KAMPUNI ya
Shell ya Uingereza,iliwalipa fedha wanamgambo kuwaua wanaharakati wakati
walipoandamana huko Niger Delta, kupinga makampuni hayo ya kigeni kuchimba
mafuta eneo hilo wakati wakiharibu
mazingira,bila kulipa fidia.
Tumeona juma
lililopita,kwamba Niger Delta hakukuwa na mafuta na huduma za kiuchumi
hazikuwepo licha ya mapipa mengi kuchimbwa eneo hilo la Kusini mwa Nigeria.
Kampuni ya
Chevron ya Marekani,iliwalipa mishahara polisi na jeshi kuwaua wanaharakati
kama Ken Saro-Wiwa, kwa sababu walipinga uhalifu wa makampuni haya kwa
maandamano makubwa ya amani.
Watu wajinga
wanapoona Afrika polisi wakikabiliana na waandamanaji,akili inawatuma Ulaya
hawakabiliwi. Kumbe, Ulaya na Marekani walikuwa nyuma ya vikosi vya Sani Abacha
kuwaua wanaharakati waliopinga makampuni ya kigeni kuharibu mazingira bila
kuleta maendeleo kwa raia hata licha ya kuchimba mafuta katika eneo hilo.
Sasa, kama
Gaddafi alishambulia waandamanaji wa Benghazi,akapinduliwa kasha kuuliwa kwa
risasi, Kiongozi wa Syria, Bashar al Assad naye anawashambulia raia wanaompinga
anashughulikiwa na Ulaya na Marekani,kwanini Shell na Chevron yalishinikiza
serikali ya Nigeria kuwaua waandamanaji?
Huko Burma,(siku
hizi ni Myanmar) kampuni kubwa la Unocal la Marekani, lilitiliana saini mkataba
na jeshi kuilinda,ilipokuwa ikitekeleza ujenzi wa Bomba la gesi asilia kama
hiyo ya Mtwara, kupelekwa nchi nyingine.
Bomba hilo
lilikuwa likijengwa kutoka Yadana,wanakijiji walitumikishwa pasipo
ujira,walibakwa,waliuliwa.Waliteswa na wanajeshi,Marekani wakiwa
pembeni,wakatumikishwa kitumwa.
Wapo
wajinga,wataanza kusema,ilikuwa kampuni siyo serikali ya Marekani,subiri uone!
Wanakijiji
walifungua kesi ya madai dhidi ya kampuni hilo la Unocal,kulitumia jeshi la
Yangon kuua vibarua,kubaka na kuwatumikisha kitumwa,pasipo malipo ili gesi
iende nchi nyingine.
Shirika la
Habari la Agence France Presse(AFP) likasema miaka saba iliyopita kwamba,
Unocal walipobanwa wakasema ukweli,wakakubali kuzungumza na wanavijiji wa Burma
ili kesi iondolewe mahakamani,walikubali kuwalipa fidia na kuwasaidia
kuimarisha maendeleo.
Nimesema
Unocal; ni kampuni la Kimarekani la kuchimba gesi.Mahakala ilikuwa inakaribia
kuwapa ushindi wanavijiji wa Burma waliofungua kesi Califonia.
Nikusimulie
kidogo.Jumanne,Desemba 10, mwaka 2003 kampuni hili katili la Kimarekani
lilipandishwa kizimbani huko California ili kujibu mashitaka ya hao wanavijiji
wa Burma, na kuhalifu haki za Binadamu.
Nchi ya
Burma wakati huo ilikuwa chini ya utawala wa kiimla wa kijeshi ambao Marekani
hujidai sana kuupinga hapa Barani Afrika,kumbe sehemu nyingine wanajali maslahi
tu.
Hii ‘Brutal
Military Junta’ waliwalazimisha raia kujenga bomba la urefu wa kilomita
62,waliokataa waliuliwa,akina mama wakabakwa na kuumizwa bila fidia.
Bomba
lenyewe lilikuwa la kilomita 62 sawa na maili 39 ili kupeleka gesi kutoka
Myanmar kwenda Thailand.
Basi, Unocal
walipobanwa wakakubali kulipa fidia maana kazi waliyofanya wanavijiji hawa wa
Myanmar mwaka 1990s ilikuwa ya thamani ya Dola bilioni 1.2.
