Tuesday, May 15, 2012

OBAMA AMETANGAZA UHURU DHIDI YA AMRI 10 ZA MUNGU!!



BARACK OBAMA, ni Rais wa Taifa kubwa kuliko yote Duniani(Marekani), ametangaza kuunga mkono Ndoa za Jinsia Moja,Mei 10 mwaka huu.
Tangu uhuru,Julai 6 mwaka 1776,hakuna Rais wa Marekani,miongoni mwa marais 43 waliomtangulia, aliyewahi kuunga mkono ushoga na usagaji.
Obama, ni Rais wa 44 wa nchi hii inayofananishwa na MWANAKONDOO mwenye pembe mbili(Tazama Ufunuo wa Yohana 13:11-18) katika Biblia.
Nchi iliyowatunza Wakristo na kuwapa upendo(lamblike beast) yenye kutenganisha masuala ya dini na siasa(separation  of powers), inaoneshwa katika unabii huu kuwa ilikuwa na pembe mbili(two horned).
Pembe,katika unabii ni mamlaka(Zaburi 18:2,Luka 1:69).Pembe mbili zinatafsiriwa vizuri katika sanamu liitwalo, THE STATUE OF LIBERTY; umewahi kuliona?


sanamu la uhuru,Mwenge na BIBLIA,sasa Rais Obama ametangaza uhuru dhidi ya AMRI 10 za Mungu, hususan zinazopinga ushoga!


