Tuesday, May 22, 2012

OBAMA NA ROHO TATU ZA VYURA



Juma lililopita tukaona kuanguka kwa Ukomunisti na kuinuka kwa Dola la Madola ya Ulaya na Marekani; na namna yalivyoanza kuwafyeka Wakomunisti Duniani.
Carlos, aliitwa ‘The Jackal’ na Gazeti la The Guardian la Uingereza, kufuatia  riwaya(novel) yaa Fredrick Forsyth.
Carlos, alisuswa na Chama cha Ukombozi cha Palestina(PFLP) baada ya wale magaidi wa BLACK SEPTEMBER kuvamia wanariadha wa Israeli katika kijiji cha Olimpiki huko Munich,Ujerumani Septemba 5, mwaka 1972.
Nitaeleza tukio hili kwa kina sana wakati michezo ya Olimpiki ya London itakapoanza mwezi Julai,mwaka huu-usipange kukosa TAZAMA upate darasa.
Ilikisiwa kwamba, Carlos aliwasaliti PFLP hadi wale magaidi wake wakauawa na makomando wa Kijerumani, hiyo Septemba,mwaka 1972.
Carlos,chakaramu mpenda vimwana warembo, mvuta sigara aliyekubuhu na mpenda starehe hususan, ‘kilaji’ alianza kuwa gaidi wa kukodishwa hadi alipotiwa mbaroni mjini Kharthoum,Sudan mwaka 1994.
Naam, chakaramu mpenda anasa(playboy) alishiriki Operesheni tele za kigaidi katika miaka ya 70 mna 80,tangu kuuliwa kwa hao wanariadha 11 wa Kiisraeli mjini Munich.
Hata ile ndege ya Ufaransa,Air France Air Bus, iliyotekwa na Wapalestina na kulazimishwa kutua Entebbe,mwaka 1976 zama za Dikteta Idi Amin Dada, Carlos alisuka mpango-nitaeleza kisa hiki kwa utulivu miezi michache ijayo.
Hata hivyo, Carlos anasema hajawahi kuua mtu kwa ajili ya pesa, “Nimeua watu kwa sababu ya ukombozi wa Palestina”, anasema.Ndivyo wafanyavyo al-Qaeda, na al-Shabaab, violence resistance!
 Wakati wa Mkutano wa Mawaziri wa Mafuta wa OPEC,mjini Vienna, Austria,walitekwa nyara watu 70,na Carlos alishiriki kufanya tendo hili na kuua wana usalama.Waliachiwa huru nchini Algeria, baada ya Carlos The Jackal kulipwa kikombozi cha Dola za Marekani Milioni moja ambazo sasa ni kama Bilioni 1.6 HIVI.
Fedha hizi,wanasema alilipwa na Muammar al Qaddafi, aliyekuwa akiunga mkono kitendo cha kuwateka nyara mawaziri wa OPEC huko Vienna.
 Nataka msomaji atambue uhusiano uliokuwepo kati ya Carlos, Osama, Saddam Hussein na wanaharakati wengine waliopinga ubeberu wa Kimagharibi kwa mabomu na mtutu wa silaha.
 Fedha hizi zikamgombanisha Carlos na magaidi wenzake wa Kipalestina.OPEC walishindwa kufanya mikutano kwa jumla ya miaka 25, hatimaye PFLP wakamkataa Carlos.
Akafanya makazi yake Syria(kunawaka moto wa mabomu hata leo),Lebanon(nako wako hatarini) na mahali pengine walikoungwa mkono kama Berlin Mashariki.
 Ile roho ya akina Carlos ingalipo Syria na mahali pengine,na ndiyo maana unasikia vuguvugu la vibaraka wa Marekani na Ulaya wakipingwa wasikamate utawala katika nchi hizo sasa.
 Tunajadili vuguvugu la vibaraka wa Magharibi kukamata sukani za utawala katika nchi za Ulimwengu wa Kiarabu, na kuinuka kwa ‘Roho Tatu’ za Freemasons,Illuminati na mawakala.
Wasomaji wataniuliza kama Carlos aliwahi kuoa? Naam, Magdalena Kopp,walizaa naye mtoto wa kike. Kopp alikamatwa na vilipuzi(explossives) huko Ufaransa, akafungwa jela.
