Monday, May 7, 2012

unataka utajiri?-(7)


                                           
                                        *NO SEX” ni kampeni ya Freemasons
NILIONA mkono wa Freemasons katika vita vya wenyewe kwa wenyewe huko Sierra Leone, mwaka 1191-2002.
 Vita hivi vya Waasi, Revolutionary United Front( RUF) dhidi ya serikali ya mjini Freetown, ambavyo vilidumu kwa miaka 11,viliwatajirisha sana mafisadi wa Ulaya.
Miaka 11 ya vita,ni kipindi cha biashara ya magendo ya ALMASI ZA DAMU, zilizopelekwa kuuzwa London, Brussels, na hata Antwerp,hata kama kulikuwa na mikutano ya mataifa makubwa kama G-8, ya kuzuia magendo ya almasi toka nchi hizi za migogoro Afrika.
Licha ya marufuku iliyopigwa mikutanoni na Wazungu hawa, bado walifanya biashara hiyo haramu ya kubadilishana ALASI ZA DAMU kwa bunduki(Guns-for-Diamonds) kati ya Waasi wa RUF,Taylor kwa upande wa pili, na washirika wao wa Ulaya ama Marekani.
 Juzi, tulimwona Charles Taylor(64) akitiwa hatiani na Mahakama ya ICC, THE HAGUE,Uholanzi, kwamba alifanya makosa 11 ya uhalifu kwa hiyo miaka 11 ya vita nchini Sierra Leone.
Akihukumiwa Mei 30 mwaka huu kuanza kutumikia kifungo cha miaka 80 bila shaka nchini Uingereza,London,ndiyo mwisho wa maisha yake uraiani-TAYLOR aliyewahi kutoroka jela huko Marekani, sasa ni ndege wa jela.
Hilo naliacha.
Nijadili kidogo Tangazo la wanaume wa Kiislam nchini Misri kuruhusiwa na sheria kufanya tendo la ndoa na maiti za wake zao,pindi wanapofariki,katika kipindi kisichozidi saa sita tangu umauti kuwakumba!
 Naam, kufanya mapenzi na maiti!
Mila hizi zingalipo hata mkoani Mara,Rorya/TARIME na hata Musoma vijijini.Wapo wanaume hufanya mapenzi na maiti,amini usiamini.
Mwanamke wa kabila Fulani anapoaga dunia(kama alishafiwa na mumewe) basi maiti yake hunajisiwa na dume jingine,eti ili atakaswe kabla ya maziko! Unyama huu huandamana na malipo-FEDHA,Utajiri?!!
 Wilayani Ukerewe,Mkoani Mwanza,mume akiaga dunia, kabla ya matanga kumalizika,mkewe huingiliwa kimwili na janadume linguine liitwalo, “OMWESYA” ili mwanamke huyo     ATAKASWE kutola laana ya kifo!
Fikiria kama Marehemu alifariki kwa maradhi hatari ya UKIMWI,halafu huyo OMWESYA kaenda kumtakasa huyo mjane,tena pasipo Kondom!!
 Ndivyo Ibilisi awadanganyavyo mazuzu hawa, ambao hulipwa ujira  wa ng’ombe kati ya wanne hadi 10, na pesa taslim ambazo si zaidi ya 200,000.
Naam, nazungumzia tamaa ya UTAJIRI. Unataka UTAJIRI? Nenda Ukerewe ukawe Omwesya, ila usiniuliza huo uzuzu,mimi sijui tafadhalini!
 Naam, Misri kuna miungu wengi.Sobek,huyu eti aliumba dunia.Mapiramidi yaliyojengwa na wana wa Israeli wakati wa utumwa wa miaka 400,na hata Waafrika walijenga,huabudiwa mno na Freemasons.
 Ziko sayari,nyota na mwezi-tumeonaa kwamba karibu kila kabila waliziabudu.Mungu-jua,TAMUZI aliabudiwa kila mahali. Huko Kom Ombo,kuna hekalu la mungu,Sobek ambaye ati aliumba dunia.
 Horus ni Mungu wa vita wa Edfu.Memphis,Sakkara na hata Cairo kuna ‘Museum’ ambamo wafu wamekaushwa,wakahifadhiwa(hawakuzikwa) wakaadhimishwa.
 Tuendako, teknolojia hii iliyoahifadhi mafaraoh wa Misri, ili waadhimishe ama waabudiwe milele, italetwa hata Tanzania na kutungiwa sheria.
