JANUARI
MOSI,mwaka huu mpya,2013 nilikuwa Buswelu,katika Halmashauri mpya ya wilaya ya
Ilemela, kwa mapumziko ya mwisho wa mwaka na mwanzo mwaka mpya.
Nimebaini
kuwa wenyeji wa eneo hilo wameuza mashamba yao na kujiondokea.Wanapisha jiji
linalokua kwa kasi ya ajabu. Mwanza ni Jiji la wakazi milioni moja, ambalo
majumba ya fahari yanamea kama uyoga,na vitega uchumi vipya huanzishwa,zikiwemo
taasisi za kigeni.
Inawapasa
wenyeji kuuza viwanja na mashamba yao na kuuhama mji;wanatafuta pa kwenda
kuishi.
Umasikini
unapoongezeka vijijini, kuna watu hulazimika kuuza ardhi:Mashamba,viwanja na
mifugo na kuingia mijini,wakijaribu kufanya biashara ndogo kwa mitaji
midogo,ili kujinusuru.
Kufuatia
hali hiyo ya baadhi ya wanakijiji kuhamia mijini, “Urbanization” hata Wazungu
hununua mashamba ya wenyeji pembezoni mwa mji kama Buswelu,Buhongwa,Bugogwa n.k
Wakati
wamasikini wa mjini huuza viwanja na mashamba na kujiondokea, wale wa vijijini
huuza masahamba ma viwanja vibanda vyao na kuingia mijini,kujitafutia
ajira,maana maisha ni magumu vijijini,na hakuna miundo mbinu.
Kwa sababu
hiyo,ukosefu wa ajira, “Unemployment” unakimbia kutoka asilimia 30 hivi,kwenda
asilimia 50.Ombaomba ni wengi,wengine huvalia suti na tai, na watoto wa
mazingira magumu hashikiki.
Ukisikia
‘bomu’la watoto wa mitaani,basi Mwanza linakaribia kulipuka,litawalipukia
watawala usoni.Mtu akiwapa chakula akawaambia waandamane na kufanya vurugu ama
kupora maduka ya watu,hawatasita aslani.
Vurugu,maandamano
na fujo za Mwanza,hufanywa na watu wa kariba hii,baadhi yao sasa ni watu wazima
wasio na makazi.Huishi mitaloni na vibarazani mwa maduka ya Wahindi.Mvua
yao,jua lao,na baridi za usiku wanazijua wao.
Vitendo vya
ukahaba,ushoga,ujambazi,uporaji na unyang’anyi sasa hufanywa na kundi hili.
Jiji kama New York, asilimia 80 ya wafungwa na
wanaoswekwa rumande ni watu wa kundi hili,hususan Wahamiaji Weusi kutoka Latin
Amerika au Caribbean.
Wakati
watoto wa matajiri na wenye fursa bora za ajira na ukwasi, wakisoma shule na
vyuo bora,wanajiandaa kushika nafasi za uongozi serikalini na katika jamii.Masikini
hawana uchaguzi mwingine zaidi ya kuwa watumishi ama watumwa na watwana wa hawa
‘supervisors, principals and rulers’.
Licha ya
serikali kuajiri polisi vijana na wengine askari wa Jiji,Mwanza hushuhudia
uvunjaji wa sheria wa makusudi na mapambano ya kila mara ya wanamgambo wa
Jiji,polisi na makundi ya vijana wanaojiita,Wamachinga.
Maisha
magumu,husababisha uvunjaji wa sheria na vifo kila siku. Uhalifu,uvutaji
bangi,ubwia unga,kutafuna mirungi. Hawa, “Drug addicted burglars” hutamani vita
vitokee,wenye maduka makubwa, ‘shopping malls’ watimue mbio,wao wajimilikishe
kile kinachosalia!
Nataka
nikwambie,kwamba Mwanza hapa,vijana wanawachukia polisi na wenye mamlaka,kuliko
kawaida. Mwanza kunanuka machafuko ‘violence’ kila kunapokucha,sababu kubwa ni
umasikini kuongezeka-money shortage!
Watu
wanakosa kulipa kodi ya pango(inaongezeka kila mchana na usiku),mtu huachia
chumba na kwenda kujibwaga mtaloni.Fedha hazipatikani,ni balaa za
pesa-financial doom.
Kila siku,
polisi hufukuzana na machangudoa wanaouza miili yao katika mahoteli makubwa ya
wageni,katika vilabu vya usiku na maeneo mengine ya starehe.
Unaweza
kukutana na msichana wa mwaka wa pili au wa tatu katika Chuo Kikuu hapa,
anajiuza ili apate mahitaji.Wengine ni wasichana warembo, na hawapendi kuitwa
changudoa,wanataka waitwe ‘Wafanyabishara’ au watoa huduma ya ngono,
“Commercial Sex Workers” kwa kifupi,waite “CSW”.
Maisha
magumu eti yameleta uwekezaji wa ajabu na miradi ya kushangaza,biashara ya
ngono,picha za uchi “Pornography”na zingine hupigwa na Wazungu mchana
kweupe,wakati mamlaka ikiangalia,na kukosa meno.
