Tuesday, May 1, 2012

unataka utajiri?-6


                              
                   *Kuna mkono wa Freemasons katika kesi ya Charles Taylor
APRLI 26 ,mwaka huu wa 2012,Rais wa zamani wa Liberia,Charles Ghankay Taylor, amepatikana na hatia ya makosa 11 katika Mahakama ya Uhalifu wa kivita,(ICC) huko Hague.
Hukumu kamili ya Taylor inatazamiwa kutolewa baadaye mwishoni mwa mwezi huu. Bila shaka, atatumikia kifungo jijini London,Uingereza.
Tangazo la hukumu dhidi ya Charles Taylor kupatikana na hatia ya makosa thenashara, jijini Hague hook Uholanzi, hunikumbusha Filamu iitwayo, BLOD DIAMOND.
Naam, niandikapo safu hii hapa, nilikuwa nimeshikilia mkononi DVD yenye mkusanyiko wa sinema tisa,miongoni mwa hizi ni hiyo ‘BLOOD DIAMOND’.
Hakika.hii ni filamu inayosimulia vita vya aibu sana Afrika vilivyoanza mwaka 1991-2002 huko Sierra Leone, ambako eti Charles Taylor aliwafadhili waasi wa Revolutionary United Front(RUF) waliokuwa wakiongozwa na Fodday “Poppy” Sankoh, wakaua watu,wakabaka akina mama na kuwateka nyara watoto kasha kuwatimikisha katika harakati za kivita hook Kono na maeneo mengine.
Hawa vijana wadogo walifundishwa ukatili,wakaua hata wao walijigamba kwamba walikuwa, “Baby Killers” ama “Master Disasters” na inakisiwa Afrika kulikuwa na wanajeshi watoto zaidi ya 200,000.
Taylor, aliwafadhili hawa RUF silaha, nao wakampa almasi. Maswali ya kujiuliza ni kwamba: Taylor alipewa silaha na akina nani ili awape hao RUF?
Taylor, alifanya biashara hii ya kifo huko Sierra Leone na akina nani? Liberia kulikuwa na kiwanda cha silaha kama AK 47 n.k?
Majibu ya maswali haya machache tu,hupatikana katika filamu hii ya tashtiti-The Blood Diamond. Umeiona? Penda maarifa, achana na akina Kanumba!
 Narejea kuitazama filamu hiyo kwa mara nyingine tena. Namwona motto aitwaye Dia Solomon Vandy, babaye ni Solomon na mamaye aliitwa, Jassie waliotekwa nyara mnini Freetown,familia ikasambaratishwa, wakatekwa nyara, Jassie akajikuta katika kambi za wakimbizi huko Guinea,wakati Dia alijikuta akiwa ‘Baby Killer’ huko Kono!
Solomon Vandy, alipotiwa mbaroni na RUF alipelekwa kuchimba almasi, kazi aliyofanya chini yam tutu wa bunduki za rashasha.
Raia waliogoma kutekwa nyara waliulizwa: “Long leave or long sleeve?” Jibu lako lingefuatiwa na shoka kali kufyeka miguu yako ama mikono!
Namwona Daniel(Danny) Archer-Mzungu tapeli akienda katika makambi ya Waasi wa RUF, na vikosi vya Kulinda amani vya Umoja wa Mataifa,ili kufanya biashara haramu ya silaha na Almasi za Damu.
Nawakumbuka akina Kapteni Rambo na Kamanda Zero! Naam, sinema tamu hii,lakini nakumbuka niko kazini,naacha kuitazama filamu hii ya tashtiti na kurejea kuandika makala hii,UNATAKA UTAJIRI?
 Wazungu (akina Danny Archer) waliwauzia silaha hawa RUF, hata kama Charles Taylor aliwafadhili pia. Charles Taylor alipopewa hizi almasi za damu, aliziuza Ulaya.
Unafiki wa Jumuiya ya Kimataifa wakapinga Almasi za damu zisinunuliwe kutoka nchi yenye vita,kwamba ni kuzidisha vita kati ya Waasi wa RUF na serikali ya Freetown.
Nikwambie msomaji, hawa Wazungu-Blood Diamond Smugglers-kwanini hawakukamatwa na wapelelezi wa Umoja wa Mataifa kwa kuzidisha vita huko Sierra Leone?
  Kwani hawa hawakujua kwamba Taylor hakuwa peke yake katika kuwalea wale RUF ili wazidishe vita halafu almasi ziporwe?
Ajabu! Aprili 26 mwezi uliopita, Mahakama ya ICC mjini Hague ikamkuta na hatia Taylor peke yake,kwamba aliwafadhili RUF, ETI wamemkuta na makosa 11 ambayo hakuna Mzungu hata mmoja aliyehusika!!
