. Hata Yesu alilipa kodi kwa Kaisari.
Mji huu ukapata mali nyingi kutoka Misri, wakapata hata dhahabu kutoka Kushi(Ethiopia),la sivyo wangekufa njaa hawa.Siku hizi,Rome ni Makao Makuu ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo(FAO).
 Utajiri na fahari ya raia wa Rome, vilitoka katika makoloni yao. Hawa watumwa 650,000 waliwatumikia Mabwana wakubwa wa mjini Rome,waliokula wakiwa wamelala. Hata siku hizi za mwisho wa wakati,kutakuwa na utumwa kwa jiji ambalo nitalisema punde, ambalo linaanza kuwa kitovu cha uchumi wa dunia(Ufunuo 13:16-17).
Tumetazama katika makala zilizotangulia,namna masanamu ya Makaisari yalivyotapakaa jijini humo na katika mlki yote,na yaliabudiwa kama miungu(Ufunuo13:14).
 Nataka kusema kwamba, MILKI,mamlaka,enzi, fahari na utajiri huandamana na kulazimisha watu kuabudu ama kusujudia wenye vyote hivi. Hata sasa, wenye mamlaka,enzi,fahari na utajiri wataabudiwa kama miungu. Nazungumzia utajiri haramu, kama mihadarati,fedha chafu,bidhaa bandia,magendo, biashara ya viungo vya binadamu kama albino n.k Na watu huwatoa kafara hata wake,waume na watoto.
 Waarabu wanatumia nguvu ya silaha,majambia,makombeo na mabomu kuzuia ibada hii ya miungu watu-lakini Biblia inatushauri kutumia silaha tofauti na hizi,ili kushinda majaribu haya.
Sasa, nataka utambue kwamba Yule Mtume wa Yesu,Petro, alifika jijini Rome ili kupeleka Injili mwaka 42 AD. Ulikuwa wakati wa Kaisari Claudius, siyo? Haya, Petro aliuawa mwaka AD 67 kwa kutundikwa msalabani kichwa chini-miguu juu.
 Wee uwasikie tu Makaisari wa Kirumi, aliuliwa na Kaisari Nero mkatili kuliko Shetani mwenyewe. Hata mwisho wa wakati Watakatifu watauawa(Ufunuo  17:6 na Ufunuo 13:4-7).
 Kosa la Petro lilikuwa kukataa kuwasujudia Makaisari na sanamu zao,na kuwahubiri watu kwamba kuna Ufalme wa Yesu,badala ya ule wa Kaisari-UCHOCHEZI!!
Wafuasi wa akina Petro walishikilia msimaso wa kutokwenda katika mahekalu ya wafalme kuwasujudia na kupigia magoti masanamu yao, wasisitiza ibada ni kwa Mungu tu, Allah,Yahweh, Adonai,Elshadai, Nyasaye,Nyamuwanga , orodha ya majina ni ndefu.
Tulimwona Socrates(BC 490-400) AKIKATAA kusujudia miungu 391 ya Wagiriki juu ya Mlima Olympus, Wakristo wengi waligoma pia kuwasujudia Makaisari, waliuawa,waliraruliwa na wanyama wakali katika viwanja vilivyoitwa, Colloseum. Historia inajirudia, demokrasia itaondoka na uhuru wa kuabudu uko hatarini.
 Nero, alichoma moto sehemu ya jiji la Rome,mwaka AD 64 ili apate fursa kuwasingizia akina Petro,kwamba ndiyo waliochoma mji-Propaganda! Ndiyo akili za Freemasons na Shetani kuwasingizia watu ili wapate kuwaua!
  Unajua sababu? Injili ya unyofu(ya Yesu) ilikuwa hatari kwa utawala wa Rumi,ilizuia ibada na kicho kwa masanamu yao,na unajua matajiri wote wa dunia walikuwa wakiishi jijini Rome,biashara kubwa zilikuwa homo, na watu maarufu, meli kubwa za fahari zilitia nanga bandarini,zilizleta bidhaa nyingi, shangwe na kiburi vilitamalaki, sasa watu hawakutaka kusikia “Upuuzi” unaoitwa UFALME WA MUNGU!
