AZIMIO LA
ARUSHA ,lilipoanzishwa mwaka 1967, liliwafanya baadhi ya mafisadi waliojichotea
mali za mabilioni kutimkia uhamishoni?
Kwa sababu
hiyo, miongoni mwa ‘mabilonea’ hao, labda ni Oscar Salathiel Kambona?
Tujadili
msuala ya zamani kidogo,ili kutazama kwa kina ujanja wa siasa. Kambona alishika
nafasi nyingi,nyeti sana serikalini na katika Chama cha Tanganyika National
Union(TANU) zama hizo.
Alikuwa
waziri katika wizara nyeti, tena akawa Katibu Mkuu wa TANU,kabla ya kutimkia
Uingereza mwaka 1967 baada ya kukosana na Hayati Baba wa Taifa,Mwalimu Julius
Kambarage Nyerere. Ilikuwa kuhusu Azimio la Arusha.
Kambona, ati
alikuwa na mali nyingi za mabilioni ya fedha,majumba mengi ya kupangisha jijini
Dar es salaam na kwingineko nchini.
Wakati wa
Azimio la Arusha kumiliki mali nyingi ilikuwa kuhalifu sera za nchi,na ulikuwa
Ubepari.Kambona alipingana na Nyerere.
Aliteuliwa
kuwa waziri kwa mara ya kwnza katika serikali ya MADARAKA.Septemba 9 mwaka 1960
wakati Tanganyika ikijiandaa kupokea uhuru kutoka kwa ukoloni wa Kiingreza.
Aliteuliwa
waziri wa Elimu,wakati huo Julius Kambarage Nyerere alikuwa waziri
Kiongozi,wadhifa sawa na Waziri Mkuu.Aliendelea kuwa waziri wa Elimu chini ya
Waziri Mkuu,Kambarage Nyerere,na baadaye Rashid Mfaume Kawawa.
Madaraka
hayo yalimpa kuheshimiwa sana na kupendwa na wananchi.Baada ya nchi kuwa
Jamhuri,Desemba 9,mwaka 1962,Kambona aliteuliwa kuwa waziri wa Mambo ya Nchi za
Nje,baadaye tena akaongezewa madaraka na
kuwa waziri wa Mambo ya Nchi za Nje na Ulinzi.
Alikuwa na
kawaida ya kuchana nyewele zake akazipinda pembeni kidogo mwa uso wake.Mtindo
huo ulijulikana sana miongoni mwa vijana wa wakati huo kama, “Kambona Style”,wakati
huo kabla hujachana nywele kwa mtindo huo wa Kambona,basi ulionekana wa kuja.
Kambona,ndiye
aliyezima uasi wa jeshi lililotaka kumpindua Mwalimu,Januari 20 mwaka 1964.Siku
hiyo wakati Jeshi likiasi,Rais NYERERE,Makamu wa Rais Kawawa na mawaziri
wengine walitimkia mafichoni kusikojulikana.
Baadaye,jeshi
likavunjwa likaanzishwa Jeshi la Wananchi wa Tanzania(JWTZ), lakini baadaye
baada ya kuanzishwa Azimio la Arushwa,mwaka 1967 Kambona akapinga,kwa kile
wanachosema, alikuwa na mali nyingi ambazo zilikuwa mbioni kutaifishwa na umma.
Alijifanya
kuugua, akaenda Nairobi nchini Kenya kutafuta tiba. Akiwa Nairobi,yeye Kambona
na mkewe,Flora na binti yao wakakwea ‘pipa’ kwenda London,Uingereza.
Alipofika
London,akaomba ukimbizi wa kisiasa.Wakati huo,Mwalimu alikuwa amevunja uhusiano
wa kibalozi na Uingereza,wakati huo ikiwa serikali ya Waziri Mkuu,Harold
Wilson,kufuatia mgogoro wa Rhodesia, siku hizi ni Zimbabwe.
Uhusiano wa
kibalozi wa Tanzania na Uingereza ulivunjwa kuanzia mwaka 1966 hadi 1969.
Kufuatia
hali hiyo,Kambona alikubaliwa ukimbizi wa kisiasa Uingereza, huku byuma aliacha
wafuasi ambao wengine walitiwa mbaroni na wengine kutimkia ng’ambo.
Dk.Masha mshirika wa Kambona?
Kambona
akatimuliwa uanachama wa TANU,akaondolewa ubunge pamoja na wenzake wanne.
