Thursday, January 17, 2013

TUNA NG'OMBE KIBAO,TUNA IMPORT MAZIWA!

Tanzania  kuna takriban ng’ombe milioni 19.Ni ya tatu hapa Barani Afrika kwa kuwa na mifugo mingi.
Kulingana na Kituo cha Uwekezaji nchini(Tanzania Investment Centre) mwaka 2010, ilikisiwa kwamba kulikuwa na uhaba wa lita 170 za maziwa hapa nchini.
Ta
 
 
 Takriban asilimia 80 ya maziwa hugemea ng’ombe wa asili(zebu) ambao uzalishaji wao wa  maziwa kwa siku 180 za unyonyeshaji wa ndama,wastani wa uzalishaji kila ng’ombe anayekamuliwa ni  kama lita 400 tu za maziwa.
 Inakisiwa kuwa Tanzania kuna ng’ombe milioni 3.4 wa maziwa. Kati ya hawa,milioni 2.8 ni wa kienyeji,na ng’ombe wa kisasa wa maziwa ni 630,000 tu.
Ng’ombe wote kwa pamoja hutoa takriban lita milioni 4.1 kwa siku.
Mwaka 2009 kulikuwa na jumla ya viwanda 33 vya kusindika maziwa nchini,na kati ya hivyo viwanda 12 vilishafungwa.
Maziwa yaliyokuwa yakisindikwa ni wastani wa lita 580,000 kwa siku. Baada ya viwanda 12 kufungwa,maziwa yanayosindikwa sasa ni lita 60,000 tu.
Kwa sababu hiyo, Tanzania hulazimika kutumia fedha za kigeni kuagiza maziwa nje, wakati kuna mifugo mingi.
Viwanda vya maziwa hapa nchini ni Musoma Diary chenye uwezo wa kuzalisha lita 120,00 kwa siku,Tanga Fresh kina uwezo wa kuzalisha lita 30,000 kwa siku,bahati mbaya viwanda hivi huzalisha chini ya kiwango.
Kulingana na Sekta ya Maziwa,ukanda wa Ziwa VICTORIA una mifugo mingi. Wapo wafugaji ambao kila mmoja ana  ng’ombe takriban 1,000 ambao thamani yao ni shilingi milioni 400.
Hata hivyo, wafugaji hawa hawajatambuliwa na rasilimali hizi hazijarasimishwa wala kupewa ithibati ya utambulisho na Kituo cha Uwekezaji nchini(TIC).
Thamani ya ng’ombe 1,000 hupita kiwango cha Dola 100,000 ambazo mtu huhitajika kuwa nazo ili atambuliwe na TIC kama mwekezaji.
Licha ya maziwa kuwa naviini lishe,bado serikali haijatilia mkazo sekta ya maziwa hapa nchini.
Kulingana na Mamlaka ya Mapato(TRA) mwaka 2008,zilikusanywa shilingi bilioni 5 za kodi kwenye maziwa yaliyoingizwa hapa nchini kutoka nje ya nchi.
Wadau wa sekta ya maziwa wanasema,sekta hii ikiboreshwa itatoa ajira rasmi kwa watu 2,133 na zisizo rasmi 40,000.
Tanzania inaweza kutumia fursa ya maziwa kujipatia kipato katika Soko la Pamoja la Afrika Mashariki(The East African Common Market).
   AJABU
Ni kwamba, Kenya ndiyo inayoongoza Afrika Mashariki kwa kuwa na mifugo mingi,hususan ng’ombe na mbuzi,lakini Kenya ndiyo inayoongoza kwa kuzalisha lita milioni 9.5 kwa siku;kasha husindika lita milioni 1.3 kwa siku.
Sekta ya maziwa ndiyo ya kwanza Kenya katikakuondoa umasikini. Uganda huzalisha lita 400,000 kwa siku wakati Tanzania huzalisha lita 60,000 tu.
Rwanda,imeanzisha mpango wa kila familia kuwa na ng’ombe wa maziwa ifikapo 2015.Wanatarajia kuzalisha lita 431,000 kwa siku.
Kwa sababu hiyo, lita 60,000 zinazosindikwa hapa Tanzania hutokana na viwanda viwili tu vya Musoma Diary na Tanaga Fresh.
Ukanda wa Ziwa Victoria humuliki ng’ombe milioni 8,mbuzi milioni 5  na kondoo milioni 1.2.
TANZANIA hufuga ng’ombe wa asili,waitwao,Tanzania shorthorn Zebu, ambao hustahimili mazingira magumu,lakini hawazalishi maziwa mengi.
Kuna ng’ombe wa kisasa wa maziwa 560,000 hapa nchini,na wanaokamuliwa ni 224,000 ambao hutoa lita milioni 485 za maziwa yasiyosindikwa,na hayajarasimishwa kuingia katika soko rasmi.
Ng’ombe wa asili milioni 5.6 hukamuliwa na kutoa lita milioni 950 za maziwa ambayo hayasindikwi,kwa hiyo hayauzwi katika soko rasmi.
Wakati Tanzania imeweka Mkazo katika uwekezaji wa migodi ya madini kama Tanzanite,dhahabu,almasi,ruby,nickel na mafuta,makaa yam awe na gesi, imesahau sekta ya mifugo na mazao yake kama ngozi na maziwa.
Hadi sasa kuna takriban migodi 10 hapa nchini:Williamson Diamond,Golden Pride(Resolute),Geita Gold Mine, Mererani/Tanzania One,Bulyanhulu Gold Mine,North Mara Gold Mine, na Kabanga Nickel Project.
Kufuatia hali hii, shilingi mabilioni zinazotumika kuagiza lita milioni 170 za maziwa nje ya nchi, zingetumiwa kwa kazi nyingine kama maziwa ya hapa nchini yangesindikwa na kuuzwa katika soko hilo kubwa.
Kwa nini Tanzania iwe na mifugo mingi halafu izidiwe na Kenya kuzalisha mazi

No comments:

Post a Comment