“Mke wake
alikuwa amesafiri;sasa nikalazimika kulala na watoto wa Pastor Marco Pollo(siyo
jina lake halisi).
Siku ya kwanza nikalala na watoto,ya pili akasem, “Sarah
nakupenda!”
“Nikamuuliza,
umenipendaje? Akasema,unaona mke wangu hayupo… nilikataa!”
Baada ya
siku tatu,akaingia kwa nguvu chumbani,akanishika na kuniziba mdomo,akanibaka!
Siku hiyo nilishika mimba!”
Mwandishi wa
safu hii alimuuliza Sarah,kwa nini keshoye hakumchukulia hatua za kisheria
Mchungaji huyu,Marco,ili sheria ichukue mkondo wake?
“Niliona
aibu; lakini nilimwambia dadangu, akanifukuza nyumbani kwake,nikaenda
Kitangiri,kwa kaka yake Mchungaji Marco." Sarah akasema.
Nilikutana na Sarah mwaka 2003, wakati huo nikiandika habari za uchunguzi katika gazeti moja la Jijini Mwanza.
Naam,
ilikuwa Machi 4,mwaka 2003, mwandishi huyu alipofika Bugarika,jijini Mwanza
kumuuliza Mchungaji huyo kwa kanisa moja la Walokole jijini Mwanza:
Kwa nini
alimbaka Sarah, usiku mmoja,wakati
alipokuwa akifanya kazi za ndani nyumbani kwake,mke wake alipokuwa safarini?
Sarah(21)
alikuwa akiishi Bugarika,Jijini Mwanza, na alifanya kazi za ndani nyumbani kwa Mchungaji huyo, Bugarika
B, wakati yeye alikuwa akiishi huko Maina,Nyakato.
Baada ya
kubakwa,Sarah alishika ujauzito mwaka 2001.Alijifungua watoto mapacha Oktoba Mosi,2002. Mapa wawili wa kiume na kike.
Sarah,
alisema Mchungaji Marco Pollo alikataa kuwahudumia mapacha wale, hata yule wa
kiume alifariki Julai 9,mwaka 2003.
Sarah,
alifungua kesi Mahakama ya Mwanzo iliyoko Barabara ya Makongoro,Jijini Mwanza
ili kudai Mchungaji huyo achukuliwe hatua.
Mahakama
ikamwamuru Mchungaji huyo kulipa shilingi 20,000 kila mwezi kwa ajili ya
matunzo ya pacha aliyenusurika,baada ya mwenzake kufariki dunia.
Huyu pacha
aliyenusurika,Lucy aliishi kwa taabu na mamaye,baada ya pacha mwenzake,Robert
kufariki.
Basi,
Mwandishi wa makala hii akamuuliza Mchungaji; “kwa nini wewe ni Mchungaji
halafu unambaka msichana wa kazi,unamsababishia ujauzito,kisha unakataa
kumhudumia hadi pacha mmoja anapoteza uhai?”
Akanitazama,kisha
akaendelea kupiga kinanda. Nilimuuliza ikiwa Wachungaji wanaruhusiwa
kubaka,kuwapa ujauzito wasichana kasha kuwatelekeza?
Akaacha
kupiga kinanda na kusema angejinyonga; kwa sababu kazi hii hiyo ya Uchungaji
ndiyo iliyomwezesha kula na kuvaa. Kwamba hakuwa na kazi nyingine isipokuwa
hiyo.
Alikiri
kufanya kitendo hicho, akasema kama ‘stori’ hiyo ingeandikwa gazetini,
angetimuliwa kazi; kwa hiyo aliona ilikuwa heri kujinyonga!
Naam, kwa
miaka 10 niliazimu kutoandika ‘stori’ hiyo ya Mchungaji Marco kumbaka Sarah(21)
ili kunusuru maisha yake.
Hata
hivyo,nimeamua kuandika kisa hiki ili kuwaonesha wasomaji wetu namna gani
ilivyohatari kuwaamini na kuwategemea
wachungaji,maaskofu,mitume,masheikh,maimam na manabii wa siku hizi wanaoota
kama uyoga hapa nchini!
Ukisikiliza
mahubiri yao yamejaa uchochezi na fitina.
Baadhi yao
wameanzisha vituo vya redio,ambazo sasa tunajua kusudi siyo kuhubiri DINI bali
uchochezi,fitina na uchafu-bahati mbaya sana wanatumia vitabu vitakatifu,Qur’an
na Biblia kuhalalisha uchochezi wao.
Utaona,wanavurugana
mno na washiriki wa makanisa na misikiti wanayoongoza.
Wakati
mwingine wamebaka hata vichekechea,wamepora wake za waumini wao, wanapowatisha
kwa nguvu zao za MIUJIZA na ushetani uliodhahiri,mwisho hujipatia pesa na
kununua magari ya fahari.
Rai yangu
katika safu hii leo ni kwamba, kama serikali ya Tanzania itaendelea kuwaamini
wachungaji,maaskofu na manabii hawa wanaomea kama uyoga, basi Tanzania iko
hatarini sasa kuliko jana.