Sasa
jiulize,wewe shabiki wa hawa Marekani na Ulaya, Utumwa kwa wananchi waaa Burma ndiyo Haki za Binadamu? Utumwa huu
katika karne ya karibuni?
Unocal
walishirikiana na kampuni la Ufaransa,Total kupeleka gesi Thai.
Tutazame
wanavyoharibu mazingira ya dunia,hasa nchi za dunia ya tatu na kukataa kusaini
mikataba ya upunguzaji wa hewa za sumu angani,ili tupatwe majanga ya asili.
Mapigo Saba ya Mwisho-
haya ni majanga ya kiasili ambayo
ukiyachunguza yataletwa na kiburi cha Moabu,Marekani na washirika wake,kwa
kuchafua sana anga la dunia,kukataa kusaini mikataba kama ule wa Kyoto(Kyoto
Protocol) ili maji yachafuke,viumbe wafe kwa Ongezeko la joto na mabadiliko ya
tabianchi, mafuriko kila mahali,
vifo majanga, kansa, ukimwi,vyanzo
vya maji kuwa damu,kutoboka kwa utando wa Ozone n.k
Moabu ya kiroho(Marekani)
iligoma kutia saini Mkataba wa Kyoto mwaka 1997,kwa sababu kufanya hivyo
kungeleta hasara kwa wafanyabiashara wan chi hiyo-Wakaona heri kuongeza madhara
kwa kumwaga hewa chafu angani ili wajipatie UTAJIRI.
Miongoni mwa shughuli za kiuchumi za
binadamu zinazoharibiwa sana na uharibifu wa mazingira na mabadiliko ya tabia
ya nchi ni pamoja na kilimo, ufugaji, uvuvi n.k
Mkutano wa New
York ulioanza Septemba 22 mwaka huu wa 2009, umefanyika takriban miaka 12
kamili tangu mkutano wa Kyoto, Japan ufanyike Desemba mwaka 1997.
Katika mkutano wa
Kyoto, viongozi wa mataifa zaidi ya 150 duniani walikutana wakaweka
itifaki ambayo ingewezesha kupunguza hewani kiwango kikubwa cha gesi au hewa
chafu ya sumu zinazoletwa na hewa ya ukaa(C02) na gesi nyingine
kama CH4,N20, HFC8, PFC8 na SF6.
Mkataba huo
uliojulikana kama itifaki ya Kyoto(Kyoto Protocol) uliokusudia kupunguza
gesi za sumu duniani kwa silimia 5.2 kabla ya kufika mwaka 2012.
Mataifa yaliyoshurutishwa
kusaini mkataba huo wa Kyoto ni nchi zote 38 zenye viwanda duniani..
Mataifa yote 15 ya Umoja wa
Ulaya(EU) yakakubali kupunguza asilimia nane ya taka hewa zake duniani.
Marekani ilitakiwa kupunguza asilimia saba ya gesi zake inazotupa angani.
Japan, ilitakiwa kupunguza
asilimia sita ya taka sumu inazotupa angani, na nchi zinazoendelea zilitakiwa
kupunguza kiwango chochote kwa uhuru wake.
Marekani ilisaini mkataba huo
Novemba 12, mwaka 1998, lakini kutokana na kitisho kutoka kwa matajiri wenye
viwanda nchini humo, serikali ya Rais Bill Clinton ilichelea kupeleka ajenda
hiyo katika Bunge la seneti.
Kwa sababu, kusaini mkataba wa
Kyoto na kuutekeleza, maana yake ni kwamba viwanda vya Marekani vingelazimika
kupunguza uzalishaji.
Ni kwa sababu hii serikali ya
Clinton iliufyata.
Mkutano mwingine wa kujadili
upunguzaji wa taka za sumu hewani ulifanyika Bonn, Ujerumani Julai 2001.Utawala
wa George .W. Bush ulitangaza kujitoa katika mkataba wa Kyoto kwa madai kwamba
uliweka zigo kubwa katika nchi zilizoendelea bila kuzingatia usawa.
Marekani, waligeuka wapinzani
wakubwa katika ajenda za kupunguza hewa za sumu duniani, tangu huko mjini Bonn,
Ujerumani na mahali pengine, kwa sababu ya maslahi yake na ya viwanda vyake,
bila kujali madhara makubwa yaliyotokana na wingi wa viwanda vyake kutupa
angani hewa chafui zenye kusababisha majanga makubwa kwa Ulimwengu mzima..
