Tuesday, April 24, 2012

UNATAKA UTAJIRI?-5

                                            *Mtafute nyoka aitwaye Asclepius
DESEMBA 21, MWAKA 1988, Boeing 747 ya Pan American World Airways (Pan Am) ililipuliwa na waliodhaniwa magaidi,kutoka Libya.
Ilianguka eneo la Lockerbie, nchini Scotland, na kuua watu 270, kati ya hawa 11 walikutwa ardhini.
 Hiyo ndege, Flight 103 ya Pan Am,kumbe haikulipuliwa na akina Basset Ali al-Meghri, kama ilivyokuja kujulikana hivi karibuni.
 Freemason, walipanga ajali hiyo, Shetani akalamba damu za watu hao 270,kisha wakasingiziwa ‘Mashushushu’ hao wa Libya.
 Kanali Muammar al-Gaddafi akitaka kujikomba Magharibi, akamkabidhi al-Meghri, Aprili 5 mwaka 1999 kwa Wamarekani, wakamhukumu kifo  Januari 31 mwaka 2001 kwa kosa ambalo wamekuja kusema hivi karibuni kwamba al-Meghri na wenzake hawakuhi kulifanya-Walionewa!
 Basset al-Meghri, ameachwa huru,yupo Tripoli ambako anagugumia kwa maumivu ya Saratani.
 Nimerejea kisa hiki hapa, ili msomaji makini atafakari vitu vingi sana hapa,hata kumaizi nyumerali hizi hapa ambazo pia hutumiwa na Freemasons.Halafu, nataka kufafanua utajiri unaopatikana kupitia UTATU MTAKATIFU wa Ulaya,Marekani na Mfumo Mpya wa dini unaokuja duniani, ambao nitauita, Yezebeli.
 Naam, leo najadili ‘UTATU MTAKATIFU’ ambao pia ni “UTATU MTAKAVITU” ambao ulitumiwa na Biblia katika kueleza matendo ya Balaam, Balaki na Yezebeli,katika Ufunuo 2:14-20.
Hawa, Balaam,Balaki na Yezebeli, wametajwa kuishi miongoni mwa watumishi wa Mungu,katika makanisa  ya Pergamo na Thiatira,huko Asia Ndogo.
 Balaam, Balaki na Yezebeli huwakilisha watu wa ‘tabia tatu’ tofauti ambazo nakusudia kujadili katika sehemu hii. Bahati mbaya, watu wengi wanenipigia simu kutaka niwaoneshe namna wanavyoweza kujipatia utajiri kwa kutumia Freemasons. Hawa wazingatie maelekezo haya hapa chini.
  Kwanza, Balaki alikuwa Mfalme wan chi ya waabudu sanamu na mizimu ya Moabu. Balaki alimshauri Nabii Balaam ‘Kuwalaani ‘ Waisraeli bila kupata mafanikio. Tazama Kitabu cha Hesabu sura mbili za 23 na 24.
Yezebeli, alikuwa ‘MALKIA’ alifefadhili Manabii wa Baali na Ashtoreth(1Wafalme18:19),Miungu hii ingalipo na huabudiwa katika ulimwengu wa sasa na watu pasipo kujua,kama nitakavyofafanua.
Badala ya Nabii Balaam kuwabariki hao watu wa Mungu, badala yake laana alizoitwa kutoa kwa ujira wa fedha ili awe tajiri, zikageuka Baraka maridhawa.
 Kupenda pesa kupita kiasi, ni chimbuko la uhalifu na mabaya tele duniani(1Timotheo6:10).
Huyu nabii Balaam hutajwa pia katika AGano Jipya mara tatu(2Petro2:15,Yuda 11,na Ufunuo 2:14),Balaam ni kielelezo cha tamaa ya utajiri haramu,fedha chafu na dhambi.
 Alikuwa tayari kufanya jambo lolote,mradi ajipatie fedha-hata kama ni kutoa kafara watoto na jamaa zake kwa Shetani-ndivyo dunia ilivyo leo.