Mkeo akiaga dunia,nawe ulimpenda sana, basi anakaushwa kama wale “Mummies” wa Misri,ili uendelee  ‘kula naye uroda?’ Siyo?
 Itafika wakati, na hauko mbali sana, watu watanunua maiti za wanawake warembo sana walioheshimiwa sana,  ili wafanyiwe “Mummifying Process” wasioze,ili watu waendelee kula  nao uroda hata kwa ujira.
Hii nayo fursa ta biashara bwana, wee acha tu. Si unataka utajiri? Katika Mwanzo 6:5 imesemwa kwamba siku hizi kila analowaza binadamu hapa duniani ni ovu kupindukia.
  Watu wanawaza Utajiri. Naam, utajiri.Wajinga wanazidi kuniuliza hata usiku wa manane niwape mbinu haramu za utajiri, nimewaunganisha  sauti zao kwenye simu yangu  na simu za  Poilisi na Usalama wa Taifa,ili watiwe mbaroni .
 Nijadili kidogo Tangazo moja redioni siku hizi, ambamo mwanamke anagomea kufanya tendo la ndoa na mumewe-eti ni kuhamasisha watu kuacha ukatili majumbani!
Mume au mke kudai haki ya ndoa ni ukatili majumbani? Naam, Haki za Binadamu,haki za wanawake!
 Mambo ya faragha ya mume na mke chumbani, siku hizi yanarushwa ‘live’ redioni.ili hata watoto wasikie kilichojiri vyumbani,baina ya wazazi wao! Zama za Ukweli na Uwazi(Transparency) wakati huu wa Utandawazi bwana!!
  Tuseme ukweli. Tangazo hili ni ovu sana,halina athari chanya,bali hasi.Huchochea harara(sexual drive) kwa vijana,maana sauti ya mwanamke huyo ya kukataa kumpa mumewe unyumba, inaleta harara,tamaa ya kufanya ngono-hakuna   somo lolote hapo,upuuzi tu.
Hiyo sauti ya chumbani ya huyo mwanamke kukatalia unyumba, huzidisha maradufu hamu ya ngono kwa wanaomsikiliza asubuhi. Mambo ya faraghani ya mume na mke,ati yameletwa redioni na kwenye televisheni, yanatangazwa!
 Eti hii ni kampeni dhidi ya ukatili wa wanaume kwa wanawake vyumbani! Haki za Binadamu!!
Hawa watu wa Haki za Binadamu, wanakiangamiza kizazi hiki. Wameshindwa kuzuia vita huko Congo,Somali,Sudan na Sudan Kusini n.k sasa wanazuia wanandoa kutimiziana haja zao.
 Wanafundisha kwamba, akina mama wawanyime unyumba akina baba kwa kupiga makelele redioni,midhali wanazo Haki za Binadamu.
Hii kampeni ya “NO SEX” ilianza zamani sana,katika mwaka wa 5 BC huko Ugiriki. Alikuwepo mwanamke jina lake,Lysistrata, aliwahamasisha wanawake wenzake wawanyime waume wao unyumba hadi hapo watakapokaa meza moja na adui zao na kuacha vita-cease fire Agreement.
Hata hivyo,tatizo lilikuwa vita, kwenye vita akina mama na watoto ndiyo waathiriwa wakubwa,kwa hiyo Lysistrata akaona awahamasishe wanawake wenzake wakatalie unyumba,ili wanaume wapenda vita, wakome ubishi-NO SEX!!
  Wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe Kenya, Desemba 2007,baada ya uchaguzi mkuu,Mke wa Rais,Lucy Kibaki,na Mke wa Waziri Mkuu,Mamaa Ida Odinga, walihamasisha akina mama wa Kenya nao kuwanyima unyumba wazee wao ili wakae meza moja na kurejesha amani nchini mwao.
Sasa, usiniulize kama amani  Kenya ililetwa na ‘No Sex Campaign’ maana sijui. Tumuulize Kofi Annan na wenzake waliosuluhisha mgogoro huo ambao kuna kila dalili uchaguzi wa mwaka kesho utarudi.
  ‘No Sex  Campaign’ leo ni silaha kali kuzidi misaili na ‘Biological weapons’ dhidi ya akina baba vyumbani!
