Thursday, May 31, 2012

MASKINI CHARLES TAYLOR

  TITANIC,
TUREJEE kidogo katika somo la Kuzama kwa Meli ya Titanic.
Kwamba, ilizama kwa maelekezo ya Freemasons. Nahodha wa Meli ya Titanic, E.J.Smith, alielekezwa kuizamisha meli ili kuwaulia mbali matajiri waliokuwemo.
Mhariri wa Makala wa Gazeti hili, Markus Mpangala,Mei 22 mwaka huu akawataja matajiri hawa walioangamia katika ajali hiyo kwamba ni John Jacob Astor,Archibald W.Butt,Charles M. Hayes,na mkewe na binzi zao, W.T.Stead,Benjamin Guggenheim, F.D.Millett na G.D.Widher.
Wengine walioangamia ni Isidor Strauss, na mkewe,J.B Thayer,J,Bruce Ismay,Henry B. Harris na mkewe na Washington A.Roebling.
Sina haja ya kulumbana na mtu kwamba Freemasons ambao kimsingi ni mawakala wa Ibilisi hawasababishi ama wanasababisha kutokea kwa majanga. Sote tunajua kuna nguvu mbili zinazoshindana duniani, nguvu ya wema na ile ya kufanya mabaya. Freemasons ni mawakala wa Ibilisi wenye kazi maalum ya kuhadaa watu,wakidhani wanafanya mema.
 Hata hivyo, Alex Mayoge wa Moshi,Kilimanjaro aliniandikia SMS kusema kwamba TITANIC ILIZAMA ili kuwaua matajiri hao ili Freemasons wapore fedha zao kwenda kugharimia VITA VYA KWANZA VYA DUNIA.
Titanic ilizama Aprili 1912 na ni miaka miwili baadaye,mwaka 1914 vita kuu ya kwanza ya Dunia ikaanza kwaka 1914.
 Vita vila lengo Fulani, na aghalafu vita wanavyoanzisha Freemasons ni vya kupora rasilimali ama kuweka mamlaka yao mahali wanapopingwa,nguvu za ushawishi zinaposhindikana.
Vita vya Pili vilianza 1939 vikakoma 1954. Tulishajadili jambo hili kwa kina,na anayetaka aangalie Blog yangu kuhusu vita hivi na matokeo yake.
Malengo ya maharamia hawa yangalipo duniani,ndiyo maana kuna vita leo Congo na maeneo mengine kama Sierra Leone, tuliona Revolutionary United Front wakipewa silaha kuharibu serikali ya mjini Freetown,ili wapore ALMASI ZA DAMU.
Mwisho wa siku Fodday Sankoh alikamatwa na kupelekwa The Hague ambako eti alifariki ama kunyamazishwa, leo niandikapo hapa Taylor anahukumiwa kifungo cha miaka mingi huko jijini London,Uingereza?
 Soma  tamthilia hii kama kichekesho tu(Satire) cha Taylor huko Mahakamani Hague, dhidi ya wakubwa.
     CHARLES TAYLOR 64 + 80
 
 
ASKARI:           Koooortiiiii?
 
(Mahakama ya Umoja wa Mataifa,ICC,inaanza kikao chake, ‘session’ mjini The Hague, Uholanzi.
Washitakiwa, maofisa wa Mahakama wanaingia,na watu  wote ndani ya mahakama hiyo wanasimama wakati wa majaji kuingia kortini, ambamo Taylor anashitakiwa kwa makosa 11 ya uhalifu wa kivita huko Sierra Leone tangu 1991 hadi 2002, akiwasaidia United Revolutionary Front).
 
KARANI:       Charles Ghankay Taylor dhidi ya Haki za Binadamu?
 
TAYLOR:      Timamu, Mheshimiwa Jaji, Lussick. Hata hivyo nashangaa,katika kesi hii washitakiwa wenzangu, akina mabwana George W.Bush na Tony Blair wameachwa. Haidhuru! Nimamaizi Mheshimiwa Jaji, mahakama hii ya ICC hapa Hague ina makengeza!
 
