Monday, January 28, 2013

Ulaya na Marekani hakuna haki za binadamu

KAMPUNI ya Shell ya Uingereza,iliwalipa fedha wanamgambo kuwaua wanaharakati wakati walipoandamana huko Niger Delta, kupinga makampuni hayo ya kigeni kuchimba mafuta  eneo hilo wakati wakiharibu mazingira,bila kulipa fidia.
Tumeona juma lililopita,kwamba Niger Delta hakukuwa na mafuta na huduma za kiuchumi hazikuwepo licha ya mapipa mengi kuchimbwa eneo hilo  la Kusini mwa Nigeria.
Kampuni ya Chevron ya Marekani,iliwalipa mishahara polisi na jeshi kuwaua wanaharakati kama Ken Saro-Wiwa, kwa sababu walipinga uhalifu wa makampuni haya kwa maandamano makubwa ya amani.
Watu wajinga wanapoona Afrika polisi wakikabiliana na waandamanaji,akili inawatuma Ulaya hawakabiliwi. Kumbe, Ulaya na Marekani walikuwa nyuma ya vikosi vya Sani Abacha kuwaua wanaharakati waliopinga makampuni ya kigeni kuharibu mazingira bila kuleta maendeleo kwa raia hata licha ya kuchimba mafuta katika eneo hilo.
Sasa, kama Gaddafi alishambulia waandamanaji wa Benghazi,akapinduliwa kasha kuuliwa kwa risasi, Kiongozi wa Syria, Bashar al Assad naye anawashambulia raia wanaompinga anashughulikiwa na Ulaya na Marekani,kwanini Shell na Chevron yalishinikiza serikali ya Nigeria kuwaua waandamanaji?
Huko Burma,(siku hizi ni Myanmar) kampuni kubwa la Unocal la Marekani, lilitiliana saini mkataba na jeshi kuilinda,ilipokuwa ikitekeleza ujenzi wa Bomba la gesi asilia kama hiyo ya Mtwara, kupelekwa nchi nyingine.
Bomba hilo lilikuwa likijengwa kutoka Yadana,wanakijiji walitumikishwa pasipo ujira,walibakwa,waliuliwa.Waliteswa na wanajeshi,Marekani wakiwa pembeni,wakatumikishwa kitumwa.
Wapo wajinga,wataanza kusema,ilikuwa kampuni siyo serikali ya Marekani,subiri uone!
Wanakijiji walifungua kesi ya madai dhidi ya kampuni hilo la Unocal,kulitumia jeshi la Yangon kuua vibarua,kubaka na kuwatumikisha kitumwa,pasipo malipo ili gesi iende nchi nyingine.
Shirika la Habari la Agence France Presse(AFP) likasema miaka saba iliyopita kwamba, Unocal walipobanwa wakasema ukweli,wakakubali kuzungumza na wanavijiji wa Burma ili kesi iondolewe mahakamani,walikubali kuwalipa fidia na kuwasaidia kuimarisha maendeleo.
Nimesema Unocal; ni kampuni la Kimarekani la kuchimba gesi.Mahakala ilikuwa inakaribia kuwapa ushindi wanavijiji wa Burma waliofungua kesi Califonia.
Nikusimulie kidogo.Jumanne,Desemba 10, mwaka 2003 kampuni hili katili la Kimarekani lilipandishwa kizimbani huko California ili kujibu mashitaka ya hao wanavijiji wa Burma, na kuhalifu haki za Binadamu.
Nchi ya Burma wakati huo ilikuwa chini ya utawala wa kiimla wa kijeshi ambao Marekani hujidai sana kuupinga hapa Barani Afrika,kumbe sehemu nyingine wanajali maslahi tu.
Hii ‘Brutal Military Junta’ waliwalazimisha raia kujenga bomba la urefu wa kilomita 62,waliokataa waliuliwa,akina mama wakabakwa na kuumizwa bila fidia.
Bomba lenyewe lilikuwa la kilomita 62 sawa na maili 39 ili kupeleka gesi kutoka Myanmar kwenda Thailand.
Basi, Unocal walipobanwa wakakubali kulipa fidia maana kazi waliyofanya wanavijiji hawa wa Myanmar mwaka 1990s ilikuwa ya thamani ya Dola bilioni 1.2.