Nadhani,
tunakumbuka kilichotokea Kanungu,Uganda,zama za Father Kibwetere na
wenzake.Waliteketea raia 530 katika ndimi za moto,kwamba hiyo ndiyo staili ya kuendea motoni!
Wamebaka
watoto,hata wanafunzi.Hawa mafather wamelawiti watoto wa kiume,wamekwapua wake
za waumini.
Wanafanya
biashara ya maji ya Baraka toka Israeli na kutajirika; wanaendesha magari ya
fahari kuliko hata wabunge. Pesa walitoa wapi kama si ufisadi wa kutisha?
Bahati mbaya
sana, serikali ya Tanzania imeendela kuwaamini sana matapeli hawa wanaotaharukisha
umma kwa kutumia uchawi na nguvu za giza kutoka Nigeria,Jamhuri ya Kongo na
Marekani!
Wamewatapeli
Watanzania kwa njia anuwai,serikali ikiwa kimya.Sasa wanachochea vita miongoni
mwa Wakristo na Waislam.
Wachochezi
hawa wamejivika Uislam wenye itikadi kali na Ukristo wenye itikadi kali, “Extremism”
wanawachochea waumini wao kwamba kifo ni kifo hata usipokufa kwa risasi za
polisi,utakufa kwa Ukimwi!
Migogoro,maandamano
na fujo vimeanzia makanisani na misikitini ambako wachungaji,maaskofu,manabii
na mitume hawa hupora zaka na sadaka za waumini wao hadi wanapoaanza kupigana
wenyewe kwa wenyewe serikali ikiwa kimya!
Kwa nini
wakwapuzi hawa wa fedha za Watanzania hawachukuliwi hatua za kisheria?
Katazame
miradi ya ujenzi wa makanisa. Ilishasimama miaka 30 iliyopita,baada ya sadaka
kuporwa.Hawana aibu, wana ndimi za Ibilisi, na jeuri na wafedhuli
kupindukia.Hufika wakati wakaitisha hata serikali,kwamba wataiombea ipinduliwe!
Kuna baadhi
ya viongozi wa siasa wanaoshirikiana na hawa kufanya usihiri na uchawi ili
wachaguliwe wakati wa chaguzi za kuwapata viongozi wa kisiasa.
Sasa,Watanzania
tunashuhudia misikiti na makanisa yanavyoshindana nani awe rais wa Tanzania
mwaka 2015!
Inawezekana
Kenya wasipigane katika Uchaguzi wa Machi mwaka huu 2013,lakini mwaka 2015
Tanzania iko hatarini kuliko wakati wowote lilipoanza kuwapo Taifa,Desemba
9,mwaka 1961.
Hayati
Mwalimu Nyerere aliwakemea watu hawa,viongozi tulio nao wanawaogopa;wanachelea
kuwachukulia hatua kali za kisheria.
Matokeo yake,
Tanzania sasa iko mikononi mwa hawa watu wa dini ambao wanachochea waumini wao
kupigana,kwa sababu ya tofauti na itikadi za kidini.
Hakuna
kuvumiliana tena,makanisa yanachomwa moto na Waislam hao uchwara,na sasa
Wakristo nao wanataka kujibu mapigo!
Wanasema ni
ujinga kusamehe 7 mara 70 kama alivyosema huyo Yesu wa Nazareti.
Tanzania iko
hatarini kuteketea katika miali ya moto wa mapigano ya kidini.
Ibilisi,
anapojivika ngozi ya chui na kujilisha ‘kondoo’ walionona;kuwabaka wasichana
kama Sarah na kuwapa ujauzito, serikali hii ya Jakaya Kikwete inapumbazwa kwa
kupigiwa gitaa,inalala usingizi na kudhani kuna amani na salama misikitini na
makanisani!
Amani ya
nchi inanajisiwa misikitini na makanisani siku hizi,kuliko wakati wowote.
Shime,
serikali iwamulike kwa kurunzi kali hawa masheikh,maimam,mitume na manabii na
wachungaji wa siku hizi, ambao ni wachungaji wa mishahara tu wanaojilisha kwa
kondoo walionona kama akina Sarah!
Alamsik
watumishi wengi wa Mungu wametelekeza kazi ya Mungu na kutamani starehe na kuendekeza kujionyesha kwenye mitandao na ndoa na kufanya Happy birthday zao kwa mamilioni ya pesa wakiacha kondoo wakiwa kwenye hali ya sintofahamu na wale ambao hawajafikiwa wakibaki kwenye hali ngumu. hadi sasa kuna vijiji ambavyo havina makanisa lakini watu hawajali kuna kila sababu ya watumishi wa Mungu kudaiwa damu za watanzania wanaokufa kila siku pasipo wokovu huku watu wakipiga kampeni za kupata vyeo na kutafuta heshima huku maelfu wakiwa taabuni ebu wapendwa tuokoe kwanza roho za watu watoke kwenye ufalme wa giza tunawashukuru WAnawake wa Tanzania Assemblies of God kujali UMISHENI NA KUCHANGIA ZAIDI KAZI YA MUNGU NI VIZURI SOTE TUIGE MFANO HUO WA KIMUNGU SANA HONGERA MKURUGENZI KWA MOYO ULIONAO WA KIMUNGU MAMA FARAJA HAMULI.
ReplyDelete