  Basi, baada ya Petro kuuawa mwaka 67 na Kaisari Nero, akazikwa mjini Rome-bila shaka alipozikwa ndipo lilipojengwa kanisa kubwa kabisa St. Peters  hapo Rome. Wao wanasema,lilijengwa katika mgongo wa Petro-‘juu ya mwamba huu,nitalijenga kanisa’.
 Siku hizi, Kanisa Katoliki hutuambia Petro aliyeuliwa jijini Rome, ndiye PAPA WA KWANZA,muasisi wa Kanisa hilo la Rumi.
  Kwamba, Petro,amewatangulia jumla ya mapapa wasiopungua 302 hivi. Papa wa pili eti alikuwa Mtakatifu Linus(67 AD). Yule Papa aliyetiwa mbaroni Feburuali 1798 wakati wa Maasi ya Wafaransa, Papa Pius VI  na aliyerejeshewa heshima na akina Mussolini Feburuali 1929 ni PAPA PIUS XI.
Huyu aliyepo ni Papa Benedict XVI, yaani wamepita ma-Benedict 15. Ukristo mjini Rome umepitia changamoto tele, hadi kujikomba kwa Makaisari ili kukubali yaishe na kupunguza mateso kwa wakristo.
 Ilifika wakati,kanisa likawa na wapagani, watambikia mizimu na waabudu sanamu na waumini waadilifu kwa pamoja. Ukafika muda,vikaanzishwa vyeti vya msamaha-certificates of pardon,ili mtu akitaka kutenda dhambi kwa uhuru,basi anunue vyeti hivi kwa fedha nyingi ili akatende jinai huko-hatahesabiwa dhambi, maadam keshalipa fedha!
 Hizi ni dhana za kibinadamu(human theories) zilizoko makanisani leo ili kumfurahisha ibilisi na wakala wake Freemasons. Ili kupata fedha, vikauzwa vyeti(sale of indulgencies) makanisa yakajengwa ya fahari sana, ndani yake kulikuwa ibada ya sanamu na miungu.
Mbona tunawafahamu akina Tetzel ambao walifanya biashara hiyo ya vyeti vya misamaha ili kupata fedha nyingi. Msamaha wa dhambi ukaenda kwa matajiri na wenye fedha tu.Huu ndiyo mwanzo wa wenye mali wakifa roho zao kwenda Purgatory, lakini fukara akina eti roho inakwenda Jehanum. Kumbe masikini Mungu hampendi? LA HASHA.
 Pamoja na kwamba, ukipinga mambo haya unakuwa mwasi, lakini kumbe BIASHARA YA KIFO ilianza siku nyingi, hata leo wenye enzi na mamlaka wanafanya madhambi hata makanisani lakini wanaoondolewa ni fukara tu.
 Marekani na washirika wao nao wana, “Certificates of Pardon” wakienda kushambulia nchi yoyote na kuua watu, hawachukuliwi hatua, nchi masikini akina Joseph Kony,  Gbagbo ,Pierre Bemba, Taylor, Uhuru Kenyatta na wenzao wakikisiwa tu,ni kuswekwa rumande-THE HAGUE!
Mpaka wakubwa wapigiwe magoti na sanamu zao szisujudiwe(Ufunuo 13:7-8) halafu hizo sanamu zao zinawafanya watajirike kwa utajiri haramu wa Ibilisi(Ufunuo 13:3-10),twazungumzia utajiri wa damu za watu(Ufunuo 17:6).
 Msomaji aitwaye Mary, ameniandikie SMS kuuliza: “Nimesoma makala ya Machi 27;tufanyeje sasa,kama mambo ni hay? Mbona tunazidi kuchanganyikiwa?”
 Katika mwaka wa 490 BC zama za Sokrati, Dario I  akatoka na jeshi kubwa la Wamedi ili akapambane na hao Wagiriki mahali paitwapo,Marathon.