Sasa jiulize,wewe shabiki wa hawa Marekani na Ulaya, Utumwa kwa wananchi waaa      Burma ndiyo Haki za Binadamu? Utumwa huu katika karne ya karibuni?
Unocal walishirikiana na kampuni la Ufaransa,Total kupeleka gesi Thai.
Tutazame wanavyoharibu mazingira ya dunia,hasa nchi za dunia ya tatu na kukataa kusaini mikataba ya upunguzaji wa hewa za sumu angani,ili tupatwe majanga ya asili.
Mapigo Saba ya Mwisho-
haya ni majanga ya kiasili ambayo ukiyachunguza yataletwa na kiburi cha Moabu,Marekani na washirika wake,kwa kuchafua sana anga la dunia,kukataa kusaini mikataba kama ule wa Kyoto(Kyoto Protocol) ili maji yachafuke,viumbe wafe kwa Ongezeko la joto na mabadiliko ya tabianchi, mafuriko kila mahali,
vifo majanga, kansa, ukimwi,vyanzo vya maji kuwa damu,kutoboka kwa utando wa Ozone n.k
 Moabu ya kiroho(Marekani) iligoma kutia saini Mkataba wa Kyoto mwaka 1997,kwa sababu kufanya hivyo kungeleta hasara kwa wafanyabiashara wan chi hiyo-Wakaona heri kuongeza madhara kwa kumwaga hewa chafu angani ili wajipatie UTAJIRI.
 
Miongoni mwa shughuli za kiuchumi za binadamu zinazoharibiwa sana na uharibifu wa mazingira na mabadiliko ya tabia ya nchi ni pamoja na kilimo, ufugaji, uvuvi n.k
    Mkutano wa New York ulioanza Septemba 22 mwaka huu wa 2009, umefanyika takriban miaka 12 kamili tangu mkutano wa Kyoto, Japan ufanyike Desemba mwaka 1997.
   Katika mkutano wa Kyoto, viongozi wa mataifa zaidi ya 150 duniani walikutana wakaweka  itifaki ambayo ingewezesha kupunguza hewani kiwango kikubwa cha gesi au hewa chafu ya sumu zinazoletwa na hewa ya ukaa(C02) na gesi nyingine kama     CH4,N20, HFC8, PFC8  na SF6.
   Mkataba huo uliojulikana kama  itifaki ya Kyoto(Kyoto Protocol) uliokusudia kupunguza gesi za sumu duniani kwa silimia 5.2 kabla ya kufika mwaka 2012.
  Mataifa yaliyoshurutishwa kusaini mkataba huo wa Kyoto ni nchi zote 38 zenye viwanda duniani..
Mataifa yote 15 ya Umoja wa Ulaya(EU) yakakubali kupunguza asilimia nane ya taka hewa zake duniani. Marekani ilitakiwa kupunguza asilimia saba ya gesi zake inazotupa angani.
 
 Japan, ilitakiwa kupunguza asilimia sita ya taka sumu inazotupa angani, na nchi zinazoendelea zilitakiwa kupunguza kiwango chochote kwa uhuru wake.
 Marekani ilisaini mkataba huo Novemba 12, mwaka 1998, lakini kutokana na kitisho kutoka kwa matajiri wenye viwanda nchini humo, serikali ya Rais Bill Clinton ilichelea kupeleka ajenda hiyo katika Bunge la seneti.
 Kwa sababu, kusaini mkataba wa Kyoto na kuutekeleza, maana yake ni kwamba viwanda vya Marekani vingelazimika kupunguza uzalishaji.
Ni kwa sababu hii serikali ya Clinton iliufyata.
  Mkutano mwingine wa kujadili upunguzaji wa taka za sumu hewani ulifanyika Bonn, Ujerumani Julai 2001.Utawala wa George .W. Bush ulitangaza kujitoa katika mkataba wa Kyoto kwa madai kwamba uliweka zigo kubwa katika nchi zilizoendelea bila kuzingatia usawa.
 Marekani, waligeuka wapinzani wakubwa katika ajenda za kupunguza hewa za sumu duniani, tangu huko mjini Bonn, Ujerumani na mahali pengine, kwa sababu ya maslahi yake na ya viwanda vyake, bila kujali madhara makubwa yaliyotokana na wingi wa viwanda vyake kutupa angani hewa chafui zenye kusababisha majanga makubwa kwa Ulimwengu mzima..
