Thursday, April 19, 2012

UNATAKA UTAJIRI?


                                                                       Unataka Utajiri? (4)
                                *Laana ya Rasilimali ni zao la hujuma za Freemasons
RAIS Barack Obama, amemteua Mmarekani mwingine, Jim Yong Kim(52) kuwa Rais wa Benki ya Dunia(WB).
Lengo mahsusi, ni ili kushikilia uchumi, mipango  ya maendeleo na fedha za Dunia nzima-hii ni AJENDA YA SIRI ya Freemasons.
Fuko la Fedha la Kimataifa(IMF) linaongozwa na Mfaransa, Christine Lagarde, baada ya ile kashfa ya Mfaransa mwenzake, Dominique Stauss-Khan(DSK).
Hii ni kusema kwamba, mataifa  ya Dunia ya Pili, Brazil,Russia,India,China na South Africa(BRICS) nyendo zao za kutaka kuzipokonya Marekani na Ulaya uongozi wa Taasisi hizi nyeti za kifedha dunia,IMF na WB zimekwama sana.
BRICS, wanadhaniwa kutaka kuanzisha Benki yao ili wakopeshane wenyewe pasipo kuwekewa masharti na kuingiliwa sana kama inavyofanya Benki ya Dunia(WB) na IMF. Masharti ya IMF na WB ni kwamba lazima wakuingilie sana na wakupe masharti wayatakayo wao, ambayo mengi ni ya kitapeli na yamejaa matokeo hasi yaliyozaa umasikini na ukosefu wa ajira hata hapa kwetu baada ya kuuza viwanda na mashirika ya umma.
Ukitaka mikopo,lazima kuzipigia goti IMF na WB. Ukikosana nao kama Mugabe, Ayatollah Ali Khamenei, Gaddafi n.k unawekewa vikwazo vikali na hawa mabwana wa Ulaya na Marekani.
 Ukomunisti unakwisha; unapotoweka, sasa nafasi yake inachukuliwa na kitu kingine,na ni UKATOLIKI unaofika mahali ambapo haukuwepo kama Cuba,Korea Kaskazini,China, Japan na utafika Libya,na nchi nyingine.
 Dunia inakaribia wakati wa utatu mtakatifu wa Muungano wa siasa, dini na sera moja ya uchumi duniani.
Siku hizi, Makao Makuu ya Uchumi wa Dunia ni Washington Dc.Zamani, Makao Makuu ya uchumi wa dunia yalikuwa mjini Rome,jiji hili lilijengwa mwaka 753 BC na Romulus.
Bila shaka,tutajadili Rome na Washington DC watakavyobadilishana kuukalia uchumi wa dunia kwa mara nyingine, siku chache za usoni mwetu.
Nataka kusema kwamba, Benki ya Dunia(WB) na Fuko la Fedha la Kimataifa(IMF) ni mambo yote siku hizi.
 Hata Kombe la Dunia na mashindano kama Olimpiki yatakayoanza jijini London, siku 100 zijazo kuanzia siku ninapoandika hapa, yamewekewa mikono  na mawakala wa Freemasons. Kombe la Dunia(FIFA WORD CUP) yalianza mwaka 1930; leo ni mradi unaoingiza mabilioni ya Dola za Marekani.
 Na tabia za ubaguzi wa rangi,unyanyasaji hasa dhidi ya Afrika hudhihiri sana wakati wa Kombe la Dunia,na mashindano kama Olimpiki.
Katika makala zilizotangulia, nikaandika kwamba,Hitller, naam Yule Dikteta wa Ujerumani, Adolf Hitler, ndiye alijenga uwanja wa Olimpiki wa Berlin mwaka 1936 yalikofanyika mashindano ya Olimpiki ya mwaka huo wa 1936,Hittler akamwita Mweusi,Jesse Owens wa Marekani kwamba ni mnyama.
Miaka 70 baadaye, katika mwaka 2006, wakati wa Fainali za Kombe la Dunia, kati ya Ufaransa na Italia, Marco Materrazzi akamtukana Zenedine Zidane matusi ya kibaguzi katika siku ya fainali uwanjani hapo hapo Berlin.
 Ubaguzi ungalipo hata leo, hata WEUSI wa Marekani wamebaguliwa kila mara hata wakati wa janga la Katrina. Freemasons ndiyo wanaoongoza mambo haya machafu duniani. Kombe la Dunia lenye umri wa miaka 82, mwaka 2010 lilifanyika Afrika ya Kusini kwa mara ya kwanza kabisa,na liliingiza Dola za Marekani Billioni 10,huku Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa(UN) akisema ni ‘nyenzo ya kutengeneza fedha’.