 Usiponunua nguo za sikukuu-‘ No Sex’ ukikosa fedha,ukaja nyumbani bila kitu siku hiyo-No Sex! Looh, mtatuua,Kenya huko Central Province wanaume fukara wananyimwa unyumba na wanadundwa!
  Hii No Sex Campaign ilitumiwa na wanawake wa Kenya,chini ya Mwavuli wa Gender-10,kwa sababu ya machafuko yaliyoua watu 1400 wakati wengine 600,000 walikosa makazi. Hapo ndipo ilipoundwa serikali ya      GNU iliyoanza kumomonyoka.
 Hii migomo ya kimya vyumbani haiwezi kutulizwa na FFU wala GSU. Hiyo migomo ya unyumba, “Sex Strike” inayoungwa mkono na Haki za Wanawake na kuhamasishwa waziwazi redioni kila asubuhi,jioni na usiku,na mabinti zetu wanasikiliza, sijui itatufikisha wapi?
 ‘Sex Strike’ inapoungwa mkono na Haki za Binadamu ni Janga la Dunia,amini msiamini.
 Watoto waamkapo asubuhi, wanasikia Tangazo hili likieleza kilichojiri vyumbani mwa wazazi wao-kwamba Baba kanyimwa uroda,tena live!
 Naam, kampeni kali ya ‘NO SEX’ kwa wenzi wa ndoa ni dhidi ya muasisi wa ndoa-Mungu Mwenyezi,na muumbaji wetu.
Mungu,alishapiga marufuku kampeni hiyo tangu zamani.Migomo ya wanaume na wanwake vyumbani,ni marufuku.
Mtume Paulo,katika 1Wakorintho 7:3-6 amepiga marufuku, ‘No SEX campaign’ iliyotangazwa na akina Lysistrata, Ida Odinga na Lucy Kibaki,kwa sababu ya tishio la vita. Sasa nyie mnakatalia unyumba,kuna vita wapi?
 Mungu kaweka maelekezo kupitia mashauri haya ya Paulo ili wanandoa wenyewe kuzungumza kwa faragha,kupatana,kuongea kwa utulivu na kutulizana kwa faragha,ili watoto wasisikie kwamba baba au mama kala wa chuya leo.
  Sasa, Freemasons wanawachochea hawa wanawake kupitia Human Rights, inatangazwa redioni kampeni ya ‘No Sex’ tena mbele ya watoto chekechea!
 Hiyo kampeni ya NO SEX huondoa makubaliano kati ya wanandoa kama isemwavyo katika 1Wakoritho 7:4-5.
 Bila shaka, sasa tunaambiwa kwamba,ukijaribu kudai unyumba upigiwe kelele,kama siyo redioni,basi polisi,kwa Balozi wa nyumba 10,ili utiwe mbaroni kwa ukatili majumbani-domestic violence!!
  Huko ndiko tunakopelekwa na Freemasons,kwa mwavuli wa Haki za Binadamu kupinga ukatili. Ukatili ni kumpiga mama, au kumnyanyasa kumnyima haki za msingi.
 Kunyimana haki za ndoa, ni jambo jingine kubwa zaidi na Mungu amesema, “Mke hana Amri(mamlaka,nguvu) juu ya mwili wake,na Mume kadhalika hana Amri juu ya mwili wake kwa mkewe!Soma 1Wakorinto 7:1-6.
 Tangazo lile linalenga kuondoa utaratibu wa mazungumzo ya faraghani kati ya mume na mke,ili mwanaume peke yake aonekane ndiye katili anayedai unyumba kwa nguvu,ili apelekwe polisi! Mtatumalizia jela. Hivi hakuna akina mama wanaodai haki zao za ndoa kwa wenzi wao wa ndoa,kama hakuna sababu kama ugonjwa, mfadhaiko wa akili au shida Fulani ya muhimu?
 Watu wanajadiliana faraghani vyumbani,mambo yao ya ndoa, halafu ninyi mnayaanika redioni tena mbele ya watoto,mnasema ni Haki za Wanawake-Upuuzi ulioje?
  Huu ni mwanzo wa wanawake kugomea unyumba kwa baba watoto wao,kwa sababu wametimiza haja zao mitaani kwa ma-‘Serengeti Boys’ wao. Akina baba nao wakiona sasa ‘Too Much’ wanakwenda kwa Machangudoa ama nyumba ndogo, ndoa zinavunjika,UKIMWI unaingia,baa la watoto waishio mazingira magumu linapamba moto!