Miongoni mwa
wabunge waliotimuliwa mwaka 1968 ni Dk.Fortunatus Lwantyantika Masha(Mbunge wa
Jimbo la Geita Mashariki zama hizo),Joseph Kaselabantu(Nzega Mashariki),Wilfred
Mwakitwange(Taifa),Stephen Kibuga(Mufindi) na Modestus Chogga(Iringa Kusini.
Wengine ni
Eli Anangisye(Rungwe Kaskazini),Gervas Kaneno(Karagwe) na Jeremiah
Bakampeja(Ihangiro,Bukoba).
Januari
22,mwaka 1968,kikao cha kwanza cha Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
kikatajiwa mali nyingi za Oscar Kambona,aliyetimkia Uingereza.
Kwamba,kabla
hajatimkia London,aliingiziwa katika akaunti zake katika benki moja ya
Uingereza shllingi 500,000 ambazo leo ni kama milioni 600 hivi.Ilikuwa Desemba
6,mwaka 1966 miezi miwili kabla ya Azimio la Arusha.
Kauli hiyo
ilitolewa na Kawawa,wakati huo Waziri Mkuu, alikuwa akijibu swali la Mbunge wa
Rombo,Alphonce Maskini,bungeni.
KAMBONA
FISADI?
Baada ya
Azimio la Arusha,ikatangazwa kwamba Kambona alimiliki majumba mengi ya
kupangisha Dar es salaam,Morogoro,Songea ambayo thamani yake ilikuwa shilingi
485,612 sasa ni kama shilingi milioni 500 hivi.
Kawawa
alisema pia kwamba,KATI YA Juni 1965 na Desemba 1966 Kambona aliweka katika
akaunti yake ya Jijini Dar es salaam kiasi cha shilingi 896,800 ambazo leo
zingekuwa na thamani kama shilingi
bilioni moja hivi.
Matokeo ya
uchunguzi wa Benki Kuu(BoT)ULIBAINI PIA KWAMBA,Juni 1965 Kambona aliingiza
Pauni za Uingereza 65,800 ambazo leo ni kama shilingi milioni 165.Julai 1967
eti aliweka Pauni 60,000 ni shilingi milioni 150 za sasa.
Na
kwamba,alikuwa akiingiza pesa nyingi kwenye akaunti zake,na alimiliki majumba
mengi yaliyojengwa Dar kwa mabilioni ya shilingi.
Ati, Mwizi Mkubwa?
Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alimtaja Kambona kama ‘mwizi
mkubwa’ leo tungesema Fisadi Kubwa lililojilimbikizia mali nyingi.Benki kuu ya
Tanzania(BoT) Ikamwandikia barua aeleze alikopata fedha za kigeni kumwezesha
kukwea ‘pipa’ kutoka Nairobi hadi London.Kumbuka wakati huo kupata fedha za
kigeni ilikuwa ‘mbinde’ siyo kama siku hizi kuna Bureau De Change, tena kuna dola nyingi na Euro kwenye Black Market.
Haya
yalielezwa Bungeni na Waziri Mdogo wa Fedha,Bwana S.Rashid alipokuwa akijibu
swali la Mbunge wa Bagamoyo,Bwanga Mgaza.
Kambona
akiwa Uingereza alishinda Bahati Nasibu, ‘Bingo’ ya kimataifa na kulipwa
mamilioni ya pesa.
Wakati vyama
vingi vikianzishwa hapa nchini mwaka 1992,Kambona alirejea nchini na mkewe,Flora
na binti yao.
Bilionea,Masikini
gani huyu?
Aliishi
Sinza, katika nyumba ya kawaida sana.Alidai arejeshewe nyumba yake ya
Msasani,ambayo ilidaiwa ilikaliwa na Rashida Kawawa.
Huyu
anadaiwa kuongoza majaribio ya kutaka kumpindua Mwalimu Nyerere,mapinduzi
ambayo aghalabu yalishindikana.Kambona alikanusha kuteka ndege ya abiria kutoka
Mwanza hadi London,mwaka 1982,nilishasimulia kituko hicho.
Mwaka 1992,
aliporejea Tanzania Kambona akachaguliwa kuwa Rais wa Chama cha TADEA.Alipokonywa
uraia akaambiwa ni Mnyasa wa Malawi,akaamuliwa aondoke nchini.
Alikaidi,
akabaki Dar lakini mwaka 1993 serikali ikamrejeshea uraia wake kwa sababu za
kiutu.Alifariki akiwa London,Uingereza mwaka 1997,mwili wake ukarejeshwa Dar es
salaam kwa mazishi.