 Jeshi dogo la Ugiriki likawaotea mahali hapo,likawashambulia ghafla Wamedi ambao walikuwa na jeshi kubwa sana na magari ya deraya ya chuma.Wamedi wakapigwa na kuteketezwa kabisa.
 Baada ya ushindi, Jemedari akamtuma askari mmoja shujaa aitwaye Pheidipides  kwenda mjini Athens kutoa HABARI NJEMA kwamba walikuwa wamelishinda jeshi la adui.
 Basi, Pheidipides akatimua mbio kali kwenda Athens kutoka hapo Marathon,umbali ambao ni maili 29. Alipofika sokoni mjini Athens akasema huku akihema kwa nguvu.
“Tumepigan-nna vita,tumemshind-ddaa… add-ddui!!” Akaanguka mchangani na kufa! Ili kumuenzi shujaa huyu, Pheidipides, siku hizi kuna mbio za Marathon zilizoanzishwa ili kukumbuka ushujaa wake wa kumshinda Dario Mmedi-soma kitabu cha Danieli.
Mashindano ya Olimpiki yalianza Ugiriki karne tano hivi kabla ya Yesu, yamekuja kuboreshwa mwaka 1896. Hivyo Juni mwaka huu huko London,mbio za marathon bado zitamkumbuka huyu shujaa Pheidipides aliyejitoa uhai wake ili KUPELEKA HABARI NJEMA za wokovu. Alikuwa mwaminifu hadi kufa.
 Naam, uaminifu hadi kifo,kama Pheidipides shujaa, kuna akina Socrates(490-400 BC) alishikilia msimamo wa kutoabudu sanamu za Olympus,hadi akauliwa kwa sumu-uaminifu kwa kumwabudu Mungu tu, siyo sanamu za Shetani na mawakala zake, Freemasons.
  Mtume Muhammad(570-632 AD) alipozaliwa mjini Mecca, Saudi Arabia, akawakuta Waarabu wakiabudu sanamu hizi hizi. Ibada ya sanamu ilikuwa Ulaya,Arabuni na ziko bado Ulaya hata Marekani,lakini wapumbavu wanadhani waabudu sanamu ni Waafrika tu!
 Basi, Mtume Muhammad akaazimu kuwapa Waarabu dini safi,ya kumwabudu Allah tu. Allah huyu ndiye Yehovah, Yahweh,Nyasaye,Nyamuwanga,Katonda,Nyamujakhuma!!
 Mjini Mecca,kulikuwa na patakatifu palipoitwa, ‘Kaaba’ kwa Kiarabu eneo hili lenye pande sita zenye kulingana,lilijengwa vizuri na kulikuwa na sanamu nyingi.
 Katika kona moja ya jengo hilo, kulikuwa na JIWE JEUSI ambalo eti lilianguka kutoka angani. Mtume Muhammad aliwaona watu wengi wakitoka mahali pengi duniani wakienda hija (pilgrimation)  hapo al Kaaba,ili kulibusu hili jiwe jeusi. Alikusudia kuwapa dini nzuri-naam Dini saafi! Soma The golden book encyclopedia (DELUXE Edition)kilichoandikwa na Bertha Morris Parker. Mimi sikusema haya.
Barack Obama, alikwenda Seoul,Korea Kusini,kupanga mikakati na wenzake wa China,Urusi,Korea Kusini na Japan ili kuidhibiti Korea Kaskazini,iachane na kiburi chake cha makombora ya Nyuklia huko Ghuba ya Korea.
 Korea na Iran ni mataifa ya Kikomunisti, Korea Kaskazini hakuna Mungu kabisa,ila miungu sasa jamaa wanasema huko Korea hakuna demokrasia na uhuru wa dini, wanataka kwenda kupindua. Iran wanasema Ayatollah Ali Khamenei analazimisha watu kutokuwa na uhuru wa dini nyingine.
  Halafu, nikamwona Papa Benedict XVI akienda Santiago de Cuba na Havana,ili kukutana na Rais Raul Castro Ruz na Rais Mstaafu Fidel Alejandro Castro Ruz.
