Wananchi wadai mabomu ya machozi,risasi
za moto ,magereza makubwa, siyo suluhisho
Na conges mramba,mwanza
NI UKWELI
USIOPINGIKA, kwamba Jiji la Mwanza linakabiliwa na ‘milipuko ya Volkano’ya
machafuko mara kwa mara.yaletwayo na makundi ya vijana wasio na ajira
rasmi,kila kunapokucha.
Kwa miaka
mitatu sasa Mwanza inashuhudia,mirindimo ya risasi za moto,mabomu ya machozi na
virungu, ambavyo hutumika kuwatawanya na kuwadhibiti vijana wenye
mawe,magongo,matofali na magogo ya miti waofunga barabara,kuchoma moto magari
na majumba,wakati mwingine huvunja maduka hususan ya wafanya biashara wa Kiasia
na kupora mali nyingi za thamani.
Siku moja
baada tu ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010,(Jumatatu,Novemba Mosi) makundi ya
vijana,waliodaiwa wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA)walifunga
barabara ya Makongoro iendayo Uwanja wa ndege,mahali paitwapo,Nera na kuichoma
moto ofisi ya CCM ya kata ya Isamilo,ambayo iliteketea pamoja na mali nyingi za
thamani.
Jumanne,
wiki iliyopita(Januari 22,mwaka huu) katika barabara hiyo ya Makongoro,jirani
na eneo hilo la Misheni na Nera, kundi kubwa la waendesha pikipiki maarufu kama
‘Bodaboda’ walikivamika kikosi cha polisi(TASK FORCE) kilichokuwa kikiendesha
kampeni kamambe ya kudhibiti makosa ya Usalama Barabarani.
Ilikuwa saa
3.30 hivi,asubuhi, polisi waliwatia mbaroni waendesha Bodaboda wasiozingatia
sheria na kuwatoza faini.
Wakavamiwa
na makundi ya waendesha bodaboda na kupigwa mawe hadi walipolazimika kufyatua
mabomu ya machozi na risasi za moto hewani,ili kuwatawanya.
Kamanda wa
Polisi Mkoani Mwanza,Ernest Mangu, amesema waendesha bodaboda wasiozingatia
sheria waligoma kukamatwa na waliazimu kuwatorosha wenzao waliokuwa chini ya
ulinzi.
“Hawakuwa na
leseni,na wengine walipakia abiria zaidi ya mmoja kwa wakati mmoja,maarufu kama
mishikaki,hawakuwa na kofia ngumu,helmet,wakati mwingine hukatisha barabara na
kuwagonga waenda kwa miguu na kutokomea pasipo kujali…tumeamua tu ‘deal’nao,tuliwatoza
faini ndipo wakatokea wahuni kutaka kupora pikipiki zilizokamatwa kwa nguvu”,alisema
Kamishna Msaidizi wa Polisi,Ernest Mangu,Jumanne iliyopita.
Kamanda
Mangu akaongeza kuwa hao Bodaboda walikuja juu wakafunga barabara hiyo iendayo
uwanja wa ndege kwa mawe makubwa na matofali,polisi wakawadhibiti na kuwatia
mbaroni baadhi yao wengine wakatokomea.
Alisema
kwamba, waendesha bodaboda 26 walitiwa mbaroni,10 kati yao wakalipa faini
wakati wengine waligoma kufanya hivyo wakaanzisha vurugu.
“Tumewadeaka
wanne wanaisaidia polisi na pikipiki 13 zilikamatwa za wale wengine waliotimka
wakaacha pikipiki zao nyuma,wakichelea kutiwa mbaroni na kufikishwa mbele ya
sheria”,amesema Kamanda Mangu akipa kuwa ni lazima jeshi la polisi lisimamie
sheria za usalama barabarani.
“Hatutakubali
Bodaboda wavunje amani ya nchi.Wanasababisha ajali nyingi;vifo vingi vya wasio
na hatia,na hata wakimgonga mtu hukimbia,hawataki kusimama..tulifikiri
tuwavumilie tuwafundishe kuihshimu sheria,kumbe hawataki…wamejipalia makaa ya
moto vichwani!”amesisitiza.