Hizi ndizo haki za binadamu Ulaya na
Marekani?
Kwa shingoupande, walikubali
kupunguza hewa hizo za sumu ili kutekeleza huo mkataba au itifaki ya Kyoto ya
1997.
Katika makubaliano ya mjini
Bonn, mataifa makubwa yenye viwanda yanayomwaga kwa wingi hewa za sumu angani,
yalishauriwa kufuata malengo waliyowekewa ya kupunguza hewa ya ukka katika
anga.
Kulingana na Shirika la
Kudhibiti Uharibifu wa mazingira, hewa ya ukaa(carbon dioxide) imeongezeka sana
angani kutoka mwaka 1990 hadi sasa; na hii ni kutokana na shughuli za binadamu,
ikiwa ni pamoja na viwanda na migodi.
Wakati hewa za sumu
zinapoongezeka sana duniani, misitu ama miti inayopunguza kwa kiwango kikubwa
hewa ya ukaa kwa kutengenezea chakula chake(starch) inatoweka kwa kasi na kwa
kiwango cha kutisha sana.
Tazama nchi zinavyoongeza
sana kiwango cha hewa za sumu angani.
Mashariki ya Mbali pamoja na Oceania
wanachafua anga kwa kiwango cha asilimia 28.9.
Amerika ya Kaskazini huchafua anga
kwa kiwango cha asilimia 28.8.
Marekani
pekee inachafua anga la dunia nzima kwa moshi wa magari na viwanda vyake kwa
asilimia 24.7.
Ulaya Magharibi, kwa
pamoja huchafua anga la dunia kwa asilimia 16.5, wakati Amerika Amerika ya
Kusini nzima na Kati huchafua anga la dunia kwa kiwango cha asilimia 4.3.
Ulaya Mashariki, na
iliyokuwa Jamhuri ya Kisovieti(USSR) huchafua anga la dunia nzima kwa kiwango
cha asilimia 12.8. Mashariki ya Kati huchafua anga kwa kiwango cha asilimia
4.7.
Afrika,
inachangia katika uchafuzi wa anga la dunia kwa asilimia 3.9 tu.
Hii
ni kwa mujibu wa Ripoti za Energy Information Administration, kuanzia mwaka 1999.
Afrika inayochangia kwa
kiwango kidogo sana katika uchafuzi wa hewa angani, ndiyo inayoathiriwa sana na
madhara makubwa ya uchafuzi wa hewa angani unaoleta mabadiliko ya tabia
ya nchi.
Mifugo ya Afrika, hususan
Kenya na hapa kwetu hufa kwa ukame
unaoletwa na uchafuzi wa mazingira ya anga. Uchafuzi wa anga ndiyo chanzo cha
ukame huko kwetu Afrika. Ukamwe huu ndiyo unaochangia jangwa kuongezeka, ukame
na njaa na vifo vya watu pia.
Kulingana na uchafuzi huo wa
hewa angani, Benki ya Dunia(WB) ilishasema mwaka 2001 kwamba kila mwaka watoto
wachanga wapataao 500,000 wangepoteza maisha duniani pote kwa sababu ya
uharibifu huu mkubwa wa anga.
Vifo huletwa na viwanda vya Ulaya na
Marekani siyo? Kumnyang’anya mtu uhai siyo haki za binadamu sawa?
Kunatokea mvua za sumu(acid
rains) zitakazosababisha uharibifu mkubwa sana wa misitu hasa ya Afrika, na
wala mvua za sumu hizi za viwanda vya mataifa makubwa haziharibu huko kwao peke
yake.
Nataka kusema kwamba, Marekani
inaongoza duniani kwa uchafuzi wa anga, lakini athari zake tunapata sisi huku;
tunakufa kwa njaa na matokeo ya ukame na hata vimbunga kama Mitch, tsunami na
Katrina ambavyo vikitokea, huua maelfu ya watu bila kujali mipaka ya nchi za
viwanda na zisizokuwa na viwanda.
Ni kwa sababu hii, ubeberu wa
Marekani wa kukataa kutia saini mikataba ya upunguzaji wa hewa na taka za sumu,
kama huo wa Kyoto wa mwaka 1997, ni hatari kwa maisha ya watu, hasa tuishio
nchi masikini.