Sanamu hili, tangu mwaka 1886 linaashiria Dunia nzima kwamba Marekani kuna uhuru wa kusema na uhuru wa kuabudu. Lilisanifiwa na kujengwa na Mfaransa, Frederic Auguste Bartholdi(1834-1904).   
Wafaransa waliwakabidhi Wamarekani sanamu hili la Uhuru ambalo lipo mbele ya lango la Bandari ya mjini New York. Sanamu hili ndilo huwakaribisha wakazi wote wa Dunia mjini New York ambao hufika nchini humo kwa meli.
 Kuna mwenge unaoshikiliwa na mkono mmoja wa sanamu hili, unamaanisha UHURU na demokrasia, na mkono wa pili unashikilia Biblia kuonesha uhuru wa dini,ama uhuru wa kuabudu,tofauti na ilivyokuwa Ulaya.
 Sanamu hilo lilikamilika kujengwa Mei 21, mwaka 1884. Uzito wake ni Pauni 450,000 au tani 225. Sanamu hilo ambalo ni makumbusho ya Taifa, mkono wake wa pili umeshika Biblia, kuonesha uhuru wa watu kuabudu,bila kulazimishwa.
Sanamu hili la uhuru linalotenganisha masuala ya dini nay a kiserikali,na linalohamasisha demokrasia na uhuru wa dini,kwa karne nyingi, limeashiria demokrasia na uhuru ukiwemo wa ibada katika nchi hii.
Hata hivyo, kwa Tangazo la Rais Obama kwamba yeye na mkewe,Michelle, na  bintize, Malia  na Sasha, na rafiki zao wa karibu,hawaoni ubaya wa ndoa za jinsia moja,na kwamba wanawaunga mkono mashoga na wasagaji, maana yake ni kama ifuatavyo:
Kwanza, Obama ni Rais wa Taifa kubwa duniani. Kauli yake ni kama Amri ya 10 ya Mungu Duniani! Mivuto yake katika dunia ni mikubwa sana kwa watu wengi.Sasa kutangaza kutoona ubaya wa ushoga na usagaji,maana yake ni kuutangazia Ulimwengu kwamba wanaopinga ushoga,ni wajinga na wapuuzi hivi.
Maana yake ni kwamba, ni kusisitiza nchi masikini duniani kubadili Katiba zao ili kuunga mkono ndoa za Jinsia moja, kwa kuwa hata Obama anaona hazina shida, ndiyo maana hata yeye mwenyewe alishawachagua mashoga takriban 200 katika nafasi za juu za utumishi wa umma serikalini mwake.
 Sasa, tunaingia rasmi katika Sodoma na Gomora. Marekani iliyokuwa nchi ya uhuru wa siasa na Dini, imeanza kunena kama JOKA-Ibilisi, Obama kutangaza kuunga mkono ushoga,maana yake ni kuutangazia Ulimwengu UHURU dhidi ya Sheria za Mungu muumbaji, na uhuru dhidi ya mbinyo wa AMRI 10 ZA MUNGU.
Katika Ufunuo 13:11 Biblia inatabiri kwamba,Marekani yenye uhuru,demokrasia na haki za binadamu katika katiba yake, sasa ingeutumia UHURU huo na demokrasia kuachana na Mungu na matakwa yake na kwenda katika njia ya Shetani(kunena kama Joka).
 Makamu wa Rais wa Obama, Joe Biden na Waziri Mkuu wa Uingereza,David Cameron  ni miongoni mwa watu wakuu duniani wanaounga mkono ushoga na usagaji.Wewe nani hadi upinge? Ukipinga, unapinduliwa, tena wanyimwa msaada,unawekewa vikwazo-economic sanctions!!
 Marekani,nchi ya Waprotestanti,Wakatoliki ni wachache. Marekani inaanza kunena kama JOKA ambaye ni Shetani. Nchi hii ya Wakristo wengi wanaoamini kwamba NDOA ni muungano kati ya watu wawili wa jinsia tofauti, ndoa iliyohasisiwa na Mungu mwenyezi katika Bustani ya EDENI, sasa imeanza kutangazwa kwamba ni muungano wa watu wawili,mradi wawe na umri kuanzia miaka 18.
 Dini ya Angican(Malkia Elizabeth ndiye Mkuu wake) ilishakubali ndoa hizi za mashoga, ingawa Kanisa hili hapa Afrika linapinga jambo hili na kusisitiza kuwa ndoa iwe muungano wa hiari kati ya mume na mke.
Askofu, V. Gene Robinson wa Jimbo la Hampshire huko Marekani ndiye askofu wa kwanza mume kuolewa na mwanaume mwenzake aitwaye Mark Andrew. Ni miaka michache tu iliyopita, na hawa walifunga ndoa kanisani tena mbele ya ndugu zao wa pande mbili.
 Majimbo takriban 10 ya Marekani yamekubali ndoa hizi, na majimbo mengine mashoga wanafunga ndoa kwa leseni. Haya mambo yamefika hadi Afrika ya Kusini,na Kenya nayo iko hatarini, hata Tanzania katiba yetu inaweza kuwekwa kipengele cha haki za  mashoga na wasagaji kuoana.
 Naam, huu ndiyo uhuru na demokrasia tunayotaka, ndiko tuendako,ukurasa mpya umefunguliwa na Obama na David Cameron, huu ni UHURU DHIDI YA MUNGU!
 Unaweza kujiuliza kwamba, Marekani inaheshimu sana demokrasia na uhuru wa watu? Mbona gereza la Guantanamo huko Cuba,linawatesa wafungwa na raia wanahukumiwa katika magereza ya kijeshi,hata kama ni magaidi?