 Carlos alikuwa mshirika wa Shirika la Ujasusi la Urusi(KGB) siku hizi linaitwa KFB, hivyo majasusi wa CIA na mashushushu wa Ulaya, hususan Ufaransa walimsaka sana,wakaja kumnasa Khartoum, Sudan mwaka 1994.
Kwa nini?
 Ni baada ya kuanguka kwa UKUTA WA BERLIN na kuparaganyika kwa Dola la Urusi,yaani kuanza mchakato wa ‘Kukaushwa kwa Mto Frati’ vita Baridi vikatoweka duniani, Carlos akakosa hifadhi, akatiwa mbaroni,kwa sababu dunia ilikuwa ikiungana, muungano haramu.
Carlos amehukumiwa kifungo cha maisha,Desemba mwaka 1997 katika gereza la Clairvaux, Ufaransa.
Hata hivyo, alibadili dini na kuwa Muislam,akamuoa kidosho mmoja Mwanasheria wake,Isabelle Coutant-Peyre,mwaka 2001.
 ‘Revolutionary Islam’ ni kitabu chake cha mambo yake ya Harakati zake za kigaidi. Anajitetea katika kitabu hicho,kusema alitumia risasi na mabomu kutafuta HAKI.Anamuunga mkono Osama Bin Laden, anasema alikuwa ‘Mrithi’ wake mahsusi.
 Carlos aliwahi kuandika waraka akiwa gerezani ukafika hata kwa Barack Obama.ANAILAUMU sana mahakama ya Haki za Binadamu kwa kunyimwa haki ya kuonana na wafungwa wenzake na anavyonyimwa matibabu.
 Rais Hugo Chavez wa taifa alikozaliwa, Venezuela, anamuenzi Carlos kama “Mwanamapinduzi Mpiganaji”.
Waliomuunga mkono Carlos: Saddam Hussein, Osama aliyeuliwa Mei Mosi mwaka jana,Fidel Alejandro Castro Ruz na Hugo Chavez. Mto Frati ulishaanza kukauka tangu mwaka 1994,na wafalme wa Dunia wanaanza kuunga mkono kila Marekani na washirika wake wanachosema, kukiwemo kubadili katiba na kukubali ushoga!
 Carlos akiwa gerezani anakotumikia kifungo cha amaisha, siku moja akapelekwa tena mahakamani kujibu mashitaka ya mauaji ya mawakala wa Usalama.
Alipelekwa mbele ya Jaji  Jean-Louis Bruguiere, ambako alishitakiwa kuua na kuharibu mali kwa milipuko huko Ufaransa kati ya mwaka 1982-83.
Unamfahamu Jaji Bruguiere? Nitakupa stori: Mwaka 2006 alitaka Rais wa Rwanda Jenerali Paul Kagame, akamatwe na kushitakiwa kwa makosa ya kulipua ndege iliyowabeba marais wawili wa Rwanda na Burundi, Juvenal Habyarimana na Cyprien Ntaryamirwa, Aprili 6 mwaka 1994 katika anga ya Mjini Kigali.
Wakati huo Kagame alikuwa Kamanda wa vikosi vya Waasi wa Rwandese Patriotic Front(RPF)kwamba aliwaamuru Waasi wa RPF kutungua ndege iliyowabeba marais hao waliokuwa wakijiandaa kutua wakitokea Dar,mkutanoni.
 Siku 100 za Mauaji ya Kimbari zilianza wakati huu na zikasababisha watu 800,000 kufa. Hili niliache.
Nijadili kidogo Illuminati na Freemasons wanavyopanga kupindua serikali za     dunia na hata viongozi wa makanisa yenye nguvu duniani.
Jumanne, Mei 8 mwaka huu, mwandishi Gideon M. alimkariri Peirs Comptons kupitia kitabu chake THE BROKEN CROSS  akisema kwamba Illuminati walikuwa na mpango kamambe wa kumpindua Papa Benedict XVI.
Nimemsikia Papa huyu akitangaza kutaka kuachia madaraka, nikajiuliza: Mapapa takriban wote hufia madarakani; iweje yeye astaafu,ikiwa ametawazwa Mei mwaka 2005?