JAJI  LUSSICK:    Mwendesha Mashitaka una hoja?
 
MWENDESHA MASHITAKA:    Mshitakiwa aliwafadhili Waasi wa RUF walipoua watu huko Sierra Leone, akawatumikisha watoto maelfu jeshini kwa muda wa miaka 11; naye ana makosa 11.
 
JAJI LUSSICK:    Mshitakiwa, Charles Taylor,Rais wa zamani wa Liberia, unapaswa kuieleza mahakama hii tukufu, una maanisha nini kusema mahakama ina makengeza? Mahakama ina macho?
(kicheko cha kwikwi toka kwa wasikilizaji)
 
TAYLOR:   Mheshimiwa, sina maana kwamba mahakama ni kipofu; ila ina makengeza! Haina macho, mahakama ina ‘double standards’ yaani upendeleo, haiwaoni Wazungu tuliosaidiana nao kuwafadhili United Revolutionary Front(RUF) ili wapore ALMASI ZA DAMU ili ‘deal’ hii itupe utajiri? Sasa mheshimiwa, kazi tumefanya wote na akina Bush na Blair, eti ‘zengwe’ nasukumiwa mimi peke yangu. Hiyo noma Mheshimiwa!
JAJI LUSSICK: Okay! Okay! Nimekupata Mr. Taylor, ohh..samahani, Mr. X-President! Hata hivyo hujakana shitaka lolote kati ya haya 11 unayokabiliwa nayo?
TAYLOR:      Nikanushe nini Mheshimiwa wakati mlikwishaamua kunitosa?
JAJI LUSSICK:   Tumuulize Mwendesha Mashitaka Mkuu,Louis Mareno-Ocampo. Kwanini Taylor? Why Taylor, and why not Wazungu in this TRIAL?
OCAMPO:    Mheshimiwa Jaji,Lussick, Rais Mstaafu wa Liberia, Bwana Caharles Taylor alishatakiwa na wenzake kama Fodday Sankoh,kiongozi wa RUF.
 TAYLOR:  Mheshimiwa, nataka Ocampo aieleze hii mahakama ya Fisi ambako mimi Mbuzi leo nasulubiwa kinyama! ‘Poppy’ Sankoh ni mshitakiwa namba ngapi katika kesi hii?
 OCAMPO: Sankoh hayupo hapa mahakamani. Kama mahakama inakumbuka, alifariki akiwa rumande hapa mjini Hague.Waasi wengine wakikamatwa upelelezi ukikamilika nao tutawashitaki, hakuna ‘impunity’ kwa mkosaji yeyote.
TAYLOR:  Mheshimiwa, inakuingia kichwani kwamba mimi peke yangu ningeweza kufadhili RUF kuua watu,kubaka,kukata raia viungo na kupeleka watoto 200,000 vitani,kama siyo msaada wa Bush,Blair na ‘Wadosi’ wengine wa huku ‘majuu’ mheshimiwa, kama siyo kunionea?
JAJI:                   Swali jingine?
TAYLOR:       Mimi peke yangu ningewezaje kumpa Poppy Sankoh ‘shavu’ kwa miaka thenashara, hadi akombe ALMASI ZA DAMU Sierra Leone? Eti wanasema mjini Johannesburg nilimhonga yule kimwana, Naomi Campbell bonge la almasi ghafi. Hizo almasi nilizipataje na nilikuwa namuuzia nani, Mzungu au Mwafrika,Mweupe au mfupi, mnene au kimbaumbau? Ebo! Noma mheshimiwa!!
(kicheko cha kwikwi kutoka kwa wasikilizaji mahakamani)
BRENDA HOLLIS:    Taylor na Sankoh walishirikiana kufanya uhalifu Sierra Leone,KWA MTUTU WA BUNDUKI, walipora almasi za damu na kuziuza kwa wateja wao Ulaya na Marekani
TAYLOR:    Tena huyu Brenda Hollis,Mwendesha Mashitaka ni mpuuzi kabisa, afadhali Ocampo, tuliua watu kwa bunduki? Umesikia Liberia kulikuwa na kiwanda cha bunduki kama AK 47?
OCAMPO: (anasimama) Mheshimiwa Jaji, ALMASI ZA DAMU zilisafirishwa kwa magendo hadi Afrika Kusini hadi Ulaya na Marekani ambako walibadilishana na Wazungu kwa almasi kwa bunduki yaani Guns for Diamonds mheshimiwa!