Naam, nazungumzia fedha, zinazoshikiliwa na taasisi nyeti duniani ambazo ni mawakala wa Freemasons. Mimi sizungumzii utajiri wa mtu mmoja, msinisumbue kwa visimu, mimi siyo Freemasons.
 Nazungumza utajiri wa rasilimali za dunia. Dunia nzima inapokwenda kutumia fedha moja. Ulaya sasa wanakwenda kutumia euro ingawa Uingereza haijatia mguu wake kwa pesa hii,kwa kuwa Pound  yake ingali na thamani kubwa dhidi yah ii Euro ambayo inaizidi Dola ya Marekani.
 Jumuiya ya Afrika Mashariki nayo iko mbioni kutumia fedha moja ama sarafu moja katika itifaki iitwayo, THE EAST AFRICAN MONETARY UNION (EAMU).
Hii EAMU, ilitazamiwa kuanza mwaka huu 2012,bahati mbaya haitaanza, walitumwa wataalamu kujifunza huko Ulaya ili kufuatisha namna ya euro ilivyoanzishwa na inavyofanya kazi. Yumkini EAMU ikaanza kazi baadaye mwakani.
 Sekretariati ya Jumuia ya Afrika Mashariki(EAC) na Benki Kuu ya Ulaya(European Central  Bank)walishakaa pamoja,wakatoa tamko kwamba sasa kila kitu tayari ili sarafu ya Afrika Mashariki ianze,kilichobaki ni raia watoe maoni tu,na wadau waseme ili maoni haya yapelekwe kwenye sekretarieti ya EAC.
 Naam, sarafu moja ya EAC kusimamiwa na kuratibiwa na Ulaya,yaani  Central Bank of Europe?!! Kwamba, nchi tano za Afrika Mashariki, Tanzania,Kenya,Uganda,Rwanda na Burundi wataanza kutumia itifaki ya sarafu moja hivi karibuni sana, sarafu inayolingana na kile Central Bank of Europe wamekitaka sana!
 Kichekesho ni kwamba, hata Uingereza ambayo imesita sana kujiunga kutumia euro, nao wangependa sisi kutumia sarafu ya pamoja ya Afrika Mashariki, eti ili kuinua uchumi wa watu wetu,ili kutumia mfumo mmoja wa kibenki(Union of Banking System).
Muungano wa kidunia wa biashara ulikuwepo zamani jijini Rome, na Rome uliitwa kwa jina siri kwamba ni “Babeli ya Siri”(Ufunuo 18:1-19). Itifaki hii ya ‘Single Currency” ina Baraka ya Freemasons,na lengo ni kushikilia mabenki yote, biashara zote duniani, rasilimali zote na ndiyo utajiri wote wa watu wote.
 Mipango yote ya maendeleo na uchumi wa dunia hufanywa na mawakala hawa wa Ulaya,Marekani na Freemasons,na asiwepo wa kuwapinga.
Huu mji wa siri ambao ni ‘Center of economic life of Modern World’ yaani Rome mambo sasa, watakuwa kitovu cha uchumi wa dunia-mabenki na fedha zote za dunia vitakuwa mikononi mwake,na kutolewa kwa masharti yake.
 Makao ya hawa Freemasons ndiyo yatakuwa makao makuu ya mabenki haya na mashirika haya ya fedha na mipango ya uchumi duniani.
 Haya makao makuu ya uchumi ni Babeli ya kiroho iliyoanguka kwa kuacha usafi na utakatifu sawa sawa na neon la Mungu(Ufunuo 19:1-5,Ufunuo 18:2-3 na Isaya 21:9). Babeli hawa wameacha usafi,wamekuwa ngome ya pepo wachafu na ndege wachafu kama bundi na kuna machafuko na chimbuko la ushetani mwingi duniani.
 Nataka kusema kwamba, wanachofanya Benki ya Dunia na Fuko la Fedha la Kimataifa(IMF) baada ya Mungu wa mbinguni kuacha kuidhibiti dunia,na roho wake kupingwa vikali na watu siku hizi, ni mipango kamambe ya kuiangamiza na siyo kuiimarisha dunia.
 Ndiyo maana, nchi za BRICS (Brazil,Russia,India,China na South Africa) wamechekecha vichwa,wakaona IMF na WB hawana mpango wa kuendeleza nchi yoyote, wanampango wa kuanzisha Benki yao ili kuepukana na ujanja ujanja wao na ukoloni wao.
  Ili upewe msaada ama mkopo,lazima uwapigie hawa magoti na ulambe madole gumba yao. Misaada yao ni ghiliba tupu na ufisadi na mipango kama ya Milenia (MDGs) ni maneno matupu na ghiliba kwa raia masikini, amini usiamini.