 Kwamba Illuminati wanampango wa kumweka ‘mtu wao’ katika nafasi hiyo nyeti sana, kwamba kitabu hicho ukurasa wa saba na nane Peirs aliandika mpango wa kuunganisha dini zote duniani.
 Kwamba, Illuminati wana ajenda ya siri ya kuuteka Upapa na kumweka mtu wao katika ‘Kiti cha Enzi’ kinachoitwa, Sedia Gestatoria,kiti cha dhahabu chenye rangi nyekundu, ni kitu cha kuleta tashtiti.
 Mtu Fulani kutawazwa kushika mahali pa ‘Mrithi wa Mtume Petro’ maana yake siyo kuongoza Kanisa Katoliki tu,ni kuongoza Jumuiya za Kikristo,Kibudha,Waislam, Bahai’s,Orthodox,Protestants n.k
 Huyu Peirs ni kasisi wa Kanisa Katoliki na aliwahi kuwa Mhariri wa Gazeti la Universe la Kanisa hili huko Mjini Vatican.Siku hizi siri hata za ufisadi zinavuja kutoka Vatican, Hamkani si shwari Vatican.
 Kumweka wakala wa Freemasons katika kiti cha enzi Mtakatifu Petro,maana yake ni Freemasons kuongoza dini zote duniani,kuongoza imani.
 Petro,Mtume wa Bwana Yesu anaaminiwa na Wakatoliki kuwa ndiye hasa muasisi wa kanisa hilo.
Alifika Rome mwaka AD 42 akaja kuuliwa na Kaisari Nero mwaka 67 AD.Kanisa Katoliki wanasema Petro alianza Upapa mwaka 32-67 AD.
Kanisa la Mtakatifu Petro, St.Peter’s Basilica limejengwa juu ya kaburi la Petro. Papa ni Mrithi wa Petro,PAPA aliyemrithi Petro ni Linus(67-76 AD),ni Mkuu wa Vatican analindwa sana na Swiss Guard, ni Askofu wa Rome,ni mwakilishi (The Vicar of the son of God) wa Yesu duniani,ni Mkuu wa mitume wote katika zama zote,wakiwemo mitume wa siku hizi,yuko juu ya Judaism, Hinduism, Budhism,Islam n.k?
 Naam, tuzilinganishe habari hizi na mafungu ya Biblia Takatifu.
Papa anayetangazwa na moshi mweupe, ni miongoni mwa viongozi wa dini wanaoenziwa mno na mamlaka za dunia.
Tulijadili sanamu la mwanamke aketiye juu ya mnyama mwekundu sana mbele ya ofisi za Makao Makuu ya Umoja wa Ulaya(EU) huko mjini Brussels.
Angalia picha hiyo na ile ya Ufunuo 17:1-7. Mwanamke katika unabii wa Biblia huwakilisha kundi Fulani la waabuduo madhehebu Fulani. Katika Biblia kuna wanawake wawili: Ufunuo 12:1-6 na Ufunuo 17:1-18.
 Huyu mwanamke wa Ufunuo 17 anaitwa ‘kahaba’ ama mzinzi na amezaa watoto(wa kike) nao ni makahaba(Ufunuo 17:5).
Mwanamke huyu pia huwakilisha jiji kubwa duniani uitwao Babeli ya SIRI. Gideon M. AMEANDIKA kwamba kiti cha enzi cha Mji huu kinanyatiwa na Freemasons.
 Na mji huu uko juu ya vilima saba(Ufunuo 17:9) na wakati wa Nabii Yohana aliyeandika kitabu cha Ufunuo mwaka 96 AD ni mji uliokaliwa na watu wengi sana yanayofananishwa na maji mengi(Ufunuo17:15,18).
Siku hizi, miji yenye wakazi wengi ni Tokyo,wenye wakazi zaidi ya milioni 28,Mexico City,Mumbai, Sao Paulo, New York, Los Angeles,Lagos,Calcutta,Shanghai, Buenos Aires, Dhaka,Karachi, Jakarta na Osaka.
 Hata hivyo, miji yote hii katika karne ya Kwanza AD haikuwepo, na haikuwa na sifa za kuwa na wakazi wengi.
Katika karne ya kwanza, wakazi wa dunia hawakufika milioni 500.Mwaka 1AD Kulikuwa na watu milioni 200 tu duniani, siku hizi kuna bilioni saba.
 Itaendelea

0754 324 074


No comments:

Post a Comment