Novemba 10 mwaka 2004, askari wa Kiingereza,
Brett Richard(20) na Nigel David(23) walidaiwa kumbaka kwa zamu na
kumsababishia kifo msichana wa Kitanzania, Conjesta Ulikaye.
Nigel David na Brett Richards, walikuwa mapumzikoni jijini Dr es salaam.
Waitokea vitani, Irak, hivyo wakawa wanajiburudisha
katika fukwe za jiji la Dar es
salaam .
Wakiwa
katika fukwe za Hoteli ya Silver Sands, tukio la mauaji ya msichana huyo
likatokea.Walitiwa mbaroni, shauri lao
likashughulikiwa kwa siku 36 tu.
Walifikishwa mahakani Novemba 16 mwaka huo; yaani kesi yao ilifika mahakani
siku sita tu baada ya tukio.
Ilipofika Desemba 22 mwaka huo wa 2004,
kesi dhidi yao ikafutwa na Mkurugenzi wa Mashitaka(DPP) kwa kile kilichoelezwa
kwamba ni kwa mujibu wa kifungu namba 91(1) cha sheria ya Mwenendo wa
Makosa ya Jinai ya mwaka 1985.
Aliyekuwa DPP wakati huo, Godfrey Shaidi, alisema ushahidi uliokuwepo
haukutosha, hivyo hao Wazungu, askari wa Uingereza vitani Irak wakaachwa huru
huria.
Ofisi ya DPP imekuwa ikisema kesi
zinacheleweshwa mahakamani zinapokuwa zikingoja kupangiwa tarehe ya
kusikilizwa, wala hazicheleweshwi na ofisi ya
DPP.
Mahakama inadaiwa kuchelewesha kusikiliza kesi hasa kwa watu Weusi tena
masikini wasio na ukwasi na mvuto wowote katika jamii.
Wakati, zile kesi zinazowahusu vigogo kama akina Marehemu ‘Ditto’, Abadallah
Zombe na wengine wa kariba hiyo, na Wazungu kama hao askari wa Uingereza, kesi
huendeshwa kwa kasi ya ‘supersonic’ hadi wanapoachiliwa huru.
Ni hapa, inapokuja dhana kwamba, mfumo
wa sheria wan chi hii, haujali usawa kwa raia, bali
unazingatia rangi, kipato, vyeo n.k
Pia, inasemwa magereza ni kama
yalijengwa kwa ajili ya wahalifu masikini Weusi, na kamwe siyo kwa Wazunagu na
wenye ukwasi.
!
Mzungu, Yunus Santy(67) ambaye alikuwa
Mmisonari wa Katoliki, alifunguliwa mashitaka jijini Mwanza
kwa makosa ya kufanya ngono na wanafunzi wa kike wenye umri wa miaka 17.
Pia, alikutwa na picha za uchi na viungo
bandia vya shemu za siri za kiume(toy boy). Badala ya kutiwa
hatiani na kufungwa jela miaka 30 kwa kubaka wanafunzi hao huku wakichukuliwa
mkanda wa video wa kitendo hicho kichafu, Yunus Santy aliamuriwa kuondoka
nchini mara moja.Hiki ni nini kama siyo woga?
Ni wazi,serikali yetu iliogopa kuwatia mbaroni
hawa na kuwafunga kwa sababu Afrika haijawa huru; na iko kizimbani.
Idara ya Uhamiaji ikaamuriwa na
mahakama kuhakikisha jamaa huyo anaondoka nchini mara moja, badala ya
kufunguliwa mashitaka ya ubakaji na kufungwa miaka 30 jela akaenda kwao Italia, asikanyage jela za Tanzania, ambazo utadhani
walijengewa masiki Weusi, wanaotenda wizi mdogo, uzururaji na umachinga tu.
Miaka michache iliyopita, kulitokea
ugomvi kati ya mwekezaji Muingereza, Stewart Middleton
na mbia wake wa biashara, raia wa Tanzania , Benjamin Mengi.
Vyombo vya dola vya Tanzania
vilipomtia mbaroni Middleton, kufuatia ugomvi wa makampuni ya kilimo ya Silverdale Tanzania Limited na
Mbono Farms ya huko Hai, Kilimanjaro,
Bunge la Uingereza likachachamaa.
Mbunge toka chama cha
Mahafidhina(CONSERVATIVES),Bwana Roger Gale, akasema Bungeni Uingereza kwamba
Tanzania ilistahili kunyimwa misaada kwa sababu huyo Middleton katiwa mbaroni
na polisi huko Kilimanjaro.
Ilidaiwa kwamba, kitendo cha Middleton
kutiwa mbaroni na kushitakiwa kwa ugomvi wao na Benjamin Mengi, basi kulikuwa kuondoa mazingira
bora ya uwekezaji yanayowanyanyasa wawekezaji, hususan mabwana wakubwa wa
Uingereza!
Uingereza, kupitia Shirika lake la misaada(DFID) ilikuwa
ikiongoza kutupatia msaada kuliko nchi yoyote duniani.
