Tuesday, October 1, 2013

AL-SHABAAB,AL-QAEDA


    !                                
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa,Ban Ki-Moon, ambaye ni raia wa Korea Kusini, hana ubavu wa kusema ukweli kuhusu chimbuko la kitisho cha magaidi hapa Duniani.
Kama hajipendi, anaweza kumfuata kuzimu Katibu Mkuu wa Pili wa Umoja wa Mataifa,Dk.Darg Hjalmar Carl Hammarskjold wa Sweden!
KI-Moon, anatoka nchi kibaraka wa Mataifa Makubwa ya Magharibi, ambayo yameigawa Dunia katika mihimili miwili.
Ugaidi, ni zao la chuki za zama za Vita Baridi,kufuatia Dunia kutengwa mafungu mawili.
Korea mbili ni adui wakubwa,kufuatia kutengwa katika siasa za Kikomunisti na kibwanyenye.
Inakisiwa kwamba,Warusi(Wakomunisti) walikuwa wakidhibiti maisha nchini Somalia tangu mwaka 1968.
Walikusudia kujitanua hadi nchi zote za Upembe wa Afrika(The Horn of Africa) ambazo ni pamoja na Eritrea,Ethiopia, na Djibouti.
Kufuatia hali hiyo,Rais Jimmy Carter wa Marekani alikuwa na wajibu kuzuia Warusi kusambaza ushawishi wao Somalia,Ethiopia na mataifa ya jirani ya Kiarabu.
Urusi,ilikuwa na vituo vya kijeshi(Military Bases) katika nchi hizi za Upembe wa Afrika,hadi katika njia kuelekea Arabuni na Afghanistan na Pakistan.
Kwa hiyo,Marekani ikawa na kazi ya kuondoa ushawishi na utawala wa Kisovieti(Soviet Imperialism) katika Upembe wa Afrika.
Wakati huo, CUBA na raia wake walitoa msaada mkubwa hapa Brani Afrika.Cuba ilikuwa “Mkono Msaidizi” wa Dola kuu la Kisovieti(USSR).
Msomaji, unaweza kutambua sasa kwamba nchi zote za Ulaya Masharikizilionekana kuangukia zaidi siasa za mrengo wa kushoto wa Kambi ya Mashariki,na siasa zao za Ki-Marx na Lenin.
Kwa sababu hiyo,mataifa ya Ulaya Magharibi(ikiwemo Marekani) yalihaha kuhakikisha kuzuia Ukomunisti usisambae mithili ya saratani hadi Upembe wa Afrika, na tuseme Afrika nzima,na maslahi yao(ya kikoloni) yakawa hatarini!
Dola la Kisovieti(USSR)linasemwa kuleta silaha nyingi eneo la Upembe wa Afrika,tena nzito.Vita Baridi vilianza mara baada ya Vita vya Pili vya Dunia kwisha,mwaka1945.
Baada ya vita hivi vya Pili vya Dunia,Mataifa ya Mashariki yakiongozwa na Urusi(USSR) nay a Magharibi yakiongozwa na Mrekani yaliamkakugombea udhibiti wa Mataifa ya Ulimwengu wa Tatu,hususan Afrika,Asia na Amerika Kusini.
Kwa kuwa Warusi hawawezi kushindana na Marekani na washirika wake kwa uchumi, wao walianza kusambaza msaada wa silaha,magari ya deraya na ndege za kivita.
Hata Rais wa Somalia,Muhammad Siad Barre, alipewa msaada wa zana za kivita na USSR. Somalia ya sasa inayolaumiwa kuwafuga magaidi wa al-Shabaab,hutokana na mfuo wa kikoloni wa Kiingereza na Italia,wakijidai kuunganisha taifa mwaka 1960.
Haya ni mataifa mengine duniani yanayouza silaha nje kuliko nchi nyingine nyingi.
Wasomali ni wahamaji(nomadic tribesmen) wasiokuwa na makao maalum zama hizo.
Hawakuwa na rasilimali za kutosha,halafu uchumi wao haukuwa mzuri,kwa sababu ya kutokaa eneo moja na kuzalisha mali.
Wakati mwingine walitaka kuungana na Wasomali wenzao wa Ethiopia,Kenya na Djibouti.