 Unyumba,ni tiba muhimu kwa akili za wanandoa. Wanaoshiriki tendo la ndoa kwa furaha wamethibitishwa kuwa na afya ya akili,kuliko wenye magomvi na migomo-sex strike! Kawaulize madaktari na matabibu.
 Akina Lucy Kibaki,LYSISTRATA na Ida Odinga, walitangaza mgomo wa unyumba ili kurejesha amani.
Kinyume chake, sex strike vyumbani hulenga kuleta vita vikali, na ndoa kuvunjika.Wanawake wakidai UHURU kuanzia vyumbani dhidi ya akina baba,ndiyo yale yale ya kutaka wanawake nao waoe wanaume zaidi ya mmoja!
 Sasa ndoa nyingi zinavunjika na athari zake ni kubwa mno kwa taifa. Freemasons wanajua MWAFRIKA anaheshimu sana ndoa ya mke na mume. Unajua Wazungu siku hizi wana ndoa za wanawake kwa wanawake,wanaume kwa wanaume-same sex marriages-na ndoa za mikataba.
Mwafrika,ndoa japo ya mitala huwa ya milele,na ni kati ya mume na mke tu.Sasa hawa Freemasons wameleta uchokozi wao, wanajidai Haki za Binadamu,kumbe lengo lao ni kuvuruga ndoa za Mwafrika.
 Hii kampeni ya NO SEX kwa akina baba inatupeleka kuzimu. Mungu amewapa wanaume na wanawake kuongea mambo yao faraghani,na wapatane tena wamwombe Bwana wanapofanya mambo yao.
Sasa, hawa Haki za Binadamu, eti wanatanngaza mambo haya redioni ili watoto wajue kunyimana unyumba-Je, huu ni uungwana?
 Mwanamke hana haki ya kukatalia unyumba,na mumewe naye hana haki hiyo isipokuwa mwenzi wake,ila wakipatana-sasa majahili hawa wanataka kila mwanamke awe na haki gani ya kumnyima baba unyumba,bila sababu za msingi?
Acheni upagani wenu hapa! No sex inapotangazwa redioni kwa watoto huleta maumivu ya kisaikolojia.
Akina baba wanaonyimwa unyumba,wanaposikia tangazo hili,huugua sana, wamekosa usingizi(INSOMNIA) sasa hawana afya ya kimwili na kiakili. Tangazo hili linazidisha ‘Stress’ yaani msongo wa mawazo ambao ni chimbuko la Kiharusi,magonjwa ya moyo n.k
 Tendo la ndoa kwa wanandoa ni tiba ya magonjwa ya moyo na stress. Tendo la ndoa kwa wanandoa huleta FURAHA,AMANI na AFYA ya kimwili na kiakili na mahusiano mema katika jamii.
Huu uhuru anaojidai kuleta Shetani, maana yake ni kuzidisha migomo na vita kuanzia vyumbani katika ngazi za familia ili taifa zima liwe vitani,wanaume na wanawake wakigombea unyumba.
 Uhuru humaanisha vitu tofauti kwa watu tofauti katika muktadha tofauti. Uhuru uzikurupukiwe na hawa watu,watatumaliza. Hakuna uhuru mtu kukatalia haki ya ndoa kwa mwenzi wake, pasi na makubaliano,na mwanandoa hana haki ya mwili  alionao-Hii ndiyo Amri ya Mungu,ninyi mwatupeleka’pi?
            Acheni hizo. Ndoa ni taasisi iliyoanzishwa na Mungu, siyo Umoja wa Mataifa au haki za wanawake.
 Ndoa ni taasisi inayounda taifa salama, na utulivu mkubwa taifani,kuanzisha vita katika ndoa ni kuanzisha vita taifani na duniani.
 Afya huletwa na ndoa yenye amani. Ndoa yenye fanaka hujenga Afya bora,AFYA NI MUHIMI KULIKO UTAJIRI. Afya ni UKAMILIFU wa kimwili,kiroho kiakili na ustawi mzuri katika jamii. Penya NO SEX CAMPAIGN hakuna Afya, taifa huugua.
 Jihadharini na SEX SRIKE-ni hatari kwa uhai wa taifa.
0786 324 074
congesdaima@yahoo.com

No comments:

Post a Comment