Alikuwa kufanya chochote alichoambiwa na Mfalme wa Moabu,Balaki, mradi alipwe fedha, bila kujali madhara yake. Biblia inamwita Balaam ‘mkichaa’ ambaye hadi alikaripiwa vikali na punda aliyekuwa akisafiria.
Kwa mara ya kwanza,punda aliweza kusema kwa lugha ya kibinadamu,ili kuonya tama ya Nabii mpenda utajiri. Punda alisema mithili ya mwanadamu za za Nabii huyu chakaramu, mwenye tama ya utajiri.
 Hata siku hizi wangalipo manabii wengi bandia wanaomwakilisha Balamu, ambao kwao pesa ni bora kuliko chochote. Siku hizi, wangalipo akina ‘Balaam’ lukuki ambao husababisha vikwazo mbele ya watu wa Mungu lukuki.
 Biblia ya Kiingereza husema, hawa manabii uchwara wanaleta ukwazo, “Who taught Balak to cast a stumbling block before God’s people”.
Manabii wa zama hizi hupenda fedha maradufu kuliko Balaam, na huwafundisha wafalme(akina Balaki) kuleta vikwazo kwa  watu wa Mungu siku hizi ili wasujudie sanamu, mashetani na miungu kusudi lao likiwa kupata chakula na mahitaji ya kimwili. Tazama Ufunuo 2:14
Najadili utajiri haramu wanaotafuta manabii wa siku hizi na mitume wanaozuka kila siku na kuanzisha vijikanisa.
“To love gain from wrongdoing” ni kupenda fedha kwa njia haramu sana,kama kuuza wokovu kwa njia ya maji ya Baraka, vitambaa vya upako ambako ni sawa na ufisadi wa kiroho, rushwa,wizi n.k
Iko siku punda   watasema kwa sauti ya kibinadamu kuwakemea hawa Manabii na mitume uchwara, ambao wakati mwingine wamevunja ndoa za watu kwa uzinzi, wamebaka akina mama.
Yule punda aliyemkemea Balaam, atawakemea hawa ambao siku hizi wamezidi kufanya ufisadi wa kiroho na kimwili kuliko allivyofanya Nabii Balaam. Wameanzisha vijikanisa utatiri,kila mmoja na upako na kakanisa kake,ili ajipatie chakula,gari na maisha ya anasa.
 Wanajidai ‘kubariki’ watu wa Mungu kumbe ni laana tupu, watu wamejikuta wakizini na mijoka na pepo wachafu huko makanisani! Serikali ipo,lakini imewaacha hawa akina Balaam kuendeleza u-Balaam wao, na wanaposhuka madhabahuni, hulalama kwamba serikali imejaa ufisadi na wizi!!
 Naam, hawa ni ‘Mabinti’ wa Yule Kahaba aketiye juu ya mnyama mwekundu sana katika Ufunuo 17:1-11.
Hii hapa ni sauti ya punda( a dump ass speaking  with human voice) imekuja kutuliza kichaa cha manabii uchwara hawa, na mitume bandia wa Kristo uchwara na Ibilisi. Hawa waache kughilibu watu wa Mungu kwamba huwapa Baraka,kumbe laana tupu.
Waumini wajinga wametoa mali zao katika madhabau za Freemasons wakitegemea utajiri bandia, wengine wametoa kafara wake,waume, watoto na wazazi kwa taraja ta utajiri na Baraka, kumbe walidhani wamepata,wakapatikana!!
 Hii ni pata potea ya manabii na mitume wa siku hizi wenye tama ya pesa na tama ya utajiri wa haraka. Wamemgeuza kila mtu Balaam-watu wako machopima kuchuchumilia utajiri wasiojua chanzo chake-kazi zimeachwa,mashamba yameota magugu, watu wote wamewageukia manabii na mitume ili kupata utajiri!