Hizi ndizo haki za binadamu Ulaya na Marekani?
  Kwa shingoupande, walikubali kupunguza hewa hizo za sumu ili kutekeleza huo mkataba au itifaki ya Kyoto ya 1997.
  Katika makubaliano ya mjini Bonn, mataifa makubwa yenye viwanda yanayomwaga kwa wingi hewa za sumu angani, yalishauriwa kufuata malengo waliyowekewa ya kupunguza hewa ya ukka katika anga.
 Kulingana na Shirika la Kudhibiti Uharibifu wa mazingira, hewa ya ukaa(carbon dioxide) imeongezeka sana angani kutoka mwaka 1990 hadi sasa; na hii ni kutokana na shughuli za binadamu, ikiwa ni  pamoja na viwanda na migodi.
  Wakati hewa za sumu zinapoongezeka sana duniani, misitu ama miti inayopunguza kwa kiwango kikubwa hewa ya ukaa kwa kutengenezea chakula chake(starch) inatoweka kwa kasi na kwa kiwango cha kutisha sana.
  Tazama nchi zinavyoongeza sana kiwango cha hewa za sumu angani.
 Mashariki ya Mbali pamoja na Oceania wanachafua anga kwa kiwango cha asilimia 28.9.
Amerika ya Kaskazini huchafua anga kwa kiwango cha asilimia 28.8.
 Marekani pekee inachafua anga la dunia nzima kwa moshi wa magari na viwanda vyake kwa asilimia 24.7.
   Ulaya Magharibi, kwa pamoja huchafua anga la dunia kwa asilimia 16.5, wakati Amerika Amerika ya Kusini nzima na Kati huchafua anga la dunia kwa kiwango cha asilimia 4.3.
   Ulaya Mashariki, na iliyokuwa Jamhuri ya Kisovieti(USSR) huchafua anga la dunia nzima kwa kiwango cha asilimia 12.8. Mashariki ya Kati huchafua anga kwa kiwango cha asilimia 4.7.
 Afrika, inachangia katika uchafuzi wa anga la dunia kwa asilimia 3.9 tu.
Hii ni kwa mujibu wa Ripoti za Energy Information Administration, kuanzia mwaka 1999.
 Afrika inayochangia kwa kiwango kidogo sana katika uchafuzi wa hewa angani, ndiyo inayoathiriwa sana na madhara makubwa ya uchafuzi wa hewa angani unaoleta mabadiliko ya tabia ya  nchi.
 Mifugo ya Afrika, hususan Kenya  na hapa kwetu hufa kwa ukame unaoletwa na uchafuzi wa mazingira ya anga. Uchafuzi wa anga ndiyo chanzo cha ukame huko kwetu Afrika. Ukamwe huu ndiyo unaochangia jangwa kuongezeka, ukame na njaa na vifo vya watu pia.
 Kulingana na uchafuzi huo wa hewa angani, Benki ya Dunia(WB) ilishasema mwaka 2001 kwamba kila mwaka watoto wachanga wapataao 500,000 wangepoteza maisha duniani pote kwa sababu ya uharibifu huu mkubwa wa anga.
Vifo huletwa na viwanda vya Ulaya na Marekani siyo? Kumnyang’anya mtu uhai siyo haki za binadamu sawa?
  Kunatokea mvua za sumu(acid rains) zitakazosababisha uharibifu mkubwa sana wa misitu hasa ya Afrika, na wala mvua za sumu hizi za viwanda vya mataifa makubwa haziharibu huko kwao peke yake.
 Nataka kusema kwamba, Marekani inaongoza duniani kwa uchafuzi wa anga, lakini athari zake tunapata sisi huku; tunakufa kwa njaa na matokeo ya ukame na hata vimbunga kama Mitch, tsunami na Katrina ambavyo vikitokea, huua maelfu ya watu bila kujali mipaka ya nchi za viwanda na zisizokuwa na viwanda.
  Ni kwa sababu hii, ubeberu wa Marekani wa kukataa kutia saini mikataba ya upunguzaji wa hewa na taka za sumu, kama huo wa Kyoto wa mwaka 1997, ni hatari kwa maisha ya watu, hasa tuishio nchi masikini.