YUNUS Santy, maarufu kama Angelo(67)
alihukumiwa kifungo cha miaka mitano
jela, au kulipa faini ya shilingi 300,00 baada ya kupatikana na hatia ya kupiga
picha za uchi na visichana viwili vyenye umri wa miaka 16 na 17.
Angelo, ambaye ni raia wa Italia, alikutwa na visichana hivyo vyenye
umri wa miaka 17(bila shaka wanafunzi) katika chumba cha Hoteli ya Paradise,iliyopo
Unguja, jijini Mwanza.
Alikuwa akifanya ngono na kasichana kamoja wakati kengine kakipiga picha
ya tukio hilo.
Pia, alikutwa na viungo bandia vya sehemu za siri za kiume.-toy boy.
Bila shaka, alikuwa akivitumia
viungo hivyo bandia kuzima kiu ya ngono kwa visichana kama hivi.
Ilikuwa Septemba 20 mwaka 2007, Mtaliano huyu aliyejitambulisha kama
Mmisionari wa Kikatoliki, alipovichukua visichana hivyo katika mitaa ya jiji la
Mwanza, akavipeleka hoteli ya Paradise(Paradiso) ili kula maraha!
Wasichana hao wakaacha masomo ili
kwenda kusaka pesa zinazosakwa leo kwa udi na uvumba, kuliko utu.
Naam, Angelo aliposhindwa kutimiza ahadi kwa wasichana hao, walitoa
taarifa polisi, ambao walimtia mbaroni kisha kumfikisha Mahakamani.
Mwendesha Mashitaka, Inspekta Msaidizi wa Polisi, Inogu Kimasa,
akaiambia Mahakama ya Hakimu Mkazi wa Mwanza kwamba, Angelo ambaye ni
Mmisionari wa Kanisa Katoliki, alifanya kosa la Jinai kinyume cha Sheria ya
Kujamiana ya mwaka 1998.
Siku chache kabla ya Siku Kuu ya Idi, Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo,
Auqinea Lujwahuka, akamhukumu Angelo kifungo cha miaka mitano jela(alikiri
kosa), au kulipa faini ya shilingi 300,000.
Mmisionari huyo alilipa faini hiyo kwa kosa hilo alilotenda wakati wa mfungo wa Ramadhan.
Hata hivyo, aliamuriwa kuondoka nchini, kwa sababu makosa yake yanakiuka sheria
na Katiba ya nchi.
Akakabidhiwa kwa Idara ya Uhamiaji,
mkoa wa Mwanza ili hatua za kumwondoa nchini zitekelezwe.Angekuwa Mswahili,bila
shaka angefungwa kifungo cha maishajela au miaka 30.
Hili ni tukio moja kati ya mengi yaliyoibuka wakati wa ujio wa Wazungu,
wakiwemo watalii, wawekezaji wa migodi na wamisionari uchwara.. Hawa,
wanatambua uzumbukuku, ulafi, ushamba na ulimbukeni wa wasichana wan chi hii
kupenda sana
kuzuzukia kila kitu, mradi kililetwa na
Wazungu.
Naam, Filamu za uchi, “Nudie Film” hususan zile za ngono(sex film)
hutengeneza pesa nyingi. Kwa sababu ya jamii tuliyomo kuwa na kiu ya ngono,
anasa na pesa, filamu hizi hupendwa.
Filamu hizi zina wateja wengi, watu wa kila rika, kila tabaka; hivyo
wauzaji wa filamu hizi wananafasi ya pekee sana ya kutengeneza pesa nyingi na kujipatia
maisha mazuri kwa kipindi kifupi.
Watu wengi, hususan wanafunzi wa shule zetu za sekondari wenye umri huo
wa kuanzia miaka 17 hupenda sana
ngono na picha za aina hiyo.
Wasichana wa umri huu wamekubuhu sana
kwa ngono kupitia filamu hizo.
Hivyo, akitokea mtu mwenye fedha-awe Mmisionari au tapeli-akaahidi
kuwalipa pesa wasichana hawa, atafanya atakavyo kwa hawa wengi sana. Watatoroka masomo,
watafanya ngono hata na mbwa, midoli na chochote kile, mradi tu walipwe ujira
kidogo, juisi na hata chakula cha mchana katika mahoteli haya ya Nyota Tano.
Kisha, watarejea shuleni au nyumbani kwa na vizawadi vya kitoto, bila
walimu, walezi na wazazi kubaini, ufirauni wa Wamisionari kama
Angelo.
Kwa kutumia fedha walizolipwa na
akina Angelo, watanunua vivazi vya aibu, suruali za kubana sana makalioni na vijishati vinavyoacha
vitovu nje. Watanunua vipodozi hata vya kugeuza midomo kuwa myekundu mithili ya
radi.
Angalia vitabu wanavyosoma watu hawa. Angalia magazeti wanayopenda
kusoma. Ni yale yenye picha, maandishi ama filamu za ngono(Pornography).