 Ajenda iliyozungumzwa ni ile ile,kitisho cha UKOMUNISTI na kuwazuia watu demokrasia na uhuru wa dini.
 Eti Korea, Iran na Cuba hakuna demokrasia na uhuru wa kuabudu(hata sanamu). Hii ilikuwa ziara ya mwanzo Papa huyo kufika Cuba ya WAKOMUNISTI-wakampokea kwa maelfu -wamenyoosha mikono yao kwa  UKATOLIKI, wataachana na Ukomunisti, ukomunisti na Ukatoliki havipikiki chungu kimoja!
 Yumkini,huu ni mwisho wa ukomunisti duniani, ziara ya Papa ni dalili za kuzikwa kabisa ukomunisti mjini Havana,na katika ulimwengu wa mrengo wa mashariki-kufuatia kuuliwa kwa akina Osama,Gaddafi, Saddam yaani kukaushwa Mto Frati(Ufunuo 16) na kuangushwa kwa Ukuta wa Berlin ulioitenga dunia katika maeneo mawili-dunia iko tayari kuungana sasa! Ziara ya Papa Cuba,ilikuwa ya mafanikio ya kuiunganisha dunia.
  Tuzijadili kidogo dola zenye nguvu nyingi duniani, ambazo sasa zinaanza kuabudiwa pamoja na sanamu zao,tukitaka kupata neema! Siku hizi kuna sanamu mambo leo.
Rais wa Benki ya Dunia(WB) huteuliwa na Rais wa Marekani. George W.Bush alimteua Robert Zoellick miongoni mwa wafanyabiashara, mabwenyenye na wahafidhina, akamrithi Paul  Walfowitz,  baada ya ile kashfa ya kimwana wa Kiarabu, Shaha Ali-Riza.
 Julai 28 mwaka jana, safu hii ikaandika kwa undani sana kisa hicho, sipendi kurejea. Ukikosa TAZAMA unakosa maarifa.
Marekani,ndiyo nchi yenye mamlaka yap eke yake kumteua Rais wa Benki ya Dunia(WB)na Ulaya wana haki ya pekee katika kumteua Mkuu wa Fuko la Fedha la Kimataifa(IMF), wengine walie tu.
 Alipojiuzulu Dominique Strauss-Khan(DSK) kwa kashfa ya ngono dhidi ya mwanamke mwenye asili ya Afrika Magharibi-Diallo, akateuliwa Mfaransa mwenzake, Christine Lagarde.Kashfa ya DSK ingali inafukuta huko Marekani.
Marais wote 11 wa Benki ya Dunia ni Wamarekani,na kadhalika watendaji wote wakuu  11 wa IMF WAMETOKA ULAYA,
 Kuna mambo mawili ya kutazama hapa; wote 11 wa WB wametoka Marekani,na wakuu wote 11  wa IMF , wametoka Ulaya. 11 na 11, hii namba ni ya Freemasons na haina tofauti na majengo pacha ya WTC yaliyosimama kama 11, na yalisambaratishwa Septemba 11,mwaka 2001, hapo upo?
  Nani wa kuwapinga Ulaya na Marekani sasa,juu ya kuiburuza dunia kwa kutumia WB na IMF? Juni 30 mwaka huu, Robert Zoellic anaachia ngazi,tuone kama Obama hatamchagua Mmarekani mwingine. Rais wa Marekani anamchagua Rais wa Benki ya Dunia!!
  Leo, nimesikia kwamba,Brazil,Russia,China,India na Afrika Kusini(BRICS) wanafanya kampeni ya kuipokonya Marekani kuitawala Benki hiyo mawakala wakuu wa ukoloni duniani.
 Nataka kusema kwamba, Washington ndiyo Makao Makuu ya Uchumi wa Dunia baada ya Rome, na wataamua hiki kiti kiende wapi? Kitakwenda BRICS au Vatican?
 Itaendelea
0786 324 074
 

 






No comments:

Post a Comment