Thursday, May 31, 2012

UBAGUZI WA RANGI OLIMPICS


Mwaka 1936 Dikteta wa Ujerumani, Adolph Hitler, alikataa kutambua ushindi wa Mtu mweusi, Jesse Owens, aliyeshinda medali nne za dhahabu kwa dakika 45 tu, katika Mashindano ya Olimpiki ya Majira ya Kiangazi mjini Berlin .
   Hitler, alisema Jesse Owens(Mmarekani mweusi) alikuwa mnyama. Kulingana na Hitler, haikuwa haki mnyama(Owens) kushindana na Binadamu(Mzungu) katika mashindano yoyote! Binadamu hushindanishwa na binadamu na wanyama na wanyama wenzao.
  Viongozi wetu wanaweza kujidai kusahau dharau za akina Hitler, wakadhani ubeberu na unyang’au wa Wazungu umekoma. Wanafikiri ubaguzi wa rangi haupo. Huku ni kujidanganya sana ...huyo Watson hajakurupuka, kasema wanavyoamini wao.
   Jumapili, Julai 9, mwaka 2006. Italia ikapambana na Ufaransa katika Fainali ya Kombe la Dunia, katika uwanja huohuo wa Berlin aliojenga Hitler miaka 70 iliyopita na kusimika hirizi ya unyanyapaa na ubaguzi dhidi ya mtu mweusi.
    Marco Materazzi wa Italia akamtukana Zenedine Zidane ‘Zizou’ matusi yanayokaribiana na ubaguzi wa rangi. Zizou, akamtwanga Materazzi na kumwangusha chini…kapewa kadi nyekundu na mwamuzi na kutolewa nje. Alizua mjadala mkali wa kisiasa.
Zizou ni raia wa Ufaransa, mwenye asili ya Algeria , Afrika.
   Siyo Berlin tu ilikozikwa hirizi ya ubaguzi wa rangi; hata Uhispania akiana Samuel Eto’o Fils hudhaniwa nyani. Hata Seneta wa Italia, Roberto Calderoli anaamini watu weusi ni mkosi, tena si binadamu wenye akili kama Mzungu.
    Seneta Calderoli, alisema Timu ya Taifa ya Ufaransa iliyoundwa na weusi wengi, akina Eric Abidal, Claud Makelele, Thierry Henry, William Gallas, Louis Saha, Patrick Vieira, Djibril Cisse , Zizou na wengineo ndio walioitia mkosi Ufaransa ikashindwa na Italia mwaka 2006.Laiti ingeundwa na binadamu, Wazungu! Kujaza weusi wengi katika kikosi chake kukasemwa kuwa ni sababu ya Ufaransa kushindwa mjini Berlin hata miaka 70 baada ya Hitler kuujenga uwanja huo!
    Haya yalishasemwa na akina Ian Douglas Smith wa Rhodesia ya zamani sasa Zimbabwe ya Mugabe, Kaburu Balthazar Johannes Voster na P.W. Botha wa Afrika Kusini. Wanafunzi 250 wa Kiafrika waliouawa na polisi wa Makaburu mwaka 1976 kwa sababu ya kukataa kuimba Kiafrikana(lugha ya binadamu) wamesahaulika akilini mwa vigogo wetu?
   Naam, hawa ndio akina James Watson leo wanaosema Mwafrika hana akili; na huwezi kumfanya daraja moja na Mzungu!
Wazungu wengi wanaamini Mwafrika nyani; hayawani. Tunadhihirisha hili kwa kujikomba na kuwapa rasilimali zetu ili wauze na kutugawia kidogo.
   Rasilimali zetu zinajenga kwao, wanakula minofu sisi mifupa halafu tunampigia magoti Malkia, akina Gordon Brown na akina Bush. Tunakosa cha kwetu.
Tunajidai kusahau kuwa Wazungu ni walewale jana hata leo. Wao wanaona ni daraja la kwanza sisi mwisho; chetu chao, chao si chetu…kwanini hatung’amui?
   Enzi zile tulisema tumeonewa kiasi cha kutosha, tumedharauliwa sasa tunataka mapinduzi. Mbona mapinduzi hayaonekani, isipokuwa tunarejea utumwani? Itaenelea tolea lijalo.
   0786 324 074
 

Looking for last minute shopping deals? Find them fast with Yahoo! Search.
   

No comments:

Post a Comment