TADEA Kimeongozwa
muda mrefu na RIFA Chipaka,Mshirika wa Kambona aliyewahi kufungwa kwa makosa ya
uhaini,mwaka 1971 baadaye alisamehewa.
Azimio la
Arusha likatokomezwa miaka ya
karibuni,kwa sababu hiyo Kambona angekuwa hai na mali zake angekuwa ‘tycoon’
la Afrika kama siyo duniani.
Sasa
jiulize,pesa zake zilikwenda wapi? Majumba yake yalikwenda wapi? Angekuwa
mwekezaji!
Oscar Salathiel
Kambona, alizaliwa Agosti 13, mwaka 1928 kandoni mwa ufukwe wa ziwa Nyasa
ambalo linaleta kasheshe baina yetu na Joyce Banda,mjukuu wa Kana-Ka
Mzizi,Banda.
Alizaliwa
katika kijiji cha Kwambe,Mbamba Bay eneo la wilaya ya Mbinga.
Rafiki
Mkia wa Fisi?
Walikutana na Mwalimu,Julius(Butiama walimwita Kambarage
tu)Nyerere katika sekondari ya Tabora Boys.Wakati huo,Mwalimu alikuwa
akifundisha katika shule ya St. Mary’s ya Wakatoliki pale Tabora. Baadaye sasa ndipo
Kambona aliteuliwa Katibu Mkuu wa TANU.
Wakati wa
maasi ya jeshi la kikoloni,Januari 1964,Kambona alijitoa mhanga akawafuata
wanajeshi Calito(Lugalo) jeshini;badala ya kurushwa kichura akaongea nao na
wakakubaliana.Akina Nyerere na Kawawa na mawaziri walishajificha kabisa.
Askari
walitaka nyongeza ya mishahara,na walitaka wale askari wa Uingereza wapishe
vyeo askari Weusi wazalendo,ilikuwa ngoma nzito,Nyerere na Kawawa walishatoroka-Mapinduzi!
Kambona
katuliza fujo,mambo yakawa shwari,ukawa urafiki mkubwa na Mwalimu.Wakati
Kambona anamwoa aliyekuwa Miss Tanzania,Flora,Nyerere alikuwa Best Man!
Kumbe,rafiki
mkia wa fisi? Kambona na Nyerere wakakorofishana,Kambona katimkia London, Julai
mwaka 1967akawa anafanya kazi ya mshahara mdogo,na nyumba ya kuishi alilipiwa
na Uingereza kwa ruzuku ya serikali. Utajiri alipeleka wapi?
Kufuatia
kuondoka kwake,nduguze,Mattiya na Otini Kambona walitiwa mbaroni na serikali.
Unacheza wee!
Jaribio la
mapinduzi la Oktoba 1969 alisemwa kuhusika,alihukumiwa akiwa
uhamishoni,aliporejea nchini mwaka 1992 akaahidi ‘kutoboa siri’ mahali Nyerere na Kawawa walipoficha
mabilioni ya fedha walizouibia umma wa Watanzania!!
Kumbe, ‘geresha’ tu, wanasiasa bwana! Kambona
hakuwahi kuwatajia Watanzania fedha walizoiba Nyerere na Kawawa tangu Uhuru.
“Credibility”
ya Kambona ilishuka,watu wakamwona aliyechanyikiwa tu,akazidiwa kete na akina
Mtikila na Mrema, alisema uongo. Hadi anakufa London Julai mwaka 1997 hakuwa na
mvuto tena katika siasa za Tanzania.
Atakumbukwa
kama mkimbizi wa kwanza wa Tanzania London, alipigia debe mfumo wa vyama vya
upinzani,na alijaribu kumpindua Mwalimu.
Propaganda,chenga ya mwili ama Danadana?
Hayati Mwalimu Nyerere na
Kawawa,walisema
Kambona aliiba mabilioni ya shilingi na kutokomea nayo Uingereza.
Wakati Oscar
Salathiel Kambona, alipofika uwanja wa ndege wa Dar wakati anarejea toka
uhamishoni,akasema angemwaga mtama mahali Nyerere na Kawawa walipoficha pesa
walizoiba nchini!
Hata hivyo,
hawa wote watatu wamefariki.Nasi tungali tunajiuliza, “Hizo fedha zilizodaiwa
kuibwa(na pande mbili za shilingi) na Nyerere,Kawawa na Kambona, zilifichwa
wapi? Ama,ndiyo mabilioni ya Uswisi?
Bila shaka,
hapakuwa na mwizi mahsusi kati yao wote watatu,bali propaganda tu kati yao na
kuchafuliana majina!
0713 324 074
No comments:
Post a Comment