  Kwa bahati mbaya sana, hata madhehebu ya dini yanajidanganya na mabenki yao waliyoanzisha ambayo sharti kupewa Baraka za taasisi hizi nyeti kwa ukoloni,ushetani na ufreemason.
Dhambi za Babeli,ni kuuhadaa ulimwengu, wakati hao hao hao wanapopanga mauaji makubwa kwa raia masikini duniani kwa sera za ghiliba zilizojaa ufisadi mkubwa. Mashirika ya dini kumiliki mabenki kwa sera na sheria za IMF na WB?
 Jiji la Rome,limejulikana sana kwa ibada ya sanamu na miungu kama Venus aliye binti wa Zeus, Ares,Diana, Saturn, Pluto, Mercury, Neptune, Uranus, Jupiter na Juan a hata Mwezi! Huu mfumo wa ibada ya jua,nyota na sayari ulipoabudiwa Misri uliitwa Isis,Waperizi waliita Mithras na ndiyo Tamuzi aliyeitwa Ugiriki Demeter.
 Duniani siku hizi, haya masanamu ya Mungu jua,Helios, Artemi(Diana),Zeusi(Jupiter) na Mapiramidi ya Misri yaliyoabudiwa hata miaka 2500 BC KANDONI mwa Mto Nile huko Khufu,na Bustani za Babeli,ndiyo MAAJABU SABA YA DUNIA.
 Sasa,kama unabisha, kawaambie Wazungu waabudu Ziwa Nyanza,maana ndiyo baba mzazi wa Mungu wa Wamisri yaani Mto Nile, “Ra” Wanapinga.Kwanini Ziwa Nyanza mnaloita Victoria halimo kwenye maajabu saba ya Dunia, sembuse Mlima Kilimanjaro?
 Freemasons wanaujua Mlima Kilimanjaro?Wanazijua mbuga za Serengeti? IMF na Benki ya Dunia(WB) wanataka madini,mafuta,gesi na rasilimali za thamani kubwa-zinapogunduliwa kwako wewe hauwi tajiri,ila watakuhujumu hadi wao wawe tajiri kupitia hata vita. Jambo hili tumeliona Nigeria, tunaliona mahali pengi na huitwa, The Resources Curse.
 Nataka nikwambie msomaji, maboss wa IMF na WB wengi ni mawakala wa kifo walioteuliwa kushikilia taasisi hizi kuua watu masikini wa dunia.
Bahati mbaya,tunashabikia kila uchafu toka ng’ambo,tunashabikia timu zao, sinema zao kama Jaws,Star Wars,Pscho,Silence of the Lambs,Godfather n.k.Tunashangilia hata Bigbrother Africa(BBA) na kila mitindo michafu ya kutumaliza kabisa.
 Niijadili kidogo dini ya marasta(Rastafarianism) huko Jamaica, na wanasema asili yake ni Ethiopia, yaani walimwabudu Mfalme(emperor) Haile Selassie?
 Wanamuziki nguli kama Mr.Robert(Bob) Marley WALIABUDU kwa kuadhimisha kwa mitindo ya nywele ya rasta(drearock),hata Tanzania kuna rasta wengi, hawali nyama na wanavuta bangi!
 Hawa Rastafarians walipinga ubeberu wa WEUPE,wakiloni dhidi ya WEUSI na walitunga nyimbo tamu kuwaita Wazungu-Babylon!
 Babylon ni Babeli,yaani machafuko, ule mji ulioanguka, ambao Babilia inataka tuuache.Bahati mbaya, hawa Rastafarians wanarejea kosa la ibada ya sanamu na wanadamu kama Emperor Haile Selassie, ambaye wanasema ni mungu!? Hii ni ibada ya sanamu.
Tunaujadili ukweli na haki,bila kuacha kitu hata kama wengine watatukemea sana. Tunakemewa hata na wachungaji makanisani.
 Ufisadi wa kiroho na kiuchumi ni tawi la Freemasons na Illuminati.Vyombo vya habari kila siku humshangilia Ibilisi anavyofanya mauaji,vituko na unyama wake. Bunge la Tanzania linajadili ufisadi wa mali unaoletwa na ufisadi wa kiroho.
 Hata masheikh na makasisi wameacha kuujadili na kukemea ufisadi wa kiroho wanakemea zao la ufisadi huu yaani wizi na uporaji wa mali ya umma,dhuluma(Isaya 59:14).
Wenye kudhulumu wana zidi sana kudhulumu,wakati hakuna juhudi za kutakasa myoyo kama Mungu apendavyo. Kuna wizi hata wa sadaka, zaka, watu wanabuni kuiba kupitia mafuta ya Baraka ya mizeituni, vitambaa vya Baraka, uzinzi, ushoga,hata maaskofu ni mashoga na wafiraji. Mbona hata Papa anaomba radhi kwa ufisadi huu?
 Itaendelea
0765 324 074