Katika
makabiliano hayo ya wiki iliyopita,hakuna aliyefariki dunia. Lakiki,katika
matukio yaliyotangulia, watu walikufa ama kujirehiwa kwa risasi za moto.Mwaka
2004, wakati wamachinga wakichoma moto matairi barabarani,mtu mmoja alifariki
kwa kupigwa risasi alipojaribu kuvamia duka la SH Amon,Barabara ya Nyerere.
Kamanda
Mangu,alipoulizwa kuhusu hali za polisi waliodaiwa kujeruhiwa vibaya katika
vurugu hizo, alisema alipatwa michubuko midogo tu,kitu ambacho hutegemewa kila
mara na Jeshi hilo wakati wa makabiliano na wahalifu.
Mwaka 2011
makundi ya vijana waliojiita Wamachinga, walifanya vurugu na kuvamia maduka na
nyumba za ibada za Wahindi katika mitaa ya Rwagasore,Lumumba,Makoroboi na
Barabara ya Nyerere nakuvunja na kupora mali nyingi za thamani,huku wakisema ‘Wahindi
waondoke’.
Vurugu hizo
zilifuatia kampeni ya Halmashauri ya Jiji ya Usafi wa mazingira, hali
iliyosababisha aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani,Shamsi Vuai Nahodha kufika
Mwanza ili kujionea uharibifu.
Kulingana na
wasifu, wa Jiji la Mwanza(Mwanza City Profile) Jiji hili lina watu wasio na
ajira rasmi wanaovuka asilimia 30, ambao hukaa vijiweni kutwa wakisubiri
machafuko yatokee ili wakapore ngawira madukani na majumbani mwa watu.
Kufuatia
hali hiyo,Mwanza kuna makundi ya vijana na watoto wa mitaani, ambao huota
vurugu iwepo ili wapore mali za watu.
Changamoto lilimuuliza
RPC,Mangu kwamba sasa sura ya Jiji la Mwanza ni ipi,ikiwa RPC Liberatus Barlow
kauliwa Oktoba 13 mwaka jana huko Minazi Mitatu,Kitangiri, maduka ya Wahindi na
nyumba za ibada zimeporwa,majumba yamechomwa moto na vijana hawa?
Je,wawekezaji
toka nje wanaweza kuwa na moyo mgumu kuja kuwekeza Mwanza yenye vurugu za
wamachinga na waendesha bodaboda za kila siku?
“Mwanza ni
shwari ka ukuaji wa uchumi na vitegauchumi,isipokuwa wakorofi wachache ambao
tutawadhibiti”,alisema.
Wataalam wa
Soshoolojia waliofanya mazungumzo na gazti hili wiki iliyopita,wamesema
changamoto kubwa inayolikabili Jiji la Mwanza na makundi ya watu kutoka
vijijini katika mikoa yote ya Kanda ya Ziwa,na hata Sindiga,Rukwa na Kigoma ili
kuja Mwanza kutafuta ajira.
Wanapokuta
ajira hakuna na maisha ni magumu,chakula hakuna,hujiingiza katika vitendo vya
uvunjaji wa sheria.
“What the
hell do you do about a whole generation of unemployed people? What they do is
turn to crime”, wamesema wataalam hao kwa masharti ya kutotajwa
majina,wakimaanisha kwamba kizazi cha wasio na ajira,wasio na kazi hugeuka kuwa
wahalifu,endapo serikali haitafanya mkakati wa kuboresha uchumi na miundombinu
ya uchumi huko vijijini ambako vijana hukimbia ili kuingia mjini kutafuta
maisha.
Wananchi
waliofanya mahojiano na Changamoto wamesema,kama serikali haitaanzisha sheria ya Nguvu Kazi iliyokuwepo zama za
Mwalimu Nyerere na kuboresha miundombinu vijijini,vijana watazidi kuingia
mjini,kufanya vurugu na kupora mali za watu,wengine watakuwa bodaboda
wasiozingatia sheria.
“Sheria
kali,kuimarisha na kujenga magereza makubwa,magari ya upupu,mabomu ya machozi
na risasi za moto hazitakomesha machafuko,fujo na maandamano na uhalifu wa kila
siku Jijini Mwanza,ikiwa serikali na jamii hawatatafuta njia mwafaka ya
kupunguza tatizo la ajira na wimbi la vijana kukimbia vijijini na ku
No comments:
Post a Comment