  Serikali inahangaika kutafuta mafisadi katika Baraza la Mawaziri la Rais Kikwete? Wengine wako makanisani, wana utajiri usiojulikana, wanaendesha magari ya fahari kuliko wabunge, makatibu wakuu wa wizara, wakurugenzi n.k
Fedha na fahari wametoa wapi? Wameuza kitu gani kama siyo biashara haramu ya maji ya Baraka, vitambaa vya upako na utapeli kwa kutumia majoka?
 Juzi, Bunge liliwaka moto,wabunge wakilaani ufisadi, mwingine uko ndani ya vijikanisa,kwa manabii wa siku hizi na mitume bandia wa Kristo!
 Waziri Mkuu Pinda, akiachia ngazi kwa sababu ya ufisadi wa mawaziri wake, na hawa wasiachwe kuendelea kutapeli raia kwa jina la Yesu!
 Tamaa ya utajiri ilimfanya Balaam kushindwa kumwona Malaika wa Bwana,lakini Punda akamwona. Hawa ni vipofu,na wasithubutu kuniombea vibaya kwa miungu yao,Freemasons, watanibariki mno!!
 Naam, manabii wengi na mitume wa siku hizi ni vipofu,hawaoni na afadhali punda wana macho ya kuona vitu vitakatifu. Hujipendekeza kwa wafalme akina Balaki,mradi wapewe fedha, hata kama kwa kufanya hivyo ni kumkosea Mungu wanayejidai kumtumikia.
 Ndiyo maana siku hizi utasikia ubakaji misikitini na makanisani,kuvunja ndoa za watu,makasisi kuwatia mimba wake za watu na kutelekeza watoto! Kuna Mungu wapi bwana huko siku hizi?
Ukiwaambia wanakutafuta kukuua kwa jina la masangoma!Sasa, hawa watu wa Mungu wa wapi, serikali nayo inaacha kuwatia mbaroni ili wafungwe jela kwa makosa mengi ukiwemo utapeli, rushwa na mauaji ya watu wasio na hatia.
 Kazi yao siku hizi ni kugombania waumini. Hawa ni waabudu sanamu,ni wachoyo kama Akani, ni akina Gehazi wanaoenda vileleni mwa milima katika madhabahu za Baali kujipatia chumo la faida. Naam chumo la aibu kwa kutumia vijikanisa utitiri ambamo hakuna kitu bali kuwanga kwa makelele ya kiruu na aibu-serikali haioni?
 Hawa ni manabii wa Yezebeli, Ibilisi na Joka. Tumjadili kidogo Yezebeli wa kanisani Thiatira.Aliwafundisha watu kuabudu sanamu.Sanamu ni uzinzi wa kiroho, hivyo hata watumishi wa Mungu wakaanza kuabudu Baal-Peori! (Hesabu 25:1-3)
Yezebeli wa leo ni MALKIA aketiye migongoni mwa wafalme wa dunia(Ufunuo 17:3-18), hawa ni kundi la watu wanaojidai kumwabudu Mungu kumbe wana ajenda ya UTAJIRI na MAMLAKA YA ULIMWENGU.Makusudi yao ni kuwakosesha watu wajikwae na kula vyakula vilivyotolewa kwa sanamu(Ufunuo 2:20).
 Tumjadili pia mfalme wa Moabu,yaani Balaki.Balaki ni tajiri, ana fedha na huwalipa manabii hawa uchwara fedha na utajiri ili walete Baraka bandia kwa watu duniani-hizi ndizo ishara zidanganyazo.
 Mfalme Balaki wa Moabu ya siku hizi anafanya kila jambo hata kama kuwasingizia watu ili wapate kuwafunga jela,kama walivyowafanya wale mashushushu wa Libya, akina Basset Ali al-Meghri.Watazidi kuwaua watu huko mbele ya safari Ufunuo 13:14-17.