 Nimejiuliza,na hata sasa najiuliza. Ikiwa Kiongozi wa Waasi wa RUF, Fodday “Poppy” Sankoh alishakamatwa na kupelekwa Hague rumande ambako alifia,kwa sababu gani Mzungu hata mmoja  waliobadilishana na Waasi, wakiwamo akina Kamanda Zero,hawajatiwa mbaroni?
Hata mashirika ya Kimataifa kama UNHCR,WFP n.k walitaka vita viendelee ili wadumu kupora almasi za Sierra Leone!
 Majeshi ya Kulinda Amani huko nayo yalishiriki kupora mabonge ya almasi za damu.
 Mbona mahakama hii haikuona haja ya kuwatia mbaroni akina Danny Archer kuhusiana nah ii biashara haramu ya ALMASI ZA DAMU?
Hii ndiyo “Double Standards” kwamba hawa jamaa wana macho makengeza katika kuona ukweli wa mambo pindi wanapochochea vita hapa Afrika,lakini wanaokamatwa na kushitakiwa ni akina Taylor, Laurent Gbagbo,n.k
Hakika, niliona unafiki katika mikutano ya G-8 ati ya kuzungumzia vita Sierra Leone,mikutano iliyofanywa mjini Antwerp, Ubelgiji. Unafiki mtupu,maana wale wale walinunua almasi zile walizojidai kuzuia zisiuzwe, ni kama walishirikiana na Waasi wa RUF kuua na kuteka nyara watoto na kuwaingiza vitani huku wakiwaambia kuua baba na mama zao-“Shed their Blood! Shed their Blood”!
Nataka kusema wazi kwamba, nimeuona mkono wa Freemasons katika vita vya Sierra Leone na Waasi wa Ruf 1999/2002.
Sababu za vita zimesemwa katika filamu hii, BLOOD DIAMOND. “Ivory” yaani pembe za ndovu, Oil yaani mafuta na Diamond yaani almasi. HAWA MAJAHILI walipeana shime kwamba, “This is Africa” kwa kifupi walitamka” TIA” yaani kughilibu raia ili wapigane kwamba wanasaka demokrasia,halafu wao wapore almasi, pembe za ndovu,mafuta ya Afrika na almasi!!
  Bahati mbaya, kesi imewaendea waliotumiwa na Freemasons hawa, wahusika wamebaki na aslani hakuna wa kuwagusa! Charles Taylor aliwahi kusema jambo hili,kwamba Adui yako anapokuwa ndiye Boss Wako,basi wewe ni marehemu tu-aliwasema Marekani.
  Mahaka ya Hague ni yao,wapelelezi ni wao wenyewe na wao wenyewe ndiyo wenye kuanzisha uasi na kuumaliza, halafu huwatia mbaroni washiriki wao ili kuwaziba midomo!
 Hawakuanza leo kufanya huu unyama.Vita na mapinduzi hapa Afrika vina mizizi Ulaya na Marekani.
 Guinea ya Ikweta. Mwaka 2004,nchi hii ya tatu kwa kuzalisha sana mafuta Afrika,nusura ipinduliwe na maluki.  Ilinyatiwa na Wazungu hawa mamluki waliofadhiliwa silaha na fedha na mtoto wa Waziri Mkuu wa zamani wa Uingereza, Margaret Thatcher, aitwaye Sir Mark Thatcher.
 ‘Sir’ ni mtu ambaye anaheshimiwa sana na Malkia wa Uingereza, lakini ana mamluki wanaokuja kupindua serikali hapa Afrika ili wajipatie mafuta,almasi,pembe za ndovu,dhahabu,wanyamapori n.k
Huyu jambazi, Mark Thatcher, alituma mamluki ili wakapindue serikali ya Rais TEODORO Obing Nguema Mbasongo wa Guinea ya Ikweta.
 Lengo lilikuwa wapore mafuta,na ndivyo wanavyofanya sasa Libya, hata Misri,Congo na mahali pengine.
 Ndiyo desturi ya Freemasons, wanapanga vita na mauaji makubwa kwa kisingizio cha demokrasia na Haki za Binadamu, halafu Waafrika wajinga wanapewa posho ama mishahara na kupewa silaha,wanaanza mapambano, wanapindua serikali,halafu utajiri unakwenda,wao wanapewa silaha wazidi kuuana tu-Guns for Diamonds or Guns for Ivory!!
 Huu ni uzuzu wa Mwafrika. Wale mamluki wa Thatcher walitiwa mbaroni mjini Harare, Zimbabwe, si unajua Mugabe naye haziivi na hawa majangili?
 Sasa, walikamatwa pale, wakajitetea eti ndege yao ina silaha kwenda migodini. Nakwambia ni kweli hata migodini wanaleta silaha za kivita na wanaajiri Mwafrika ili amuue Mwafrika mwenzake ili Mzigo uende!
