Mei 25 mwaka huu itakuwa siku ya kumbukumbu ya kuanzishwa Umoja wa Nchi Huru za Afrika
miaka 50 iliyopita.
Umoja huo ulioitwa,
Organization of African Unity(OAU) ulianzishwa Mei 25 mwaka 1963, ukiwa na
jumla ya nchi 32.
Mwaka 2001 umoja
huo ulikuwa na jumla ya nchi 53. Lengo hasa la kuanzisha umoja huo lilikuwa
kuimarisha amani, usalama na ustawi na maendeleo ya Waafrika. Makao yake Makuu
yako mjini Addis Ababa , Ethiopia .
Leo, Afrika iko mbioni kuwa nchi moja kama ilivyo Marekani, yaani
Waafrika wako mbioni kuwa Taifa moja(United States of Africa), lengo lao likiwa
kukataa kuwapigia goti mabwana wakubwa wa Magharibi na mashirika yao
yaliyoanzishwa zama za Kikoloni, kama Benki ya Dunia(WB), Fuko la Fedha la Kimataifa(IMF)
na vikundi kama Paris Club, G-7,8,20, WTO, Jumuiya ya Madola(Commonwealth) n.k
Afrika, ni Bara tajiri, lakini watu wake ni
fukara sana .
Afrika ina ukubwa wa maili za mraba 11,667,000 sawa na kilimita za mraba
30,218,000.
Kuna milima mirefu kama Kilimanjaro wenye kimo cha futi 19,340 sawa na mita
5,895. Mlima Kenya una urefu
wa futi 17,058(mita 5,199); Afrika kuna maziwa makubwa kama Victoria lenye ukubwa wa maili za mraba
26,418.
Ziwa Tanganyika lina ukubwa wa maili za
mraba 12,700. Ni miongoni mwa maziwa yenye kina kirefu zaidi Duniani,
lililowahi kuwaleta wapelelezi maarufu kama
David Livingston.
Afrika kuna vivutio halisi vya kitalii, licha rasilimali zilizomo. Ziwa
Nyasa lililoanza kugombaniwa na TANZANIA na Joyce Banda, lina ukubwa wa maili za mraba 11,430.
Afrika kuna mito
kama Nile unaoanzia mto Kagera na kukatisha Ziwa Victoria
hadi maporomoko ya Owen huko Uganda .
Kuna Kongo, Limpopo, Zambezi , Niger , Orange , Senegal na
mingine kama Tana, Kagera na Ruvuma ambayo haikauki msimu wote, lakini
Waafrika tuna
njaa.
Watawala wetu waliwahi kutia saini mikataba ya hila ya mwaka 1929 na
1957 ya kuwauzia Bonde la Mto Nile watawala wa Misri, ili Waafrika wasije siku
moja wakatumia maji ya Nile kwa kilimo cha
umwagiliaji, wakati Misri wanalima jangwani kwa kutumia maji haya haya
yanayotoka MtoKagera.
Iko siku watatia saini Wahaya,
Wajitta, Waganda, Waluo, Wasukuma n.k wasivue samaki kutoka Ziwa Victoria, ili
samaki wote na rasilimali zingine view mali ya Wazungu na Wahindi wenye viwanda
vya Umoja wa Ulaya(EU) vinavyosindika samaki hapa.
Afrika ina misitu mikubwa inayozalisha mbao za
thamani. Kuna mbuga kubwa za wanyama kama
Serengeti, zenye mamilioni ya wanyama wakubwa ambao hawapo mahali popote
pengine duniani.
Mbuga za Serengeti zina eneo la kilomita za mraba 14,763 na wanyama
wakubwa zaidi ya milioni tatu.
Mbali na Serengeti, Tanzania kuna Ngorongoro,
Tarangire, Hifadhi ya Ziwa Manyara, Ruaha, Selous, Mafia(Marine Park),
Zanzibar, Olduvai Gorge anakodaiwa kuishi binadamu wa kale duniani, lakini
Watanzania hawa zahanati na maji vijijini.
Afrika nzima kuna mito ,
maziwa, madini, mbuga za wanyama, ardhi yenye rutuba, bahari n.k lakini
Waafrika wana njaa.
Asilimia 70 ya almasi yote duniani inatoka
Afrika hasa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo , Ghana , Afrika Kusini ,
Botswana , Namibia , Angola ,
Tanzania
n.k
Asilimia 55 ya dhahabu yote
Ulimwenguni hutoka Afrika:Afrika ya Kusini, Ghana, Zimbabwe, Kongo, Tanzania
n.k Afrika kuna Nickel, shaba za kumwaga, makaa yam awe n.k Kuna Tanzanite
ambayo haipatikani popote duniani isipokuwa Mererani, lakini Wahindi na Wazungu
huuza kwa wingi Tanzanite kuliko sisi.
Mauzo ya Taninite katika soko la dunia kabla ya mtikisiko wa uchumi
yalikuwa wastani wa dola za Marekani milioni 400.
Tanzania ilikuwa ikiambulia dola
milioni 16 tu; hizi njama za mafisadi vibaraka wa Mzungu Barani.
Mwaka 2007 mauzo ya madini ya Tanzania nje
yalikisiwa shilingi bilioni 825
Kulingana na Multilateral Investment Guarantee
Agency(MIGA) serikali yetu iliambulia kama
asilimia 15 ya fedha hizo bilioni 825kupitia kodi na mrabaha.
Hali iko hivyo hata kwa rasilimali nyingine
kama mafuta n.k hususan Ghana ,
Sudan , Nigeria , Libya ,
Angola , Guinea ya
Ikweta. Kuna uranium na ruby. Uranium yaweza kutumiwa kuwa chanzo cha nishati
ya umeme, lakini Afrika kumetanda kiza totoro. Hapa nchini Shirika la Umeme, TANESCO
linatugawia kiza badala ya umeme.
Afrika kuna kila kitu, lakini
hakuna manufaa, Waafrika wangali wakisubiri msaada wa chakula kutoka Shirika la
Chakula na Kilimo kama FAO, WFP, na wasamaria wengine.
0786/0715-324 074
Itaendelea
No comments:
Post a Comment