 Mfalme wa Moabu Balak hana tofauti kubwa na Barack(OBAMA) wa Marekani(Moabu ya kiroho) ambaye huwalipa fadhila manabii utitiri. Aina hii ya madhehebu imezuka kwa wingi Marekani,na huchangiwa fedha kuja kuendesha hadaa na utapeli huku.
  Hawa, watashirikiana na Ibilisi na Freemasons ili kujidai kuleta Baraka kwa dunia. Mfalme Balak wa Moabu ya kiroho atakubaliana na UTATU MTAKAVITU wa Yezebeli,Balaam  ili kutengeneza sanamu(Ufunuo 13:14) watafanya biashara kwa vibali maalum na wasiotaka wamewekewa vikwazo vya uchumi ili wasifanye biashara Ufunuo 13:17.
 Dunia nzima itaabudu sanamu Ufunuo 13:12. Utatu Mtakavitu wa Yezebeli, Balaki na Balaam utakusanya watu kwa vita ya Har-Magedon(Ufunuo 16:13-16) lengo ni kumpinga Mungu wa kweli kwa ishara na maajabu!
  Miujiza! Balaki, Balaam na Yezebeli, watasababisha Mapigo Saba ya Mwisho- haya ni majanga ya kiasili ambayo ukiyachunguza yataletwa na kiburi cha Moabu na washirika wako,kwa kuchafua sana anga la dunia,kukataa kusaini mikataba kama ule wa Kyoto(Kyoto Protocol) ili maji yachafuke,viumbe wafe kwa Ongezeko la joto na mabadiliko ya tabianchi, mafuriko kila mahali, vifo majanga, kansa, ukimwi,vyanzo vya maji kuwa damu,kutoboka kwa utando wa Ozone n.k
 Moabu ya kiroho(Marekani) iligoma kutia saini Mkataba wa Kyoto mwaka 1997,kwa sababu kufanya hivyo kungeleta hasara kwa wafanyabiashara wan chi hiyo-Wakaona heri kuongeza madhara kwa kumwaga hewa chafu angani ili wajipatie UTAJIRI.
Soma Ufunuo 16:1-20 uone majanga haya ambayo yanaitwa MAPIGO SABA YA MWISHO-ambayo kimsingi chanzo chake ni kiburi cha hawa Freemasons na utatu mtakavitu wao.
 Hivyo, Balak, Balaam na Yezebeli na mawakala wa Freemasons,mwisho wao umeandikwa katika Ufunuo 18:8-17. Utajiri haramu huu utakomeshwa Ufunuo18:17-19.
Balak ni Mfalme na Balaam ni nabii, wote huwakosesha waumini wa kidini na kuwapeleka kwa Yezebeli ili awalee na kuwakosesha.
 Naijadili kidogo miungu iliyowahi kuishi Mlima Olympus. Iliishi pamoja na waliokufa-mizuka!
Zeus,Titan,Poseidon ambaye ni mungu wa maji,Hades ambaye ni Pluto ambaye pia ni munguwa wafu,Hestia,Hera,Ares ambaye ni mungu wa vita-orodha ya miungu ni ndefu.
Siku hizi tunamwabudu mungu wa dawa wa Ugiriki Aesculapius (Kilatini huitwa ASCLEPIUS) ambaye huonekana akiwa kashika fimbo huku nyoka akiwa amezinga hiyo fimbo.
Nyoka ni ishara ya upya unaoleta ujana kwa sababu hujivua magamba. Siku hizi kuna falsafa ya kujivua gamba,chanzo chake ni nyoka.
 Fimbo aliyojizinga huyu ni ishara ya uponyaji kutoka kwa huyu mungu wa dawa Aesculapius-Compton’s a  Britannica Publications, Vol. 1 ukurasa wa 87.
 Huyu ndiye Yule nyoka aliyeko katika nembo ya Shirika la Afya la Umoja wa Mataifa(WHO) na ndiye nyoka Yule Yule aliyeko katika noti ya zamani ya shilingi 500. Huyu ndiye nyoka ambaye huponya ukata,umasikini,ufukara n.k Mimi sijui aliko,msiniulize namba zake za simu!!
0786 324 074
 
 
 
 
 
 
 

No comments:

Post a Comment