Wanaua hata ng’ombe na binadamu kwa kemikali,nani aseme?
Basi, walipoona ingekuwa ‘soo’ rushwa ikatembea tangu Harare hadi kwa Thabo Mvuyelwa Mbeki,wakati huo Rais wa Afrika ya Kusini, akazibwa mdomo, ile siri ikawa siri sirini.
 Halafu, wanasema Afrika ni nyumba ya Madikteta kama Mobutu, Amin, Banda wa Malawi, Nguema,Bokassa n.k Nani anawalea hawa kama siyo Paris,Washington na London,ili wawatumie kama co…halafu wawatose?
 Congo(DRC) wamekamatwa akina Pierre Bemba ili wakashitakiwe huko Hague,Uholanzi, lakini walishirikiana na Wazungu wengi ambao huwaoni wakiitwa mjini Hague!.
 Vyombo vya habari vinauhadaa ulimwengu kwamba(mimi sidanganyiki) kwamba akina Bosco Ntaganda ni Waasi wanaohitajika sana ICC mjini Hague-sawa.
 Makosa ya Ntaganda ndiyo yale ya akina Fodday Sankoh, akina Thomas Lubanga na waasi wa Lord’s Resistence Army(LRA) akina Joseph Kony huko Uganda, akina Jonas Savimbi huko Angola-kuua,kupora almasi,mafuta,pembe za ndovu na kubadilishana na bunduki!
 Watoto kupelekwa vitani, ni Mzungu anayeleta vita ili waasi wawakamate watoto na kuwaingiza vitani,wao wapate kazi ya kufanya na kupora mali asili za Afrika-hii ni roho ya shetani.
 Feburuari 3, mwaka jana tu,ndege kutoka Nigeria ilitua Goma(Kongo wanapigana hadi leo) huko Kivu.Katika ndege kulikuwa na Dola za Marekani milioni 6.5 taslim. Hawa ‘Mafias’ walipeleka hizi fedha nyingi kwa majenerali Waasi(akina Ntaganda,Thomas Lubanga, akina Nkundabatware) ndiyo sawa tu na akina Jonas Savimbi ,Joseph Kony n.k hao waasi walijaza ndege hiyo kwa dhahabu na almasi za damu zenye uzito wa kilogram 400 ambazo thamani yake eti ni Dola za Marekani Milioni  19.
 Huu ni utajiri wa mtu mweusi unavyoporwa na Freemasons,halafu wakichoka kupora wanawakamata hao vibaraka wao na kuwaziba mdomo huko The Hague…aibu!
 Hawa wababe wa vita( African warlords)wanasaidiwa na Mzungu, Mafia na Freemasons,ibilisi n,k ili kuleta vita Afrika na vifo, halafu wanaimba, “Afrika Bara la Giza” na ninyi mnakubali, ‘Ndiyooo!!”
 Hamnazo?!! Mimi sidanganyiki.
 Hawa ‘Messengers of Death’ ama Mafias hawakamatwi na kupelekwa Hague-utasikia akina Uhuru Kenyetta wanakamatwa,lakini wao Shwari. Halafu tunashangilia ikitangazwa na BBC au VoA, kwamba waafrika wamekamatwa, nyie zoba siyo?
 Vita vya Sudan Kusini dhidi ya Sudan,ni vita vya mafuta,vita vya rasilimali ya Mtu Mweusi,ili zienda Ulaya na Marekani-Guns for Oil.
 Mwafrika anapewa bunduki ili akumuue mwenzake,mali iende,huu ni ujinga wa watu kupenda kutumiwa kwa ushabiki tu. Ndiyo maana hamlali usingizi Man U wanawapowashinda Barcelona! Hamnazo? Mzungu kawashwa pilipili Bercelona,huku nyie mwalia na kupiga kelele?
 Kila penye rasilimali: Mafuta,almasi,dhahabu kuna vita. Umoja wa Mataifa huu upo kuwalinda Freemason na Mafia. Siku nyingine nitaandika alivyouliwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Dk. Darg Hammarskjold, aliyekwenda Congo kutafuta amani.
Huyu, aliuliwa na CIA, WAKATI ULE AKITAKA kuwatetea akina Patrice Lumumba huko Katanga na Shaba.
JAMANI, huko   Niger Delta,makampuni ya Uingereza na Marekani yalimchochea ABACHA akawaua akina Ken Saro-Wiwa, huko Cabinda, Angola kuna vita vya kupora mafuta,Kongo kuna almasi na madini mengine hata vikosi vya kulinda amani vinapora utajiri-wanaomba hivi vita vidumu,wanasema, “This is Africa!!” kwa kifupi TIA!
Nani aletaye vita?Siku nyingine nitajadili Freemasons walivuzamisha meli ya Titanic, The Unsikable. Usinikose.
Tchao
0786 324 074
 

No comments:

Post a Comment