Mwaka 2003\2004 misaada toka Uingereza
iliongezeka kutoka pauni milioni 80(sh. Bilioni 208) hadi pauni milioni 110(sh.
Bilioni 286) mwaka wa 2005 na 2006. Asilimia 70 ya fedha zote hizo zilikuwa
zikiingia moja kwa moja katika bajeti ya serikali.
Nataka kusema kwamba, katika mazingira
kama hayo, vyombo vya dola vya Tanzania na mfumo wa kutoa haki wan chi hii,
ulikuwa na ubavu gain kuthubutu kuwatia mbaroni Waingereza hata kama walifanya
uhaini hapa?
Tunadhani, kwa sababu ya misaada
tupewayo na mataifa ya Ulaya na Marekani, basi raia wao wameanza kuabudiwa kama
miungu na mabunge yao na serikali zao huogopwa kama radi ama ngurumo na
mafuriko.
Ni kwa sababu hii tu, tunadhani wale
Wazunagu wawili waliokuwa mapumzikoni, Silver sands, Dar es salaam (wakitokea
vitani, Irak) waliogopwa kutiwa hatiani kwa kumbaka Conjesta Ulikaye kwa zamu
hadi alipokata roho.
Naam, Serikali ya mjini Dar es salaam,
wakati huo ilichelea kuwatia hatiani na kuwahukumu Wazungu wale kutoka
Uingereza kifo cha kitanzi hapa hapa jijini Dar, habari zisije kufika London, halafu misaada yote
ikakatwa, na vigogo woote wa hapa wakazuiliwa kukanyaga London!!
Ilikuwa siyo rahisi Nigel David na Brett
Richards kutiwa hatiani na kunyongwa hata kufa
kwa kamba jijini Dar, lisije Bunge la Uingereza likajua, likafoka, misaada huku
ikakatwa na mashirika mengine kama Oxfam yakafunga virago hapa.
Ni kwa sababu hii, tunadhani hakuna haki
na usawa katika mfumo wa sheria wan chi hii iliyowahi kutawaliwa na wakoloni
Waingereza.
Bado mawaziri wakuu wa Uingereza:Harold
McMillan,(waziri mkuu wa Uingereza 1957-63 wakati Tanzania inapata uhuru), Alec
Douglas Home, Harold Wilson, Edward Heath, James Callaghan, Margaret Thatcher,
John Major,, Tony Blair na Gordon Brown wanaogopewa bungeni na katika ikulu ya
Dar es salaam kama mizuka.
Utadhani sisi siyo watu huru tuliopata uhuru
toka Uingereza Desemba 9 mwaka 1961. Bado tunamwogopa sana Malkia wa Uingereza,
Elizabeth II(alitawazwa Feburuari 6, mwaka 1952) kiasi kwamba tunaondoa haki na
uhuru wa watu wetu ili kumpigia goti
Mzungu?
Naam, tunawapigia goti Wazungu, makaburu
na wenye pesa hadi raia masikini wan chi hii wananyimwa haki au kucheleweshewa
haki zao, tangu polisi hadi mahakamani.
Mzungu tapeli akionyesha pua yake polisi, hapo hapo anadhaminiwa asije
kufikishwa nyuma ya nondo. Lakini, Mweusi fukara, mpaka utoe rushwa.
Ikitokea
masikini Mweusi umedhulumiwa na Mzungu au mwenye pesa, basi mfumo wetu wa
sheria unawa ‘gwaya’ hawa, sheria zinapindishwa ‘fasta’ hadi wanaachiwa huru.
Hapa jamii yetu inaona imetengwa katika
madaraja kama zilivyokuwa zama za Ukaburu, Afrika
ya Kusini.
Ziko wapi
sheria zinazojali haki na usawa. Iko wapi Katiba ya haki na usawa wa binadamu
sasa?
Kwa
majuma mawili tumejadili ushoga,shuruti za mataifa haya na usawa katika sheria
za Tanzania unavyodhulumiwa na mahayawani wachache, kwa tama zao au kwa ubaguzi.
Ni furaha kwamba wanasheria wameanza
kujadili jambo hili kupitia kituo cha televisheni cha Star cha jijini Mwanza.
Tunakusudia haki za waliowengi zinarejeshwa, na usawa uliowekwa na katiba kisha
ukaporwa na baadhi ya watu, unarejeshwa haraka.
Kwanini tutengwe katika madaraja ya
walionacho na wasio nacho, Weusi, Wazungu, machotara, mabwana
na watwana
n.k utadhani zama za Ukaburu na ubaguzi wa
rangi Afrika ya Kusini?
Nakupongeza Rais Kikwete,kwa
ushindi,lakini nimekukumbusha haya ili awamu hii Watanzania waheshimiwe na
serikali yao inayopigia goti wageni na magabacholi, na kuwapuuza raia
wazalendo.
Tunapaswa tangu sasa kukemea tabia hii ya
ukaburu na ukoloni wa Wazungu kama David
Cameron na wenzao
|
0786-324 074
No comments:
Post a Comment