Hivyo,ili kutimiza azma yao walihitaji silaha tena kali.Ikulu ya Marekani(White House) ilipokawia kuwafadhili bunduki,Ikulu ya Urusi(Kremlin) ikawapa bunduki kali hawa Wasomali wanaosemwa kuwa ‘Wakali’ wanapoishi kuzunguka Bandari kuanzia Mogadishu, hadi Ghuba ya Aden na Bahari ya Hindi.
Sasa utaona Pwani BAHARI YA Hindi kuanzia Mogadishu,Pwani ya Djibouti,Aden,Yemen,Kenya na Tanzania ni eneo hatari hata leo kwa maharamia wa Kisomali wenye bunduki za rashasha za Kirusi.
Wamarekani waliwahi kusema, ingawa Siad Barre alijidai kutumikia Warusi na falsafa za  Marx na Lenin, mvuto wake ulielekea kwenye Uislam.
‘Doctrines’ za Kirusi hazikufua dafu Somalia, ila bunduki zao walizipeda sana, nazilipatikana kwa wingi;wakazitumia kwa njia yoyote kupatia chakula na mahitaji mengine.
Inasemwa,Mfalme Haile Selassie wa Ethiopia aliunga mkono siasa za Magharibi; akapinduliwa kwa nguvu za jeshi kutoka Urusi,ili kundi la Wakomunisti washike nchi hii muhimu.
Habari hizi, zikubaliwe au zikataliwe na ubongo wako,lakini tunapata picha halisi kwamba, vita upembe huu wa Afrika(The Horn of Africa) yaani Somalia,Djibouti,Ethiopia na Eritrea ni matokeo ya Ikulu mbili-Kremlin na White House-kunyukana eneo hili tete hata leo,na matokeo yake wamezaliwa al-Shabaab wanaoua watu Kenya,Uganda labda watakuja Tanzania siku si nyingi!
Mungu apishilie mbali!!
Nani adhibiti ushawishi wa eneo hilo,ndiyo shida inayoleta changamoto za visasi vya magaidi hapa kwetu Afrika Mashariki.
Utawala wa Mengistu Haile Mariam(Mkomunisti) baada ya Haile Selassie,ukasemwa na Magharibi kwamba ulileta, “Terror” hofu kuu Ethiopia!
Neno hili, “Terror” hofu.ukiliongezea “ism” unapata  ‘TERRORISM’ maana yake Ugaidi.
Kwa hiyo Kambi ya Magharibi inasema aliyeleta ugaidi eneo hilo ni Urusi. Na tukumbuke Propaganda za Kimagharibi.Bila nguvu nyingine ya Magharibi kutaka kujitanua huko,Urusi wasinge sogea.
Ni kwa sababu hii, twapata picha kwamba chimbuko la ugaidi eneo hilo lote ni Madola makubwa ya Marekani na Urusi kujitanua huko.
Wakati Urusi inatawala mataifa haya kwa ‘remote’ White House hawakuchoka,wakawasaidia wafuasi wao ndani ya nchi hizi fedha na bunduki,ili kukamata Ikulu ambayo ingetawala Bandari za tangu Mogadishu,Djibouti,Aden, na Mlango Bahari wa Shamu,YEMEN,kuelekea Pakistan na Afghanistan.
Sasa unaona umuhimu wa kudhibiti eneo hilo la Bahari ya Hindi na Bandari hizo?
Bahari ya Shamu, ambayo Waisraeli wa zama za Musa waliivuka kwa miguu bila boti,ni muhimu sana kuunganisha Bahari za Hindi na Mediterranean.
MFEREJI WA SUEZ,uliochimbwa na Wafaransa na Uingereza huko Misri ni muhimu eneo hilo ili kuunganisha safari za meli kati ya Bahari za Mediterranean ,Shamu(Red Sea) na Hindi.
Mto Nile,unaoanzia Ziwa Nyanza na kutiririka umbali wa kilomita 6,900 unapita eneo hilo pia.Huu ni mto ambao ni damu itiayo uhai nchini Misri(the life blood to Egyptians), ni muhimu kusafirisha mafuta,bidhaa muhimu kwa uchumi wa Ulaya,Mashariki ya Kati,ya Mbali na Amerika na Afrika.
