Ziwa
Victoria, ni kiungo muhimu cha usafirishaji wa abiria na mizigo katika nchi za
Mawziwa Makuu.
Gazeti moja
litolewalo kila siku hapa nchini kwa lugha ya Kiingereza, katika toleo lake la
Mei 23 mwaka jana, lilisema kwamba,mwaka 1996 Mv.Bukoba ilipozama na kupoteza
maisha ya abiria wake takriban 1,000; miongoni mwao alikuwemo Abu Ubaidah
al-Banshiri, ambaye alikuwa nambari mbili katika kundi la kigaidi la Al-Qaeda.
Kauli hii ni
kuashiria kuwa malaka ya serikali sasa inapaswa kuchukua hatua thabiti za
kuimarisha usalama katika ziwa hili
Naam, kundi
hili la AlQaeda, lilianzishwa na Osama bin Muhammad bin Awad bin
Laden,Feburuari mwaka 1998 kwa jina la WORLD ISLAMIC FRONT ,ili kuhujumu
maslahi ya Marekani na washirika wake mahali popote duniani,hata kama ni Ziwa
Victoria,
Osama
alikuwa mshirika wa Marekani na shirika lao la Ujasusi(CIA) mwaka 1979 wakati
majeshi ya Warusi walipovamia Afghanistan.CIA walimfadhili mabilioni ya Dola za
Marekani kuanzisha kambi ya mafunzo ya Makhtab al-Khidamat(MAK).
Lakini,baada
ya Urusi kuondoka Kabul mwaka 1989, Osama akageuka kuwa adui wa MAREKANI na
washirika wao, akaungana na Taliban na Mullah Muhammad Omar kuendesha ‘Jihad’ dhidi
ya Marekani na washirika.
Nataka
kusema kwamba,mwaka 1996 wakati Mv.Bukoba inazama ziwa Victoria, al-Qaeda
tayari walikuwepo,na wangeweza kufanya madhara hapa nchini kwa mashambulizi
yenye kulenga shabaha Wamarekani ama maslahi yao hata hapa Tanzania.Tumeona
Nairobi na Kampala ikishambuliwa na magaidi hawa,na hatusahau mashambulizi ya
Agosti,7 mwaka 1998 yaliyoua zaidi ya watu 200 Dar na Nairobi.
Hata hivyo,
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Everest Ndikilo, amesema serikali imeimarisha ulinzi
katika Ziwa Victoria,kwa kuwa zipo boti za doria zinazozunguka ziwani, na raia
wanapaswa kutoa taarifa pindi wanapoona mienendo yenye mashaka ama kitisho cha
magaidi wa al-Qaeda ama al-Shabaab!
Mamlaka ya
Udhibiti wa Usafiri Nchi Kavu na Majini(SUMATRA) ndiyo wanaopaswa kusimamia
ukaguzi na usalama kabla ya safari kuanza.
“Changamoto ya SUMATRA,Mwanza kuna boti zaidi
ya 10,000 zinazosafirisha abiria na mizigo kwenda visiwani na Sengerema,Ukerewe
na Geita. Huwezi kusema, asilimia mia zote hufuata sheria, na kuzingatia
maelekezo.SUMATRA Mwanza, tuna wakaguzi watatu tu,lakini tunao
mtandao(usiotosha) wa kuwadhibiti wasafirishaji wasiopenda kutii sheria pasipo
shuruti. Kumbuka, Ziwa siyo barabarani ambako utaweza vizuizi njiani na kufanya
ukaguzi ili kuwabaini wakosaji”, anafafanua ofisa Mfawidhi wa SUMATRA,Mwanza,
Alfred Wariana.
Polisi
na Watendaji wa vijiji wapo katika maeneo ya vituo vya kibiashara,ambako boti
hizi hutia nanga na kupeleka bidhaa,wanapaswa kuwatia mbaroni wasafirishaji
wasiozingatia sheria za Usafirishaji wa Majini.
Kulingana na
SUMATRA,Mwanza, ziko changamoto kuwafikia wamiliki wote wa vyombo vya
majini,hususan vidogo vidogo,na kuvikagua kila mara.