Ingekuwa heri kama Mkutano wa
New York na Afrika ya Kusini ungeipa kibano
kikali Marekani kwa kiburi chake na kuwelka mbele maslahi binafsi ya viwanda
vyao, huku ng’ombe wa masikini wanapokufa kwa maelfu huku kwetu, pasipo fidia.
Marekani, hukimbilia
kuliburuza Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuzitenga nchi nyingine kaidi
kutekeleza mikata kama ya Nyuklia n.k Ni Marekani hiyo hiyo inayotaka
Iran na Korea Kaskazini na Iran zitengwe au zishambuliwe kijeshi kwa kukataa
kutia saini mkataba wa kupunguza silaha za nyuklia.
Mbona yenyewe inakataa
kwa ubabe kutekeleza mkataba wa Kyoto, unaotaka hewa za sumu zinazoleta
majanga duniani kudhibitiwa. Ongezeko la joto duniani linaloleta hayo majanga
kama tsunami, huleta madhara hadi huku Bahari ya Hindi na kusababisha vifo hata
Kenya, Tanzania na Somali. Kwa nini Marekani haidhibitiwi ama kupewa kibano au
kushambuliwa kijeshi, kama yenyewe ilivyozishambulia Irak na Afghanistan,
na iko mbioni kuzishambulia Iran na Korea Kaskazini kwa kukataa kutekeleza
mikataba ya upunguzaji silaha za sumu?
Sumu inayoua watu si ndiyo
iliyo,o pia katika silaha za atomiki na ndiyo ile inayorushwa angani na viwanda
vya Marekani na Ulaya, bila kudhibitiwa na mtu, tena kibabe?
Ni kwa sababu hii, viongozi wa
Afrika waliokwenda New York kujadili kitisho cha hewa za sumu angani na
mabadiliko ya tabia ya nchi, wanapaswa kutoa tamko kali la kuikemea
Marekani au ikibidi kuiwekea vikwazo vya kiuchumi na kuitenga na Jumuiya za
Kimataifa, kwa vitendo vyake vya kibabe vya kuleta maafa Ulimwenguni.
Dunia haina ubavu wa kuitenga
Marekani?
Marekani haiwezi kushambuliwa
kijeshi na dunia nzima ili kuishikisha adabu iache kuiangamiza dunia kwa
kumwaga sumu tani mamilioni kwa siku, huku ikikataa kutia saini kila mkataba
unaowataka kupunguza sumu?
Wakuu wa nchi za
Afrika(akiwemo Rais Kikwete) wanaporejea kutoka New York, wanapaswa kuwaambia
wananchi wao, ni namna gani wamembana Barack Obama, kwa sababu nchi yake ina
kiburi cha ubeberu, kuendeleza uzalishaji wa taka sumu, zinazoleta saratani ya
ngozi huku, kuleta jangwa ama ukame na kuua mifugo Afrika, hususan Tanzania na
Kenya.
Shughuli za kilimo na ufugaji,
ambazo hufanywa na masikini huku Afrika Mashariki zinatatizwa sasa na
mabadiliko ya tabia ya nchi na ukame. Chakula cha binadamu hakuna, kwa sababu
Afrika inakuwa jangwa, kwa sababu Jangwa la Sahara lililoko Kaskazini
linakaribia kushikana na lile la Kalahari, lililopo Kusini.
Sasa, mvua itanyesha jangwani?
Ni kwa sababu hii, tunasema,
kiburi cha Marekani kimekwisha kuleta majanga makubwa hapa Kwetu Tanzania tangu
wakate kusaini Mkataba wa Kyoto Desemba 1997 hadi mkutano huo ulipofanyika New
York, Septemba, 2009.
Ni kwa sababu hii, Rais
Kikwete na ujumbe wake, wanapaswa kuwaambia Watanzania, Rais Obama wa Marekani,
ameambiwa kwa kiwango gani kulipa fidia ya mifugo ya Wamasai, Wajitta,
Wasukuma, Wakurya na wafugaji wengine ambao mifugo yao inaangamia kwa sababu ya
ukame ulioletwa na sumu na taka za hewani kutoka viwanda vya Mabwanyenye wa
Marekani?
Vinginevyo, Obama ana kesi ya
kujibu Dar es salaam, asijidai kukemea utawala mbaya huku na ufisadi, kumbe
nchi yake huchangia mvua kukoma kunyesha na vifo vya mifugo huku.
Je,huu ni uungwana? Ni haki za
Binadamu?
0713 32 40 74
No comments:
Post a Comment