Hili ni eneo muhimu sana kiuchumi,ndiyo maana madola makubwa hupigana vikumbo kulikamata kwa usalama wa nchi zao, au usalama wa uchumi wao.
Haya madola makubwa-Urusi na Marekani- ndiyo waliochochea vita kati ya Somalia na Ethiopia,kupigania Jimbo la Ogaden, eneo ambalo ni moja ya tano ya Ethiopia.
Ethiopia,Somalia na Jamhuri ya Kidemokrasi ya Yemen,hukodolewa macho na udenda na madola haya makubwa ili kuweka ‘interests’ zao.
Mpango mkubwa(master plan) wa mataifa makubwa ni kukamata eneo la Kusini mwa Afrika, na Mataifa tajiri ya Mafuta katika Ghuba ya Arabia.
 Chuki za Magharibi dhidi ya Fidel Alejandro Castro Ruz, ni kufika Afrika kusaidiana na washirika wao Urusi,kukomesha ukoloni wa Ulaya Magharibi huku Afrika Kusini.
Walikuja hata kushawishi Somalia kugeukia siasa za Ki-Marx.Utaona hata Shirika la Ujasusi la Marekani(CIA)likahaha kushawishi Muungano wa Tanganyika na Zanzibar jijini Dar es salaam mwaka 1964,ili Zanzibar sisjekuangukia Ukomunisti!
Rais Jimmy Carter alitoa amri kwa Waziri wa Mambo ya Nje,Cyrus Vance,na Mshauri wake wa Usalama wa Taifa,Zbignew Brzezinski,kuhakikisha(to move to every possible way) yaani hata kwa ugaidi ama mabomu, alisema “to get Somalia to be our friend”.
Hii ni kauli ya Jimmy Carter,ili SOMALIA iwe ‘rafiki’ yao tena kwa gharama yoyote!
 Tazama kilichofanyika! Marekani chini ya Shirika lake la Ujasusi,CIA wakaanza kuipa Somalia msaada wa silaha! Huo ni mwaka 1977.
 Ilisemwa eti ili ‘kujilinda’ ila wasitumie silaha dhidi ya Djibouti na Kenya!
WAPI MAGAIDI WANAPATA SILAHA ZA HATARI?
Sasa silaha za West Gate zimetoka wapi?
‘Msaada’huo wa silaha kutoka MAREKANI kwenda Mogadishu ,ulikuwa na masharti kwamba Marekani isiwasaidie wanamgambo wa KISOMALI(Somali Liberation Front) huko Ogaden.
Msomaji anapofikiri vizuri, aone kwamba Marekani inapotoa msaada hata kwa Waasi,huwa na kwa sababu ya maslahi,vyama vya ukombozi navyo hunyimwa au kupewa msaada kwa sababu ya maslahi.
Hawa Wasomali wameishi Ogaden zaidi ya miaka 500
.Sasa MAREKANI wanaibembeleza Somalia iwakate URUSI ili wao wasaidie Mradi wa kukomboa Ogaden.
Unaanza kuona Somalia inapigana na Ethiopia,Marekani wakiwa nyuma ya Somalia!
Urusi inaleta MiG-21 Jets, vifaru vipya vya kisasa 400,Mi-8 ambazo ni helkopta za kivita 30 na maelfu ya silaha kuizuia Marekani kulitawala eneo hilo.
Huku nyuma,BBC,VoA,SKY NEWS.CNN n.k wanatangaza kwamba,Somalia na Ethiopia wanapigana kwa sababu ya Ogaden!
Mbumbumbu wa Tanzania wanasema,”Afrika Bara la Vita! Bara la Giza ,Magonjwa,na Machafuko!!”
Mabwana wa Vita wa Afrika(war lords) wanabebwa na mataifa haya ya Ulaya,na huwezi kuyaona mpaka uwe na macho matatu.
‘Satellites’ na ‘radar’ za Marekani za upelelezi zinategwa tangu Misri hadi Pakistan,zinaletwa upambe huu wa Afrika ili kukoleza vita,ili Urusi wapigwe waondoke!
Antonov-22 na Ilyushin-76 za Kirusi nazo zinajongea Upembe huo ili kubyesha mabomu makali kupambana na Marekani aliyekificha nyuma ya pazia,mgongoni mwa Msomali,katika vita baina ya Somalia na Ethiopia.