 

6 comments:

  1. To join Illuminati is easy...Join the Illuminate cult online today where ever you are and get instant sum of 10,000,000,00 USD[dollars] with a free home any where you choose to live in the world and many other benefit as follows.we make your business grow faster and empower you...Joining the Illuminati brings you into the limelight of the world in which you live in today your financial difficulties are brought to an end your inseams lengthen we support you both financially and materially to ensure you live a comfortable life in comfortable slacks You can join from wherever you are,any part of the world[country] you are..from the UNITED STATE down to the most remotes part of the earth we bring you all you want, it dose not matter being Literate OR Illiterate Rich nor Poor anybody is advice to join If you are interested contact us now for all you seeks in life will comes to Reality. email us now:[illuminatipower666brotherhood@gmail.com]... /...or call +2348155285233 / whats-app
    say bye bye to poverty by joining Illuminati i never believe not until i finally join but now i am rich..this man is real he made me what i am today and i am very proud of me begin a Illuminati member... if they, can make me rich make me become something in life why don't you join also for you to also be rich the money always flows through the members like an ocean that never runs dry it dose not matters if you have been scam before contact him for help to join :::: NOTE; that in this Great Brotherhood Of Illuminati No Bloodshed And No Humans Sacrifices is involved [We Don't Kill For Anything] OK... Do not miss this opportunity THANKS.

    ReplyDelete
  2. Jiunge na illuminati leo na kutafuta mwanga. Fedha, nguvu, umaarufu na utajiri kuwa kichwa chake katika kizazi chako na kuona jinsi ndoto zako zinavyoweza kutokea. Ikiwa una nia ya kujiunga na makao makuu ya oda ya Illuminati ulimwenguni kote (USA), tuma barua pepe leo. Barua pepe: illuminatiworldwideorder@gmail.com
    Au nini tutumie .. +19292811087

    Kwa uanzishaji wako mtandaoni.
    Haijalishi wapi. Hakuna umbali unaweza kuathiri kazi ya baphomet yetu.

    Kumbuka .. Hatukubali kile kinachoitwa simu.

    https://www.gaia.com/article/what-is-the-illuminati

    ReplyDelete
  3. Salamu kutoka kwa MFANO mkubwa wa ILLUMINATI kwa umoja wa serikali na duniani kote, huu ni fursa ya wazi ya kujiunga na ndugu ya Mwangaza ambapo unaweza kupona ndoto zako zilizopotea, na pia ambapo unaweza kuona mwanga wa utajiri na furaha bila dhabihu yoyote ya damu. Na sisi pia kulipa jumla ya dola 700,000 kuwakaribisha wanachama wapya wote kama wao kujiunga na urafiki na pia nyumba ya uchaguzi wao na eneo na uwekezaji, pamoja na fursa hii katika maisha kwa wao kuwa maarufu.
    MATUMIZI YA KUTAWA KWA WAKAZI WAKATI ambao wanakuja.
    1. Malipo ya fedha ya USD $ 700,000 USD.
    2. Sleek Dream CAR mpya ilifikia dola $ 150,000 USD
    3. Nyumba ya ndoto inunuliwa katika nchi ya uchaguzi wako
    4. Pasipoti ya kidiplomasia kusafiri kwa nchi yoyote ya uchaguzi wako na mengi zaidi
    5. Malipo ya kila mwezi ya $ 1,970,000 katika akaunti yako ya benki kila mwezi kama mwanachama
    KUMBUKA; unaweza kujiunga na udugu wa Illuminati kutoka popote duniani India, Uturuki, Afrika, Marekani, Malaysia, Dubai, Kuwait, Uingereza, Austria, Ujerumani, Ulaya. Asia, Australia, nk,
    KUMBUKA: ikiwa una nia ya kuwasiliana nasi kupitia barua pepe yetu: illuminatitemple91212@gmail.com
    Salamu ILLUMINATI TEMPLE UNITED STATES