“Hata
hivyo,mtandao wetu wapaswa kukagua na kuhakikisha kila chombo ni salama kabla
ya kuanza safari,na kila chombo cha usafiri chapaswa kuwa na cheti cha kufaa-sea
worthiness.
Katika Ziwa Victoria,SUMATRA wana
ofisi Mwanza, Bukoba na Musoma. Ziwa Victoria kuna visiwa takriban 60, Ukerewe
pekee kuna visiwa 38 vingine hukaliwa na wavuvi tu.
Mei
21, mwaka 1996,Meli iliyomilikiwa na lililokuwa Sherika la Reli(TRC) ilizama
umbali wa mail inane(kilomita 12) za majini, jirani na Bandari ya Mwanza,
uelekeo wa Bwiru.
Mv.
Bukoba, ilipinduka kasha kuzama,ikasababisha vifo vya zaidi ya watu 800.Wengine
zaidi ya 100 walijeruhiwa,wakipoteza mali nyingi za mamilioni ya
shilingi,hususan mikungu mingi ya ndizi.
Kwa
mujibu wa Ripoti ya Tume ya Jaji Robert Kissanga, iliyochunguza chanzo cha
Ajali hiyo,usiku wa kuamkia siku ya ajali,Mv.Bukoba ilipakia abiria kati ya 750
na 800 pamoja na wafanyakazi 37 wa Meli hii.
Kati
ya hao, 114 waliokolewa wakiwa hai, wakati 391 waliopolewa wakiwa
wamefariki wakazikwa katika Makaburi ya Igoma,nje kidogo ya Jiji la Mwanza.
Miili mingine ilichukuliwa na jamaa zao kwenda kuzikwa kwao. Jumla ya miili 332
haikupatikana.
Kila mwaka, ifikapo Mei 21, serikali inayosema Haina Dini, huongozana na
viongozi wa madhehebu ya dini na waganga kwenda eneo la ajali,kufanya
‘matambiko’ na kumwaga mchanga eneo majini!
Serikali
iliwashitaki katika Mahakama Kuu aliyekuwa Nahodha wa Mv.Bukoba,
Jumanne Rume-Mwiru, (ambaye sasa ni Marehemu),Mkaguzi wa Mamlaka ya
Bandari(wakati huo THA),Gilbert Mokiwa, aliyekuwa Meneja wa Bandari ya Bukoba,
Alphonce Sambo, na aliyekuwa Maneja wa Bandari ya Kemondo, Prosper Lugumila.
Kesi
hiyo Nambari 22 ya mwaka 1998, ilianza kusikilizwa Mei 14 mwaka 2001. Miongoni
mwa waendesha mashitaka katika kesi hiyo ni Eliezer Feleshi, ambaye sasa ni
Mkurugenzi wa Mashitaka nchini(DPP).
Hukumu ya kesi hii ilitolewa Ijumaa, Novemba 29 mwaka 2002,majira ya saa sita
mchana hadi saa 9 na Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu, Juxton Mlay(amestaafu).
Washitakiwa
wote walishinda kesi hiyo,kufuatia Hukumu yenye kurasa 118 iliyosomwa kwa
dakika 160 na Jaji Mlay,kusema Mv.Bukoba ilizama kwa sababu haikuwa na uwiano
wa majini, na siyo uzembe wa washitakiwa.
Serikali
ikakata rufaa, hadi leo majaliwa na rufaa hiyo hayajulikani,na baadhi ya
washitakiwa wamefariki dunia,bila kujua hatma ya kesi hiyo na stahili zao.
Mv.Bukoba ilikuwa ‘Kaburi’ lenye kuelea Ziwa Victoria. Ilikwishapigwa
marufuku,kwa kuwa haikuwa na viwango vya ubora-sea worthiness.
Ilijengwa na
Kampuni ya Kibelgiji,ikazinduliwa Julai 27 mwaka 1979.Siku ya uzinduzi,
ilibainika haikuwa thabiti,na ilikosa uwiano,ilitaka kumtosa Baba wa Taifa,
Hayati Mwalimu Julius Nyerere ambaye alikuwa Rais wan chi wakati huo.