Yemen inatumika kama ‘depots’ za silaha za Mrusi.
Cuba nao wanaleta askari 15,000 toka Angola(Angola ilisaidiwa ikawa huru 1975) sasa CUBA anajitoa mhanga kupambana bega kwa bega na Mrusi ili kumzuia Marekani kutwaa Ogaden, mgongoni mwa Msomali!
General Vasily Petrov wa Urusi anaongoza mapambano huku, akina Vance nao wanachochea upande huu, basi Afrika inanuka riha ya baruti na risasi,kwa maslahi ya madola ya Ulaya!
Somalia inazidiwa,inaomba silaha Magharibi,vita ngumu Ogaden.
Shah wa Iran(alikuwa Kibaraka wa Marekani) anaonywa asije akapeleka silaha yoyote aliyopewa na Marekani katika nchi za Dunia ya Tatu,zisije zikatumika kumsaidia Ethiopia na Warusi,vita ngumu hii bwana!
White House, inatoa amri-hakuna kuuza silaha mEthiopia ili Ogaden itekwe na Msomali!
Ili Urafiki wa Marekani na Msomali upatikane! Naam, maslahi ya mataifa makubwa hupatikana kwa damu mbichi ya Mwafrika,Mwarabu,Mhindi ama Mhindi Mwekundu wa Bara la Kusini mwa Marekani.
Viongozi wa Kiarabu,tangu Sudan hadi Saudi Arabia wanaamrishwa na White House,kuisaidia Somalia, msaada MUHIMU wa silaha(a significant  military aid).
Lengo,ni ili Ukomunisti ushindwe Afrika. Hawa akina Brzezinski walishatengeneza Ukimwi mwaka huo wa 1975 ili kuwaua Waafrika,kuwapunguza ili wao wachukue mali kwa gharama yoyote, sasa wako Somalia.
Wanapoona Warusi na Wacuba wameingia wenyewe vitani,na vita vinamwelemea Msomali,wanaanza kutangaza mikataba ya kusimamisha utengenezaji wa silaha!
Wanaita kwa Kingereza, “Arms-limitation talks” ama Arms Limitation Treaty!
Sasa wanasema Mrusi akiendelea kuwasaidia Wahabeshi, basi mazungumzo hayo ya kupunguza silaha duniani yatakuwa hatarini kuvunjika!
Msomaji,sijui unaona unafiki huu wa Marekani! Kumbuka hii siyo hadithi ya Paukwa Pakawa! Ni ukweli kutokana na Historia.
Urafiki wa Marekani na Somalia unakuja kwa njia ya kuchochea vita Ogaden,Cuba nao wanaleta ‘artillery’ na MiGs zinanyesha mabomu tani nyingi,Wasomali wanapigwa wanakimbia nyuma milimani huko JIJIGA!
Damu ya Wasomali inabubujika kama mto,mvua ya mabomu inaendelea,wanakatwa vipande vipande kwa mabomu-maguruneti kwa uchochezi wa Kimarekani inayotaka kuikamata Somalia kwa gharama yoyote.
Majeruhi walikuwa maelfu.
Nataka ujue ugaidi wa Somalia ulianza lini?
 Kwa nini na kwa sababu gani?
Kumbuka,vita baina ya Somalia na Ethiopia vimechochewa na Rais Jimmy Carter ili ajifanye rafiki wa Somalia,kumzuia Mrusi kujitanua Upembe wa Afrika.
Hii kampeni iliitwa,  ‘THE SOMALIA’S OGADEN CAMPAIGN’ unaweza kufuatilia ujue ninachoandika hapa.Wajinga wanaposema,Wasomali wapenda vita!
 Jiulizeni nani yuko nyuma yao?
 Nani huwapa pesa na silaha? Ni Mwarabu? Mchina? Mzungu!!
Wamarekani wanapoona Msomali kachakazwa vikali,damu inavuja puani, wanaandika barua ya rangi ya njano na nyeusi kusema!
“Serikali ya Somalia itoe tamko, sisi(Marekani) tumeona katika vita hivyo vya Ogaden,kuna mkono wa Mrusi”,Barua ilisema.