    ReplyDelete
  4. Ahadi ni ya wale wanaoiandaa leo, Njia ya kupata pesa haraka bila kumuumiza mtu yeyote katika maisha na kuwa bora zaidi kwenye maisha, ni kwa kuungana na agizo la Freemasonry, Wewe, tunapata tamaa zako zote za moyo, Mtu mwenye busara kutatua tatizo, kwanini mtu mwenye busara aepuke, ikiwa una nia, WhatsApp +31687718900 Unaweza kutuma kwa urahisi ujumbe moja kwa moja kupitia Instagram kwa kurasa rasmi, @Freemasonry001 au Email: agentpatrick5@gmail.com Kukaa kila wakati kutoka kwa watu hasi wana shida kwa kila suluhisho.

    ReplyDelete
  5. Hello everyone my name is Alexis Andrewi am from Italy i'm giving a testimony on how I joined the illuminati brotherhood, I was trying to join this organization for so many years now, I was scammed by fake agent in south Africa and Nigeria, I was down i could not feed my self and my family anymore and I tried to make money by all means but all in vain, I was afraid to contact any illuminati agent because they have eat my money, one day I came across a post of someone giving a testimony thanking a man called David Mark for helping him to join the illuminati brotherhood, then I looked at the man's email and the phone number that was written there, I was afraid to contact him because i was scammed a lot of times by scammers and went away with the money then I was very confused so I decided to contact the person that was given the testimony and i called him and I communicated with him on phone calls before he started telling me his own story about when he wanted to join he told me everything to do, then I made up my mind and called the agent David Mark and he told me everything to do and I was initiated, surprisingly I was given my benefit of being a new member of the great illuminati brotherhood I was so happy, for those of you trying to join this organization this is your opportunity for you to join CONTACT MR David Mark on WhatsApp number +2348140101327

    ReplyDelete
  6. hamjambo nyote naitwa Alexis Andrewi natokea Italy natoa ushuhuda jinsi nilivyojiunga na illuminati brotherhood,nilikuwa najaribu kujiunga na shirika hili kwa miaka mingi sasa,nikatapeliwa na wakala feki huko south Africa na Nigeria, nilikuwa chini sikuweza kujilisha tena mimi na familia yangu na nilijaribu kutafuta pesa kwa njia zote lakini haikufanikiwa, niliogopa kuwasiliana na wakala yeyote wa illuminati kwa sababu wamekula pesa yangu, siku moja nilikutana na post ya mtu. akitoa ushuhuda wa kumshukuru mtu anayeitwa David Mark kwa kumsaidia kujiunga na udugu wa illuminati, kisha nikatazama barua pepe ya mtu huyo na namba ya simu iliyoandikwa hapo, niliogopa kuwasiliana naye kwa sababu nilitapeliwa mara nyingi na matapeli. na kwenda na zile pesa ndipo nilichanganyikiwa sana nikaamua kuwasiliana na mtu aliyepewa ushuhuda nikampigia na nikawasiliana naye kwa simu kabla hajaanza kunisimulia stori yake ya lini anataka kujiunga. aliniambia kila kitu kufanya, ndipo nilipoamua na kumpigia simu wakala David Mark na akaniambia kila kitu cha kufanya na mimi nilianzishwa, cha kushangaza nilipewa faida yangu ya kuwa mwanachama mpya wa udugu mkubwa wa illuminati nilifurahi sana, wale wanaojaribu kujiunga na shirika hili hii ni fursa yako kwako kujiunga WASILIANA NA MR David Mark kwa WhatsApp namba +2348140101327

    ReplyDelete