Vitabu vya ngono, magazeti ya watu
wanaotembea uchi, au waliopigwa picha wakifanya ngono; na wengine
waliofumaniwa! Magazeti ya aina hii hupendwa sana na watu wakizazi cha zinaa.
Siku hizi kuna mitandao ya Intaneti; humo kunapatikana picha nyingi za
ngono na za wasichana warembo walioacha utupu maungo yao ya tashtiti. Katika vibanda vyenye
kompyuta za intaneti, tunaambiwa wanazuia watu kuangalia picha za ngono.
Lakini, siku hizi hata katika simu za mkononi
kuna intaneti; na mtu aweza kupokea picha ama kuzituma kwa yeyote. Siku hizi,
visichana hujipiga picha vikiwa maliwatoni vikioga, picha hizo za utupu
husambazwa kwa njia za kisasa sana kama ‘broadband’ wakati mwingine vitendo vya
ngono na fumanizi hurushwa moja kwa moja.
Wiki
chache zilizopita, zaidi ya wanafunzi 20 wa Seminari ya Nyegezi inayomolikiwa
na Kanisa Katoliki,walitimuliwa masomo kwa kosa la kujihusisha na ushoga!Wavulana
hao wa sekondari,walibainika ni mashoga,wakafukuzwa shule,kwa sababu Kanisa
Katoliki limesema,halitavumilia matendo hayo ambayo ni kinyume na maadili ya
dini.
Sasa,unaweza
kuna namba Mwanza,vijana wa kiume na kike wanavyohama kwa kasi ya ajabu ‘KUTOKA
ANOLOJIA KWENDA DIGITALI’.
Mwanza,kiunga
cha Sodoma na Gomorrah,kwa sababu mamlaka inakaribia kurasilimisha biashara ya
ukahaba na ngono-sexual entertainment businesses.
Biblia,inapinga
ushoga:Mambo ya Walawi 18:22.Lakini katika zama hizi za maisha magumu na uchumi
mbaya,nani amfuate Bwana Mungu ili akafe njaa?
Aliyekuwa
Kamanda wa Polisi Mwanza,Zelothe Stephen(sasa kastaafu) aliwahi kusema, “Haijatungwa
sharia ya kuwatia hatiani watu wenye mwelekeo wa ushoga ama
makahaba.Tunapowatia mbaroni,tunawashitaki kwa makosa ya Uzembe na uzururaji”,
alikuwa akitoa maelezo kwa wanahabari juu ya mvulana aliyekutwa asubuhi akiwa
kavaa heleni,vivazi vya kike, ana akiwa kapaka wanja wa midomo huko Mabatini!
Mwenyekiti
wa Wenye Viwanda,Biahsra na Kilimo(TCCIA)Joseph Kahungwa, hawezi kusema
biashara ya ngono nayo itambuliwe na Chamber of Commerce!
Labda,wanafanya
hivi kwa kuwa Rais Jakaya Kikwete aliwahi kusema,Mwanza utajengwa ili kuwa
mithili ya Los Angeles.Uwekezaji mkubwa!
Jiji lenye
uhaba mkubwa wa ajira,lenye wahamiaji wapya,wageni wanywa mchuzi wa mbwa(hot
dogs) fukweni mwa maji ya ziwa kubwa Victoria. Jiji hili ni vigumu ku ‘accommodate
the latest influx or poor marching guys!
Jiji la
vijana wanaoishi ghetto,ndani ya majengo ya magorofa marefu, skyscrapers, wakati
wengi wanapoishi vilimani.Naam, mapangoni na mtaroni. Ndani ya makazi ya mbavu
za mbwa-slums!
Umasikini,panya,magofu ndani ya
Jiji la fahari
Nihitimishe
kwa kusema, Rais Jakaya Kikwete akifanya ziara katika makazi ya polisi,hususan
Kigoto, atakutana na mabango makubwa ya watoto wa polisi na wake zao
yameandikwa hivi:
“Rais tuokoe
mapanya buku yanatumaliza huku!” Lingine litaandika, “Tumechoka kukaa katika
maghala ya Wahindi kama pumba!” na linguine litasema, “Walinda usalama wa raia wakati hatuna
usalama katika magofu yaliyoachwa na Wahindi!”
Naam,Rais
akifika Kigoto na kukumbana na mabango haya ya jamaa za polisi(nasikia polisi
wenyewe wamekula kiapo cha kutoandamana au kubeba mabango kama raia wa Mtwara)basi
Kikwete atashuka kwenye Limousine yake na kuahidi kuwasaidia hao akina mama
wenye kuhema kwa kubeba mabango yenye ujumbe mzito! Ataahidi polisi kupewa makazi bora.
Vinginevyo,mapanya
buku yaliyojazana katika magofu ya Kigoto wanakoishi polisi wa
Mwanza,yatawamaliza vidole,yanakomba hata mboga chunguni! Usalama wa Raia
pasipo usalama wa Polisi?
0786 324 074
No comments:
Post a Comment