Sasa eti ndiyo MAREKANI wanaona kwamba kuna Mrusi ameleta MiG-21 zipatazo 48, na kuna marubani wa Cuba wako mstari wa mbele kuisaidia Ethiopia, vifaru 150 vimetoka Msumbiji nchi nyingine ya siasa za Ki-Marx,sawa na Zimbabwe ya Robert Mugabe ambaye wanamchukia sana.
Hadi Iran kule ambako kuna mafuta ushawishi unaendelea wametoka akina Ahmadnejad,sasa utawala unajipendekeza Marekani. Ni Urusi,Marekani!
Wacuba wanafundisha Wayemen kutumia bunduki za Mrusi,akina Carlos The JACKAL walifunzwa ugaidi na wa Cuba,Warusi ili kupambana na ubeberu wa Kimarekani.Akina Osama walifundishwa ugaidi na Marekani ili kupambana na Ukomunisti walipovamia Afghanistan mwaka 1979!
Muktadha wa makala hii,ni ili msomaji ajue kwamba,Marekani na washirika wake  huwa hawana ‘Clear Policy’ kuhusu BARA LA AFRIKA.
White House na Kremlin huchochea vita hapa Barani;hufunza wanamgambo eneo hili lote kuanzia Somali,Urabuni,Bara Hindi hadi Pakistan na Afghanistan.
Hata Osama Bin Laden, alitokana na makambi ya kigaidi yalifofadhiliwa na Marekani,lengo likiwa kupambana na Urusi waliotaka kusimika Ukomunisti pindi walipovamia Kabul mwaka 1979.
Wanamwaga silaha na mabomu,wanachochea chuki;vita vinapouma wanaitana mkutanoni Ulaya ili kuitisha “ARMS-LIMITATION TALKS”
Waziri kama John Kerry anakwenda Moscow,inadaiwa wanajadili kumaliza vita,ama kuepusha vita Syria,Misri,Libya,IRAK nk.
“Negotiations” zinazofanywa na kutangazwa na vyombo vya habari vya Kimagharibi, si kitu bali uongo na Propaganda.
Wanataka kujitakasa dhidi ya lawama kwa kuwa vitanga vya mikono yao huchuruzika damu mbichi za Waafrika,Waarabu,Wahindi ama raia wa Ulimwengu wa Tatu! Kila mahali penye maslahi ya kisiasa na kiuchumi.
Vita ya Madola Makubwa ni “To conquer The Third World” ama kuutawala Ulimwengu wa Tatu,wa nchi changa,hasa zenye utajiri wa almasi,dhahabu,mafuta,gesi n.k
Wakiona Waafrika mnapukutika kwa vita,damu inamwagika,Putin na Obama wanaitana Moscow ama popote,wanakaa wanaambizana kupeana zabuni.
Wanaunda ushirika wa kiuchumi, “economic co-operation’ mambo yanatulia!
Wanapigana kwasababu ya maslahi ya uchumi na siasazao za kibabe.Watu mwingine Marekani wakiona Putin ni kichwa –ngumu kuhusu maslahi yake,labda ya Syria ama Iran, wanamwacha na kuungana na ‘Western Powers’ zingine ili kupambana dhidi ya maslahi ya Urusi na washirika wake.
Dunia ilikuwa imegawanyika katika kambi mbili za Mkataba wa Wasaw(Poland) na zile za Mkataba wa Northern Atlantic Treaty Organization(NATO).
Syria haitengenezi silaha za sumu;kuna  super power hupeleka silaha hizo Syria,lakini lawama haziendi kwa wenye viwanda,huangukia mtumiaji wa silaha hizo za sumu-Biological and chemical weapons!
Usishangae, Uingereza au Marekani wakawauzia Syria silaha hizo za maangamizi ili wamalizane,iwe rahisi kuwakamata kama ilivyo Iraq,Misri na sasa Syria watakapokuwa wamechoka kabisa.
Kuna kitu kinaitwa, “Counter force against Soviet-bloc Intervention”.Wamarekani wanaweza ku-train rebels- kuwapa mafuzo waasi mahali popote ili wakakamate Jimbo lenye utajiri wa madini!
Sasa,vita vikizuka watu wanaona wanaohasimiana ni wajinga sana! Kumbe ni biashara inafanywa.