  Ingekuwa heri kama Mkutano wa New York  na Afrika ya Kusini ungeipa kibano kikali Marekani kwa kiburi chake na kuwelka mbele maslahi binafsi ya viwanda vyao, huku ng’ombe wa masikini wanapokufa kwa maelfu huku kwetu, pasipo fidia.
  Marekani, hukimbilia kuliburuza Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuzitenga nchi nyingine kaidi kutekeleza mikata kama ya Nyuklia n.k Ni  Marekani hiyo hiyo inayotaka Iran na Korea Kaskazini na Iran zitengwe au zishambuliwe kijeshi kwa kukataa kutia saini mkataba wa kupunguza silaha za nyuklia.
 Mbona yenyewe inakataa kwa  ubabe kutekeleza mkataba wa Kyoto, unaotaka hewa za sumu zinazoleta majanga duniani kudhibitiwa. Ongezeko la joto duniani linaloleta hayo majanga kama tsunami, huleta madhara hadi huku Bahari ya Hindi na kusababisha vifo hata Kenya, Tanzania na Somali. Kwa nini Marekani haidhibitiwi ama kupewa kibano au kushambuliwa kijeshi, kama yenyewe ilivyozishambulia Irak na Afghanistan,  na iko mbioni kuzishambulia Iran na Korea Kaskazini kwa kukataa kutekeleza mikataba ya upunguzaji silaha za sumu?
 Sumu inayoua watu si ndiyo iliyo,o pia katika silaha za atomiki na ndiyo ile inayorushwa angani na viwanda vya Marekani na Ulaya, bila kudhibitiwa na mtu, tena kibabe?
 Ni kwa sababu hii, viongozi wa Afrika waliokwenda New York kujadili kitisho cha hewa za sumu angani na mabadiliko ya tabia  ya nchi, wanapaswa kutoa tamko kali la kuikemea Marekani au ikibidi kuiwekea vikwazo vya kiuchumi na kuitenga na Jumuiya za Kimataifa, kwa vitendo vyake vya kibabe vya kuleta maafa Ulimwenguni.
 Dunia haina ubavu wa kuitenga Marekani?
Marekani haiwezi kushambuliwa kijeshi na dunia nzima ili kuishikisha adabu iache kuiangamiza dunia kwa kumwaga sumu tani mamilioni kwa siku, huku ikikataa kutia saini kila mkataba unaowataka kupunguza sumu?
  Wakuu wa nchi za Afrika(akiwemo Rais Kikwete) wanaporejea kutoka New York, wanapaswa kuwaambia wananchi wao, ni namna gani wamembana Barack Obama, kwa sababu nchi yake ina kiburi cha ubeberu, kuendeleza uzalishaji wa taka sumu, zinazoleta saratani ya ngozi huku, kuleta jangwa ama ukame na kuua mifugo Afrika, hususan Tanzania na Kenya.
 Shughuli za kilimo na ufugaji, ambazo hufanywa na masikini huku Afrika Mashariki zinatatizwa sasa na mabadiliko ya tabia ya nchi na ukame. Chakula cha binadamu hakuna, kwa sababu Afrika inakuwa jangwa, kwa sababu Jangwa la Sahara lililoko Kaskazini linakaribia kushikana na lile la Kalahari, lililopo Kusini.
 Sasa, mvua itanyesha jangwani?
 Ni kwa sababu hii, tunasema, kiburi cha Marekani kimekwisha kuleta majanga makubwa hapa Kwetu Tanzania tangu wakate kusaini Mkataba wa Kyoto Desemba 1997 hadi mkutano huo ulipofanyika New York, Septemba, 2009.
  Ni kwa sababu hii, Rais Kikwete na ujumbe wake, wanapaswa kuwaambia Watanzania, Rais Obama wa Marekani, ameambiwa kwa kiwango gani kulipa fidia ya mifugo ya Wamasai, Wajitta, Wasukuma, Wakurya na wafugaji wengine ambao mifugo yao inaangamia kwa sababu ya ukame ulioletwa na sumu na taka za hewani kutoka viwanda vya Mabwanyenye wa Marekani?
 Vinginevyo, Obama ana kesi ya kujibu Dar es salaam, asijidai kukemea utawala mbaya huku na ufisadi, kumbe nchi yake huchangia mvua kukoma kunyesha na vifo vya mifugo huku.
Je,huu ni uungwana? Ni haki za Binadamu?
   0713 32 40 74

No comments:

Post a Comment