 TAYLOR:   Basi poa, Mheshimiwa Jaji, sasa wanataka mimi nikanushe nini kama hata wao wanajua Mzungu alifanya vikao vya G-8 vya kinafiki huko Antwerp, kukataza biashara ya almasi za damu,kumbe naye alizimaindi?
  JAJI:          kama sijakosea, swali la mshitakiwa ni kwamba, kwa nini upande wa mashitaka haujawaleta mahakamani walionunua almasi za damu toka Sierra Leone,badala yake wamewaleta wauzaji peke yao?
TAYLOR:   Hewaa! Jaji,kumbe hukusoma mwembeni na kupata digrii za ‘madensa’ ila umebukua sheria! Umenipata! Huyu Ocampo kwao ni Buenos Aires, Argentina, sasa ni kibaraka wa Mzungu wa Ulaya hajui EU walipora almasi za damu licha ya sheria kupiga marufuku biashara hiyo, halafu anatukamata Waafrika tu! Wapi Wazungu hapa bwana? Hiyo siyo ‘Fair Play’ ni Unfair kabisa, Noma msikaji!!
  (minong’ono na miguno inasikika mahakamani)
OCAMPO:    Waheshimiwa Jopo la Majaji, mshitakiwa athibitishe kauli yake kama ICC inawashitaki Waafrika tu,na aslani hakuna Mzungu hata mmoja! Hiki siyo chombo cha Umoja wa Mataifa(UN) na nchi 54 za Afrika hazijaridhia Mahakama hii tukufu?
TAYLOR:    Hawa mabwana wanatutuma kazi,tunatesa raia,tunakwiba rasilimali na fursa zao nyingi,ili Punda afe Mzigo ufike! Halafu baadaye wakitosheka wanaanza kutuchonganisha na raia na maandamano kama walivyofanya Libya,Misri kwa Mubarak,Tunisia kwa Ben Ali n.k Je huu ni uungwana Mheshimiwa? Tunapora nchi zetu kwa ufisadi na kuleta mzigo halafu kisha wanatusaliti! Huu siyo uungwana mheshimiwa!
JAJI: Hujaitajia mahakama Waafrika wangapi wamekamatwa peke yao na kushitakiwa The Hague?
TAYLOR:  Mimi ningali Rais halali wa Liberia, huyo Hellen Johnson Sielief, wamemleta wao ili atawale kisha mimi waninyonge! Wanasema hakuna ‘Impunity’ wakati Blair,Bush wanavamia na kuua hakuna mashitaka! Mnataka nife kama Gaddafi na Saddam?
JAJI:  Enhe, wewe na wengine kina nani? Wataje mlioshirikiana kuua raia mkapora utajiri wa Afrika na kuuficha Ulaya na Marekani.
 TAYLOR: Simple, Fodday Sankoh, Laurent Nkundabatware, Jean-Pierre Bemba, Laurent Gbagbo, hawa ‘Ocampo Six’ mmewaacha mkachagua ‘Ocampo Four’, halafu mnamtaka Omar Hassan Al Bashir, Tomas Lubanga,Joseph Kony,Paschal Ntaganda.
JAJI:                  Umemaliza?
TAYLOR: Mobutu, Savimbi,mbona hamsemi mliwasaidia hawa kupora utajiri wa Afrika na kuuhamishia Ulaya na Marekani sasa Afrika ni The Shame of poverty in   Plentiful?
OCAMPO:  Mheshimiwa,huyu jamaa sijui hamnazo, au kachapa kilaji! Amesahau Slobodan Milosevic wa Serbia naye alishakamatwa mwaka 2000? Atasemaje kwamba tunawakamata Waafrika tu?
TAYLOR: Mimi siyo mlevi,ninakupa ‘facts’ usianze chuki zenu hapa. Mimi ni Rais halali Liberia wananchi wananipenda, Marekani wamenitumia nikapora almasi za damu na kuwapelekea,sasa wanasema mimi
 muuaji. Guns for Diamond ningefanyaje miaka 11 bila kushirikiana nao? Wazungu, acheni kufikiri Mwafrika zoba, hamnazo?
(kicheko mahakamani, zinasikika kelele za mashabiki wake nje ya mahakama wakishangilia)
 