.Zaire ya zamani kuna jambo hilo,siku hizi huitwa Congo,DRC.
Taarifa za hivi karibuni husema,Katibu Mkuu wa Pili wa Umoja wa Mataifa,Dk.Dag Hammarskjold wa Sweden,ndege yake iliangushwa kwa kombora wakati ikitua mjini Ndola,Zambia. Huu ni ugaidi wa wazi dhidi ya Katibu Mkuu wa UN.
Ripoti za hivi karibuni, husema Katibu Mkuu wa Pili wa Umoja wa Mataifa,Dk. Hammarskojold aliyeshika wadhifa huo Mkuu wa UN mwaka 1953-61 alikuwa katika kinachoitwa,Peace Mission huko Kongo, wakati DC-6 iliposhushwa kwa kombora kali, usiku wa Desemba 17 kuamkia 18,mwaka 1961 kilomita chache tu njiani kutoka Ndola Zambia.
Eneo hilo,wakati huo lilitawaliwa Wazungu wa Rhodesia(Zimbabwe), hawakutaka Katibu Mkuu huyo kukomesha vita vilivyowaletea faida ya madini ya Congo,zama hizo za Patrice Lumumba.
Ripoti husema,kilichofanya ndege ile kuanguka ni bomu.
Sababu kubwa ni Wazungu:
Weupe wa Rhodesia,Wabelgiji na Waingereza waliokuwa na migodi katika Jimbo lenye utajiri wa Madini,Katanga, waliokuwa katika hali ya kutoelewana na Umoja wa Mataifa na wanaharakati wa Kiafrika, wenye itikadi za kimapinduzi, African Nationalism.
M-23 ni wanamgambo wa kuleta utajiri kutoka majimbo tajiri Kongo kwenda hata Ulaya na Marekani.
 Tawala zitaangukia kwa akina Kagame na wenzake,wakati anayefaidika mno amejibanza nyuma ya pazia la unyama na machafuko ya vita!
Wacuba,Walifundisha Waasi,wakakamata Jimbo la Shaba lenye utajiri.Zaire iakaomba msaada Ufaransa,Cuba wakaondoka.
Ukiuliza Waasi au Magaidi hapa Afrika,unaambiwa kwa Kiingereza,
“We have the men , just to give us the tools to fight!”
Wanasema wana rafiki zao Ughaibuni(huwa hawawataji,ni siri sirini) wanawapa zana za vita ili kupigana na serikali za Afrika,Asia ama  popote palipo na utajiri wa rasiliali.
Sasa,utauliza al-Shabaab aa al-Qaeda wanapata wapi pesa za kununua silaha? Wanapata wapi pesa za kulipa mishahara na gharama za vita?
Somalia,kuna kiwanda cha kutengeneza SMG,AK-47 au maguruneti?
Akina Andrew Young, wakati huo Balozi wa Marekani Umoja wa Mataifa,walishashindwa kuzuia Urusi na Marekani kuivamia Afrika.
Kila mara “US Troops” huja Afrika na meli na manowari za vita,huja na drones n.k nia yao ni kujenga ‘military base’ za kuizuia Urusi na zana zake na ushawishi wake kuitawala Afrika.
Marekani ilianzisha al-Qaeda chini ya Osama ili kuwazuia Warusi Afghanistan mwaka 1979, hupandikiza chuki, huleta silaha halafu tunaanza kudhani wabaya ni Waafrika?
 Wasomali!Waarabu?Waislam?
Kabla ya kuanza kulaumu Waafrika/Waarabu/Waislam na ugaidi WestgatE, Nairobi,tutafakari.
·       Nani anamwaga silaha Afrika? Bila shaka jibu ni Super Powers
·       Nani anafunza wanamgambo mafunzo ya kivita kama hawa al Shabaab walioleta majanga Nairobi,kasha kutokomea?
·       Nani analeta chuki?Nani analipa gharama za ugaidi?
Jawabu ni SUPER POWERS!
Tufanjeje?
Jibu ni Afrika itakapoamka na kukataa kutumiwa mithili ya vinyangarika,ili nayo iwe SUPER POWER!
                 www.congesmrambatoday.blogspot.com
0786 324 074





No comments:

Post a Comment