Kuanzia hapa,tunamaizi kwamba Mungu ameanza kupingwa waziwazi na sheria zake zinazopingwa ushoga na usagaji zimewekewa kibanzi,ili zisitumike,ndiyo Marekani kunena kama JOKA.
                                                          (ii)
Nijadili kidogo kuanguka kwa ukuta wa Berlin mwaka 1994,kwamba kuliashiria kumalizika kwa VITA BARIDI,baada ya Vita vikuu vya Pili vya Dunia 1945.
 Kumalizika kwa vita Baridi,vilivyoanza baada ya vita vya pili kwisha, maana yake ni kuufagilia mbali UKOMUNISTI.Dola la Urusi la Kisovieti(USSR) liliparaganyika tangu mwaka 1991.
Ukuta wa Berlin ulioitenga dunia katika Mihimili miwili ya Magharibi na Mashariki ulishavunjwa na kuifanya dunia kuwa kama kijiji kimoja. Kuanguka kwa Ukuta wa Berlin na Kuparaganyika kwa Dola la Kisovieti la Urusi(USSR) ni kuonesha kwamba ubepari ulikuwa umeushinda ujamaa duniani.
 Tunaishi katika zama za MWENYE NGUVU MPISHE.Kuanguka kwa ukuta wa Berlin na UKOMUNISTI maana yake ni kwamba “Mto Frati” uliokuwa ukiitenda dunia ya zama za Waisraeli kati ya Mashariki na Magharibi, ulikuwa umeanza ‘kukaushwa’.
MMchakato wa kukaushwa maji ya Mto Frati(the dries up process of the River Euphrates) ulishaanza,ili njia itengenezwe wafalme watokao nji za Mashariki(UCHINA,INDIA,JAPAN n.k) wapiti na kwenda kuungana na madola ya Magharibi. Tumeona mataifa ya Kisovieti yakijiunga NATO na Umoja wa Ulaya EU.
 Tumeona, Uchina,Urusi, Japan,Korea Kusini,Pakistan,India n.k wakishirikiana na Mataifa ya NATO hata kutoa ardhi zao kwa majeshi ya NATO na mashirika ya kijasusi kama CIA na MOSSAD kutekeleza Operesheni anuwai za kijeshi.
Tumeona nchi za Kiarabu zikigeuza ardhi zao kuwa Base za kijeshi za Marekani na washirika wake, tunaona juhudi za mataifa ya Mashariki hata kujiunga umoja wa sarafu moja ya Euro-Euro Zone , tunaona juhudi za Mashariki kushiriki Soko la Pamoja Ulaya European Common Market n.k
 Ufunuo 16:12-16 huonesha wazi kwamba nchi za Kisovieti na zingine za Mashariki na mrengo wa kijamaa, zitaungana na Ulaya na Marekani, na zitaachana na imani zao na ibada zao na kwenda kuungana na roho za  mashetani, za Freemasons na Illuminati,ndiyo ROHO ZA VYURA na manabii wa Uongo(Ufunuo 16:13-16)
 Har-Magedon, ni vita dhidi ya Mungu na Amri 10. Mataifa yote ya Dunia yataungana ili kumpinga Mungu,yataungana na Ibilisi kwa misingi ya kusaka uhuru na demokrasia.Pepo wachafu wataungana na wanadamu ili kukataa mafundisho ya Mungu na maagizo yake,wanaanzia kwenye kanuni za ndoa na imani ya kweli.
 Dunia nzima itaungana kiuchumi,kisiasa, na wale waliokuwa na itikadi za Carl Marx(Marxists) wataondolewa kwa nguvu kubwa.
Hadithi ya Illich Ramirez Sanchez(Carlos The Jackal) inatuonesha namna hawa Wa-Marx walivyoshindwa na ubepari.
Carlos The Jackal(63) alizaliwa Caracas,Venezuela mwaka 1949. Babaye alikuwa mfuasi wa siasa za Karl Marx akawahusudu mno wanamapinduzi wa Amerika Kusini: Carlos Merighella, Camillo Torres na Che Guevara.
Carlos, ni mfano wa Osama bin Laden wa zama hizo, alipinga ubeberu wa Magharibi kwa njia ya nguvu za kigaidi,Mungu hataki kutumia njia hizo ili kuleta haki duniani.
 Alisoma katika Chuo cha kijeshi cha Mantanzas huko Havana,Cuba na akatokea kuwa Komandoo kutokana na walimu wa medani za kijeshi wa                   Urusi.
 Babaye hakumwamini Mungu na mamaye alikuwa Mkatoliki,wakaachana. Carlos alikwenda London, baadaye akapelekwa kkusoma katika Chuo Kikuu cha wanamapinduzi cha Patrice Lumumba,huko Moscow.
 Carlos, alikuwa ‘troublemarker’ dhidi ya maslahi ya mabeberu wa Magharibi. Akajiunga na Chama cha Popular Front for The Liberation of  Palestine(PFLP) Wakateka nyara watu na ndege za Magharibi ili kudai uhuru wa Palestina.
 Carlos, alijiunga na PFLP mwaka 1970 akapewa jina la Carlos kwa sababu ya asili yake ya Venezuela, Amerika ya Kusini.
 Aliitwa, The Jackal na gazeti la The Guardian la Uingereza kufuatia kisasiri(novel) cha Mwandishi Fredrick Forsyth.
Itaendelea
    0786 324 074
 
 
 

No comments:

Post a Comment