Miaka michace iliyopita, meli nyingine ya MSC, Mv. Butiama, ilizimika
injini zake jirani tu na Bandari ya Mwanza, lakini ikaelea kwa zaidi ya saa
mbili,huku abiria wakihaha bila msaada. Ilikuja kufahamika kwamba, meli hiyo
haikuwa na mawasiliano!
Meli
nyingine ya mizigo, Mv.Nyamageni,ilizama ziwa Victoria ikiwa na abiria zaidi ya
20 waliosafirishwa pamoja na masanduku ya soda kwenda visiwani.
Feburuari
mwaka 2012, Mv. Pacific iliyokuwa ikisafiri kati ya Mwanza na kisiwa cha
Ghana ilizama, ilikuwa na abiria 17, mmoja alifariki wengine wakaokolewa.
Kwa
mujibu wa SUMATRA, Boti nyingine iliyokuwa na abiria 31 ilizama huko
Musoma,mkoani Mara,abiria wote wakaokolewa kwa kutumia zana za
uokozi.
Kwa
mujibu wa Alfred Wariana, Ofisa Mwandamizi wa SUMATRA, katika ajali tatu za
mwaka jana 2012, kati ya watu 81 waliokuwemo katika boti hizo,ni mmoja tu
aliyefariki dunia,na anasema hii huonesha kwamba sheria zimeanza kufuatwa.
Kabla
ya vyombo vya majini kuanza safari ni sharti kukaguliwa ili kuthibitishwa
usalama wake.
Hata hivyo,
Wariana anasema bado usafiri wa majini Ziwa Victoria ni salama zaidi kuliko
barabarani.
“Usafiri wa
barabarani hata wa ndege hapa Afrika ndiyo ‘Moving Coffins’ (majeneza
yanayotembea),Barabarani kuna magari kuna pikipiki zinazochinja watu kila
siku”, anasema Wariana.
Akizungumza
kuhusu ushindani wa kibiashara, Ofisa huyu wa SUMATRA amesema, kuimarishwa kwa
miundombinu ya barabara, hususan kutoka Mwanza hadi Musoma, Tarime
na hata Kenya,kumesababisha abiria wengi kususia usafiri wa meli.
Tangu
barabara ya lami ya Mwanza hadi Musoma ikamilike mwaka 1985, hakuna tena abiria
wanaosafiri kwa meli kwenda Musoma,Shirati au hata Kisumu,Kenya.
Upungufu huu ni wa abiria wa meli ni wa takriban asilimia 50.
Kaimu
Meneja Masoko na Biashara wa Kampuni ya Meli(MSC)Kapt. Obedi Nkongoki, anasema
mwaka juzi,Kampuni hii ilisafirisha jumla ya abiria 235,794 tu ambao ni chini
ya uwezo wake. Mizigo iliyosafirishwa ni tani 54,212.
Kulingana
na Kapt. Nkongoki, MSC ina jumla ya meli 15 zinazosafirisha abiria na mizigo
kati ya Mwanza na Musoma,Bukoba,Kemondo,Jinja(Uganda),Kisumu(Kenya),Port
Bell Uganda, na Ukerewe.
Mv.Victoria
ndiyo meli kongwe kuliko zote; ilijengwa mwaka 1960. Imekuwa ikifanyiwa
matengenezo na ukarabati mkubwa na mdogo.
Kaimu
Meneja Mkuu wa Marine Services Company(MSC)Projest Kaija, anasema Mv..Victoria
ina umri wa miaka 52, lakini imefanyiwa ukarabati mkubwa na mdogo mara nyingi.
Mara ya mwisho ilifanyiwa ukarabati mkubwa(Major Rehabilitation) mwaka 2008
ambako ilikaa miezi sita katika Bandari ya Mwanza South Port bila kufanya
huduma.
Ina
uwezo wa kuchukua abiria 1,200 na tani 200 za mizigo;lakini kufuatia abiria
kupungua siku hizi inachukua abiria 500-800,chini ya uwezo wake. Inafanya
safari zake kati ya Mwanza-Kemondo-Bukoba-Mwanza.
No comments:
Post a Comment