  JAJI: Order! Hapa tuko mahakamani,hatupo baa! Utulivu tafadhali! Enhe, Taylor endelea kuuliza swali kama unalo; lakini wewe siyo among the wealthiest in the world?
TAYLOR:   Umbeya tu mheshimiwa. Hawa wanatuchonganisha na wananchi wetu halafu wanasanua deal kwa mitandao yao kama weakleaks, wanachochea maandamano kwa facebook na twitter
OCAMPO: Kwani Wazungu hawakamatwi?
TAYLOR: Baada ya Adolf Hittler baada ya Vita ya Pili ya dunia nani aliyehukumiwa Hague,kama siyo mimi mnataka kunionea eti nifungwe miaka 80,sasa nina 64, ndiyo nini kama siyo kuniziba mdomo nisiseme mlivyopora ALMASI ZA DAMU huko Kono, Sierra Leone? Eti mnataka kunifunga Uingereza!!
  JAJI: Hoja yako ni ipi hapa?
TAYLOR:   Ukiacha wale NAZIS, hawa jamaa ni matapeli hawajamkamata Mzungu, wanatukamata sisi Waafrika tu, wana ‘double standards’ mheshimiwa Jaji na mambo haya hapa siyo kesi ni siasa tupu-This massive inequality can be traced back to cold war politics!!Sikubaliani na ukoloni wa ICC,WALA hakuna human rights wala transparency international wala nini!!
JAJI:  Wakili wa mshitakiwa una swali?
WAKILI: Taylor, kina nani wengine wanaonewa na ICC?
Taylor:  Hata mashirika ya wakimbizi na mengine ya Umoja wa Mataifa Congo,Dafur, Sierra Leone n.k wizi mtupu, dunia haina amani ni utapeli tu,vita wachochee wao,tushitakiwe sisi akina Taylor, Mobutu Sseseseko,Jonas Savimbi, Bosco Ntaganda,Thomas Lubanga,Jonas Kony,orodha ni ndefu mheshimiwa! Hawa wote husaidiwa na Wazungu kuharibu amani,uchumi na usalama wa Afrika,halafu hugeuka chameleon?
(anainamisha kichwa kuonesha ameridhika, anaketi)
JAJI:   Badala ya kukanusha mashitaka  unalalamika sana kwamba umeonewa,kwamba ICC inawaonea Waafrika tu. Mahakama imeona una hatia ya mashitaka yote thenashara! Upande wa Mashitaka una hoja?
 
BREBDA HOLLIS:    Huyu jamaa afungwe miaka 80, ukijumlishe umri wake wa miaka 64 maana yake ni kwamba afie ‘nondo’ ama mangenge ili liwe fundisho kwa ‘masera’ wenzake wanaoua raia!
JAJI:      Hukumu KAMILI Mei 30 mwaka huu 2012.
ASKARI:       Kooooortiii!!
 Mei 30, magazeti ya Tanzania yanaandika, “Taylor anyeshewa mvua ya miaka 80 jela!” mara, ‘Taylor kunyea mtondoo!”
                                   TAMATI
0786 324 074 ama www.congesmrambatoday.com
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 

No comments:

Post a Comment